SOMO; UPONYAJI WA NDOA YAKO
Waebrania 13:4
“Ndoa Na Iheshimiwe Na Watu Wote Na Malazi Yawe Safi,Kwa Maana Waasherati Na Wazinzi Mungu Atawahukumia Adhabu”
Wapo Wanandoa Wengi Sana Hapa Duniani Ambao Wanaishi Katika Migogoro Ambayo Sio Tu Imeondoa Amani Na Upendo Wa Awali bali Imeharibu Hata Kizazi Chao Na Sio Tu Kizazi Chao Bali Imeenda Mbali Na Kuharibu Mpaka Kusudi La Mungu Katika Ndoa Hiyo.
Kwanza Ieleweke Kuwa Ndoa Ni Agano Kati Ya Mungu Mwenyezi Na Hao Wanandoa,Hii Utaipata Katika Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu Akasema, Si Vema Huyo Mtu Awe Peke Yake, Nitamfanyia Msaidizi Wa Kufanana Naye”
Biblia Inaposema Msaidizi Katika Msitari Huu Haina Maana Ya Msaidizi Wa Kupika,Wala Kufua,Wala Kulima,Wala Kuosha Vyombo Bali Inazungumza Msaidizi Kwa Habari Ya Kusudi La Mungu Ambalo Mungu Ameweka Ndani Ya Adamu.
Mwanzo 2:15 “ Bwana Mungu Akamtwaa Huyo Mtu,Akamweka Katika Bustani Ya Edeni,Ailime Na Kuitunza.”
Kwahiyo Kutokana Na Mwanzo 2:18 Ambayo Inamleta Msaidizi Maana Yake Hawa,Akiwa Kama Msaidizi Aliletwa Kwa Kusudi La Kusaidiana Na Adamu Kuilima Na Kuitunza Bustani Ya Edeni Ambayo Alikabidhiwa Adamu.
Watu Wengi Leo Wanapoenda Mbele Za Mungu Kuomba Mke Au Mme Hawaombi Kiagano,Kwahiyo Kinachotokea Utakutana Na Mtu Ambaye Kwakweli Hajabeba Chochote Cha Kusaidia Kusudi La Mungu Ndani Yako,Na Baada Ya Hapo Kinachotokea Ni Kutimiza Mapenzi Binafsi yako Na Sio Mapenzi Ya Mungu,Ndio Maana Wako Watu Kabla Ya Ndoa Huwa Na Moto Mkubwa Sana Katika Huduma Na Mungu Huwatumia Kwa Viwango Vya Juu Sana Lakini Wanapoingia Katika Ndoa Muda Mfupi Baadae Huduma Hiyo Huanza Kupoa Na Wengine Huduma Hiyo Hufa Kabisa Na Ukijaribu Kuwauliza Kwa Habari Ya Huduma Yao Kupoa Au Kutokuhudumu Hujaribu Kujitetea Kwa Kusingizia Majukumu Ya Ndoa Lakini Sio Kweli Na Wengi Wa Hao Pia Wanaotoa Majibu Ya Namna Hiyo Hawajui Kama Si Kweli Wanachokizungumza, Vinginevyo Mungu Hasingelikupa Hiyo Ndoa Ikiwa Anajua Akikupa Mke Au Mme Kusudi Lake Ndani Yako Litakufa.
Ieleweke Tu Kwamba Sababu Kuu Ya Mungu Kukupa Hiyo Ndoa Ni Kwa Ajili Ya Kusudi Lake Kutokana Na Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu Akasema, Si Vema Huyo Mtu Awe Peke Yake, Nitamfanyia Msaidizi Wa Kufanana Naye” Hayo Mengine Ya Kuzaa Nk Ni B Ya Mungu Lakini A Ya Mungu Ni Kusitawi Kwa Kusudi Lake Ndani Yako Na Siku Zote Unapokuwa Kwenye Ndoa Kumbuka Hilo Husisahau Kwasababu Hapo Ndipo Shetani Anapatumia Kwa Ajili Ya Kuvuruga Kusudi La Mungu Kwa Wanandoa Na Badae Kujikuta Wanafanya Mapenzi Yao Badala Ya Mapenzi Ya Mungu.Kwasababu Wako Watu Pia Wakikosa Watoto Katika Kipindi Fulani Katika Ndoa Zao Migogoro Huanza Na Wengine Huachana Kabisa,Hili Ni Kosa Kubwa Sana Mbele Za Mungu Kwasababu Mnapoachana Hamvunji Ndoa Bali Mnasimamisha Agano,Kwahiyo Kama Mnasimamisha Agano Ni Sawa Mnamwambia Mungu Kwamba, “Aiseee Hili Agano Halifai Kabisa” Na Bahati Mbaya Sana Nyie Wahusika Ndio Mnaovunja Katika Ulimwengu Wa Mwili Lakini Katika Ulimwengu Wa roho Agano Linaendelea Kuwepo Isipokuwa Halitumiki Tu.
Ndio Maana Biblia Inasema Luka 16:18 “Kila Amwachaye Mkewe Na Kuoa Mwingine Azini,Naye Amwoaye Yeye Aliyeachwa Na Mumewe Azini”
Sasa Sikia Sote Tunajua Kuwa,Mzinzi Ni Yule Anayetembea Nje Ya Ndoa Yake,Kwa Maana Hiyo Sasa Katika Msitari Huu Biblia Inaposema Azini Maana Yake “Fulani Ametoka Nje Ya Ndoa”Ndoa Ileeee Ambayo Ninyi Mnasema Mliachana,
Utauliza Ni Kwanini Lakini Ni Kwasababu Huwezi Kubeba Maagano Mawili Yanayofanana Kwa Wakati Mmoja Na Kwa Maana Hiyo Ya Uzinifu Inamaanisha Kwenye Ulimwengu Wa roho Wanapotazama Wanaliona Lile Agano La Ndoa Yako Ya Kwanza.Unaweza Ukajitetea Unavyoweza Kutokana Na Sababu Zilizowapelekea Mpaka Mkaachana Tena Wakati Mwingine Ukaweka Na Maandiko Juu Ya Huo Utetezi Kama Mathayo 5:31 Inayosema ‘Imenenwa Pia Mtu Akimwacha Mkewe Na Ampe Hati Ya Talaka” Lakini Mathayo Hiyohiyo Inakwambia Tena Katika Mathayo 5:32 Lakini Mimi Nawaambia Ninyi Kila Mtu Amwachaye Mkewe Isipokuwa Kwa Habari Ya Uasherati,Amfanya Kuwa Mzinzi Na Mtu Akimwoa Yule Aliyeachwa Azini”
Swali La Kujiuliza Ni Kuwa,Ikiwa Mtu Ameachwa Pengine Pasipo Kosa Lolote Na Akaamua Kuwa Katika Mahusiano Mengine Ya Kindoa Je Mtu Huyu Kosa Lake Liko Wapi Mpaka Ahesabiwe Dhambi Ya Uzinifu???
