100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

UTAKATIFU UNAANZIA DUNIANI

 UTAKATIFU UNAANZIA DUNIANI



Zaburi 16:3
“Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.”


WHATSAPP GROUP 👇🏼
https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf

Haleluya tena wana wa Mungu, ni saa nyingine tena tunakutana kutafakari Neno la uzima kutoka katika kitabu cha zaburi,
Ni wimbo wa Daudi unaoonyesha uthabiti wa imani lakini pia na namna ambavyo mtu anaweza kupata usalama wa kutosha akiwa karibu na Mungu kwa kila aina ya mazingira yanayoweza kuwa yanamzuka au kumkabiri.

ukisoma kuanzia msitari wa 1 mpaka wa 11 utaweza kuelewa kiundani sana lakini pointi yangu ni hii kwamba,
Pamoja na Changamoto na majaribu na uovu ulioitapakaa dunia bado nataka nikuhakikishie mtu anaweza kuitwa na kuwa mtakatifu akiwa bado kwenye duniani hiyohiyo iliyotapakaa uchafu wa kila namna na wako watu wengi wanaoishi humo ambao ni watakatifu haswa,
 kwasababu biblia haijipingi.
Vinginevyo kusingelikuwa na sababu ya Yesu kuja ulimwenguni maana kinyume cha utakatifu ni dhambi kwahiyo ikiwa unaamini kwamba duniani hamna mtakatifu maana yake unauaminisha ulimwengu kuwa hakuna mtu atakayeingia mbinguni kwasababu mbinguni hakiingii kichafu wala kinyonge.
Nilimsikia mtu mmoja akisema "walokole wanajifanya watakatifu, huku akijihoji mwenyewe kuwa unawezaje kuwa mtakatifu wakati haujafa?? "

Kwa maneno hayo nikagundua mtu huyu katika matatu kuna moja linamsibu,
Kwanza pengine hana neno La Mungu la kutosha ndani yake,
Au pili haijui biblia vizuri juu ya kile inenacho,
Ama tatu ni mpinga Kristo na yuko tayari kubadili fikra za watu na kubadili muelekeo mwema wa imani za watu.lakini pia nikagundua ndio maana maandiko yanasema
“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;..............”Hosea 4:6

Kwa maneno hayo sina maana kwamba naidhinisha kuwa warokole ni watakatifu, la hasha!!! kwasababu Yesu aliwambia wanafunzi wake ya kwamba ndugu zake ni wale wanaolicha na kulitii neno la Mungu maana yake ni kwamba unaweza ukawa mrokole na mbinguni husiende lakini zaidi sana biblia iko wazi kabisa kwamba “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
” Mathayo 7:21

Kwahiyo dini yako haitaingia Mbinguni bali roho yako ndio inayotazamiwa, kwasababu wako watu wanaamini dini zao ndizo njia halisi ya wao kufika mbinguni.
Kasome biblia yako vizuri maandiko yanasema,
mwana-punda aliyekuwa amembeba Yesu hakuruhusiwa kuingia hekaluni kwa kigezo cha kumbeba Yesu bali aliishia mlangoni, kwahiyo dini yako haitaingia mbinguni, Ishukuru tu kwakuwa imekukutanisha na Mungu lakini husiitazamie kama njia ya wewe kwenda mbinguni maana biblia inaweka wazi kwa habari ya njia ya kweli ya kuelekea mbinguni “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
” Yohana 14:6

Unaweza ukasema labda hapo Yesu alikuwa akiwaambia wanafunzi wake lakini alikuwa akinena kwa habari ya ulimwengu sawasawa na... “Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
”Yohana 3:17

Kwahiyo haizungumzwi dini hapa bali anatajwa Yesu na ukombozi wake juu ya ulimwengu,
maana wako wakristo wanaamini Yesu ni wa kwao peke yao, lakini leo nataka nikwambie Yesu hakuleta dini duniani bali alileta ukombozi duniani.

Turudi kwenye somo letu,
Kwa kusema hivo sina maana kwamba ni rahisi sana kuyaishi maisha matakatifu bali huko msaada pekee wa kutuvusha hapo kama neno la Mungu lisemavyo katika wafilipi “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
” Wafilipi 4:13

Inamaanisha pasipo yeye huyo atutiaye nguvu hatuwezi kufanya jambo lolote.
Vijana wengi wanajua kwamba ziko tabia nyingi na mihemuko mingi ya kipindi cha ujana ambazo kwakweli kuziacha ni ngumu sana kiasi ambacho ukianza kumuhubiri kijana kwa habari ya utakatifu ataanza kuwaza habari za boyfriend au girlfriend wake ama starehe ambazo atazikosa kwa kufuata njia hiyo ya utakatifu na kwa wale walio na wapenzi wao manake wanatenda uasherati, huanza kukumbuka ahadi zao walizowekeana na wengine wakidanganyana kwa kuambizana kwamba hawawezi kuishi bila ya wenzao,Najua sio wewe unayesoma ujumbe huu lakini ukimsikia mtu anamuhaidi mwenzake maneno kama hayo msaidie kiroho kwasababu kilichofungwa ni ufahamu wake au fikra zake maana biblia inaniambia “Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu..................
” Matendo ya Mitume 17:28

Maana yake ni kwamba hata kama hauna girlfriend au boyfriend, ikiwa tu unaye Yesu ndani uwe na uhakika utaishi na kula mema ya nchi na kutembea katika utakatifu lakini zaidi sana huyo boyfriend wako au girlfriend wako atakuwa wa thamani sana mbele zako,mbele za jamii na mbele za Mungu kama ataitwa mme au mke katika Bwana kwako kuliko kuwa na utambulisho wa majina mengine ambayo hatahivo hayana ushuhuda mwema kwako na hayampi Mungu utukufu.

Ninayo mengi ya kusema kwa habari ya maisha ya vijana na si hilo tu linalovuruga utakatifu wa vijana bali yako mambo mengi sana ambayo roho mtakatifu akitupa kibali cha kunena tutayaainisha katika somo husika la maisha na utakatifu wa vijana lakini zaidi sana tukiwa kama vijana yatupasa kufahamu ushirika wetu katika kuujenga ufalme wa Mungu ni wa muhimu sana kuliko tunavyoweza kujitazama maana maandiko yananena kuwa 
“.................... Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
” 1 Yohana 2:14

Neno hilo tu linatosha kututia nguvu kama vijana kutembea katika utakatifu na kufanyika sababu ya watu wengine kuyaishi maisha ambayo kwao wanafikiri ni vigumu, sizungumzi na vijana peke yao bali nazungumza na kila mwenye mwili.
Nimalize kwa kusema
“Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;
” Wafilipi 1:27

MUNGU WANGU MWEMA AKUBARIKI SANA NA ZAIDI SANA ROHO MTAKATIFU AKAFANYIKE MWALIMU KWAKO KUHAKIKISHA UNAPATA KILE ALICHOKUSUDIA UPATE KATIKA NENO HILI.

Post a Comment

0 Comments