100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

MAOMBI YA YATIMA NA MJANE

MAOMBI YA YATIMA NA MJANE

Haleluya

DRAYWADRAY MINISTRY

Kutoka 22:22-24

Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.

Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,

na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu, 

Nikukaribishe tena  tukajifunze kwa pamoja Neno la Mungu.

 WHATSAPP GROUP 

https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf


Kama ambavyo tumesoma hapo juu katika kitabu cha KUTOKA tunaona na kushuhudia ni kwa kiwango gani Mungu wetu ni wa huruma na rehema kiasi gani juu yetu.

Lakini katika mistari hiyo hapo juu kuna kitu cha ajabu kidogo ambacho ningependa ukakione, Mungu anasema kwamba yatima na wajane wakimlilia hakika hasira yake itawaka, alafu anasema nitawaua ninyi kwa upanga 

Maana yake hasira yake imebeba mauti ndani yake, lakini swali la msingi la kujiuliza ni akina nani watakaopatwa na hiyo adhabu au hiyo mauti? Ni wazi kuwa ni wale wanaowaonea yatima na wajane. 

Ebu twende mbele kidogo uone kitu cha ajabu anasema, nitawaua ninyi kwa upanga na wake wenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa mayatima

(kupitia msitari huu mtu mmoja akaniuliza kwahiyo Mungu naye ni sababu ya yatima kuwepo duniani???) 

sasa unaweza ukapata shida kidogo hapa kuelewa kwamba, Mungu anawahurumia yatima na wajane kiasi ambacho yeye yuko tayari kuua watu watakaowaonea lakini hapo juu tumeona yeye mwenyewe anaweza kuwa chanzo cha yatima na wajane kuwepo duniani katika kutekeleza hiyo adhabu yake maana anasema wake wenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa mayatima, lakini kisikuumize akili hicho kwasababu Mungu hawezi kuwaua watu wake aliowaumba bali hicho kinachozungumzwa hapo ni matokeo ya dhambi ya mtu mwenyewe maana sote tunajua yakuwa dhambi imebeba mauti na unaweza kuwa yatima wa kimwili kwa kukosa wazazi wa kimwili lakini pia unaweza kuwa yatima wa kiroho kwa kukosa walezi wa kiroho, maana yake wazazi wako unao kimwili lakini katika ulimwengu wa roho  hawako na wewe tena. 

UNASIKIA NILICHOKISEMA???

KWAHIYO kimwili kuna aina mbili za wajane na mayatima huku duniani, 

 kwanza wale waliotokana na mapenzi ya Mungu. 

pili wale waliotokana na makosa ya wazazi au vizazi vilivyotangulia kabla yao na Mungu akaachilia hiyo adhabu juu ya vivazi vinne kutokea kwa wahusika, kama maandiko yasemavyo. 


Yamkini ziko aina nyingine lakini leo nataka tutazame hizi mbili tu na namna ambavyo watu hawa wanaweza kupata msaada wa Mungu. 


SASA SIKIA aina hizi mbili zote ni ukweli kwamba wako huku duniani pengine ni mimi au wewe au huyo jirani yako lakini nani ajuaye yakwamba sababu ya yeye kuwa yatima au mjane imetokana na sababu ya kwanza au ya pili???? 


Asante Yesu kwasababu Roho mtakatifu ananishuhudia kuwa kuna aina ya watu maneno haya ni mapya kabisa kwao lakini asante Yesu pia kwasababu saa ya ukombozi imewadia ndio maana Neno hili limeachiliwa kwetu.

Pengine hujanielewa sawasawa pale ninaposema kuwa unaweza kutumikia adhabu hisiyokuwa ya kwako mpaka mtoto wako anaweza kutumikia adhabu ya kosa ambalo hukulitenda wewe

Ebu tazama maandiko hapa chini 

Kutoka 20:5-6

Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.


Nafikiri unaweza kuona ni namna gani ambavyo unaweza kubeba mzigo husiokuwa wakwako lakini pia ni namna ambavyo unaweza kuwa sababu ya vizazi vingine kuumia kutokana na dhambi au makosa yako. 

POINTI yangu sio hiyo, ninachotaka tutazame ni hiki hapa >> hakika yangu nitasikia kilio chao ndivyo biblia inavyosema lakini swali je watakaosikiwa ni kundi lipi? Ni wale waliokuwa mayatima na wajane kwa mapenzi ya Mungu akiwa na nia njema na kwa sababu zake ambazo kibinadamu hazituhusu sana mpaka yeye mwenyewe atake kusema au pengine safari yao ilikuwa imewadia na kazi yao ikakamilika na hivyo wakalala kwa amani au ni wale walioitwa mayatima na wajane kwa adhabu na ghadhabu ya Mungu iliyotokana na makosa ya wazazi wao? 

Na je watu hawa wakienda mbele za Mungu kuomba msaada kama mayatima na wajane wataenda kwa sitahili moja? 

Hallelujah !!! Hallelujah!!! 