Jibu La Swali Hili Ni Kwamba Husije Ukafikiri Ni Rahisi Kuachana Kinamna Hiyo Kwa Sababu Gharama Ya Kuachana Inaweza Kuwa Kubwa Kuliko Ya Matengenezo Kwasababu Kutokana Na Mathayo 5:31 Inayompa Uhuru Mtu Kumpa Talaka Mkewe Kwa Habari Ya Uasherati, Lakini Gharama Ya Kuishi Katika Msitari Huu Ni Kubwa Mno Kuliko Unavyoweza Kufikiri,Kwasababu Unapotoa Talaka Maana Yake Unamwambia Mungu Kuwa,”Kuanzia Leo Sitaoa Tena Mpaka Huyo Niliyempa Talaka Atakapokufa,Sasa Bahati Mbaya Pia Huna Uhakika Mtu Huyo Pia Ataishi Kwa Muda Gani Maana Yake Akiishi Mpaka Uzee Wake Na Wewe Hauwezi Kuoa Tena Mpaka Uzee Wako Inategemeana Mmeachana Katika Umri Gani Na Hii Utaipata 1wakorintho 7:10-11 Inayosema “Lakini Waliokwisha Kuoana Nawaagiza,Wala Hapo Si Mimi Ila Bwana,Mke Asiachane Na Mumewe,Lakini Ikiwa Ameachana Naye Na Akae Asiolewe Au Apatane Na Mumewe, Tena Mume Asimwache Mkewe”
Kwa Maneno Hayo Unaweza Kuona Ni Gharama Kiasi Gani Utakutana Nayo Baada Ya Kupeana Talaka,Hata Hivyo Biblia Kutokana Na 1wakorintho 7:11 Inamtaka Kila Aliyeachana Na Mwanandoa Mwenzie Kupatana Na Kurudiana Lakini Pia Unapoachana Na Mwenzi Wako Maana Yake Katika Ulimwengu Wa Roho Umepoteza Msaidizi Wa Kusudi La Mungu Ndani Yako.
Na Mimi Nimewasikia Watu Wengi Sana Wakiwashutumu Wake Zao wakisema, “Hata Kama Tukiachana Hana Msaada Wowote Kwangu” , Lakini Sio Kweli Kwamba Mkeo Hana Msaada Wowote Kwako,Huko Ni Kulishusha Thamani Agano La Mungu,Vinginevyo Pasingelikuwepo Na Sababu Ya Hawa Kuletwa Kwa Adamu Kama Hasingelikuwa Na Umuhimu Au Kitu Alichokibeba Kwa Ajili Ya Kusudi La Mungu Ndani Ya Adamu, Mwanzo 2:18.
Katika Swala La Kuoa Au Kuolewa Na Mtu Mwingine Unaweza Kuwa Salama Tu Pale Ambapo Mmojawapo Kati Yenu Amefariki.Hii Ni Kutokana Na Warumi 7:1-3 Ndugu Zangu Hamjui (Maana Nasema Na Hao Waijuao Sheria) Ya Kuwa Torati Humtawala Mtu Anapokuwa Yu Hai,Kwa Maana Mwanamke Aliye Na Mume Amefungwa Na Sheria Kwa Yule Mume Wakati Anapokuwa Yu Hai,Bali Akifa Yule Mume,Amefunguliwa Ile Sheria Ya Mume.
Basi Wakati Awapo Hai Mumewe Kama Akiwa Na Mume Mwingine Huitwa Mzinzi,Ila Mumewe Akifa Amekuwa Huru,Hafungwi Na Sheria Hiyo Hata Yeye Si Mzinzi Ajapoolewa Na Mume Mwingine.
Swali La Kujiuliza Hapa Ni Kuwa Kwanini Ni Mauti Tu Ndio Inayompa Mtu Nafasi Ya Kuoa Au Kuolewa Na Mtu Mwingine???
1.Ni Kwasababu Kwanza Kama Tulivyosoma Mwanzoni Kwamba Ndoa Ni Agano,Hivyo Ikitokea Mmoja Amekufa Maana Yake Hilo Agano Linakuwa Na Pengo Mahali Kwasababu Huyo Mmoja Aliyebaki Atakapohitaji Msaada Wa Kiagano Hatoupata Kwasababu Yule Ambaye Angesimama Pamoja Na Yeye Hayupo Ndio Maana Mungu Anatoa Nafasi Nyingine Ya Kuziba Hilo Pengo Ili Agano Lake Liendelee Kuwa Imara,Na Mungu Atakuletea Mtu Ambaye Ndani Yake Amebeba Kitu Kilekile Ambacho Yule Aliyeondoka Alikuwa Nacho, 1timotheo 5:14 basi napenda wajane,ambao si wazee,waolewe,wazae watoto,wawe na madaraka ya nyumbani,ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu.
2.Sababu Nyingine Ya Pili Ni Kutokana Na Warumi 7:1 Ndugu Zangu Hamjui (Maana Nasema Na Hao Waijuao Sheria) Ya Kuwa Torati Humtawala Mtu Anapokuwa Yu Hai
Kwa Tafisri Hiyo Ni Wazi Kwamba Mtu Ambaye Ni Mbeba Agano Anweza Kufa Lakini Agano Lenyewe Halifi.
Ndio Maana Musa Alipokufa Aliinuliwa Yoshua Kuchukua Nafasi Yake,Vinginevyo Kama Mtu Angekuwa Anakufa Na Agano Alilolibeba Uwe Na Uhakika Wana Wa Israel Hakuna Hata Mmoja Ambaye Angeingia Nchi Ya Ahadi,Kwasababu Mbeba Agano Alikuwa Ni Musa Na Musa Huyohuyo Amekufa Kabla Ya Safari Kufika Mwisho.
Yoshua 1:2 Musa Mtumishi Wangu Amekufa,Aya Basi Ondoka Vuka Mto Huu Wa Yordani Wewe Na Watu Hawa Wote,Mkaende Hata Nchi Niwapayo Wana Wa Israeli.
Mungu Angeweza Akanyamaza Kabisa Baada Ya Musa Kufariki Lakini Hakuna Namna Ambavyo Mungu Anaweza Kuacha Agano Lake Lisimame/Liangamie,Kwahiyo Hata Kama Musa Wako Hayupo Uwe Na Uhakika Mungu Atakuinulia Yoshua Na Ng’ambo Ya Mto Yordani Utafika Salama
.
JAMBO LA KUZINGATIA PALE UNAPOMUOMBA MUNGU KWA AJILI YA NAFASI YA MTU ALIYEFARIKI KATIKA NDOA
Tukirejea MWANZO 2:18 Biblia Inaposema ………………………Nitamfanyia Msaidizi Wa Kufanana Naye”
Kila Mtu Anavyo Vipaumbele Vyake Anapofikia Wakati Wa Kutafuta Mwenza Wake, Lakini Hapa Sizungumzii Vijana Jinsi Ya Kuomba Mke/Mme Kwa Bwana, Bali Nazungumzia Kwa Habari Ya Mtu Aliyeondokewa Na Mme Au Mke Kwa Njia Ya MAUTI.
Ukiwa Kama Mwangalizi Mkuu Uliyebaki Kwa Ajili Ya Agano;
1.Husiache Kuliombea Agano
2. Omba Toba Kwa Ajili Ya Makosa Ya Kiagano Mliyotenda Wewe Na Huyo Mwenzi Wako Aliyefariki,Hii Itaondoa Adhabu Kwa Mtu Anayeandaliwa Kuja Kuchukua Nafasi Ya Huyo Aliyeondoka,Ikiwa Kuna Makosa Ya Kiagano Aliyoyafanya Au Mliyoyafanya Kwa Kujua Na Kutokujua Na Mmoja Kati Yenu Akafariki Kabla Hamjatubia Makosa Hayo.
