SOMO: NGUVU YA IMANI
WAEBRANIA 11:1
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana”
WARUMI 1:17
“kwa maana haki ya mungu inadhihilishwa ndani yake toka imani hata
imani kama ilivyo andikwa mwenye haki
ataishi kwa imani.”
IMANI KATIKA KRISTO
v
IMANI ni mwitikio chanya wa roho yako ikubaliane
pasipo shaka kuhusu neno la Mungu linavyosema kuhusu wewe na mazingira
yanayokuzunguka.
v
IMANI ni mwitikio chanya wa kimatendo mema
yanayochochewa na kweli ya neno la Mungu.
v
Kutokana nawaebrania
11:1maana yake imani zaidi ya kile unachokiona katika ulimwengu wa mwili.
Zaidi sana imani ni kuweka moyo
wako,macho yako,mdomo wako na vitendo vyako view ndani ya neno la kristo.
·
IMANI siyo hisia
·
IMANI siyo kujitutumua
·
IMANI siyo kupata ulichokuwa unatafuta alafu
ukakitendea kazi na ukasema umepata kwasababu ya IMANI.
·
Mathayo 17:14-20 ukiangalia mistari hii katika
biblia yako utagundua kuwa Yesu aliamua kufundisha imani kwa msisitizo mkubwa
mno eneo hili;
“nao walipoufikia mkutano , mtu mmoja akamjia, akampigia magoti,
akisema, Bwana umrehemu mwanangu kwakuwa ana kifafa na kuteswa vibaya, maana
mara nyingi huanguka motoni na mara nyingi majini.nikamleta kwa wanafunzi wako
wasiweze kumponya .
Yesu akajibu akasema,enyi kizazi kisichoamini , kilichopotoka, nitakaa
pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini?mleteni huku kwangu.
Yesu akamkemea pepo naye akamtoka , Yule kijana akapona tangu saa
ile.kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema mbona sisi
hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia
kwasababu ya upungufu wa imani yenu, kwa maana amini nawaambia mkiwa na imani
kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu,ondoka hapa uende kule , nao
utaondoka , wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.”
Kwa maandiko hayo machache utaona ni kiwango gani cha imani
tunatakiwa nacho ili tuwe na nguvu na uwezo ndani yetu wa kutembea na kusimama
mahali popote na katika mazingira yoyote kwa nguvu tu ya imani.
KILICHOPO KWENYE IMANI YA NAMNA HII
HABAKUKI 2:4
“tazama roho yake hujivuna haina unyofu ndani yake lakin mwenye haki
ataishi kwa imani yake.”
Kuna kanuni ndani yake ambayo inawawezesha watu wenye imani
hiii kupata wanachotaka kwaMungu
I.
Ukiokoka maisha ni imani bila hivyo maana yake
sehemu hautaruhusiwa kupenya .
II.
Ikifeli imani ndani yako , inamaanisha umefeli
kila kitu cha kimungu ndani yako.
III.
Imani siyo kichwa, siyo fikirabali Imani ni ya moyo.
IV.
Mungu hasikii lugha za wanadamu bali Mungu
husikia na kutazama kiwango cha imanikilichoko
ndani yako kwa kulinganisha na kitu unachohitaji kupata au kupokea kutoka kwa
Mungu kwa wakati huo.
V.
Imani ilimfanya sara apate mtoto uzeeni (
wanasanyansi wakakaa kimya, maana imani
iliwavunjia kanuni za kisayansi kwa
sara)
( MWANZO 18:9-14) “wakamwambia yu wapi sara
mkeo? Akasema yumo hemani, akamwambia hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani
, na tazama , sara mkeo atapata mwana wa kiume, sara akasikia mlangoni pa hema
iliyokuwapo nyuma yake.
Basi ibrahimu na sara walikuwa wazee, na
umri wao mkubwa, na sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake, kwahiyo
sara akacheka moyoni mwake akisema, niwapo mkongwe nitapata furaha na bwana
wangu mzee? Bwana akamwambia iburahimu
mbona sara ameckeka akisema , mimi kweli
nitazaa mwana nami ni mzee?
kuna neno gani lililo gumu la kumsinda BWANA? Kwa muhula
wake nitakurudia wakati huu huu mwakani na Sara atapata mwana wa kiume.”
