100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

MUNGU WAKO NI MKUU KULIKO KILICHO MBELE YAKO

 
MUNGU WAKO NI MKUU KULIKO KILICHO MBELE YAKO
2 Wafalme 7:3-4,6

Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu.Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.

WHATSAPP GROUP
Kribu katika group letu la whatsapp kwa kubonyeza link hii hapa chini
https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf

Nakusalimia tena katika jina la Yesu lililo kuu kupita majina yote.
Ni wakati mwingine tena tunapata kibali cha kukutan pamoja katika meza ya Bwana kwa ajili kupata kile alichokusudia tuweze kupata

Leo tunatazama kwa habari ya watu wa Mungu hawa waliofanya maamuzi sahihi ya kukimbilia kwa Mungu katika wakati mgumu waliokuwa nao na huku mauti ikiwa mbele yao,
Biblia inasema mji mzima wa Samaria ulikuwa katika hali mbaya ya njaa kiasi ambacho watu walianza kupeana mawazo ya kula watoto wao,
Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani njaa hiyo ilikuwa kuu mno,

Kama ambavyo mimi na wewe tunaweza kujichukulia maamuzi binafsi pasipokujari maamuzi hayo yatatuumiza kiasi gani kwa kutazama tu tatizo lililoko mbele yetu kwa wakati huo.
Ni ukweli kabisa kwamba inawezekana tatizo hilo ni kubwa mno na limeondoa amani,furaha, heshima na nguvu ndani yako kiasi ambacho huna tumaini tena lakini niko hapa leo kukwambia yakuwa, Haijalishi unaona wingi wa jeshi kubwa kiasi gani mbele yako lakini Jeshi lililo upande wako katika ulimwengu wa roho ni kubwa mno kuliko jeshi la maadui zako.
Inawezekana kwa namna ya mwilini adui zako wana nguvu kuliko wewe na hata ukijitazama unajiona kupigwa mapema sana maana yamkini wewe ni mmoja lakini wao ni kundi kubwa lakini kumbuka hili litakusaidia sana yakwamba, nguvu za maadui yako zinaweza kuwa katika maeneo mawili pekee,

1.nguvu yao inaweza kuwa katika silaha zilizo katika mikono yao au nguvu kwa namna ya mwilini,lakini nguvu zako ziko katika Neno la Mungu.

2.inawezekana pia nguvu za maadui zako ni chanzo cha miungu iliyoko nyuma yao lakini ikiwa hivyo ndivyo basi ujue nguvu yako iko katika Mungu wa miungu, maana yake hata hiyo miungu iko chini ya Mungu wako na haina nguvu za kutosha kumkabiri.


Mtumishi wa Mungu Elisha alipoona hali ya hofu ndani ya yule mtu aliyekuwa upande wake baada ya kutokewa na majeshi ya shamu chini ya mfalme Ben-hadadi na wakati huo biblia inasema Elisha alikuwa amezungukwa pande zote na majeshi ya shamu yamekaa katika pande zote kuuzunguka mji wa samaria, ambapo kikawaida hasingeweza kupigana nao kwa jinsi ya mwilini, kwa vyovyote vile ilikuwa ni lazima Mungu wake aingilie vita yake................

Maandiko yanasema
2 Wafalme 6:15-16
Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje?Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.


Ndivyo ambavyo mara nyingi pia watumishi wa Mungu wengi wamejawa na hofu ndani yao pindi tu adui anapojitokeza mbele yao, lakini ukitambua nguvu iliyo nyuma yako utashangilia ushindi wa vita kabla hujapigana hiyo vita,

Ndiyo maana ni muhimu sana kuwa na uwezo wa kuona rohoni, hii itakusaidia kuona kitakachotokea kabla maadui zako hawajajua hatima ya vita wanayotaka kupigana na wewe,
Njia pekee ya kuondoa hofu na mashaka vilivyokuwa ndani ya mtumishi wa elisha ilikuwa ni kumuonyesha jinsi ambavyo jeshi la Mungu limewazunguka, wakati maadui zao wakifikiri wamewazunguka kumbe hawakumzunguka Elisha bali wamezunguka uzio wa jeshi la Mungu lililoachiliwa kutoka juu mbinguni kuhakikisha mtumishi wa Mungu anakuwa salama.

