100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

MAZINGIRA UNAYOYAPITIA YASIONDOE TUMAINI LAKO KWA MUNGU

 


MAZINGIRA UNAYOYAPITIA YASIONDOE TUMAINI LAKO KWA MUNGU

Mhubiri 3:1-8

Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.

Haleluya tena mwana wa Mungu,ni saa nyingine tena iliyokubalika  tunakutana mezani pa Bwana kupata chakula cha kiroho kama ilivyo kawaida ya mwili ili uendelee kuishi lazima upate chakula cha kila siku,vivyo hivyo kwa watakatifu wa Mungu ili tuzidi kukua na kusitawi  kiroho lazima tupate chakula cha rohoni kila kuitwapo leo,ndivyo biblia inavyosema “Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” Mathayo 4:4

Somo letu leo nimelipa kichwa cha somo MAZINGIRA UNAYOYAPITIA YASIONDOE TUMAINI LAKO KWA MUNGU,

Pamoja na changamoto zote unazoweza kuwa unapitia na saa nyingine hakuna hata mmoja anayekutia moyo wala kusimama upande wako wala kukuonyesha njia lakini leo niko hapa kukutia moyo kupitia neno la Bwana yakwamba saa ya kicheko chako yaja haijalishi utadumu katika hali hiyo kwa wakati gani kwasababu biblia inasema “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.”  Wagalatia 6:9 , maadamu hujamuacha Bwana uwe na uhakika ahadi zake zitatimia juu yako  hata kama unafunga na kuomba alafu huoni majibu yakitokea lakini husijaribu kufanya jambo lolote la kujitenga na Mungu wako maana sio kwamba Mungu hasikii au haoni wakati unaoupitia bali kinachongojewa ni saa ya Bwana,

Mungu alimwambia HABAKUKI “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.” — Habakuki 2:3, Inawezekana nabii Habakuki alichoshwa na   hali iliyokuwa imeuzunguka mji na pengine aliomba muda mrefu kama wewe, na pengine alifunga kama wewe,na pengine alingoja mabadiliko kwa muda mrefu kama wewe,ndiyo maana katika sura ile ya 1 anasema  “Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa.” — Habakuki 1:2, anaposema “hata lini“  inamaanisha alilia vya kutosha kama ni kulia na kama ni kuomba aliomba vya kutosha mpaka akafikia mahali pa kulalamika na kulia  tena inafika saa habakuki anaisi ni kama Mungu hamsikii lakini cheki kitu Mungu anasema katika sura ya 2 ya kuwa “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa” inamaanisha pamoja na kuumia kwake habakuki pamoja na kuona hali mbaya ya uovu ikishamiri mbele yake lakini alitakiwa kufanya jambo moja tu nalo ni KUNGOJA WAKATI WA ULIOAMRIWA NA MUNGU.

Biblia inasema Kwa kila jambo kuna majira yake maana yake ni kwamba haijalishi una uhitaji na hicho kitu kwa kiwango gani lakini husijaribu kumlazimisha kuku kutotoa kifarana kabla ya siku 21 maana hata hivyo hakitakua,kitatokea lakini baada ya Muda kitakufa tu maana muda wa kutokeza kwake ulikuwa bado,

Haijalishi una hamu ya kukumbatia mtoto kwa kiasi gani lakini kama ujauzito haujafikisha miezi 9 husijaribu kufanya opereshen na kujifungua kabla ya muda uliopangwa vinginevyo utaua hicho kiumbe kilichoko tumboni.

Dada mmoja akaniambia,anataka kuachana na mmewe kwasababu amedumu naye kwa muda wa miaka 9 na bado hana mtoto nikamwambia na kumshauri namna nilivyoweza lakini akashupaza shingo yake kwa maana alikuwa tayari kashakata shauri,mwaka mmoja baadae akaingia katika mahusiano Na kijana mwingine baada ya muda wakapata mtoto lakini miaka miwili tena mbele mtoto huyo akafariki hali ikawa hivyo mpaka kwa mtoto wa tatu,ujauzito unaingia,mimba inakua,mtoto anazaliwa lakini baada ya muda anafariki. Hivyo ndivyo watu wengi wanapoomba muda mrefu na wakakosa majibu huwa wanaamua kutafuta shortcut pasipokuangalia madhara wanayoweza kukutana nayo maana ukishafika mahali pa namna hiyo hicho utakachokipata huko nje na mapenzi ya Mungu maana yake hakina ulinzi wa Mungu na hivyo kudumu kwake kunaweza kukawa kwa shida mpaka umejua namna tena ya kwenda mbele za Mungu kuomba toba na msaada wa kuvuka hapo,kamuulize Ibrahimu na Sarah nini kilitokea walipokubaliana Ibrahimu kulala na Hajiri ili wapate mtoto baada ya kukaa Muda mrefu bila mtoto,ile kwamba wana kiu na mtoto na akaamua kutafuta shortcut kwa Hajiri haikubadili mpango wa Mungu wa kumpitisha Isaka katika tumbo la sarah.

Dumu ukienda mbele za BWANA,husichoke kuomba kwa ajili ya hapo unapopapitia maana wakati wengine wanakucheka na kukukebei kwa habari ya kutokuzaa kwako,nataka nikwambie samweli atapata nafasi katika tumbo lako la uzazi lakini hawezi kuruhusiwa kutoka mpaka saa ya kutoka kwake imetimia, “Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana.” — 1 Samweli 1:20

Kicheko,furaha na huzuni ni sehemu ya ukamilifu wa maisha  lakini zaidi sana kila jambo linalotokea kwenye maisha yako ya kila siku lina sababu, husilichukulie kama huzuni maana kila kitu kinatokea kwa makusudi na kimebeba muujiza mkubwa nyuma yake ndivyo maandiko yanavyosema ” Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”

·       ==>  Nani angejua kama katika tumbo la HANA yuko mtumishi mkubwa wa BWANA samweli?

·        ==> Nani angejua kama katika tumbo la sarah  yuko isaka?

Litaendelea

 

 

 

Post a Comment

0 Comments