“Ndio Maana Esta Alipoingia Kwenye Nafasi Ya Vashti Mke Wa Mfalme Ahasuero,Alikutana Na Adhabu Hiyohiyo Iliyopelekea Vashti Mke Wa Mfalme Kuachwa Kabla Ya Esta”
Esta 1:1-22 Na Esta 4;9-11
Hii Ni Kuwa Hata Kama Wewe Hukufanya Makosa Hayo Haina Maana Kwamba Wewe Hauhusiki Kwenye Adhabu Inayoweza Kutokana Na Makosa Hayo,Ndio Maana Adamu Alishiriki Adhabu Ya Mkewe Hawa.
“MWANZO 3:17 Akamwambia Adamu,Kwakuwa Umeisikiliza Sauti Ya Mke Wako,Ukala Matunda Ya Mti Ambao Nalikuagiza Nikisema Usiyale,Ardhi Imelaaniwa Kwa Ajili Yako, Kwa Uchungu Utakula Mazao Yake Siku Zote Za Maisha Yako”
Unaweza Ukajiuliza Ni Kwanini Uadhibiwe Kwa Kosa Ambalo Ametenda Mkeo Au Mmeo,Lakini Mungu Anapowatazama Ninyi Katika Ndoa Anaona Ni Mwili Mmoja;
“MWANZO 2:24 Kwahiyo Mwanamume Atamwacha Baba Yake Na Mama Yake Naye Ataambatana Na Mkewe,Nao Watakuwa Mwili Mmoja”
Kwahiyo Hakuna Namna Ambavyo Kichwa Kitakosea Alafu Adhabu Ikapita Kikatwe Na Kuondolewa Na Ukategemea Wakati Huo Kiwiliwili Kibaki Salama Vinginevyo Haitakuwa Mwili Mmoja.
3.Kemea Kwa Jina La Yesu, Kila Roho Za Adui Zilizokuwa Zikitenda Kazi Ndani Ya Agano Lenu La Ndoa.
4.Achilia Damu Ya Yesu,Ili Inene Mema Kwenye Agano Lenu La Ndoa.Hii Itaziba Nafasi Ya Adui Ya Kukuletea Mtu Atakayekuja Nje Na Mpango Wa Mungu Kwa Nia Ya Kulivuruga Agano Pale Utakapoanza Kuomba Kwa Ajili Ya Kumpata Msaidizi Wa Kusudi La Mungu Ndani Yako.
5.Haribu Na Kuyeyusha Kwa Damu Ya Yesu,Mbegu Na Sumu Ambazo Shetani Aliziachilia Katika Agano La Ndoa Yako.
6. Ziba Kwa Damu Ya Yesu,Ufa Au Mlango Ambao Shetani Aliutumia Kuingia Na Kupata Nafasi Ya Kuvuruga Agano La Ndoa Yako.
7.Omba Ulinzi Wa Mungu Juu Ya Agano Lako La Ndoa,Ili Lidumu Kuwa Imara Sawasawa Na Mapenzi Ya Mungu Baba.
KUMBUKA; Unaweza Kuomba Maombi Haya Hata Kama Hujaondokewa Na Mwenza Wako Kimwili Lakini Kwakweli Kwa Namna Ya Rohoni Alikwisha Kuondoka Kwenye Nafasi Yake Kiagano Na Hivyo Shetani Anaweza Kuingia Na Kutoka Muda Wowote Anapohitaji Kufanya Hivyo Katika Ndoa Yako.Pengine Unaweza Kujua Au Husijue Kabisa Kama Mwenzako Hayuko Kwenye Nafasi Yake Kwahiyo Ni Muhimu Kuomba Maombi Haya Hata Kama Mko Katika Nafasi Zenu Kiagano, Maombi Haya Yatazidi Kuimarisha Na Kudumisha Ulinzi Dhidi Ya Adui Katika Ndoa Yako.
Somo Letu Ni UPONYAJI WA NDOA, Hivyo Huu Ni Msingi Tu Ili Upate Kujua Maana Halisi Ya Ndoa Kibiblia Na Msingi Huu Uweze Kukupa Mwanga Wa Kuelewa Kiundani Pale Tutakapoanza Kujifunza Somo Letu.
MAMBO YANAYOSABABISHA MIGOGORO KATIKA NDOA NA NAMNA YA KUYATATUA KWA MSAADA WA MUNGU.
1. KUFUNGA NDOA NA MTU HASIYEKUWA WA KWAKO
MWANZO 2:18
“Bwana Mungu Akasema, Si Vema Huyo Mtu Awe Peke Yake, Nitamfanyia Msaidizi Wa Kufanana Naye”
Biblia Inaposema,Nitamfanyia Msaidizi Wa Kufanana Naye,Inazungumza Kwa Habari Ya Agano Na Sio Kufanana Kimwili.
Maana Yake Kuwa Ile Kufanana Naye,Ni Kwamba,Alichokibeba Mwanamume Kiwe Na Package Ndani Yake Ya Kusaidia Usitawi Wa Kile Alichokibeba Mwanamke,Na Mwanamke Vilevile,Kile Alichobebeshwa Ndani Yake Kiwe Na Sehemu Ambayo Ni Maalum Kabisa Kwa Ajili Ya Kusaidia Kile Alichokibeba Mwanamume.
Kwahiyo Ikitokea Mmojawapo Hana Alichokibeba Kwa Ajili Ya Mwenzake Uwe Na Uhakika Kama Ni Mke Au Mume Atapwaya Kwenye Hiyo Nafasi Ya Kuitwa Mke Au Mume Kwa Ajili Ya Mwenzake,Kwasababu Madhaifu Yoyote Yale Katika Ndoa Yanafichwa Kiagano Yasipate Kutoka Nje , Hivyo Basi Inapotokea Umeingia Katika Agano Na Mtu Hasiye Wa Kwako Uwe Na Uhakika Agano Halitauficha Udhaifu Wa Mwenzako Kwako Na Ndani Yako Utakosa Nguvu Ya Kuusitahimiri Huo Udhaifu Na Baada Ya Muda Migongano Ya Ndani Ikianza Walioko Nje Watajua,Kwasababu Unaweza Kuvumilia Tu Lakini Utasikia Mzigo Mzito Ndani Yako Na Amani Na Furaha Na Mapatano Na Mashauriano Vyote Hivyo Vitaondoka Baada Ya Muda,Kitakachofuata Ni Kuvumiliana Katika Ndoa.Lakini Yote Hayo Ni Kwasababu Umembeba Mtu Wa Mtu Mwingine Hivyo Katika Ulimwengu Wa Roho Mtagongana Kwasababu Atataka Kupata Kitu Cha Ziada Kutoka Kwako Kwa Ajili Ya Kile Alichokibeba Na Bahati Mbaya Hatakipata Na Hapo Ndipo Atakapoanza Kukuona Wewe Hautoshi Kwenye Nafasi Hiyo Kwa Ajili Yake,Kwahiyo Husishangae Kumsikia Mwanamke Anamwambia Mumewe Kwamba Aliolewa Naye Kwa Bahati Mbaya Ni Kwasababu Amegundua Madhaifu Yake Na Kwasababu Ndani Yake Hana Nguvu Ya Kuyaficha,Wala Kuyabeba,Wala Kuyavumilia,Hivyo Haoni Shida Kuachana Na Huyo Mtu Kwasababu Haoni Hasara Atakayoipata.Lakini kama ulikosea hapa husiogope kwasababu damu ya yesu ipo kwa ajili hiyo pia,fuatilia somo hili mpaka mwisho na utapata majibu ya ndoa yako na namna ya kutoka hapo ulipokwama.
