100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

TOFAUTI YA KUSAMEHE NA KUPUUZA

TOFAUTI YA KUSAMEHE NA KUPUUZIA



Mathayo 6:14 "Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi."
 
Nimeona shida hii hasa kwa watu walioko makanisani naweza kusema Wakristo ambao wanajua suala la kusamehe ni la lazima.
Ambao wanajua kisasi ni juu ya BWANA na hawapaswi kuweka kinyongo kulingana na maekezo ya maandiko. Kutokana na hayo wengi niliowahudumia binafsi nimegundua shida kubwa ni kutojua tofauti ya kusamehe na kupuuzia.
Hivi vitu vinafanana kwa sehemu, unaweza kudhani kuwa umesamehe na kumbe umepuuzia tu au umeachilia tu maisha ya endelee.
Kupuuzia ni rahisi sana kizungu wanaita "Ignoring" unapopuuza ni kwamba hujali tena kitu au hujishughulishi tena na mtu, unaamua kushika mambo yako.
Lakini hiyo haimaanishi kuwa umesamehe. Unaweza kuacha kuongelea kitu na bado kikabaki kinakutafuna ndani ingawa nje unaonekana mwenye furaha na maisha yanaendelea.
 
 
UNAJUAJE KUWA HAUJASAMEHE BALI UMEPUUZA.
Msamaha ni kitu cha kimungu, na msamaha unapoachiliwa hufuta hatia yote. Huponya moyo na kuondoa kila shina la uchungu ndani. Zaburi inatuonesha
Zaburi 103:12 "Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi."
Mungu akikusamehe anakuchukulia kama hujawahi kukosea na mnaishi kama wewe ni mtu mpya. Unakuwa kama umezaliwa Leo.
Msamaha haukumbushii yaliyopita wala kuweka kumbukumbu ili kutoumizwa tena mtu uliyemsamehe.
Msamaha wa kweli hubadilisha historia.
Lakini kupuuzia kunakupa amani ya muda tu. Kupuuzia kunakufanya ujipe moyo, ujikung'ute mavumbi na kusonga mbele lakini bado hilo jambo linakutafuna ndani. Mtu aliyepuuzia kitu anaweza kuendelea na maisha yake kawaida lakini uchungu bado upo.   Lakini kwa sababu amepuuzia hataweza kujua kama kinachomsumbua ni uchungu. Adui ni mjanja hakupi nafasi ya kuona kama una uchungu ndani.
Lakini Leo macho yako ya rohoni yatafumbuka kupitia somo hili.
 
 
DALILI ZA MTU ALIYEPUUZA NA KUDHANI AMESAMEHE.
1. KULIPUKA/UKALI
Kutokana na moyo kuwa umebeba kitu ambacho hakijashughulikiwa kikaisha uwezo wa kubeba mengine huwa unakuwa haupo.
Kwa hivyo inapotekea ametendewa jambo lolote la kuchukiza huwa hawezi kuvumilia na ndio kinachopelekea kulipuka. Hasa akitendewa kosa na mtu aliyemuudhi na hajasamehe ndani inakuwa kama ametonesha kidonda cha moyoni, ndipo unashangaa ugomvi unakuwa mkubwa kuliko kosa.
 
 
2. HASIRA ZA KARIBU.
Hata jambo dogo linaweza kumtibua na kufanya tukio mpaka kila mtu akashika mdomo. Yote ni sababu ya uchungu wa ndani ambao mbaya zaidi anakuwa hata hajui kwanini anahasira za haraka, kwani kinachomuumiza anadhani alishakisamehe kumbe kakipuuza.
kuna watu huwa wananiambia
Mtumishi wa Mungu
Najisikia hasira sana na sijui ni nini
Hiyo kuna jambo lipo ndani yako hsukusamehe bali ulipuuzia tu ili lipite kwa wakati fulani
 
 
3. MAAMUZI YA KUKURUPUKA.
Mara nyingi moyo unapokuwa hauna amani mtu huwa haoni thamani katika chochote kile, anaweza kuacha kazi bila hata kufikiria mbele. Anaweza kuvunja mahusiano kwa sababu ambayo hata mtoto mdogo akiambiwa anaona sio hekima.
Mfano ukichelewa kupokea simu inaweza ikawa sababu ya kuachana.
Yote hii ni uchungu ndani ambao haujashughulikiwa. 
 
 
4. KUTOJALI KUPOTEZA
Uchungu huwa unafanya uone watu wote wabaya tu na hawaaminiki ,
hauoni mtu wa kuamini,
na hakuna unayemjali sana, hivyo  hata wakiondoka wote maishani mwako unajiona wewe ni jeshi kubwa,
Kumbe ni uchungu tu unakusumbua. Unaweza kufuta namba zote kwenye simu ukaacha za wazazi wako tu na huogopi kukorofishana na mtu yeyote, unasema nilizaliwa peke yangu,,
Hizo ni dalili kuwa una  uchungu.
 
 
5. KUJIHAMI (DEFENSIVE)
Hii pia ni dalili ya mtu aliyeumia ndani,
Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu wa jinsi hii kitu kidogo tu anakuambia "Me naona tuachane tu ili usije kunisumbua huko mbele". Yaani mnaishi maisha ya kujihami sana, kila saa anahisi utamuumiza.
Unaulizwa kama unampenda kweli. 
 
