100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

KATIKATI YA MAADUI ZAKO MUNGU ATAKUINULIA MTU WA KUSIMAMA NA WEWE

 

KATIKATI YA MAADUI ZAKO MUNGU ATAKUINULIA MTU WA KUSIMAMA NA WEWE

1 SAMWELI 19:1-3

Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi. Lakini huyo Yonathani, mwana wake Sauli, alikuwa akipendezwa sana na Daudi. Basi Yonathani akamwambia Daudi, akasema, Sauli, baba yangu, anatafuta kukuua; basi, nakusihi, ujiangalie sana asubuhi, ukae mahali pa siri na kujificha; na mimi nitatoka nje na kusimama kando ya babangu huko shambani ulipo wewe, nami nitazungumza na babangu habari zako; nami nikiona neno lo lote nitakuambia.


Nakusalimu tena katika jina takatifu la Yesu, nikiwa na imani kwamba umzima kabisa!!!!!!!!!!

Ni saa nyingine tena tunakutana mezani kupata chakula cha kiroho kitakachotusaidia kuendelea kukua vyema kiroho na hata kimwili kwasababu usitawi wa maisha yetu kimwili unategemea sana na uimara wa msingi wetu kiroho  kama ambavyo maandiko yasemavyo yakuwa,

“Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.           Mathayo 4:4


Kwa maneno hayo machache sasa tunaweza kuelekea kwenye somo letu la leo linalosema KATIKATI YA MAADUI ZAKO MUNGU ATAKUINULIA MTU ATAKAYESIMAMA NA WEWE

Pengine umesikia maneno kama haya mara nyingi ama hukuwahi kusikia kabisa lakini kivyovyote vile Roho mtakatifu akafanyike msaada kwako na kwangu pia kuhakikisha unapata na ninapata kile alichokusudia upate au nipate. 

Sote tunajua habari za Daudi namna ambavyo alipambana na adui wa waisrael Goriathi na hatimaye akapata ushindi, ushindi ambao haukuwa kwa ajili yake bali kwa taifa zima na wananchi wake, kwa lugha nyingine ni kwamba kama angeshindwa kumpiga Goriathi maana yake yeye ndo angeuawa katika mikono ya Goriathi lakini niseme hivi upako wa Mungu ukiwa juu yako utakupa nguvu ya kupenya kila mahali ambapo watu wengine wakikuona unapita hapo watashika vichwa. 

Goriathi lilikuwa ni jitu kubwa na lenye dharau maana lilikuwa likimtukana mfalme wa israel mpaka na majeshi yake ndivyo biblia inavyosema, ni ukweli kwamba hakuna aibu kubwa kwa mfalme au rais yeyote duniani kutukanwa adharani yeye na majeshi yake lakini aibu hii sauli ilimpata na hakuwa na namna ya kuishinda mpaka Daudi kijana mdogo sana kutoka katika hadhi ya chini alipoinuliwa na kupakwa mafuta kwa ajili ya kufuta aibu hii sio kwa sauli bali kwa israel.

Unaweza ukjiuliza swali gumu sana kwamba Daudi aliwezaje kumshinda Goriathi tena sio kwa siraha bali kwa jiwe tu, narudia jiwe tu linamuangusha mtu ambaye majeshi ya nchi yameshindwa kumpiga. 

Lakini upako ukisha achiliwa juu yako uwe na uhakika iwe na katika milima au mabonde au katika bahari utapenya tu tena kwa wepesi sana maana sio wewe unayetenda bali nguvu iliyo nyuma yako ndiyo itendayo kazi. 

Lakini sote tunaona mbali tu na ushindi uliopatikana kwa israel kupitia Mungu juu ya Daudi ulikuwa umebeba fursa nyingine Nyeti ya kiti cha ufalme kutambulishwa kwa Daudi. 