Nimesema,Sizungumzii Habari Za Uchumba Kwa Vijana Lakini Hapa Ni Eneo Muhimu Sana Wakati Wa Kufanya Maamuzi Ya Kuingia Katika Ndoa Kwasababu Kuoa Au Kuolewa Na Mtu Hasiyekuwa Wa Kwako Haina Tofauti Sana Na Kuoa Au Kuolewa Na Mtu Wa Imani Tofauti Na Wewe,Kwasababu Madhara Yake Ni Makubwa Mno Kwa Usitawi Wa Ndoa Na Kusudi La Mungu Ndani Ya Kila Mmoja.
2. KUONDOKA KWENYE NAFASI YAKO KIAGANO
Waamuzi 16:1-21
……………….Ndipo Alipomwambia Yote Yaliyokuwa Moyoni Mwake,Akamwambia Wembe Haukupita Juu Ya Kichwa Change Kamwe,Maana Mimi Nimekuwa Mnadhiri Wa Mungu ,Tangu Tumboni Mwa Mama Yangu,Nikinyolewa Ndipo Nguvu Zangu Zitanitoka,Nami Nitakuwa Dhaifu,Nitakuwa Kama Wanadamu Wenzangu…………………………………..Wafilisiti Wakamkamata ,Wakamg’oa Macho , Wakatelemka Naye Mpaka Gaza,Wakamfunga Kwa Vifungo Vya Shaba,Naye Alikuwa Akisaga Ngano Katika Gereza.
Unaweza Kuona Ni Gharama Kiasi Gani Anaipata Samsoni Baada Ya Kuingia Kwa Mwanamke Kahaba Ambaye Sio Wa Kusudi La Mungu Kabisa.
Ni Wanaume Wangapi Leo Maagano Yao Na Mungu Yamesimama Pasipo Kutumika Baada Ya Kuondoka Kwenye Nafasi Zao,Na Ghafla Tu Hali Ya Kiroho Na Kimwili Inapobadilika Hawakumbuki Ni Wapi Walikorofisha Na Kuanguka,Najua Kwamba Huwezi Kuelewa Kiwepesi Lakini Kosa Moja Tu La Kiagano Alilolifanya Samsoni Linaharibu Kusudi La Mungu Ndani Yake Na Sio Tu Kusudi Bali Linaghalimu Mpaka Uhai Wake.Inamaanisha Sasa Wako Watu Wengi Waliokufa Kiroho Na Wanaishi Ndani Ya Ndoa Zao Kimwili Tu Kwa Maana Ya Kutimiza Mapenzi Yao Na Sio Mapenzi Ya Mungu Katika Ndoa Hiyo Sawasawa Na Agano La Ndoa Linavyotaka.Ieleweke Tu Kwamba , Unapokorofisha Katika Agano Moja Kwa Moja Ulinzi Kwa Ajili Ya Hilo Agano Unakaa Pembeni Mpaka Utakapoelewa Namna Sahihi Ya Kurejea Na Kusimama Katika Nafasi Yako,Kama Sivyo Samsoni Angejulishwa Mapema Juu Ya Kitakachotokea Kabla Hakijatokea Lakini Mara Zote Mungu Anapokuja Kwa Mtu Wa Agano Huwa Anataka Azungumze Naye Akiwa Katika Nafasi Ileile Ya Kiagano , Ndio Maana Katika Bustani Ya Edeni Mungu Alimjia Adamu Kwa Namna Hii Baada Ya Uasi;
Mwanzo 3:9 Bwana Mungu Akamwita Adamu,Akamwambia Uko Wapi?
Kwa Swali Hilo Ambalo Mungu Alimuuliza Adamu,Husije Ukafikiri Kwamba Mungu Alikuwa Hajui Ni Wapi Adamu Alipo,Isipokuwa Alihama Kwenye Nafasi Yake Kiagano,Na Mungu Alikuwa Akihoji Nafasi Ya Adamu Kiagano Nje Na Hapo Angeweza Tu Kumfata Huko Alikokuwa Kwasababu Alikuwa Akimuona.
· Fikiri Tu Kwa Nafsi Yako Ni Mara Ngapi Mungu Amekuja Kukutana Na Wewe Na Akakuta Haupo?
· Je Ni Baraka Nyingi Kiasi Gani Umepishana Nazo Baada Ya Kukaa Mbali Na Uso Wa Mungu Kiagano?
· Je Ni Aina Gani Ya Adhabu Zimekupata Na Kuvuruga Ndoa Yako,Maisha Yako,Na Uzao Wako Kwa Makosa Hayo Ya Kiagano Uliyoyatenda?
Kwa Kosa Moja La Adamu,Mungu Aliachilia Adhabu Katika Maisha Yake Yote Na Katika Uzao Wake Wote,Hivyo Watoto Wanaweza Wakawa Wamekwama Mahali Kwasababu Ya Makosa Ya Wazazi Wao.
3. KUONDOKA KWENYE WAJIBU NA UPENDO WA KIAGANO
(a) 1PETRO 3:1-4
“Kadhalika Ninyi Wake,Watiini Waume Zenu,Kusudi Ikiwa Wako Wasioliamini Neno Wavutwe Kwa Mwenendo Wa Wake Zao,Pasipo Lile Neno.Wakiutazama Mwenendo Wenu Safi Na Wa Hofu,Kujipamba Kwenu Kusiwe Kujipamba Kwa Nje,Yaani Kusuka Nywele Na Kujitia Dhahabu Na Kuvalia Mavazi,Bali Kuwe Na Utu Wa Moyoni Husioonekana Katika Mapambo Yasiyoharibika,Yaani Roho Ya Upole Na Utulivu Iliyo Ya Thamani Kuu Mbele Za Mungu.”
Katika Sehemu Hii Ya Tatu Natafuta Kujua Ni Wanawake Wangapi Wanayaishi Hayo Tuliyoyaona Hapo Juu Katika Ndoa Zao Lakini Nasikitika Mno Kusema Ni Wachache Sana,Kwasababu Kesi Na Migogoro Tunayoishuhudia Katika Ndoa Nyingi Za Leo Ni Kwasababu Iko Jamii Kubwa Sana Ya Watu Hawajasimama Katika Nafasi Zao Ndani Ya Ndoa Zao.
Najaribu Kutafakari Tu Kwamba;
Ni Wanawake Wangapi Wanawatii Waume Zao Kama Biblia Isemavyo,
Ni Wanawake Wangapi Wana Mwenendo Safi Na Hofu Mbele Za Waume Zao,
Ni Wanawake Wangapi Namna Wanavyojipamba Na Kupendeza Kwa Nje Hivyo Ndivyo Walivyo Mioyoni Mwao,
Swali La Msingi Ni Wanaume Wangapi Wamerejea Katika Nafasi Zao Mbele Za Mungu Kutokana Na Mwenendo Safi Na Hofu Na Utii Na Uzuri Wa Ndani Wa Wake Zao!!!!
Ninapolitazama Agano La Ndoa Kwa Namna Ya Rohoni,Nasikia Huzuni Nyingi Ndani Yangu Kusema Ndoa Nyingi Zimefeli Katika Pointi Hii Na Wengi Hawajui Ni Kwanini Wamejikuta Wako Hapo Walipo,
Nimewasikia Wengi Wakilalamika Kwa Kusema,”Upendo Uliokuwepo Wakati Wa Uchumba Haupo Tena”Na Wengi Hutazamia Upendo Huo Huo Uendelee Kuonekana Lakini Huwa Tofauti,Ni Kwasababu Wengi Wao Pia Hawajajua Kama Kuna Tofauti Kubwa Sana Kati Ya Upendo Kabla Ya Ndoa Na Upendo Baada Ya Ndoa,Sikia Hii Itakusaidia Mwana Wa Mungu,Upendo Ni Uleule Lakini Upendo Hubadilika Kutokana Na Ni Wapi Umekanyaga Ukiwa Umeuvaa Huo Upendo Na Msingi Na Makusudi Ya Huo Upendo Ni Nini.