KWAHIYO;
VI.
Imani inaleta mwonekano mpya ( utukufu mwingine)
VII.
Pasipo IMANI hakuna kupokea.
VIII.
Imani humuweka mtu karibu na Mungu.
WAEFESO 6:16
zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale
yote yenye moto ya Yule mwovu.
MFANO WA MAISHA YA IMANI TEGEMEZI KWA WATU (HASARA TU)
MWANZO 19:26
lakini mkewe Ruthu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi.
ESTA 3:8-12 Hamani aliweka imani yake kwa Mfalme Ausuero
badala ya kuweka kwa Mungu (siku zote kutegemea mtu katika maswala ya imani ni
sawa na kuvua nguo wakati wa baridi, au ni sawa na kupewa urithi wa kaburi. Ni
mfano wa mtu achekaye msibani.
Mtu ataishi kwa imani yake
wala si ya jirani yake kwa kua imani ya jirani inaweza kukusogeza tu
ukatoka ulipokua umekwama lakini hauwezi kuishi kwayo.
Pasipo na imani ya kristo ndani yako , kuna hatari ya
mauti kukuzunguka pande zote kwasababu
tunaona namna ambavyo hamani hana msaada tena baada ya kuwa ameweka imani yake
kwa mfalme na mfalme huyohuyo hayuko upande wake tena.
UBABE WA IMANI
I.
Imani ikiwepo uwezo unakuja , unachipuka
, unatokeza
II.
Imani na uwezo vikiungana huleta matokeo
yafuatayo
a)
Nafasi ya mtu.ESTA 5:1-2
b)
Kiti cha mtu DANIEL 4: 34-37
Nebukadineza alipo jaa imani
Ghafula kutazama kwakwe kukawa juu na
fahamu zake zikamrudia na ufalme wake
ukathibitika tena baada ya kufukuzwa miaka saba katika ufalme au kiti chake cha
mamlaka.
III.
Imani isipokuwepo uwezo unapotea kama ifuatavyo
a)
Imani kuyeyuka MWANZO 18:12kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake akasema niwapo
mkongwe nitapata furaha na bwana wangu mzee?
b)
Imani ina poromoka MATHAYO 14:28-30Petro akajibu akasema, ikiwa ni wewe niamurunije kwako juu ya maji, 29 akasema njoo.petro akashuka chomboni akaenda kwa miguu juu ya maji ili kumwendea
Yesu.lakini alipouona upepo akaogopa akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema bwana niokoe……………
Watu wamekua mashabiki wa mambo ya imani lakini hawaamini
chochote, lolote kwa namna hii wamekua na imani yenye monekano wa kininja
kuonekana na kupotea .
Nami nataka nikwambie kuwa kama Yesu hasingelimsaidia
Petro,Petro angezama na angekufa na imani yake hiyo ndogo,SIKIA namaanisha hivi
kuna kiwango cha imani hakitoshi kabisa kukuvusha mahali haijalishi unamtegemea
Mungu kiasi gani,sote tunajua kuwa Petro alikuwa mwanafunzi wa Yesu na alikuwa
karibu naye wakati mwingi lakini kupitia upungufu wa imani yake , mauti ilikuwa
tayari kumbeba lakini asante YESU mwenye huruma alimsaidia wakati akizama,hivyo
ndivyo wakristo wengi leo wanaishi katika imani haba na kwakweli kuna mahali
wamevuka si kwasababu ya imani yao kubwa bali kwasababu yesu alikuwepo hapo
karibu na akawasaidia wasizame au kuanguka.
Huruhusiwi kuchukua chochote kwenye ufalme wa mungu bila
kuwa na fail la ushahidi ( na ushahidi ni imani nayo hutokana na neno la kristo WARUMI
10:17 basi imani chanzo chake nikusikia na kusikia huja kwa neno la kristo.
AINA MBILI ZA IMANI
1. IMANI YA KIMUNGU
Imani hii ni kuu kuliko imani zote ni ya kwanza na ya mwisho japo
zipo imani nyingi sana lakini nimeipa nafasi ya kwanza katika somoletu la leo.
