100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

ASILI YA ROHO

ASILI YA ROHO


YOHANA 14:17
'ndiye roho wa kweli,ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea,kwakuwa haumwoni wala haumtambui,bali ninyi mnamtambua maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu."
 Si jambo la muhimu kwetu kuweza kumfasili Roho Mtakatifu. Kristo anatuambia kuwa Roho na Mfariji, “ huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba.” Imeelezwa bayana juu ya Roho Mtakatifu kwamba, katika kazi yake ya kuwaongoza wanadamu katika kweli yote, “hatanena kwa shauri lake mwenyewe” (Yohana 15:26; 16:13).
 Jinsi alivyo Roho Mtakatifu ni Siri. Wanadamu hawawezi kuieleza, kwa vile Bwana hajaifunua kwao. Wanadamu wenye mitazamo ya ajabu waweza kuunganisha aya za Maandiko na kuyawekea mtazamo wa kibinadamu, lakini kukubalika kwa mitazamo hii hakutaliimarisha kanisa. Kuhusiana na siri za namna hiyo, ambazo ni ndani mno kiasi cha kutoeleweka kwa mwanadamu, ni bora kunyamaza.
 Ofisi ya Roho Mtakatifu imebainishwa katika maneno ya Kristo: “Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” (Yohana 16:8). Ni Roho Mtakatifu anayesadikisha kwa habari ya dhambi. Ikiwa mdhambi ataitikia mvuto uhuishao wa Roho, atawezeshwa kutubu na kuamshwa juu ya umuhimu wa kutii matakwa ya Mungu.
 Kwa mdhambi aliyetubu, mwenye njaa na kiu ya haki, Roho Mtakatifu hufunua Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu. “Kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari,” alisema Kristo. “atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 16:14; 14:26).
Roho ametolewa kama wakala wa wongofu, kufanikisha wokovu uliopatikana kutokana na kifo cha mkombozi. Daima Roho anatenda kazi kuelekeza fikra za mwanadamu kwa kafara kubwa iliyofanyika katika msalaba wa Kalvari, kuufunulia ulimwengu upendo wa Mungu, na kuzifunulia roho zilizosadikishwa mambo ya thamani ya Maandiko. 
BARAKA ZA BWANA ZIAMBATANE NAWE

Post a Comment

0 Comments