100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

THAMANI YAKO INATEGEMEANA NA ULICHOKIBEBA

 

THAMANI YAKO INATEGEMEANA NA ULICHOKIBEBA

LUKA 19:33-36

Walipokuwa wanamfungua yule mwana-punda, wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?”Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.”Wakamleta kwa Yesu, nao baada ya kutandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, wakampandisha Yesu juu yake. Alipokuwa akienda akiwa amempanda, watu wakatandaza nguo zao barabarani

Bwana Yesu Asifiwe Mwana wa Mungu,

kwanza kabisa, nimesikia watu wengi wanasema heshima ni kitu cha bure lakini sio kweli hata kidogo kwasababu hakuna heshima isiyokuwa na sababu.

Haiwezekani kabisa mtu akuheshimu pasipokuwa na sababu,lazima kiwepo kitu kilichotangulia kabla ya kuruhusu heshima kupata nafasi.

WHATSAPP GROUP 👇🏼
https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf

Watu wanaweza kukuheshimu pengine kwa ajili ya mamlaka uliyo nayo juu yao au kwa namna unavyojipambanua kwao au  katika jamii inayokuzunguka kwa kutoa mchango wako kwao iwe ni kifikra au kimsaada wa kibinadamu na ama kuwatetea au kuwawakilisha vyema katika nyanja mbalimbali na mengine mengi.

Lakini leo nataka tuone thamani ya punda wakati amembeba Yesu na kabla ya kumbeba Yesu.

punda ni punda tu lakini punda huyu aliyembeba YESU hakuwa kama punda wengine wakati huo amembeba Yesu,maana kikawaida katika msafara wa mtu kama Yesu mwenye umati mkubwa wa watu nyuma yake hisingekuwa rahisi punda hasiyekuwa na sababu akapata nafasi ya kuongozana na Yesu.

Biblia inasema watu walitandika nguo zao na Yesu akiwa amebebwa, na punda alikuwa akipita katika zile nguo, ingekuwa ni leo tungesema punda yuke alikuwa akitembea katika RED CARPET, na watu lazima walimpisha na walinzi lazima walisimama pembeni yake kuhakikisha punda yule anapata nafasi ya kutosha ya kupita ili hasije akazongwa na watu na kusababisha ajali kwa Yesu, 

Ni hivi ukienda benki kukopa pesa hawakupi tu hela kwasababu shida yako ni milioni kadhaa bali wanakupa pesa kwa kuthamanisha kiwango ulichoomba na hazina yako au dhamana yako,ndiyo maana unaweza kuomba milioni kumi lakini baada ya kupitia nyaraka zako afisa mikopo akakwambia kutokana na thamani ya dhamana yako benki itakuamini kwa kukukopesha shilingi milioni tano pekee.

kwa lugha nyepesi ni kwamba hawaangalii sana sababu ya kukopa pesa yao bali wanaangalia thamani ya ulichokibeba kama inaendana na kiwango cha pesa unachokitaka.

 Nataka nikwambie thamani ya yule punda ilikuwa tu ni wakati ule alipokuwa amembeba Yesu lakini Yesu alipoingia hekaluni punda yule wakati wa kurudi akiwa pekeake hasingepita kwenye red carpet wala hasingepata nafasi ya kupita katikati ya watu na wakamheshimu, 

Unaweza kujiuliza ni kwanini???

Ni kwasababu kilichokuwa kinampa heshima amekiacha nyuma, 

na hivyo ndivyo wana wa Mungu wengi wamekuwa, katika wakati ambao wakifikiri wako na yesu kumbe wako wenyewe alafu wanashangaa heshima ile waliyoitegemea kuipata hawaioni. Ama sehemu walizofikiri wangeweza kupenya kiwepesi kwasababu wanaye Yesu wanashangaa ni ngumu kuliko kawaida, ama wanashangaa mahali ambako milango ilitakiwa kufunguka kiwepesi kwasababu wanaye Yesu inakuwa migumu kufunguka.

Wakati wakijua wako na Yesu kumbe Yesu wamemuacha mjini na wamerudi wenyewe.


Rais anapata heshima anapokuwa amekalia kiti cha mamlaka hiyo au anapokuwa kwenye nafasi hiyo.

Pengine hujaelewa lakini watu wa zamani wanaelewa kwamba zamani wakati wa utawala wa kifalme kulikuweko mavazi maalum na taji maalum ambazo zilikuwa zikimtambulisha kwamba huyu ni mfalme na hasipozivaa hizo ilikuwa ikisemekana kwamba mfalme amevua enzi yake maana yake ameiacha nafasi yake na kwa lugha nyingine kile kinachompa heshima ya kutambulika kama mfalme amekiacha nyuma.


Yamkini umemuacha Yesu nyuma na hali ukifikiri huko naye lakini ni saa ya kumuita Yesu tena kwa maana pasipo yeye ni kama umeivua enzi yako kwa sababu heshima na kila chema chako kimefungamanishwa katika yeye.

Mungu wangu akubariki sana na zaidi sana roho mtakatifu akafanyike msaada kwako pindi unapojifunza na kutafakari Neno hili la Mungu.

kwa saa nyingine kama hii tutakuja na mwendelezo wa somo hili muhimu kadri roho atakavyotuongoza..............................

NAKUTAKIA BARAKA ZA BWANA 

Post a Comment

1 Comments