100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

BAADHI YA VITU VITAKAVYOKUPA WEPESI WA KUJIBIWA MAOMBI YAKO

BAADHI YA VITU  VITAKAVYOKUPA WEPESI WA KUJIBIWA MAOMBI YAKO 

Mwl:Jovin John

 KANAANI MPYA MINISTRY 

 Telegram Group

 Facebook Page

WhatsApp Group

You Tube Channel


 Bwana Yesu Asifiwe 

Ndugu katika Kristo ni vema kutambua kuwa katika maisha ya mwanadamu kuna nguvu mbili yaani (Giza na nuru), hivyo sisi kama watu tunaoamini katika Kristo Yesu hatuna msaada mwingine Zaidi ya maombi yetu sisi wenyewe kwa Mungu Baba sawa na, 

 Wafilipi 4:6

“Msijisumbue kwa neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu”

Zaidi pia biblia inasema, 

 Mathayo 7:7-8“Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa, kwa maana kila aombaye hupokea, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa. 

Lakini je tunaomba maombi ya aina gani?

Yenye vigezo gani?

Njia gani tunatumia kuomba? n.k

Ndiyo maswali ya msingi ya kujiuliza katika kuomba na kupata majibu ya mahitaji yetu.

Hivyo basi zifuatazo ni baadhi ya siri au vitu vinavyoweza kusababisha maombi yako yajibiwe mapema,nasema ni baadhi kwasababu nina uhakika roho mtakatifu aliye mwalimu wetu sote aweza kukufunulia zaidi ya hizi nitakazozitaja hapa kupitia somo hili :-


 1. KUKAA MBALI NA DHAMBI(Utakatifu)

 1 Petro 1:15-16 

 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 

Mungu wetu ni mtakatifu, hivyo basi ili tupate kibali cha maombi yetu kujibiwa haraka yatubidi tuwe watakatifu kama yeye. 

Maandiko yanasema Watakatifu ndio Mungu wetu huwasikia haraka na kujibu haja za mioyo yao maana tayari wanao upatanisho wa utakatifu utujiao kwa kuyaishi mapenzi ya Mungu Baba.

 Yonana 9:31“Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi, bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo” 

Kwahiyo twaona ya kuwa Mungu huwasikia watakatifu, ili tuweze kujibiwa maombi yetu kwa haraka tutunze utakatifu tuliokabidhiwa ambao tukiuharibu ni gharama kuurejesha na tayari uso Mungu utakuwa mbali na sisi maana tutakuwa tumeondoa ushirika wetu na Mungu.


 2.KUOMBA PASIPO MASHAKA YA KUPOKEA 

 Yakobo 1:6-8 

 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote. 

Linapofika swala la kuomba mbele za Bwana mashaka huwa ni kikwazo kikubwa katika maombi ya waamini wengi na kwaweli wengi hawapokei si kwamba Mungu hasikii bali mashaka mioyoni mwao huwaondolea sifa ya wao kupokea kile wanataka kwa Bwana, 

Biblia inasema, 

 Yakobo 4:8 

 “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.” 

  Ukiwa nanmashaka moyoni mwako unatengeneza kitu kinaitwa NIA MBILI kwasababu maana ya mtu mwenye (nia mbili) ni mtu hasiye na msimamo na kukosa msimamo ni chanzo cha mashaka ndani yako. Kwahiyo Mungu hawezi kufanya ushirika na mtu hasiye na msimamo ikiwa yeye mwenyewe ni mtakatifu anahitaji na sisi tuwe watakatifu kama alivyo yeye. 

Na huwezi kupokea kwasababu kwa maana ya msitari huo hapo juu unadhihirisha kuwa na nia mbili ndani yako ni dhambi ndio maana linatumika neno

 itakaseni mikono yenu 

Sasa huwezi kutakasa mahali ambapo hapakuwa na doa na ikiwa hivyo ndivyo basi uelewe tu kwamba mashaka ndani yako au nia mbili ndani yako ni mlango wa dhambi na kwa sababu hiyo ukikaa katika njia hiyo huwezi kupokea kwasababu Mungu hajawahi kufanya agano na wenye dhambi kwasababu ili haki ipate nafasi inadai kwanza toba ndio maana maandiko yanasema, 

 “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;” Matendo ya Mitume 3:19 

 ndani ya nyakati za kuburudisha ndimo penye haki yako kutoka kwa Mungu lakini kabla hizo nyakati hazijaja kwako lazima toba kwanza ipate nafasi. 


 NB; 

pamoja na mambo yote hayo lazima imani izungumze ndani yako na

Kuwa na moyo wa kuchangamka maana saa nyingine unaweza ukashindwa kupokea kwa kwenda mbele za Mungu huku umebeba mizigo ya hukumu wasiwasi na mashaka ndani yako na hivyo kukuondolea ujasiri ndani yako na kuruhusu wasiwasi kuingia ndani yako, inaweza kuwa kwasababu ya kiwango cha imani ulicho nacho ama ikawa kiwango cha uzito wa tatizo lako au mazingira yanayokuzunguka nk lakini biblia inasema, 

 Yakobo 5:13“ Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? na aimbe zaburi” 

Ukiisi hali ya namna hiyo omba na muimbie Bwana zaburi ili kuruhusu amani ya kristo itawale ndani yako na hivyo unapoenda mbele za Bwana unaenda ukiwa na ujasiri na nguvu ya kuwasilisha hoja zako. 