MARKO 11:12-24
inatupa picha juu ya aina hii ya imani ya kimungu (………. hata asubui yake walipotoka bethania aliona njaa. Akaona
na kwambali mtini wenye majani akaenda ili labda aone kitu juu yake na alipo
ufikilia hakuona kitu ila majani,maana si wakati wa tini ,akajibu akauambia
tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia………)
msitari wa 19 unaanza kukufunulia kitu tulicho kisoma kwenye
mstari wa 14 ilikuonyesha tatizo la wanafunzi wa Yesu kuhusu imani ya kimungu
pasingekua na tatizo mstari wa 19 na kuendelea usingekua na maana.
………….na kulipokuwa jioni
alitoka mjini,na asubui walipokua wakipita Waliona ule mtini umenyauka toka shinani.
Petro akakumbuka habari
yake akamwambia Rabi tazama mti ulioulaani umeyeyuka.
Yesu akajibu akamwambia mwaminini Mungu.
Amini nawaambia yeyote atakaye uambia mlima
huu ng’oka ukatupwe baharini,wala asione shaka moyoni mwake ila aamini kwamba
hayo asemayo yametukia, yatakua yake.
Kwa sababu hiyo nawaambia
yeyote myaombayo mkisali aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakua yenu.
Jambo ni nalotaka tujifunze
hapa ni namna wanafunzi walivyokua na
uwezo mzuri wa kusikia kwa kristo katika mstari wa 14 najambo hili lilitosha
kuwafanya wawe na imani maana kutokana na ;
WARUMI 10:17 imani huja kwa
kusikia na kusikia huja kwa neno la
kristo, sasa wanafunzi walisikia kwa kristo na ikatosha kuwafanya wawe na
imani.
Bado walikua na tatizo la
imani unapo soma mstari wa 19-24 MARKO unaona walisikia lakini hawakuamini;
Mfano;
mtu mmoja mwigizaji alipiga kelele kwenye hotel moja akisema
ananjaa sana watu wenye nafasi za kuhudumu kwenye hoteli hiyo wakapakua chakula haraka na kwa ukarimu sana wakamkaribisha
chakula, chakushangaza akabaki amekitazama chakula tu.
Huku akisema ana njaa,(njaa inaogopa mtu anayekula)
Njaa haiogopi mtu mwenye chakula alafu hana uwezo wa kula.
Jambo la kuwa na chakula ni jingine na jambo la kula ni jingine
japo ni moja .
Ukiwa na imani alafu huiamini ni sawa na muigizaji ambaye anaigiza
lakini uhalisia wa maisha yake haufanani na kile anachokiigiza.
MFANO huu utakusaidia
kuelewa , tatizo la wanafunzi na tatizo lako na tatizo la wengine kuhusu imani
ya kimungu.
Tazama tena hapa;
MATHAYO 14:28-32
Petro akajibu akasema Bwana
ikiwa ni wewe niamuru nije kwako juu ya maji,
Akasema njoo.
petro,akashuka chomboni
,akaenda kwa miguu juu ya maji.
Ili kumwendea Yesu lakini
alipouona upepo akaogopa ,akaanza kuzama ,akapiga yowe akisema,Bwana niokoe,
Mara Yesu,akanyoosha mkono wake,akamshika akamwambia,ewe mwenye imani haba
mbona uliona shaka? Nao walipopanda chomboni upeo ulikoma .
CHANGAMOTO ZA IMANI HII
Pamoja na kuwa na mafanikio makubwa sana ya
imani ya ya kimungu kwa wenye nayo
ukabiliwa na changamoto ya watu kutomuelewa japokuwa wanasikia anachosema na kuona anachofanya,bado hawawezi
kuelewa
YOHANA
11:39-44
Yesu
akasema, liondoeni jiwe.martha dada yake Yule aliyefariki , akamwambia, Bwana
ananuka sasa , maana amekuwa maiti siku nne.Yesu akawaambia , mimi sikukuambia
yakwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?. Basi akaliondoa lile jiwe , Yesu akainua macho yake juu, akasema, baba,
nakushukuru kwakuwa umenisikia.Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuz
ote,lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya , ili wapate
kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.Naye akiisha kusema hayo,akalia kwa sauti
kuu, Lazaro njoo huku nje.Akatoka nje Yule aliyekufa,amefungwa sanda miguuni na
mikononi na uso wake amefungwa leso.naye Yesu akawaambia,mfungueni , mkamwache
aende zake.
