100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

NI MUHIMU KULINDA KUSUDI LA MUNGU

 

Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.
Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.

Kila mtoto anao wajibu kuhakikisha analinda maono yake haijalishi ni mdogo kiasi gani au yupo kwenye mazingira magumu kiasi gani ndio maana MUNGU alimuuliza "YEREMIA waona nini"

WHATSAPP GROUP

Yeremia 1:4-12
Neno la Bwana lilinijia, kusema,
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.
Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.
Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
Tena neno la Bwana likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi.
Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.


Mungu hakuwa na shida na kilichokuwa mbele ya Yeremia kwa wakati huo lakini alitaka kujua kama anaona sawasawa na kusudi lililowekwa ndani yake.
Ukiwa kama mzazi husijaribu kumpelekea mtoto wako vile unavyotaka wewe, kama huna uwezo ndani yako wa kuelewa ni nini Mwanao amebebeshwa basi omba Mungu ajifunue kwa huyo mtoto kwasababu wajibu wa mzazi kwa mtoto sio kumpeleka anakokutaka yeye na kusikilizwa kwa kila kitu bali wajibu wake ni kuwa msaada wa kumfundisha na kumuelekeza kwa msaada wa Mungu katika njia bora ya kumfikisha katika hatima au saa ya kutokeza kwa kusudi la Mungu ndani yake, kama unafikiri mimi ni Muongo kamuulize YESE,
nina uhakika laiti kama angelijua kilichoko ndani ya DAUDI asingelimfanya kuwa mchunga kondoo.Bali angemlinda kwa nguvu zote na kuhakikisha anamlea kwa malezi ya kifalme.
Pamoja na kwamba daudi alikuwa na ufalme ndani yake lakini familia yake ilimsahau na kumuona kama mtoto hasiye na maana sana katika familia kias ambacho mpaka kwenye ibada alikuwa akisahaulika na sio ibada tu mpka kwenye utambulisho wa familia daud alisahaulika.ukiona mzazi wako hawezi kuona kilicho ndani yako simama kwa nafasi yako haijalishi anakutazama kwa sura gani lakin nakuhakikishia saa ikifika ataelewa nini kilichoko ndani yako na hapo ndipo Mungu ataanza kupitisha msaada kwake kama mzazi kwenda kwa mtoto lakini nje na hapo watoto wengi wamefanya mapenzi ya wazazi wao na kusudi la Mungu ndani yao limekaa pending.
Ni hivi IBRAHIMU alikuwa anaelewa ahadi ya MUNGU kwake na kwa uzao wake vinginevyo husije ukafikiri ilikuwa ni rahisi kwake kumtoa sadaka mtoto wake ISAKA ile hali akitambua ni mtoto pekee na aliyemgonja kwa muda mrefu kutoka katika tumbo la mkewe SARAI, lakini kile kitendo tu cha kutii maagizo ya Mungu ya kumtoa sadaka kilitosha tu kumtenganisha yeye na mwanae Isaka, kwasababu ISAKA yule aliyeambatana na Ibrahim kuelekea kwenye madhabahu ya kutolea sadaka alikuwa ni Isaka mtoto wa Ibrahimu lakini ISAKA aliyerudi nyumbani na ibrahimu baada ya mwanakondoo kutokea na akachinjwa badala yake, hakuwa mtoto wa Ibrahimu tena bali alikuwa mtoto wa Mungu au mnadhiri wa Mungu jwasababu kitendo kile cha sadaka kilikuwa kinamuweka wakfu ISAKA kwa Mungu na maana ya wakfu ni kitu kilichotengwa kimaalum kabisa kwa ajili ya Mungu.
Sasa tafuta kujua mtaani kwako kuna idadi ya watoto wangapi alafu peleleza ujue ni wangapi wametengwa na wazazi wao kwa ajili ya kazi ya Mungu.
litaendelea...........................

MUNGU WANGU MWEMA AKUBARIKI SANA

Post a Comment

0 Comments