Upendo Kabla Ya Ndoa Ni Wa Kihisia Na Upo Kimwili Zaidi Na Hauna Mipaka Kwasababu Hauna Sheria Nyuma Yake,Najua Hujanielewa,Lakini Yakupasa Kujua Ikiwa Ulikuwa Hujui Yakwamba Mbingu Zinatoa Mke Na Hazitoi Mchumba Kwasababu Mchumba Ni Mtu Ambaye Yuko Chini Ya Matazamio Na Unaweza Kumchagua Huyo Au Kumuacha Na Hakuna Sheria Hapo Lakini Ndoa Ni Kitu Halisi Na Kina Sheria,Kanuni Na Taratibu Nyuma Yake,Sasa Kwa Wale Ambao Hawajaoa Au Kuolewa Husijaribu Kwenda Mbele Za Mungu Unaomba Mchumba Maana Yake Unamwambia Mungu Kuwa Hata Yeye Hana Uhakika Na Huyo Mtu Kwahiyo Mpate Muda Wa Pamoja {Yaani Wewe Na Mungu} Wa Kumchunguza Kwanza,Pengine Hujaelewa Lakini Kasome Biblia Yako Vizuri Hakuna Mahali Kokote Ambako Mungu Alimpa Mtu Mchumba.
Hivyo Kama Mbingu Hazitoi Mchumba Uwe Na Uhakika Haziwezi Kuweka Sheria Nyuma Yake,Ndio Maana Taratibu Nyingi Sana Za Kuishi Katika Maisha Ya Uchumba Zinatolewa Na Madhehebu,Ndio Maana Kila Dhehebu Lina Utaratibu Wake Lakini Upendo Wa Ndoa Ni Wa Kiagano Na Una Sheria,Mipaka,Kanuni Na Taratibu Nyuma Yake.
KWA MFANO; Huwezi Kumzuia Kijana Wa Kike Au Wa Kiume Kuvunja Uchumba Na Kuanza Kutafuta Mtu Mwingine Kwasababu Hana Uhakika Huyo Aliyeko Muda Huo Kama Anamfaa Ama La Kwahiyo Ana Uhuru Wa Kuamua Kuwa Nae Au Kutafuta Mtu Mwingine Lakini Katika Ndoa Hakuna Kitu Cha Namna Hii.
Kwahiyo Kama Hukuwahi Kufundishwa Kabla Maana Halisi Ya Upendo Wa Ndoa Kibiblia,Uwe Na Uhakika Itakupa Shida Kwasababu Katika Ulimwengu Wa Roho Kanuni Zitabadilika Automatically Baada Tu Ya Kufanya Agano La Ndoa.
KUMBUKA HII;Ni Ngumu Sana Na Haiwezekaniki Kabisa Hayo Tuliyoyaona Hapo Juu Katika 1PETRO 3:1-4
Kuyaishi Kipindi Cha Uchumba Kwasababu Ni Kanuni Za Mke Na Sio Mchumba. Na Husijaribu Kuyaishi Kipindi Cha Uchumba Kwasababu Lazima Utaanguka Dhambini Na Hii Ndio Ajabu Nyingine Ya Tofauti Kati Ya Uchumba Na Ndoa,Kwasababu Ukijaribu Ku Pretend Kama Mke Wakati Wewe Ni Mchumba Uwe Na Uhakika Na Kijana Atataka Haki Zake Kama Mme Na Sio Mchumba Tena.
Kwahiyo Wengi Wamefeli Kuhama Kimwili Kutoka Katika Upendo Wa Uchumba Kwenda Katika Upendo Wa Ndoa,Na Wengi Baada Ya Kuingia Huko Wameona Kama Ni Utumwa Kwasababu Hawakujifunza Namna Ya Kutembea Katika Upako Wa Ndoa Kabla Ya Kuingia Katika Ndoa.Na Kwa Maana Hiyohiyo Sasa Wanawake Wengi Wamehama Kwenye Wajibu Wao Na Upendo Wao Kwa Waume Zao umepoa Kwa Kufikiri Wanapuuzwa “Kwamba Waume Wao Wamewachukulia Wakawaida Baada Ya Kuwaoa” Na Kujikuta Wanapuuza Vitu Vya Msingi Katika Ndoa Na Kupelekea Migogoro Kutokea,Na Wanaume Wengi Wamebeba Lawama Hizi Pasipokuelewa, Na Wakati Mwingine Wamejitahidi Kujaribu Kufanya Kama Ambavyo Wake Zao Wanataka Lakini Wameshindwa,Wakijaribu Sana Ni Siku Kadhaa Na Baada Ya muda Hali Huwa Ileile Na Malalamiko Kwa Wake Zao Huanza Tena.Lakini Unapoingia Katika Ndoa Wingu La Uchumba Linahama Pamoja Na Yote Lililoyabeba Na Linakuja Wingu La Ndoa Ambalo Nalo Limebeba Vitu Maalum Kabisa Kwa Ajili Ya Ndoa,Kwahiyo Husijaribu Kuishi Katika Ndoa Kwa Mfumo Wa Uchumba Ni Wazi Kuwa Utakwama Mapema Sana Na Safari Yako Haitafika Mbali.