IMANI YA KITHOMASO
Aina ya pili katika mpangilio wa somo hili
, imani hii inapatikana kwa watu wote wenye kuwaza kibinadamu,imani ya namna
hii haina uwezo wa kuamini mpaka ione, wakati imani ya kimungu inataka kuamini
kabla hujaona.
Nianze na aina ya mawazo ya kibinadamu
yanayodhibitisha imani ya kithomaso.
YOHANA
5:2-8
Inatosha kuichukua imani ya kristo na
kuiingiza katika mawzo ya kibinadamu,angalia
Yohana
5:2-8
Na
huko yerusalem penye mlango wa kondoo pana birika iitwayo kwa kiebrania bethzatha
nayo ina matao matano. ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala
, vipofu ,viwete nao waliopooza,(wakingoja maji yachemke.kwamaana kuna wakati ambapo malaika hushuka akaingia
katika ile birika akayatibua maji, Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji
kutibuliwa, akapona ugonjwa wake wote uliokuwa umempata.) na hapa palikuwa na
mtu ambaye amekuwa hawezi kwa muda wa miaka thelathini na minane.Yesu
alipomwona huyu amelala, naye akijua yakuwa amekuwa hali hiyo siku
nyingi, alimwambia wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu Bwana ,mimi sina
mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa ila ninapokuja mimi mtu mwingine
hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia,simama jitwike godoro lako
uende.
Tazama maandiko haya yanavyokutazamisha
shida ya imani ya kithomaso,imani ya mpaka uone,
Imani ya namna hii huwa inaongozwa na
mawazo ya kibinadamu,msitari wa 7 huu unadhihirisha ni jinsi gani mtu mwenye
imani hii anavyotegemea watu katika mahitaji yake na matatizo yake jambo ambalo
ni sawa na kuchuja mbu na kumeza ngamia au kujivunia makaburi yaliyopakwa
chokaa,nayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri bali ndani ni mifupa ya wafu na uchafu
wote.
Imani hii mungu hapendezwi nayo hata
kidogo.
kiu yake msalabani ni kuifunua imani yake
ya kweli katika maarifa ya kimbingu za kimbingu,tangu natangu,umilele wa umilele
na milele.
MADHARA YA IMANIYA KITHOMASO
Msitari
wa 7 unaonyesha laumu la mgonjwa kwa watu
ambao hawakumsaidia pia akaenda mbali akalaumu na wale waliokuwa wanamuwahi
kuingia birikani,
haya mawazo ya kibinadamu Yesu akayavunja
kwa nguvu ya agano ambaye ni yeye mwenyewe ambapo kwa asili ni mwenyezi,akasema
katika msitari wa 8..simama jitwike
godoro lako uende
YOHANA
20:26-29
Basi,
baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo ndani tena na thomaso pamoja nao , Akaja yesu
na milango imefungwa akasimama katikati akasema,amani iwe kwenu. kasha
akmwambia thomaso leta hapa kidole chako uitazame mikono yangu,ulete na mkono
wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini bali aaminiye,thomaso
akajibu akamwambia , Bwana wangu na Mungu wangu ,
yesu
akamwambia, wewe, kwakuwa umeniona umesadiki,wa heri wale wasioona , wakasadiki.
Msitari huu wa 29 unatosha kukuondoa kwenye
imani ya kithomaso ,Mwenyezi anapenda imani inayoonekana kabla ya vitu halisi.
Niliamini kuyaandika haya kabla sijajua
nitaandikaje , lini , wapi , na muda gani.
Ø
Ibrahimu aliamini kupata mtoto kabla ya kuona katika
mwili.
Ø
Daniel alimwamini Mungu kabla ya kujua kama
samba watamla au la.
Ø
Meshaki ,shedraka na Abednego walimwamini Mungu kabla hawajajua kama atakuja awe nao kwenye
tanuru la moto.
