100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

NGUVU YA MSAMAHA/HURUMA YA MUNGU

NGUVU YA MSAMAHA/HURUMA YA MUNGU


1. Zaburi 130:3
• BWANA, kama wewe ungehesabu maovu, Ee BWANA nani angesimama?
• Hii inatuoyesha kuwa ili mtu kuweza kusimama ni kwa rehema ya Mungu Mungu anapotusamehe ndipo tunapata nguvu ya kuendelea mbele zaidi, maana katika Msamaha wake kuna amani, upendo na kuhuishwa ama utukufu ambao hutusaidia kumuona BWANA. Na tena kwa uwepo wake huo kupitia msamaha hupata Nguvu za rohoni na hata kujiamini katika programu zetu na mipango yetu maaana twajua BWANA AKIWA UPANDE WETU NI NANI ALIYE JUU YETU?
2. ISAYA 16:5
• “Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema…”
• kiti cha nenzi chonyesha ni utawala ama mamlaka mbalimbali maeneo mbalimbali…
• Hivyo ili kuweza kuimarisha hicho kiti… ama kuweza kumuona BWANA akifanya mambo makubwa katikati ya watu lazima kuomba rehema kwa ajili ya mahali hapo. Maana kama twataka ufalme wa Mungu uonekane lazima na hatuna budi kuomba rehema kwa ajili ya wenye mamlaka na hata viti tulivyokalia. Iwe na kwa familia, shule, kazi, nchi, kanisa ama huduma yoyote ile itaimarishwa kwa rehema.
3. 2NYAKATI 7:14-15
• “Ikiwa watu wangu walioitwa kwa Jina langu watajinyenyekesha na kuomba, na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya, basi nitasikia kutoka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.”
• Tunapoomba toba kwa Mungu kwa msamaha huo, nchi hukombolewa na hata sisi Mungu hutusitawisha kwa msamaha huo.
4. MATHAYO 12:7
• “Laiti Mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema wala si sadaka…”
• Yamkini twaamini kuwa sadaka yaweza tenda mambo mengi sana na hata NENO la Mungu latushudia katika hayo lakini kumbe Mungu kitu anataka zaidi ni REHEMA
• Hivyo pamoja na yote hata kama una sadaka tafuta kwanza rehema ya Mungu ndipo umtolee sadaka safi isiyokuwa na MAWAA
• Kwa lugha nyingine ni kwamba REHEMA ZA MUNGU ni foundation ya
maombi na haja zetu zote.
5. ISAYA 1:16-20
• Haijalishi ni uovu wa aina gani ambao umefanyika bali Mungu anatuita kwa kiti cha rehema na kuomba Toba, na kutuhakikishia kuwa hata ingekuwa dhambi mbaya kiasi gani lakini Mungu anatusamehe hata kwa hizo.
• Na tunapotubu toba yetu iwe ya kweli yenye nia ya kujitakasa, na kuacha lutenda mabaya.
• Hivyo katika kila ombi ni vyema na kuanza na toba kabla ya kwenda kwenye hitaji la msingi.
• Yamkini tuna maombi yetu mbalimbali kama familia, kazi ,shule, mafanikio, afya, nchi , kanisa, amani etc lazima na ni muhimu kuanza na Toba.
• Unapoomba rehema simama na kuomba rehema si kwa ajili yako tu bali kwa watu wote unaowaombea kama vile mf : unapoomba rehema ya nchi pia omba rehema kwa ajili ya rais, serikali, wananchi wa nchi hiyo na hata ardhi yake pia. Unapoomba rehema ya familia omba rehema kwa ajili ya wazazi, watoto, mahali pale (ardhi), nyumba ile etc.
6. HITIMISHO
• WARUMI 6:1.
• Mpendwa kumbuka REHEMA hii ni NEEMA tu. Wala HATUKUSTAHILI. USIICHEZEE.
• Na kwa rehema hii sio maana ya kufuta uovu na kuurudia tena ama njia tu ya kupatia mahitaji bali tena na tena, bali tuone kuwa NEEMA ITUONGOZAYO KATIKA KUTUWEKA KARIBU ZAIDI NA MUNGU WETU.

Post a Comment

3 Comments