UHUSIANO ULIOPO BAINA YA SANAMU ALIYOIONA MFALME NEBUKADREZA PAMOJA NA MAISHA YETU
DANIEL 2:31-35
Wewe ee mfalme uliona na tazama
sanamu kubwa sana.sanamu hii iliyokuwa kubwa sana,na mwangaza wake mwingi
sana,ilisimama mbele yako na umobo lake lilikuwa lenye kutisha.
Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa
ni cha dhahabu safi,kifua chake na mikono yake ni ya fedha,tumbo lake na viuno
vyake ni vya shaba.
Miguu yake ni ya chuma na nyayo
za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya
udongo.
nawe ukatazama hata jiwe
likachongwa bila kazi ya mikono , nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake
iliyokuwa ya chuma na udongo likaivunja vipande vipande.
Ndipo kile chuma na ule udongo
na ile shaba na ile fedha na ile dhahabu vilivunjwa vipandevipande pamoja
vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari,upepo ukavipeperusha
hata pasionekane mahali pake,na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima
mikubwa likaijaza dunia yote.
TAFSIRI YA NDOTO YA SANAMU
·
KICHWA (DHAHABU) Ni utawala wa BABLON au BABELI
uliotawala mwaka wa 606-539 BC sawa
na miaka 67 ya utawala wa BABLON
·
KIFUA NA MIKONO (FEDHA) Ni utawala wa MEDOPERSIA uliotawala mwaka wa 539-331
BC sawa na miaka 208 ya utawala
wa MEDOPERSIA
·
TUMBO NA KIUNO (SHABA) Ni utawala wa wagiriki uliotawala mwaka wa 331-165 BC sawa na miaka 166 ya utawala wa WAGIRIKI
·
MIGUU (CHUMA) Ni utawala wa RUMI uliotawala mwaka wa 168-47
AD sawa na miaka 79 ya utawala wa RUMI
NB;(hapa kanisa liliungana na
serikali)
·
NYAYO (CHUMA NA UDONGO)Ni utawala wenye mfumo wa wana wa Mungu ambao
ni chuma kujichnganya na nafsi zao,na mbegu zao lakini hawatashikamana kama
vile chuma isivyweza kushikamana na udongo.
DANIEL 2:43
Na kama vile ulivyokiona kile
chuma kimechanganyikana na udongo na matope,watajichanganya nafsi zao kwa mbegu
za wanadamu,lakini hawatashikamana kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.
Nb;(HIMAYA ZA KIUTAWALA AU
WAFALME 10 KUTOKA MATAIFA YENYE NGUVU DUNIANI)
DHAHABU ==> BABYLON ==> MWAKA 606-539 BC
SHABA ==> MEDOPERSIA ==> MWAKA 539-331 BC
CHUMA NA UDONGO ==> RUMI ==> MWAKA 168-47 AD
DANIEL 7:2-8 , DANIEL 7:15-27
UPEPO
UKAVUMA NA WAKATOKEA WANYAMA WANNE,
Hawa walikuwa ni
viumbe wenye uhai ndani yake kwasababu kuona sanamu tu hakutoshi husipoona na
kilichoko ndani yake.
MNYAMA
WA KWANZA NI SIMBA ambaye kwenye sanamu ni kichwa cha dhahabu.
Hii inawakilisha
utawala wa BABYLON (606-539)samba mwenye mabawa ya tai akasimama kama
mwanadamu.
MYAMA WA PILI NI DUBU
MYAMA WA PILI NI DUBU
Huyu aliinuliwa
akiwa na mifupa mitatu ya mbavu kinywani mwake katika meno yake.
Wakamwambia mnyama
huyo inuka ule nyama tele;
Hii inawakilisha
utawala wa MEDOPERSIA 539-331 uliooneshwa kwenye kifua na mikono (FEDHA)
MNYAMA WA TATU NI CHUI
MNYAMA WA TATU NI CHUI
huyu alikuwa na
mabawa manne,
akapewa mamlaka
akiwa na manne kama ya ndege na vichwa vine.
Hii inawakilisha
utawala wa WAGIRIKI 331-165 BC uliooneshwa kwenye TUMBO NA KIUNO (SHABA)
MNYAMA WA NNE
MNYAMA WA NNE
Huyu ni mnyama wa
kutisha na mwenye nguvu na mwenye uwezo mwingi naye alikuwa wa kutisha.,
Alikuwa na meno ya
chuma makubwa sana na alikula na kuvunja vipandevipande na kuyakanyaga mabaki
kwa miguu yake na umbo lake lilikuwa
mbali kabisa na wale wa kwanza naye alikuwa na pembe 10 nikazitazama
sana pembe zake na tazama pembe nyingine ikazuka kati ya hizo kumi nayo ilikuwa
ndogo lakini mbele yake pembe tatu
katika zile za kwanza zikangolewa kabisa na tazama katika hiyo mlikuwa
na macho kama macho ya mwanadamu na kinywa kilichokuwa kikinena makuu.