HATA HIVYO wako watu wengi leo wakipita katika majaribu kidogo tu hufunga na kuomba ili Mungu awatoe hapo, ni wachache sana wanaouliza mapenzi ya Mungu katika hilo jaribu ni nini,   nataka nikwambie hivi kuna aina ya mapito au changamoto husipozipitia hautaruhusiwa kabisa kuvuka na kuingia hatua nyingine ya maisha yako iwe kiroho au kimwili, TAFUTA KUJUA MAPENZI YA MUNGU KWA MAHALI UNAKOPITA HAIJALISHI NI PAGUMU KIASI GANI 

Nakwambia ukishajua mapenzi ya Mungu patakuwa pepesi kwako kupenya na hata si Mungu amehusika hapo ile tu kuuliza mapenzi yake atakupa au kukuonyesha mlango wa kutokea, lakini bahati mbaya si kila mtu anajua hivi na si kila mtu anashauri hivi.na si kila mtu anakubali na kuruhusu Mungu kuingilia kati vita yake au majaribu yake.

We umewahi kufikiri kama Daudi angesita au akaenda mbele za Mungu kuomba Mungu ameupushe na Goriathi nini kingetokea????? 

Mimi sijui kama Mungu angejibu ombi hilo au la lakini kama angejibu nataka nikuhakikishie pengine daudi  hasingekuwa kwenye vitabu vya historia na pengine hasingejulikana na zaidi sana pengine hasingekuwa mfalme au kama angekuwa mfalme ingemchukua muda mwingine mwingi zaidi wa kupata tena nafasi kama hiyo, sasa fikiri tu ni mara ngapi umefunga na kuomba ukitaka Mungu akuepushe na changamoto unazopitia pasipokuelewa kilichobebwa ndani ya hiyo changamoto kina umuhimu au msaada gani kwako.maana si kila majaribu yanayokuja basi ni shetani kaleta,kuna wakati lazima tupitishwe mahali kama sehemu ya maandalizi ya kutupeleka katika nafasi zetu,kwa wale wanafunzi wanaelewa kwamba huwezi kuruhusiwa kuingia level au kupanda darasa jingine mpaka umefaulu mtihani hata kama walimu wanakuamini vipi na kila mtu anajua wewe unaongozaga darasani lakini inapofika saa ya kuingia hatua nyingine ya kupanda darasa ni lazima ushiriki mtihani na sababu pekee ya kukufanya uingie kwenye hatua mpya ni lazima ufaulu mtihani unaopewa,

vivyo hivyo Mungu hawezi kukuingiza kiwango kingine ikiwa hujafuzu kuingia hatua ya pili vinginevyo utakwama mapema sana.

Nataka niseme kwamba Mungu wetu ni Mungu anayeishi na ujumbe huu  mfupi ufanyike kama mwaliko wako kukutana na Mungu na kuona Umuhimu wa kutaka kujua mapenzi ya Mungu kwa kila jambo au kila eneo unakopita,Hii  itakusaidia sana kuvuka kuliko ambavyo ungetegemea akili zako au kuliko ambavyo ungetumia akili zako au kutegemea ushauri wa watu wengine ambao hata hivyo huna uhakika kama sauti ya Mungu iko katikati ya ushauri huo unaopewa.

 

Ni maombi yangu kwa Mungu kila atakayesoma ujumbe huu apate kitu cha kumsaidia, kwa maana hiyo kwakuwa mpaka hapa hatujaanza kujifunza somo letu linalosema  KATIKATI YA MAADUI ZAKO MUNGU ATAKUINULIA MTU ATAKAYESIMAMA NA WEWE, nisingependa ujumbe uwe mrefu sana na kuwa sababu ya watu wengine kukwazika na kupuuzia kuusoma kwa sababu kwa kupuuza tu maana yake hawatapata kile Roho mtakatifu alikusudia wapate kwa wakati huo. Mungu akinipa kibali nitarudi tena na mwendelezo utakaotutoa hapa kwenye utangulizi wa somo letu na kutupeleka moja kwa moja katika somo husika. 


Somo hili Litaendelea.................


MUNGU WANGU AKUBARIKI SANA NA NIKUTAKIE  BARAKA ZA BWANA

Post a Comment

0 Comments