Ø
hatahivyo nilimwamini mungu wakati watu wawili
waliponichukua na kuniingiza kwenye chumba cha ndani alafu wakavua nguo
zao zote alafu wakajikata na kiwembe
baadhi ya maeneo ya miili yao na wakachukua nguo mpya walizokuwanazo
wakajifutia damu iliyowatoka alafu wote kwa pamoja wakaililia miungu yao na
kuishirikisha jambo hilo alafu wakanilazimisha nguo hiyo niivae kwa nguvu kisha
wakaniacha nitoke kwenye chumba hicho wakidhani wamefanikisha mambo yao,katika
neno la bwana wote walishakufa kwa namna tofautitofauti ,wameacha familia zao
katika halia ya ukiwa sawa na mathayo
23:37-39
Ee Yerusalemu,yerusalemu uwauaye manabii na
kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya
pamoja kwako watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake
chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka.angalieni nyumba yenu mmeachiwa hali ya
ukiwa.
kwa
maana nawambia hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema amebarikiwa ajaye
kwa jina la Bwana.
AINA NNE ZA IMANI YA KIMUNGU
1.IMANI
NDOGO
Hii ni aina ya imani ya kwanza katika
mpangilio wa somo hili.
Sifa za imani ndogo ni kuanzisha jambo
lakini kushindwa kulimalizia.
Dalili za imani ndogo ni hofu,wasiwasi na
mashaka (upungufu wa neno la Mungu
rohoni)
Tazama mathayo
8:23-26
Akapanda
chomboni wanafunzi wake wakamfuata,kukawa msukosuko mkuu baharini hata chombo
kikafunikizwa na mawimbi,naye alikuwa amelala usingizi.
Wanafunzi
wake wakamwendea wakamwamsha,wakisema,Bwana tuokoe tunaangamia.
Akawaambia,mbona
mmekuwa waoga,enyi wa imani haba?mara akaondoka akazikemea pepo na bahari,
kukawa shwari kuu.
JINSI YA KUVUKA KUTOKA KWENYE IMANI NDOGO
Ni kuikuza imani yako kwa kuipandisha imani hata
imani.
Warumi
10:17 “basi imani chanzo chake ni kusikia,na kusikia huja kwa neno la Kristo.”
Imani ina tabia ya kukua kutokana na
kiwango chako cha kuingiza neno la
kristo ndani yako.
2.IMANI
KUBWA
Hii ni imani ya pili katika mpangilio wa somo
hili
Imani hii ni kubwa na ni wachache wenye
uwezo wa kuwa nayo.
Luka
7:2-10
“Na
mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa,naye ni mtu aliyempenda
sana.
Aliposikia
habari za Yesu , alituma wazee wa wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa
wake.
Nao
walipofika kwa Yesu walimsihi sana wakisema,amesitahiri huyu umtendee neno hili
.
maana
analipenda taifa letu naye alitujengea sinagogi.
Basi
yesu akaenda pamoja nao hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, Yule akida
alituma rafiki kwake, akamwambia Bwana usijisumbue maana mimi sisitahiri wewe
uingie chini ya dari yangu.
kwahiyo
nilijiona sisitahli mimi mwenyewe kuja kwako , lakini sema neno moja tu na
mtumwa wangu atapona.
kwa
maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini
yangu,nikimwambia huyu nenda uhenda na huyu njoo huja na mtumwa wangu ,fanya
hivi hufanya.
Yesu
aliposikia hayo alimsitaajabia akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata
akasema,namwaambia hata katika Israel sijaona imani kubwa namna hii.
Na
wale waliotumwa waliporudi nyumbani wakamkuta Yule mtumwa ni mzima.”
Imani ya namna hii hutengeneza njia na
kupita yenyewe pasipo kukwama.
Imani kubwa hufanya vyote kama unavyotaka,
haizuiliwi na vizuizi vya aina yoyote katika
ulimwengu wa mwili .
3.IMANI
DHAIFU
Imani ya aina hii huleta tabia ya kusitasita.
Pia huweza kuzuiliwa kwa urahisi na
itaridhia (ina maamuzi finyu)
Inatokana na watu ambao hawajifunzi utauwa kama Timotheo (jizoesheni utauwa)
Alivyoambiwa na Paulo warumi
4:17-22
“(Kama
ilivyoandikwa nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) , mbele zake yeye aliye
mwamini yaani Mungu mwenye kuwahuisha
wafu,ayatajaye yale yasiyokuwako kana
kwamba wamekuwako.
Naye
aliamini kwa kutarajia yasiyowezakutarajiwa
ilia pate kuwa baba wa mataifa mengi kama ilivyonenwa ndivyo utakavyokuwa uzao
wako.