(b) WAEFESO 5:25,28
“Enyi Waume Wapendeni Wake Zenu Kama Kristo Naye Alivyolipenda Kanisa,Akajitoa Kwa Ajili Yake…………………Vivyo Hivyo Imewapasa Waume Nao Kuwapenda Wake Zao Kama Miili Yao Wenyewe,Ampendaye Mkewe Hujipenda Mwenyewe”
Wako Wanaume Wanawachukulia Wake Zao Kama Kitu Dhaifu Sana Kiasi Ambacho Hawaoni Umuhimu Wa Kuwashirikisha Baadhi Ya Mambo Ya Kifamilia,Na Hawajajua Kuwa Manunguniko Ya Mke Yana Uwezo Wa Kuzuia Kiwango Fulani Cha Baraka Juu Yako Na Maombi Yako Kukosa Sifa Ya Kufika Mbele Za Mungu Haijalishi Wako Karibu Na Mungu Kiasi Gani,Hii Utaipata Katika 1PETRO 3:7 “Kadhalika Ninyi Waume Kaeni Na Wake Zenu Kwa Akili Na Kumpa Mke Heshima,Kama Chombo Kisicho Na Nguvu Na Kama Warithi Pamoja Na Neema Ya Uzima,Kusudi Kuomba Kwenu Kusizuiliwe”
Kwahiyo Kumheshimu Mke Wako Sio Ombi Ikiwa Unataka Maombi Yako Yapate Kibali Mbele Za Mungu . Na Wako Wengine Pia Wamejaribu Hata Kutoka Nje Ya Ndoa Wakifikiri Watapata Radha Tofauti Na Ile Wanayoipata Kwa Wake Zao Na Baada Ya Dhambi Hiyo Wakasahau Kabisa Wajibu Wao Na Wakafikiri Wako Salama Sana Lakini Maandiko Yanasema “1wakorintho 6:16 Je Hamjui Ya Kuwa Yeye Aliyeungwa Na Kahaba Ni Mwili Mmoja Naye?Maana Asema,Wale Wawili Watakuwa Mwili Mmoja” Zaidi Sana Biblia Iko Wazi Kabisa Kwamba “Mwanzo 2:24………………..Mtakuwa Mwili Mmoja” Kama Mwili Ni Mmoja Na Mwili Huohuo Unaenda Nje Kuzini Tena Kwa Kahaba, Na Haukumbuki Kutubu,Maana Yake Ni Kwamba Uwe Tayari Mwili Huo Kuadhibiwa,PENGINE Hujaelewa Lakini Ikiwa Ni Mwili Mmoja Maana Yake Kila Dhambi Ambayo Mmojawenu Anaitenda Inawatafuna Wote Wawili Kwasababu Biblia Inasema Ninyi Ni Mwili Mmoja. Ndoa Nyingi Pia Zimekwama Katika Eneo Hili Kwa Kiasi Kikubwa,Kwasababu Ni Wanaume Wachache Wanaoweza Kupata Ujasiri Wa Kuungama Mbele Za Wake Zao Baada Ya Kutoka Nje Ya Ndoa Ili Mke Nae Akiwa Kama Sehemu Ya Huo Mwili Ulitenda Dhambi Huko Nje Apate Kwenda Mbele Za Bwana Mungu Kwa Toba Sio Kwa Ajili Ya Mmewe Bali Ya Kwa Ajili Ya Sehemu Ya Mwili Wake Umetenda Dhambi Na Kuweka Hatarini Usalama Wa Agano Lao Na Mungu,Lakini Pia Kama Mwanamume Akipata Ujasiri Wa Kuwa Muwazi Mbele Za Mkewe Katika Jambo Kama Hilo Ni Wanawake Wangapi Pia Wanweza Kuelewa Na Kuomba Sio Tu Ajili Ya Waume Zao Bali Kwa Ajili Yao Pia.Wengi Baada Ya Taarifa Hiyo Hujawa Na Hasira Na Kukimbilia Kwa Viongozi Wao Wa Kiimani,Wazazi Na Wengine Viongozi Wa Kimira Kutokana Na Msingi Wa Ndoa Yenyewe Wapi Umesimama,Lakini Msaada Pekee Ni Kwenda Mbele Za Mungu,Sina Maana Kwamba Viongozi Wengine Hawana Msaada Katika Hili Lakini Husijaribu Kupeleka Nafasi Ya Mungu Kwa Mwanadamu Kwasababu Wahusika Wakuu Katika Agano Hili La Ndoa Ni Ninyi Wahusika Wenyewe Ambao Ni Mwili Mmoja Pamoja Na Mungu Mliyeingia Katika Agano Nae.
Hata Hivyo Pia Wanaume Wengine Ni Wepesi Mno Kukimbilia Katika Uovu Lakini Ni Wagumu Katika Matengenezo Na Hawajuja Bado Kwamba Wake Zao Pia Wanaweza Kuchukua Roho Za Uzinifu Kutokana Na Wao Kuzini Nje Ya Ndoa , “Ikiwa Ni Dhambi Hiyo Waliyoitenda,” Kwasababu Kama Ni Mwili Ni Mmoja ,Maana Yake Roho Ya Uzinzi Na Unajisi Na Adhabu Unazoweza Kuzipata Kutokana Na Dhambi Zako Zinahamia Mpaka Kwa Mkeo,Ndo Maana Mkeo Anaweza Kuanza Tabia Ya Uzinzi Ghafla Ama Tabia Ambazo Kabla Hukumuona Nazo,Alafu Ukaanza Kufikiri Labda Amekugundua Usaliti Wako Na Anaanza Kulipa Kisasi Lakini Kumbe Ni Roho Hizohizo Ulizozipata Wewe Baada Ya Kuanguka Dhambini Ndizo Zinazomtumikisha.(Lakini Sina Maana Kwamba Makosa Yote Atakayoyafanya Mkeo Yanatokana Na Wewe,Mengine Yanaweza Kuwa Ya Kwake Na Kwasababu Zake Lakini Hii Pia Yaweza Kupelekea Hali Hiyo Kutokea Husipowahi Mapema Kwenda Mbele Za Bwana Kwa Toba Na Kujua Namna Ya Kuomba) Na Hii Ndio Maana Halisi Ya MITHALI 6:32 “Mtu Aziniye Na Mwanamke Hana Akili Kabisa,Afanya Jambo Litakalomwangamiza Nafsi Yake.” Kwahiyo Ukizini Na Mwanamke Ufahamu Wako Unafungwa Katika Ulimwengu Wa Roho Na Nafsi Yako Inaingia Kifungoni Maana Yake Kwenye Maangamizi Na Hiyo Tu Haitoshi Bali Kwa Dhambi Hiyohiyo Ya Uzinifu Roho Ya Mauti Huingia Kwenye Maisha Ya Mtu; MAMBO YA WALAWI 20:10 “Na Mtu Aziniye Na Mke Wa Mtu Mwingine , Naam Yeye Aziniye Na Mke Wa Jirani Yake , Mtu Mme Na Mwanamke Aziniye,Hakika Watauawa” Ni Ukweli Kwamba Unaweza Husife Kimwili Lakini Maisha Yako Na Vitu Vyako Vimekwama Mahali Kwa Ajili Ya Hiyo Roho Ya Mauti Ambayo Imeshikilia Miguu Yako Na Mikono Yako.
Utajitahidi Kusogea Lakini Hatua Zako Zimekamatwa Na Utajitahidi Kumiliki Lakini Mikono Yako Imekaliwa Na Mauti,Na Wengine Kwakweli Wamekuwa Waaminifu Hawajawahi Kuzini Kimwili Lakini Walizini Katika Ndoto Na Wake Za Watu Wengine Na Wengine Hawawajui Na Baada Ya Kutoka Katika Ndoto Hawakujua Kama Nikitu Halisi Kimetokea Katika Ulimwengu Wa roho Na Kimeacha Mbegu Hapo Ambayo Baada Ya Muda Hali Yao Ya Maisha Ikabadilika Na Hawakujua Ni Kwanini,Lakini Kumbe Roho Hiyo Ilipenya Katika Maisha Yao Kupitia Mlango Wa Ndoto Na Kuvuruga Kusudi La Mungu Ndani Yao Na Kuharibu Mfumo Wa Maisha Halisi Ambao Kristo Aliwakusudia.
Yamkini Hukujua Kama Ni Kitu Halisi Kimeingia Katika Maisha Yako Pamoja Na Kusikia Kukosa Amani Kwa Muda,Lakini Saa Imefika Sasa Ya Kuvuka Hapo Ulipokwama Na Yesu Yupo Kwa Ajili Yako,Endelea Kufatilia Somo Hili Mpaka Mwisho Na Mwisho Utapata Mwongozo Na Namna Ya Kukutoa Hapo Ulipokwama,
4. KUKOSEKANA KATIKA NDOA HEKIMA NA BUSARA
MITHALI 2:11 “Busara itakulinda,ufahamu utakuhifadhi”
MITHALI 15:1 “jawabu la upole hugeuza hasira,bali neno liumizalo huchochea ghadhabu”
Katika Hali Tu Ya Kawaida Ya Kibinadamu Kukwazana,Kukoseana,Kutofautiana Lazima Kutatokea Lakini Ni Hekima Pekee Inayoweza Kuwafanya Mkamaliza Tofauti Zenu Kwa Amani Na Kila Mtu Akabaki Salama Moyoni.