Nataka niseme hao wanaofikiri wamekuzunguka watangazie wapate kujua yakuwa hawajakuzunguka wewe bali wao ndio wamezungukwa na jeshi la Bwana wa vita.....

2 Wafalme 6:17-18
Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.Na walipomtelemkia Elisha akamwomba BWANA, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.


Mwanzoni nimesema ni muhimu sana kuwa na uwezo wa kuona rohoni kwa maana ya huu msitari wa 18 unaompa nguvu Elisha ya kutamka pigo na likatokea kwa adui zake.

Ni muhimu kuona rohoni kwa sababu huwezi kupigana na adui husiyemuona,
kwa namna ambavyo elisha alikuwa amezungukwa ingekuwa ni mkiristo hasiye na nguvu za rohoni lazima katika mawili angefanya moja either kutafuta upenyo wa kukimbia na hasingefanikiwa maana kila eneo wako wanajeshi wa jeshi la adui ama pili angejilaza chini akimwambia Mungu mikononi mwako roho yangu naiweka,
ni kwanini, ni kwasababu kinachoweza kumpa nguvu mtu mbele ya adui yake ni aina ya siraha aliyo nayo na ujuzi wa kuitumia.
Elisha alikuwa na nguvu kwasababu aliona katika roho jeshi lililoko upande wake na hivyo hakuhitji kukemea bali alitamka Neno na ikawa kama livyonena na maandiko yanasema jeshi lote la adui likapigwa na upofu, hii inawezekana kwako na kwangu pia ikiwa tutakuwa na nguvu za kutosha ndani yetu na kuwa na uwezo wa kuona rohoni namna ambavyo Bwana anapigana upande wetu, hii itaachilia ujasiri ndani yetu na kuondoa hofu lakini zaidi sana pale tutakaposimama katika nafasi zetu tutaruhusu utukufu wa Mungu upate kupita,

Katika kitabu cha 2wafalme sura ile ya 7
Wakoma pamoja na udhaifu walio kuwa nao lakini wanaamua kwenda panapo chakula ile hali wakielewa mbele yao kuna jeshi la adui, lakini Mungu alivyotazama imani yao na ujasiri ulio ndani yao akaamua kuingilia kati vita yao na kubadili hatua zao kuwa kishindo kikuu mno kiasi ambacho jeshi la adui likafikiri ni jeshi kubwa linakuja kuwakabiri kumbe ni kakikundi ka watu wachache kanakuja lakini kamefunikwa na nguvu za Mungu,
Ndiyo maana popote penye nguvu za Mungu pana utisho wa Mungu.

biblia inasema wale maadui walikimbia na sio kukimbia tu mpaka wakaacha na vyakula na vitu vyao vya thamani.

Sikia, kuna wakati unahitaji kufunikwa na nguvu za Mungu na kuzungukwa na Utukufu Wa Mungu tu ili madui zao wapate kukimbia mapema hata kabla hujatia neno lolote lakini zaidi sana Imani thabiti hisiyoyumbishwa na aina ya mazingira ni siraha pekee ya kumkabili adui haijalishi ni mkubwa kumliko goriathi.

Jambo pekee unalotakiwa kufanya ni kumwambia Mungu wako aingilie kati vita yako alafu wewe ubaki pembeni kutazama namna ambavyo maadui zako wanatawanyika na kukimbia mbele zako.
Sio tu utawashinda bali utachukua na mateka yao na zaidi pia utarejea katika nafasi yako huku utukufu wa Mungu ukiwa juu yako na kila mtu atajua Mungu wako ameshinda.

MUNGU AKUBARIKI SANA
Tutaendelea na somo letu kadri roho mtakatifu atakavyotuongoza kutenda.

Post a Comment

1 Comments