 
6. KUONGELEA KOSA LILILOPITA MARA KWA MARA
Utaona mtu kila baada ya siku kadhaa anakumbushia tukio lililopita ambalo anasema ameachilia limepita, atakwambia anazungumzia lisijekutokea tena. Lakini unaweza kuhisi uchungu kwenye sauti yake au macho yake anapozungumzia hilo tukio. Maneno au maandishi yake yanakuonesha hali ya moyo. 
 
 
7. KUJIHISI KUONEWA
Mtu anaona mambo mengi mnayofanya na maamuzi yanayochukuliwa sio fair kwake. Anaona kama hamumtendei haki hata kama kinachofanyika kwake kimefanya kwa wote.
 
 
8. KUTORIDHIKA
Hii pia ni moja ya dalili kwa sababu moyo kuna kitu unakosa na hauko kawaida sio rahisi kuridhika au kufurahia maisha sababu ndani hauko sawa. Unaweza kupata ulichokuwa unatamani na baada ya kukipata bado ukawa huna raha, na unakuwa confused kwa sababu huelewi nini kinachokusumbua.
 
 
9. MACHOZI au KULIALIA
Hili hasa ni kwa wanawake, machozi yanakuwa karibu au kuna wakati unajiskia kulia na hujui hata sababu ni nini.

YAWEZEKANA WEWE IMEWAHI KUKUTOKEA
NA NIMEPIGIWA SIMU NA WAPENDWA WENGI TU
WANANIAMBIA
MTUMISHI NAJISIKIA KULIA KWA SAUTI AU NIPIGE KELELE TU
Nimeeleza huko juu kuwa kitu kinachokuumiza wewe umejiaminisha kuwa umesamehe na kumbe umepuuza. Sasa unapoumia na kusikia kulia ni ngumu kujua sababu.
 
 
10. KUKOSEA MARA KWA MARA
Uchungu unaweza kukufanya ukawa unakosea sana. Kwa sababu kichwa hakikosawa utajikuta vitu vingi hufanyi kwa usahihi. Ukishika gari utagonga, ukipika utaunguza, ukiandika unaweza kufuta kila baada mistari kadhaa, usahihi wa utendaji wako hauwi kwa viwango kwani moyo una shida.
Hizi ni baadhi tu ya dalili za mtu mwenye uchungu ndani kwa sababu ya kutosamehe.
Msamaha wa kweli unapoachiliwa hata kosa linaporudiwa uchungu unakuwa mpya, sio uchungu mara mbili. Eti unakumbusha yote yaliyopita, huo sio msamaha wa kweli. Muombe Mungu akupe Neema ya kusamehe.
 
 
1. JUA KWAMBA MAKOSA WAMEUMBIWA BINADAMU.
Hata wewe umewahi kukosea na umeomba Mungu akusamehe, so kukosea ni sehemu ya maisha na kila mtu anahaki ya kusamehewa.
 
 
2. USILIKUZE KOSA KULIKO INAVYOPASA
Unaanza kusema "kwanini anifanyie hivi" ndio ameshafanya sasa, huwezi kubadilisha kilichotokea. Ona ni kosa na linaweza kusameheka na maisha yakaendelea. Ila usilipe upekee mbali na makosa mengine.
 
 
3. MSAMAHA NI KWA FAIDA YAKO
Kumbeba mtu moyoni ni sawa na kunywa sumu huku ukitegemea mwenzako ndio afe. Achilia, shughulikia Mpaka ukilikumbuka husikii uchungu kabisa. Unaruhusiwa kulia, kuhamaki, (Efeso 4:26) Lakini huruhusiwi kutenda dhambi kwa sababu ya hasira. Kulipa kisasi au kupanga kisasi ni dhambi. Samehe ili uwe huru na uone raha ya maisha
 
 
4. TANGAZA MSAMAHA.
Kama unaweza mfikie aliyekuumiza aidha kwa simu, kwa email, face to face ikiwezekana na tangaza msamaha. Najua ni ngumu lakini ndio uponyaji wenyewe. Yesu anaonya kuwa tusiposamehe watu makosa yao hata sisi Mungu hatotusamehe.
Ikiwezekana hata kesi futa na uache Mungu ashughulikie.
Sio kila kitu lazima utetee haki yako. (Amani ya Kristo iamue moyoni mwako) Maana hata mtu akifungwa hairudishi hali kuwa kama mwanzo.
Amua kumuacha Mungu ajitukuze kupitia hali yako.
Haki ni mbinguni tu,duniani inaweza kuwa Haki yako lakini haujui kujieleza au haujui sheria na haki yako akapewa mwingine
Lakini kwa Mungu hata usipojitetea 
 

HAKI YAKO IPO
Wakati Stefano anapigwa mawe bila kosa, kabla hajafa alitangaza msamaha na kupitia huo msamaha Mungu alimuokoa Sauli na kumgeuza kuwa Mtume Paulo.
Huwezi kujua msamaha wako unaweza kufanya nini kwa maisha ya mtu.
Unaweza pia kutafuta Msaada zaidi kwa kuzungumza na mshauri au Mchungaji na kuomba naye ili Mungu akuwezeshe kuachilia na uishi maisha ya uhuru.
 
USIPUUZE_BALI_SAMEHE
Mungu Mwenyezi Atusaidie .

Post a Comment

0 Comments