Utawala huu ni wa
RUMI 168-47 AD ulioneshwa kwenye MIGUU (CHUMA)
NYAKATI ZA UTAWALA NA WAFALME WALIOTAWALA
1. Mwaka 606-539 bc utawala wa BABYLON chini ya
mfalme NEBUKADREZA mwana wa NEBOPOLASA kwenye sanamu ameonekana kama DHAHABU
(GOLD)
2. Mwaka 539-331 bc utawala wa MEDOPERSIA chini
ya KORESHI kwa mamlaka ya WAMEDI na WAAJEMI baada ya koreshi kuangusha utawala
wa babylon,kwenye sanamu alifunuliwa kama FEDHA(SILVER) (MIKONO NA KIFUA).
3. Mwaka wa 331-165 BC utawala wa UGIRIKI chini
ya ELEXANDER mkuu alikuwa jemadari wa jeshi akawaangusha wamedi na waajemi
kwenye sanamu amefunuliwa kama kama SHABA kwenye KIUNO NA TUMBO (BRONZE).
4. Mwaka 168bc-47ad utawala wa WARUMI,serikali
iliungana na katika IBADA na mwongozo wa
KIROHO baada ya maamuzi haya ya pande zote mbili kikazaliwa kitu kipya yaani
JUMAPILI (SUNDAY)
Ezekiel 8:16
Akanileta mpaka ua wa ndani wa
nyumba ya Bwana ,na tazama mlangoni pa hekalu la Bwana,kati ya ukumbi na
madhabahu walikuwako watu kama ishirini na watano,wamelipa kisogo hekalu la
Bwana na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki nao wanaliabudu jua kwa
kuuelekea upande wa mashariki.
Kingine kilichoibuka
baada ya muungano huo ni UMOJA WA MATAIFA YENYE NGUVU DUNIANI na huu
umeonyeshwa kama CHUMA na kwakuwa uliungana na mataifa dhaifu yanayoonekana na
kufunuliwa kama UDONGO na kwenye NYAYO yaani nusu chuma ni HIMAYA KUMI ZA
KIUTAWALA ZINAZOTAWALA KWA KUUNGANA NA MATAIFA DHAIFU (IRON AND CLAY)
MAELEZO MAFUPI KUHUSU KICHWA YAANI DHAHABU
KWENYE SANAMU
KICHWA ni DHAHABU;NEBUKADREZA kwa
wakaldayo,huyu alikuwa jemadari wa jeshi la babeli wakati baba yake akitawala
kama mfalme aliyeitwa NABOPOKASA baba yake NEBUKADREZA .
Jina la NABOPOLASA ni jina la miungu ya
babeli likimaanisha mungu saidia.
Huyu alianzisha dola ya kutawala dunia sawa
na DANIEL 4:22 mwaka 606
likiendeshwa na jemadari NEBUKADREZA.
NEBUKADREZA akiwa vitani alipokea taarifa
mbaya kutoka nyumbani kwani baba yake NABOPOLASA alimwacha nyumbani akiwa
anaumwa yeye akaenda vitani na akawapiga MISRI,SIRIA mpaka akafika nchi ya
uzuri ISRAELI mwaka wa 606.
Ndipo akasitisha vita baada ya kuambiwa na
kupewa taarifa za kifo cha baba yake na akarudi nyumbani kumzika babaye.na
baada ya msiba atawazwa kuwa mfalme
kasha akarudi vitani tena kwa mara ya pili Yerusalem .
Vita vikapigwa na akawateka wachache
SHEDRACK,MESHAK NA ABEDNEGO na wengine YEREMIA 46:1-4
MAELEZO MAFUPI KUHUSU KIFUA NA MIKONO (FEDHA)
KIFUA NA MIKONO NI FEDHA
Umedi na uajemi hapa tunampata mfalme KORESHI
aliyekuwa na motto aitwaye AUSHUELO katika utawala wa DARIO mwanaye.
Matukio yafuatayo ya Daniel kutupwa katika
tundu la simba,Daniel kupata kibali cha kuendelea kuwa waziri katika ufalme
mpya pia kuanzishwa kwa dora ya fedha (UTENGENEZAJI WA HELA RASMI) tangzo la
ISRAEL kurudi kwao wakajenge hekalu.