Yeye
asiyekuwa dhaifu wa imani,alifikiri hali
ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa,
( akiwa amekwisha kupata umri kama miaka
mia) na hali ya kufa ya tumbo lake sara.
Lakini
ukiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini bali alitiwa nguvu kwa imani
akimtukuza Mungu.
Huku
akijua hakika yakuwa Mungu aweza kufanya
yale aliyohaidi , kwahiyo akihesabiwa kwake kuwa ni haki.”
·
Imani dhaifu ni ile ambayo haioni ngambo ya matatizo kuna ushindi, wala haina uhakika wa
kutoka ilipokwama ( ni hatari sana kua
na imani dhaifu).
·
Ibrahim pamoja na kuwa na udhifu wa kuzeeka
hakuruhusu imani yake kuwa dhaifu.
4.IMANI
YENYE NGUVU
Imani hii ni ya nne katika mpangilio wa somo
hili niya mwisho kwa mtiriko huu wa somo mpaka hapo Mungu atakaponipa kibali
tena cha kuendelea na somo hili .
Imani hii huja kwa mtu kwa njia ya kuifanyia
mazoezi.
kuikaza imani hata imani
Imani ya namna hii ina tabia ya kufanya mambo
ambayo yakisikiwa na watu masikio yanawasha.(mambo makuu,mambo yasiyotegemewa)
Imani yenye nguvu huanzia moyoni kwa nguvu ,hutokeza bila
mpinzani, na hugusa mioyo watu.
Warumi
4:20
“Lakini
akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini,bali alitiwa nguvu kwa imani
akimtukuza Mungu.”
Tazama pia katikaMatendo ya mitume 3:1-8
“Basi
petro na yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni saa ya kusali saa tisa.
Na
mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu abaye
walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa
watu waingiao ndani ya hekalu.
Mtu
huyu akiwaona petro na yohana wakiingia
hekaluni wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka,
Na
petro akimkazia macho, pamoja na yohana akasema ,tutazame sisi.
Akawaangalia
akitarajia apate kitu kwao,
lakini
petro akasema mimi sina fedha wala dhahabu
lakini nilichonacho ndicho nikupacho.kwa jina layesu kristo wa Nazareti,simama
uende.
Akamshika
mkono wa kuume akamwinua mara nyayo zake
na vifundo vyake vya miguu yake vikatiwa nguvu.
Akaondoka
upesi akasiimama akaanza kwenda akaingua ndani ya hekalu pamoja nao,akienda
akiruka-ruka na kumsifu Mungu .”
Nilitaka uone imani yenye nguvu inavyoanzia
moyoni kwa nguvu na kutokeza bila upinzani na inafanya kazi kubwa kwa matokeo
toshelevu.
Mtu mwenye imani ya namna hii ana uwezo wa
kutawala kila kitu duniani na kufanya anavyotaka sawa na mapenzi ya Mungu;
§
Angalia Eliya alifunga mvua hisinyeshe
miaka mitatu na nusu.1wafalme 17:1
§
Angalia Musa alipasua bahari ya shamu.Kutoka 14:21-22
§
AngaliaDaudi alimuangusha goriathi. 1samweli 17:45-50
§
Angalia yoshua kwenye ukuta wa yeriko. Yoshua 6:1-20
§
Angalia Danieli kwa wale simba. Danieli 6:22
Naomba unisikilize nakukumbusha tu;
§
Esta kwa mfalme ahasuero na Mordekai kwaHamani. Esta 5:1-8:17
§
Yesu pale kisimani alipokutana na mwanamke wa
samaria. Yohana 4:1-42
§
Ayubu alivyokutana na mgonjwa .Ayubu 42:7-12
§
Medadi na elidadi katika wakati wa musa.Hesabu 11:26
§
Isaka alipochimba kisima akakiita rehobothi. Mwanzo 26:17-22
§
Korinelio alipotoa sadaka. Matendo ya mitume 10:31
§
Yohana alipotupwa katika kisiwa cha patmo.Ufunuo wa Yohana 1:9
§
Mimi binafsi nilipogongwa na magari mawili kwa
wakati mmoja.