Husijaribu Kutumia Nguvu/Mamlaka Yako Kutokana Na Nafasi Yako Katika Ndoa Kujaribu Kuficha Makosa Yako Huku Ukifikiri Ukijishusha Kwa Mwenzako Nafasi Yako Itaondoka , La Hasha , Ni Kwamba Hata Huyo Uliyemkosea Anasubiri Kuona Ukiri Wako Na Unyenyekevu Wako Ili Mtengeneze Na Kumaliza Tofauti Zenu Kwa Amani Hata Bila Jirani Kujua Kinachoendelea Kwenu,Au Hujajua Kwamba Yakobo 5:16 “Ungameni Dhambi Zenu Ninyi Kwa Ninyi Na Kuombeana,Mpate Kuponywa.Kuomba Kwake Mwenye Haki Kwafaa Sana,Akiomba Bidii” Lakini Wako Watu Wanajaribu Kujisahaulisha Makusudi Huku Wakitegemea Na Waliowakosea Watasahau,Ni Kweli Kwa Wewe Kufupaza Shingo,Akiwa Ni Mtu Wa Amani Anaweza Kujionyesha Kwako Kama Amesahau Lakini Moyoni Mwake Anao Uchungu,Uchungu Ambao Ndani Yake Umebeba Ugonjwa Wa Kufisha, Hata Hivyo Biblia Iko Wazi Kabisa Kwamba Waefeso 4:31 “Uchungu Wote,Na Ghadhabuna Kelele Na Matukano Yaondoke Kwenu Pamoja Na Kila Namna Ya Ubaya” Lakini Husije ukawa Umekuwa Sababu Ya Mwenzako Kuwa Na Uchungu Alafu Ukamsomea Huu Msitari Na Kutegemea Akuelewe Kirahisi,Tengeneza Kwanza Ndipo Ukampe Nafasi Ya Kuokoa Nafsi Yake.
Hata Hivyo Kutokana Na Mithali 15:2 “Ulimi Wa Mwenye Hekima Hutamka Maarifa Vizuri,Bali Vinywa Vya Wapumbavu Humwaga Upumbavu” Unaona Ni Namna Gani Mungu Anajaribu Kuwasihi Waliokosea Na Waliokosewa Kuachilia Hekima Na Kujitenga Na Upumbavu Kwasababu Palipo Na Upumbavu Hakuna Amani, Ni Muhimu Sana Kuachilia Amani Ya Kristo Yesu Ili Itawale Kwa Kutoa Majibu Ya Upole Ambayo Ndani Yake Hupoza Hasira Na Kubadili Maneno Makali Yenye Kuumiza Ambayo Ndani Yake Yamebeba Kuichochea Ghadhabu.
MUHUBIRI 10:12 “Maneno Ya Kinywa Cha Mwenye Haki Yana Neema,Bali Midomo Ya Mpumbavu Itammeza Nafsi Yake”
Hivyo Mapatano Ambayo Ndani Yake Yana Hekima Huwa Yamebeba Neema Ya Mungu,Kumbuka Hiyo Husisahau Pindi Utakapokuwa Katika Mapatano Na Mwenzako.
5. KUJIHESABIA HAKI NA KUMSHUTUMU MWENZAKO
WAGALATIA 3:11
“Ni Dhahiri Ya Kwamba Hakuna Mtu Ahesabiwaye Haki Mbele Za Mungu Katika Sheria,Kwasababu Mwenye Haki Ataishi Kwa Imani”
Madhaifu Ni Sehemu Ya Maisha Ya Kila Mwenye Mwili Wa Damu Na Nyama,Hivyo Husijaribu Kumtafuta Mtu Aliyekamilika Kwa Asilimia Zote Kwasababu Hutompata Vinginevyo Pasingelikuwepo Na Sababu Ya Yesu Kuja Duniani Ikiwa Wanadamu Tungekuwa Wakamilifu.
Unaweza Ukajiuliza Utawezaje Kuishi Na Mtu Mwenye Madhaifu,Kwanza Kabisa Lazima Uelewe Kwamba Wewe Mwenyewe Unayo Madhaifu,Pili Kasome Biblia Yako Vizuri Pale Inaposema…………………… Waefeso 5:33 “Lakini Kila Mtu Ampende Mke Wake Kama Nafsi Yake Mwenyewe,Wala Mke Hasikose Kumsitahi Mumewe” Biblia Hisingesema Kumsitahi Mumewe Kama Kweli Huyo Mwanamume Hasingekuwa Na Madhaifu,Kwahiyo Husijaribu Kujihesabia Haki Katika Mazingira Yoyote Yale Kwasababu Hata Wewe Unayo Madhaifu Ambayo Huyo Uliye Naye Amepewa Nafasi Ya Kuyaona Na Kuyaficha Na Siku Akiondoka Na Akaja Mwingine Ambaye Sio Wa Kiagano Ndipo Utakapoelewa Ni Kwa Kiasi Gani Una Mapungufu Makubwa Kwasababu Lazima Yatakuwa Wazi Maana Mfuniko Wa Kuyaficha Upo Kwa Yule Mwanamke Wa Kiagano Ambaye Ndani Yake Anacho Kitu Kwa Ajili Yako.Hata Hivyo Kusitahimiana Katika Ndoa Ni Muhimu Sana Kwasababu Madhaifu Ya Mtu Yakiwa Wazi Kwa Mtu Ambaye Yuko Nje Na Hilo Agano,Heshima Ya Mtu Huyo Hutoweka Na Huko Ndiko Kumvua Nguo.
6. KUPELEKA KESI AU MIGOGORO YA KIAGANO KATIKA MAHAKAMA YA DUNIANI BADALA YA MAHAKAMA YA MBINGUNI
MATHAYO 19:5
“Akasema Kwasababu Hiyo Mtu Atamwacha Babaye Na Mamaye,Ataambatana Na Mkewe Na Hao Wawili Watakuwa Mwili Mmoja”
Kwa Maandiko Hayo Mungu Anawatazama Wanandoa Kama Mwili Mmoja,Kwa Tafsiri Hiyo Inatosha Kabisa Kuonyesha Kuwa Hukumu Inayoweza Kutolewa Kutoka Katika Hizi Mahakama Mbili Tofauti Kwa Kosa Hilohilo Moja Haziwezi Kufanana,Kwasababu Mahakama Ya Mbinguni Inapowatazama Wanandoa Inawaona Ni Mtu Mmoja (Mwili Mmoja), Lakini Mahakama Ya Duniani Inapowatazama Wanandoa Inawaona Ni Watu Wawili Tofauti (Miili Miwili) Kwa Maana Hiyo Sasa Kesi Ya Kindoa Inapopelekwa Katika Mahakama Ya Duniani ,Mahakama Hiyo Inamtafuta Mwenye Haki Na Wa Kumbebesha Lawama Ili Imuhukumu, Lakini Mahakama Ya Mbinguni Kwasababu Inawaona Ni Mwili Mmoja,Hivyo Inapopelekwa Kesi, Mahakama Hiyo Inatafuta Jinsi Ya Kufuta Uhalali Wa Doa Hilo Lililochafua Mwili Huo Ili Lipate Kufutikana kutoweka.