Mwaka wa 538 chini ya kiongozi ZELUBABELI
wakarudi nao wakajenga hekalu
EZRA katika mwaka wa 500 alianzisha
masinagogi na kupanga vitabu vya agano la kale kikiwemo cha ZABURI
MAELEZO MAFUPI KUHUSU TUMBO NA KIUNO (SHABA)
Ufalme huu uliinuka ukaangusha ufalme wa
wamedi na waajemi chini ya mfalme ELEXANDER mkuu (RUMI)
Ndani ya miaka mitatu alikuwa ameipiga dunia
nzima nay eye mwenyewe akafa na hakubahatika kupata motto na kupelekea utawala
wake kugawanyika mara nne,kwasababu kabla ya kifo chake katika utawala wake
kulikuwa na majemadari wanne wa kijeshi.yaani MASHARIKI,MAGHARIBI,KASKAZINI NA
KUSINI.
Kumbuka mnyama wa pili katika Daniel 7:18 ana
mbavu tatu mdomoni mwake maana yake atawapiga wenzake wote,
Vita viliibuka wakapigana na falme mbili
zikaanguka na kusalia falme mbili wa kaskazini aliyeitwa TOLENI na wa kusini
aliyeitwa SERUKAS wao pia wakapigana akabaki mmoja mfalme wa kusini yaani
SERUKAS .
Basi naye akainuka akaanza kupigana na
mataifa baadhi na mwisho wa siku akafika Jerusalem na kuikuta Jerusalem haina
mfalme.isipokuwa ilikuwa ikiongozwa na KUHANI MATATIA aliyekuwa na watoto
wanne.
Na hawa walikuwa majemadari wa jeshi la Bwana
wa ISRAEL.
Ikawa serukas alipotangaza vita kwa kuhani
sawa na Daniel 9:27 , mathayo 24:15
kuhani MATATIA akawaita watoto wake wote 4
akawatia moyo wapigane na SERUKAS , ikawa vita ya kwanza ikalenga ibada ya
sadaka hekaluni kasha SERUKAS akamlazimisha kuhani kutoa sadaka ya nguruwe
hekaluni kwa nguvu za kijeshi wakamlazimisha
matatia na kunyoosha mkono wake madhabahuni kana kwamba anataka kuchinja na
ghafla akaugeuzia mkono wake na akakitia kisu katika kifua cha serukas mtesi na
akafa palepale ndipo vita ikainuka tena na watoto wa kuhani wakapigana mpaka
wakashinda.
Baada ya vita kuhani matatia akafanya sikukuu
ya kutakasa hekalu iliyoitwa KUTABARUKU.
MAELEZO MAFUPI KUHUSU RUMI
Huu ni ufalme ulioonyeshwa kwa sura ya mnyama
wa kutisha sana na umbo lake liko mbali na wale wa kwanza kwenye sanamu
Miguu chuma,nusu chuma,udongo kwenye nyayo.
UPAGANI unaungana na dini EZEKIELI 8:16
SIASA ilipoungana na DINI kwa pamoja
ukajengwa mnara wa babeli maana yake roho za uasi sawa na Mwanzo 11:1-9
Maana yake babeli ya leo ni roho za uasi sawa na Ezekiel 23:3-30
Maandiko haya ukiyasoma utaona kwa undani
sana kikombe cha ghadhabu ya MUNGU kwa ohola na oholebu yaani SAMARIA NA
YERUSALEM kwa maana nyingine utaelewa maana ya maombi ya YESU pale GETHSEMANE kwamba
kikombe hiki kiniepuke lakini mapenzi yako yatimizwe au usomapo
zaburi 23:5 huwa unaelewa nini?
Asante YESU kwasababu wewe ndiye jiwe kuu la
pembeni WAEFESO 2:20 lililochongwa mlimani likaipiga sanamu ikasambalatika nalo
likawa jiwe kuu likaijaza dunia.
Asante Yesu kwa alivyokusaidia kutumia muda
wako mwingi kwa kuwekeza katika ufalme wake kwa kusoma maono haya.
Mungu wangu na akubariki sana na ukapokee
sawa na kiu ya imani yako.
Maombi yako ni muhimu sana kwangu na kwa
ajili ya huduma hii ya KANAANI MPYA pia aliyenipeleka ajitwalie utukufu huu
kupitia somo hili na ardhi na mbingu zikayatie muhuri mafunuo haya yakazidi
kufanyika Baraka kwa vizazi hata vizazi na ufalme wake utujilie kama huko
mbinguni kwa neema ya damu ya mwanakondoo !!!! Ameeeen
KWA MSAADA WA MAOMBI NA MAOMBEZI
Mwl.Azory +255767-155-623 PIGA
NA
Mwl.Joshua +255620-179-783 SMS
0 Comments