§
Mtoto aliporuka tumboni mwa elizabethi baada ya
kukutana na Mariam.Luka 1:41
§
Wanafunzi wa yesu walipomsubiri roho mtakatifu.Matendo ya mitume 2:1-4
NB mungu huwa anatembea pasipo kujizuia
akishaona mtu ana imani yenye nguvu.
JINSI YA KUIFANYA IMANI YAKO IFANYE KAZI
Zipo kanuni baadhi nilizokuandikia kwenye somo
hili ila sina maana ya kwamba ndo ukomo wa kanuni hizi.Tutaendelea kujifunza
kadri Roho mtakatifu atakavyokuwa akizidi kutufundisha katika mwendelezo wa somo
hili.
Kabla ya kanuni hizi kuna maandalizi pia ya
kufanya Kwa muhusika Kama ifuatavyo;
Waefeso
6:16-18
Zaidi
ya yote mkitwaa ngao ya imani ambayo Kwa hiyo mtaweza kuizima mishale ya Yule
mwovu.
Tena ipokeeni chapoe ya wokovu Na upanga wa roho
ambao Ni neno la mungu.
Kwa
sala zote Na maombi, mkisali kila wakati katika roho, mkikesha kwa jambo hilo
na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.
1YOHANA
5:4-12
Kwa
maana kila kitu kilichozaliwa Na mungu huushinda ulimwengu Na huku ndio
kushinda kushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.mwenye kuushinda ulimwengu Ni
nani Isipokuwa ni yeye aaminiye kuwa Yesu ni mwana wa Mungu?huyu ndiye
aliyekuja kwa maji na damu ,Yesu kristo si katika maji tu bali katika maji na
katika damu, naye roho ndiye ashuudiaye kwasababu roho ndiye kweli,
kwa
maana wako watatu washuhudiao mbinguni baba
neno na roho mtakatifu na watatu hawa ni
umoja. kisha wako watatu washuhudiao dunia .
Roho
wa maji na damu na watatu hawa hupatana kwa habari moja. tukiupokea ushuhuda wa
wanadamu,ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi,kwa maana ushuhuda wa mungu ndio huu ,
kwamba ameshuhudia mwanawe.
yeye
amwaminiye ,mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake.asiyemwamini mungu amemfanya
kuwa mwogo kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu ameshashuhudia Mwanawe.
Na
huo ndio ushuhuda ya kwamba ,Mungu alitupa uzima wa milele,uzima huu umo katika
mwanawe,
yeye
aliye mwana, ano huo uzima asiye naye mwana wa Mungu hana huo uzima.
Waebrania
11:8-10
Kwa
imani ibrahimu alipoitwa aliittika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa
urithi,akatoka asijue aendako ,
kwa
imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi,kama katika nchi isiyo yake
akikaa katika hema pamoja na isaka na yakobo warithi pamoja naye wa ahadi
ileile.
Maana alikuwa akiutazamaia mji wenye misingi
ambao wenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
Mistari hii kwa namna ilivyo inatosha kwa
sehemu kukuandaa vizuri katika kuingia kwenye kanuni za imani katika kufanya
kazi.
Nimetumia neno SEHEMU , kwasababu najua
kuna nafasi ya roho mtakatifu pia kumuandaa mtu kwenda kwenye kuamini.
KANUNI TATU ZA IMANI KUFANYA KAZI
Hizi ni baadhi ya kanuni zilizopo kwenye mfululizo
wa somo hili japo Mungu atakaponipa kbali cha kuendelea nitafanya hivyo sawa na
mapenzi yake.
1.IMANI
ILETAYO MATOKEO
v
Ni lazima ianzie moyoni (chanzo kizuri cha maandalizi ya imani yako ni moyoni)
Warumi
10:10-11
Kwa
maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata
wokovu,
kwa
maana andiko lanena kila amwaminiye hatatahayarika.
Baada ya kuwa na imani ya namna hii tu moyoni
,hapo ndipo ulimwengu wa roho
hukuhesabia haki na ukihesabiwa haki panakuwa na uhalali wa jambo lolote
lililokusudiwa kudhihirishwa kwenye ulimwengu wa mwili na pasipo kuzuiliwa.