KWA MFANO; Mahakama Ya Duniani Inaweza Kuamua Wanandoa Waachane Kutokana Na Uzito Wa Kosa Lenyewe Lakini Pia Kutokana Na Maamuzi Ya Waliopeleka Hiyo Kesi,Lakini Tazama Mahakama Ya Mbinguni Inasemaje Kuhusu Wanandoa Kuachana;
MATHAYO 19:6
“Hata Wamekuwa Si Wawili Tena,Bali Mwili Mmoja,Basi Aliowaunganisha Mungu,Mwanadamu Hasiwatenganishe”
Unaweza Kuona Hapo Nini Mungu Anasema Kwa Habari Ya Kuachana , Hivyo Badala Ya Kutatua Tatizo Mnaweza Mkaingia Katika Shida Nyingine Ya Kiagano Ambayo Kati Yenu Hakuna Atakayebaki Salama Kwasababu Mmemchukiza Mungu Kwa Maamuzi Hayo Sawasawa Na MALAKI 2:16” Maana Mimi Nachukia Kuachana,Asema Mungu Wa Israeli………………………” Hivyo Jifunze Kupeleka Kesi Zako Msalabani Ili Amani Idumu Kati Yenu Na Waebrania 13:1 “Upendano Wa Ndugu Na Udum”Ili Mapenzi Ya Mungu Yatimie Katika Agano Lenu La Ndoa Badala Ya Mapenzi Ya Mwanadamu.
7. KUTOKUOMBA TOBA BAADA YA KUANGUKA DHAMBINI
ISAYA 1:18
“Haya Njooni Tusemezane Asema Bwana,Dhambi Zenu Zijapokuwa Nyekundu Sana,Zitakuwa Nyeupe Kama Theluji,Zijapokuwa Nyendu Kama Bendera Zitakuwa Kama Sufu.”
Husijaribu Kupuuzia Kutubu Kwa Kila Kosa/Dhambi Inayotendeka,Haijalishi Ni Ndogo Au Kubwa Kwasababu Kwa Mungu Hakuna Dhambi Ndogo Maana Tendo Lolote Nje Na Mapenzi Ya Mungu Linaondoa Utukufu Wa Mungu Na Utukufu Wa Mungu Ukiondoka Ni Rahisi Sana Kwa Adui Kupata Nafasi,Na Kila Dhambi Imebeba Adhabu Yake Ambapo Isiposhughulikiwa Mapema Inaweza Kuua Ndoa Yako,Maisha Yako,Na Uzao Wako Kama Tulivyoona Katika Vipengele Vilivyotangulia .
Unaweza Ukajiuliza Utajuaje Kama Umesamehewa Na Adhabu Imeondolewa Juu Yako Baada Ya Toba Lakini Lazima Uamini Kwasababu Ndio Maana Yesu Alipita Msalabani Na Damu Yake Ambayo Inaweza Kuvunja Agano La Adui Na Kusimamisha Agano La Mungu , Uwe Na Uhakika Baada Ya Maombi Hayo Ya Toba Damu Hiyo Inenayo Mema Itaachilia Amani Na Upendo Wa Awali Wa Kiagano Sawasawa Na Mapenzi Ya Mungu Baba.
Husikose Ujasiri Wa Kwenda Mbele Za Mungu Kwa Toba Huku Ukiutazama Msalaba Kama Njia Ya Kukurejesha Katika Hatua Zako Za Awali Kabla Ya Aguko Na Damu Ya Yesu Iliyo Mwagika Msalabani Kwa Ajili Ya Kila Mwenye Mwili Iko Tayari Kabisa Kukusafisha,Kukutakasa Na Kukukomboa.
ISAYA 55:7
“Mtu Mbaya Na Aache Njia Yake,Na Mtu Hasiye Haki Aache Mawazo Yake,Na Amrudie Bwana Naye Atamrehemu,Na Arejee Kwa Mungu Wetu,Naye Atamsamehe Kabisa.”
Hivyo Husione Shaka Moyoni Mwako Kwenda Mbele Za Bwana Ili upate Msaada Wa Mungu Kwasababu Katika Toba Ndipo Palipo Na Urejesho Wa Uhai Wa Kila Kilichokufa Kwa Ajili Ya Dhambi Zetu;
EZEKIELI 18:27-28
“Tena Mtu Mwovu Atakapoghairi Na Kuuacha Uovu Wake Alioutenda Na Kutenda Yaliyo Halali Na Haki Ataponya Roho Yake Nayo Itakuwa Hai.”
JINSI YA KUOMBA KWA AJILI YA UPONYAJI WA NDOA YAKO
a) Omba Toba Kwa Ajili Ya Kosa Na Jambo Lolote Lililosababisha Mlango Ukafunguka Na Shetani Akapata Nafasi.(hii ni nafasi pia kama hukufanya maamuzi sahihi wakati unaoa au kuolewa)
b) Kemea Kwa Jina La Yesu,Kila Aina Ya Mapepo Na Roho Za Adui Zilizoingia Katika Ndoa Yako Iwe Kimwili,Au Kiroho Katika Ndoto.
c) Yeyusha Kwa Damu Ya Yesu,Kila Aina Ya Mbegu Na Sumu Ambazo Shetani Ameziachilia Katika Ndoa Yako .
d) Mnyanganye Adui Kwa Jina La Yesu,Kila Kitu Ambacho Alikiteka Katika Ndoa Yako Kisha Achilia Ukombozi Juu Ya Ndoa Yako Kwa Damu Ya Yesu.
e) Omba Uponyaji Kwa Damu Ya Yesu Kila Eneo Ambalo Katika Ndoa Yako Lilijeruhika Baada Ya Mashambulizi Ya Adui.
f) Ziba Ufa Kwa Damu Ya Yesu,Mahali Ambako Boma Lilibomoka Na Shetani Akapata Upenyo Wa Kuingia Katika Ndoa Yako.
g) Omba Ulinzi Juu Ya Ndoa Yako.
Baada Ya Maombi Haya Tegemea Kuona Hali Mpya Ikitokeza Katika Ndoa Na Kila Kilichokuwa Kimekufa Au Kuibiwa Utakiona Kikirejea Kwasababu Damu Ya Yesu Inapoachiliwa Ukombozi Lazima Utokee.
Kumbuka Kuomba Kwa Mtiririko Huo Na Pale Linapotakiwa Kutumika Jina La Yesu Basi Litumie Na Panapodai Kutumia Damu Ya Yesu Basi Itumie Ipasavyo kadri Roho Mtakatifu Atakvyokuongoza,MUNGU Akitupa Neema Tena Katika Saa Nyingine Tutakuja Kujifunza Tofauti Na Jinsi Ya Kutumia Jina La Yesu Na Damu Ya Yesu Na Ni Mahala Gani Vitumike.
Na Maombi Haya Yanawahusu Wanandoa Wote Ni Muhimu Sana Mkasoma Na Kujifunza Kwa Pamoja Tangu Mwanzo Hata Mwisho Kwasababu Ninyi Ni Mwili Mmoja,
“Basi Imani Chanzo Chake Ni Kusikia Na Kusikia Huja Kwa Neno La Kristo. Warumi 10:17”
Kwahiyo Lazima Usikie Kwanza Ndipo Uamini,Na Kusikia Kunatoka Katika Neno Ambalo Ndilo Neno La Mungu,Hivyo Ni Muhimu Ukasoma Kwanza Na Kuelewa Hiyo Itakupa Kujua Ni Wapi Umekwama Na Hivyo Kukuwekea Wepesi Wa Kumsikia Roho Mtakatifu Uwapo Katika Kuomba.
NEEMA NA USHIRIKA WA MUNGU BABA VIKAWE PAMOJA NAWE
Kwa Msaada Ushauri Na Maombezi
PIGA +255767 155 623
SMS +255620 179 783
SMS +255620 179 783
“MUNGU WANGU AKUBARIKI NA KUKUTENDEA MEMA”
0 Comments