100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

WEKA NENO LA MUNGU MOYONI MWAKO UTASHINDA

 WEKA NENO LA MUNGU MOYONI MWAKO UTASHINDA

            
Tuanze Ujumbe wetu wapendwa kwa Kusoma:
                    MATHAYO  4:1-10
Kisha Yesu alipandishwa na  Roho Nyikani ,ili  ajaribiwe na  Ibilisi.
  Akafunga  siku arobaini mchana na  usiku, mwisho akaona njaa.
  Mjaribu Akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe Haya yawe mikate.
Naye akajibu Akasema, Imeandikwa Mtu hataishi Kwa mkate tu, ila Kwa Kila neno litokalo Katika kinywa cha Mungu.
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji Mtakatifu, Akamweka juu ya kinara cha Hekalu,
Akamwambia ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu,jitupe chini Kwa maana Imeandikwa,
Atakuagizia malaika zake ; Na Mikononi mwao watakuchukua ; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Yesu akamwambia, Tena Imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
Akamwambia, Haya yote Nitakupa, ukianguka kunisujudia.
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, shetani ; Kwa maana Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, Umwabudu yeye peke yake. 
 
 
Mpendwa msomaji wangu, Tunaona hapa Ya Kwamba Shetani anayajua maandiko Na Bwana Yesu Kristo anatumia Neno kumpinga shetani hoja zake.
-Lakini Ujuzi wa Shetani wa maandiko Ni Kwa ajili ya Kuwapotosha watu juu ya imani yao  Kwa Mungu.
-Hivi ndivyo Shetani anawadanganya watu wengi leo, anawatamanisha  Kwa mambo Na vitu vizuri lakini lengo Ni Kwa ajili ya kumfanya Mtu amwache Mungu.
-Kutokana wengi wetu Wakristo Leo hatupendi kabisa kusoma neno la Mungu, hivyo tunajikuta lile neno halimo ndani  ya mioyo ya walio wengi, hivyo wanajikuta wamedanganywa Na Shetani.
Sikiliza nikuambie mpendwa wangu,, Shetani haogopi cheo chako, wala haogopi uwingi wa Mali zako, Wala haogopi  unafunga  mara nyingi Kwa mwezi, au eti unafunga sana Hapana mpendwa ; wala Shetani hakuogopi kwasababu unatoa sadaka Kila mara....
-Naomba nikuambie  Laiti anamuogopa Mtu kwasababu ya kufunga Kwake, Basi asingemsogelea Bwana Yesu Kristo ; Lakini mpendwa  Shetani Anamuogopa Mtu Yule aliyelijaza  Neno la Mungu ndani ya moyo wake na  kuliishi lile neno, huyo ndiye Shetani humuogopa.
-Hivyo mpendwa Kama unaomba Sana, unafunga Kila siku, Unatoa sadaka zako Sawa, Nakuambia  Kama huna Neno ndani yako Shetani  atakufuata Na kukupoteza kabisa.
√ Shetani alitumia Neno Imeandikwa hivi..... Lakini pia Tunaona Bwana Yesu Kristo  alitumia pia Neno Imeandikwa yaani Neno lilikuwa ndani yake, Na  akalitumia, hatimaye alimshinda shetani ; Naye Ibilisi akamwacha Yesu Kristo.
-Na wewe shetani anapokuujia, Anakuja Kukujaribu,kukuibia,Kukuchinja Na Kukuaribu Anapokuta huna Neno ndani yako atakufanya atakavyo yeye.
√ Mpendwa sikuambii  kwamba usiombe, au usifunge, au Usitoe sadaka Hapana ; bali Nataka nikuambie kwamba fanya yote hayo Huku ukiwa na  Neno la Mungu ndani yako itakusaidia sana.
√ Kwa ukosefu wa maarifa ndiyo Maana watu wengi leo, wakristo wengi leo wanaangamizw ; Na maarifa yanapatikana ndani ya Neno la Mungu wapendwa.
-Hivyo tulijaze Kwa wingi neno la Mungu wetu ndani ya mioyo yetu .
√ Watu wengi leo wanakosa kuliweka neno la Mungu  ndani ya mioyo yao, Hivyo wanamwacha  Mungu  Na kumtegemea  Mwanadamu, Na kumfanya mwanadamu kuwa kinga yake.
-kuliko Kumfanya Mungu kuwa kinga, ngome na kimbilio Lao, wao wanawategemea wanadamu kwasababu ya ukosefu wa Neno la Mungu.
√Wapendwa  Imeandikwa ya kwamba
-BWANA asema Hivi, Amelaaniwa Mtu Yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
Na Moyoni mwake amemwacha  BWANA. YEREMIA 17:5
kwa. ukosefu wa Neno watu huwaendea wanadamu, Wanawategemea Na kuyafanya wao kuwa Kinga yao, Hivyo tambueni wapendwa ; unapomwacha Mungu Na kumuendea Mwanadamu kuwajuwa wewe Moyoni mwako huna Mungu, Na hivyo Umelaaniwa mpendwa wangu.
-Kwasababu ya kuwategemea wanadamu na kuyafanya wao kuwa za wengine, Leo hii tunashuudia watu wakiwa katika majonzi, Katika matatizo, Ndoa nyingi Leo zimekosa amani Na utulivu kwasababu ya kukuacha Mungu.
-Na wanamwacha Mungu kwasababu ya kulikosa Neno La Mungu.
-Ndugu yangu Kwanini ulaaniwe Kwa kumtegemea Mwanadamu Huku Mungu yupo Kwa ajili yako ?
-Ni Kweli uyapitiayo Leo yanakuumiza, lakini nakuambia Weka, Jaza neno la Mungu  moyoni mwako utayashinda Yote mpendwa.
-Usiweke maji, vitambaa, mafuta, chumvi ndani yako maana havina ushindi wako ; Bali weka Neno la Mungu ndani ya moyo wako ; shetani atakujia lakini atakukimbia tu mpendwa, Maana utashinda Kwa Neno la Mungu. 

-Neno la  Mungu Ndio ushindi wako mpendwa wangu ; Usiwe Ni Mtu wa kuzura-zura makanisani kutafuta miujiza Na kutabiriwa ; wewe weka neno la Mungu moyoni mwako tu.
         Wapendwa Katika Kristo
 
√ Neno la Kristo na likae Kwa wingi ndani yenu Katika hekima Yote, Mkifundishana Na kuonyana Kwa zaburi, Na Kwa Nyimbo, na kwa tenzi za rohoni ; Huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 

Neno Ndio kila kitu katika maisha yetu ; Huwezi kumshinda Shetani Kwa elimu yako, wala Kwa pesa yako, wala Kwa cheo chako, Wala Kwa umaarufu wako ; Bali tunamshinda Shetani pamoja na hila zake zote Kwa nguvu za Neno La Mungu. 

-Tinapoliweka Neno la Mungu kwa wingi mioyoni mwetu, wapendwa tutabarikiwa Na hatimaye utashinda nuru ningurumo za Shetani. 

-Baraka zinazotoka Kwa Mungu kuja kwetu tunazipata Kwa kulishika neno lake, kuliweka Kwa wingi moyoni mwetu. 

-Mpendwa wangu moyoni mwako wewe umejaza nini, Moyo wako wewe umemtegemea Nani, Maisha yako yote umemkabidhi Nani ayatawale ?

Post a Comment

0 Comments