2.IMANI YA
KUKIRI KINYWANI MWAKO
Imani ya kukiri kutoka kinywani mwako yale
ambayo moyo wako umeamini (moyo na mdomo
viende pamoja)
Mdomo ni kiungo muhimu sana katika
ulimwengu wa roho
mfano;
mchawi hawezi kufanya chochote bila kutamka .
v
Musa alilazimika ayatamke mapigo ya farao kabla
hayajadhihirishwa mwilini
mwanzo
1:3-31
Mistari yote hii utakuta Mungu kasema ,
mungu akasema tazama tumeumbwa kwa mfano
wake, kama yeye alisema nasi inatupasa
kutamka kwa imani (tazama pia marko
11:23) Yesu anawafundisha wanafunzi wake jinsi imaniinavyotaka mtu aseme
anachoamini moyoni ili kitendeke.
3.KUSIKILIZA
NENO LA
MUNGU
Hii ni kanuni ya mwisho katika somo hili,
ili upate la kusema kinywani mwako, ili ukasikilize akishakusikilizisha
anayathibitisha au anayafanya yatokee , sisi ni mfano wa mungu kama mwezi
ulivyo mfano wa jua.Mwezi unaakisi jua ili upate mwanga wa kutoa .
Mungu hatimizi neno la mtu yeyote bali
anatimiza neno lake, wala imani haitokani na neno la kibinadamu
bali inatokana na neno la kristo.
kwahiyo uwe na uhakika ukitaka imani yako
ifanye kazi muda wote kwa nyakati zote utamke au useme kinywani mwako neno la Mungu yaani kristo
yesu kuhusu kitu unachokitaka kiwepo , kije , kitokee, kiumbike AU kipone.
Unapotaka
kusema chochote kwa imani hakikisha
una neno la kristo la kutosha ndani
yako.
Yohana
1:1-3
Hapo
mwanzo kulikuwapo neno, naye neno alikuwako kwa mungu,naye neno alikuwa Mungu.huyo
mwanzo alikuwako kwa mungu,vyote vilifanyika kwa huyo ,wala pasipo yeye hakikufanyika
chochote kilichonyika.
Yupo pia malaika ambaye huwa anasikiliza
tunachotamka alafu anayapa nguvu na kuyatimiza tuyanenayo;
Muhubiri
5:5-6
Ni
afadhali husiweke nadhiri kuliko kuiwekausiondoe,usikiache kinywa chako kuukosesha
mwili wako wala husiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa,kwani
Mungu akukasirikiaye sauti yako na kuiharibu kazi ya mikono yako?
Yakobo
3:2
Maana
twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi,Mtu asiyejikwaa katika kunena mtu
huyo ni mkamilifu,awezaye kuuzuia na mwili
wake wote kamalijamu.
Mithali
18:21
Mauti
na uzima huwa katika uweza wa ulimi na wao waupendao watakula matunda yake.
Nilikuwa najaribu kukutazamisha mistari hii
ujue madhara ya kutamka pasipo kujua umesema katika imani ya Neno la kristo au
umetamka nje ya imani hii.(kutamka
huleta matokeo ya imani)
Nashukuru kwa kuwa umechukua muda wako kusoma
na kutafakari somo hili,Mungu wangu katika Kristo Yesu akubariki sana .
Naomba maombi yako sasa ili wakati mwingine
nije na ujumbe mzuri utakaoendelea
kufanyika nuru na msaada kwetu katika Kristo Yesu.
Ameni
ISAYA
55:11
Ndivyo
litakavyokuwa neno langu litokalo katika kinywa changu,halitanirudia bure bali
litatimiza mapenzi yangu nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Somo hili tumeliombea vya kutosha ili
lifanyike Baraka katika maisha yako na kupitia somo hili Mungu apate kukuvusha
mahali ulipokuwa umekwama kiimani na tangu sasa ukaanze kuona nguvu mpya za
kiimani zikiongezeka ndani yako na mpenyo ukitokeza juu ya maisha yako.
NEEMA NA USHIRIKA WA MUNGU BABA VIKAWE PAMOJA NAWE
Kwa Msaada Ushauri Na Maombezi
Tafadhali Wasiliana Nasi walimu Wa Neno
La Mungu;
Mwl: AZORI MICHAEL +255767 155 623 (PIGA)
NA
Mwl: JOSHUA +255620 179 783 ( SMS)
“MUNGU WANGU AKUBARIKI NA
KUKUTENDEA MEMA”
0 Comments