Katika sehemu hii nianze kwa kutoa ushuhuda wangu wa nyuma kidogo, 

Miaka 13 iliyopita niliwahi kutamka maneno haya👇🏿

 “Nalitoka tumboni kwa sababu gani, kuona taabu na huzuni, hata siku zangu ziharibike katika aibu?

" YEREMIA 20:18

Ni katika kipindi kigumu sana ambacho kwangu ulikuwa kama msiba kiasi ambacho naweza kuilaani siku yangu ya kuzaliwa na kujuta kuwepo duniani, nilimsikia Yesu lakini sikuwa nimempokea bado hata hivo Neema na Rehema za Mungu  ni kuu mno ambazo zinaweza kumfata mtu popote na saa yoyote, mpaka majalalani, mpaka kwenye matope, mpaka kwenye msitu wa wanyama wakali. 

Asante Yesu kwasababu alinijilia katika saa ambayo nalikuwa mtu wa huzuni na mpweke mno lakini yeye aliye baba wa mayatima na mme wa wajane akafanyika baba kwangu na msaada kwangu. 

Nimekueleza maneno haya makusudi kabisa ili uelewe nini namaanisha, Nilipata tabu na nikakwama kwasababu sikufahamu mimi ni yatima wa aina gani. 

Kuna aina ya makosa yanaweza kufutwa kwa DAMU YA YESU na kuna Aina ya makosa yanafutwa kwa DAMU YA MWANA KONDOO. Isikupe shida kuwaza utofauti wa Yesu na Mwanakondoo, hiki ni kitu kimoja lakini vinatumika kutegemeana mazingira na wapi umekanyaga. Hilo ni somo jingine tena. 


Nirudi kwenye somo lakini saa nilipogundua mimi ni yatima wa aina gani nilienda mbele za Bwana na kwa msaada wa roho mtakatifu nikaikaribia madhabahu ya Bwana kwa machozi kama yatima ambaye ameonewa vya kutosha na sasa anahitaji msaada wa Baba.Mungu mwema na Mungu mkuu akaona machozi ya yatima na kuyafuta, itoshe tu kusema asante Yesu kwa hivi nilivyo leo. 

Yamkini umelia mara nyingi na Mungu hajajibu na wewe ndani yako unayo mistari ya kutosha kabisa ya kukuthibitishia ya kwamba Mungu wako ni mwenye huruma na ni Mungu  anayejibu mahitaji ya watu wake na ahadi nyingine nyingi unazo ambazo amekuhaidia, lakini huzioni zikitokea kwenye maisha yako, yawezekana huzioni kwasababu kuna kizingiti au kizuizi mbele yako kwasababu kila mahali Mungu yupo lakini si kila mahali Mungu anaweza kusema au kujifunua,


 kwahiyo yamkini umekwama kwasababu ya makosa ya waliokutangulia 

Lakini leo nenda mbele za Mungu kwa toba kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya vizazi vilivyotangulia kabla yako, haijalishi ni miaka mingapi makosa hayo yaliwahi kufanyika lakini uelewe tu kwamba, yesu alikuwepo kabla ya hayo makosa kufanyika 👇🏿

1 Petro 1:19-20

bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.

 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;


KWAHIYO lazima uende kwa damu ya Mwana kondoo kama ishara ya sadaka ya kulipa fidia ya hatia iliyokuwepo juu yako kwa ajili ya makosa ya waliotangulia kabla yako. 


Nenda kwa unyenyevu mkubwa mno kwa Bwana maana yeye mwenyewe aliingoja nafasi hii kwa muda mrefu sana akitaka utubu na kurejea katika nafasi yako sawa na mapenzi yake ,

 KUMBUKA Mungu anao uwezo wa kukuondolea hiyo hatia hata kama hujaomba lakini biblia iko wazi yakwamba yeye mwenyewe hajipingi analitazama Neno lake apate kulitimiza ndio maana halisi haswa ya kusema 👇🏿

HOSEA 4:6

“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa......................... kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.


Kwahiyo kutokufahamu Neno la Mungu hakumfanyi Mungu akuonee huruma bali tafuta kujua mapenzi ya Mungu ni nini juu yako kwasababu kila mmoja amewekewa uwezo ndani yetu wa kusikia na kupokea, awe ni kipofu anaweza kusema na Mungu na hata kiziwi anaweza kusikika mbele za Mungu. 


Itangulize SADAKA ya damu ya mwanakondoo kama MWALIKO wa kukutana na Mungu na hakika utaona huruma za Mungu zikishuka kwako kama mvua na huo utakuwa ni mwanzo mpya na majira mapya ya kuanza kutembea ndani ya baraka za Mungu na hautakuwa yatima tena bali utakuwa Mwana Mbele za Mungu Baba Na kila mtu atajua unaye Baba,


tutakuja na mwendelezo wa somo hili kadri roho mtakatifu atakavyotujaria.........................


MUNGU WANGU AKUBARIKI SANA

Post a Comment

0 Comments