 3.KUWA NA IMANI KAMILIFU. 

 Waebrania 11:1

“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” 

Biblia ya kiingereza inasema, 

 “Now faith is the substance of things hoped for, the evidence of things not seen.”  Hebrews 11:1   

Kwahiyo imani ni KIINI cha uhakika wa kupokea mambo uyaombayo pia imani ni USHAHIDI wa kuthibitisha kwamba yale uyaombayo yapo japokuwa hayaonekani kwa wakati huo katika ulimwengu wa mwili. 

Sasa ikiwa ni kiini na ushahidi na sote tunajua kwamba ukiwa na kesi mahakamani kitu pekee kinachoweza kumpa mtu haki yake na kitu pekee kinachoweza kumtia mtu hatiani ni ushahidi wa kuthibitisha hicho unachokizungumza ndio maana sio kila aliyefungwa gerezani ana hatia, wengine wamekoswa ushahidi wa kuithibitishia mahakama kwamba wao hawana hatia,. 

Kwahiyo ikiwa imani ni USHAHIDI maana yake hii ni neema kubwa sana ambayo kila mwamini amepewa kwasababu tunaipata bure gharama yake ni wewe mwenyewe kujiposition kwenye nafasi ambayo imani hiyo itakuwa na nguvu ya kuleta matokeo chanya kwahiyo tunaenda mahakamani tukiwa na uhakika wa kushinda kwasababu tuna ushahidi wa kupewa haki yetu. 


Ili kupokea haja za mioyo yetu kutoka kwa Mungu kwa haraka yatubidi kuwa na imani ya kwamba yote tuyaombayo yatakuwa ya kwetu. 

Tujifunze kupitia mfano huu:- 

Marko 11:12-14“Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake, na alipoufikilia hakuona kitu ila majani, maana si wakati wa tini. Akajibu, akauambia tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako.Wanafunzi wake wakasikia”

Neno likawa:-

Marko 11:12-14“Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake akamwambia, Rabi, tazama mtini ulioulaani umenyauka. Yesu akajibu akamwambia, Mwaminini Mungu. Amini nawaambia yeyote atakayeuambia mlima huu, ng’oka ukatupwe baharini wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwasababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” 


 4. KUJUA MAPENZI YA MUNGU

 (Kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu)

Ili kupata majibu ya mahitaji yetu ni vema kuelewa nini hasa kusudi la Mungu kwetu, ili tuweze kuomba  sawa na kusudi lake kinyume na hivyo yamkini mtu asipate anachokiomba maana kama kipo nje ya kusudi la Mungu hawezi kumpatia majibu ya jambo hilo.

 Yakobo 4:3“Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.


 5.IMANI (Kuamini kuwa Mungu yupo) 

Pasipo kuamini ya kwamba Mungu yupo na anasikia kila tuombalo hatuwezi kupata haja za mioyo yetu.Yafaa sasa tujenge Imani kuwa yeye tumuombaye yupo na asikia kila ombi letu. Tukiwa na mashaka ilihali tunaenda kuomba sisi wenyewe twathibitisha dhahiri ya kuwa hatupaswi kupokea tuombalo maana hatuamini kwamba atakayetujibu (Mungu) yupo. 

Tujenge Imani kuwa Mungu yupo naye ajishughulisha na haja za mioyo yetu sawa na, 

 Waebrania 11:6“Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza, kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao” 



 6.KUWA NA MAJIBU YA MAOMBI YAKO PALE UNAPOENDA KUOMBA. 

Ili kupokea majibu ya maombi yetu yafaa kujenga Imani na kuona utendaji wa jambo tunaloombea katika ulimwengu wa roho na hatimaye katika ulimwengu wa mwili. Jambo hili humfanya Mungu kuona tumaini letu  pekee kuwa lipo kwake na kujibu kwa haraka haja za mioyo yetu.

Ni muhimu pia Tujifunze kupitia mfano huu wa Bwana wetu Yesu Kristo:

 Yohana 11: 6-16Mfano Yohana 11 :15“Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini, lakini na twendeni kwake” 

Baada ya Bwana Yesu kupata taarifa ya kuwa Lazaro amekufa anasema anafurahi ili kwamba ufufuo wake ufanyike kuwa ushuhuda kwa watu wote kwa maana alijua ya kuwa kwa maombi yake Lazaro atafufuka, hivyo tayari alikuwa na jibu la ombi lake.

 Yohana 11:40-44 Mfano Yohana 11:42“Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote, lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaoudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma” 

Bwana Yesu alikuwa na uhakika ya kwamba akimwomba Mungu Baba atasikia naye atajibu kwa kumfufua Lazaro kwaiyo moja kwa moja alikuwa na jibu moyoni mwake   ya kuwa Lazaro atafufuka akiomba. 

Hivyo basi hatuna budi kuiga mfano huu wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa kuwa na majibu mioyoni mwetu tunapoenda kuomba ili kujenga Imani thabiti kwa Mungu ya kwamba atusikia naye ajibu kwa wakati.


 Mungu akubariki sana karibu tena katika kipindi kijacho. 


 UBARIKIWE SANA

Post a Comment

2 Comments

  1. Mungu awabariki sana, mzidi kutenda yake yote yanayompendeza MUNGU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amina mwana wa Mungu barikiwa pia kuwa sehemu ya familia ya kanaani mpya ministry, nasi tunabarikiwa na uwepo wako, Mungu akubariki sana.

      Delete