100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

UMUHIMU WA MALEZI KWA MTOTO Sehemu ya kwanza

 UMUHIMU WA MALEZI KWA MTOTO



SEHEMU YA KWANZA
kuna tofauti kati ya mzazi na mlezi,
Kitu kimojawapo cha yule anayelea ni kumsaidia anayelelewa ili hasikate tamaa, kwasababu katika safari yoyote kuna kukata tamaa au kukatishwa tamaa au kuvunjika moyo.

KWAHIYO mtu yeyote aliyebeba roho ya kukulea, atahakikisha yupo karibu na wewe, atakuombea wakati wote, atakutia moyo, atakwambia songa mbele, hatakulaumu bali atakushauri, katika kipindi kigumu atazungumza na wewe kama vile matatizo ni mepesi hata kama yeye mwenyewe anaona ni magumu, na mwisho wa yote atakuhimiza kuweka tumaini lako kwa Bwana hata kama kuna sehemu nyingine ya msaada ulitarajia.


Unaweza ukawa na mzazi lakini hasiwe na sifa ya kuwa mlezi, ndiyo maana YESE alishindwa kumlea DAUDI Katika njia ya kifalme badala yake akamlea katika njia ya kuchunga kondoo na daudi aliendelea kuenenda katika njia hiyo hisiyokuwa ya kwake mpaka alipoinuliwa Samweli kuja kumpaka mafuta na kuanza kumuandaa kifalme zaidi sana analetwa Yonathani naye anapewa jukumu lile lile la Samweli katika mazingira tofauti la kumlea Daudi katika njia ya kumuandaa kuelekea kwenye kiti cha kifalme.

KWAHIYO ni wajibu wa mzazi kwa mtoto kuhakikisha anamlea katika njia bora itakayompeleka kule Mungu alikomuandaa kuketi. (kwenye kusudi la Mungu)

“Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme.
” Waebrania 11:23

Wazazi wake musa wangeweza kumkatia tamaa musa kutokana na amri ya kifalme ya watoto wote wa kiume kuuawa pindi wanapozaliwa, aina ya mazingira waliyokuwa nayo wakati wanampata musa hayakuwa rafiki kwa usalama wa maisha yake lakini pia kwa usalama wa wao binafsi ingewaweka kwenye hatari kwa kupingana na amri ya kifalme,
Lakini maandiko yanasema kwamba walimuona ni mtoto mzuri maana yake lazima waliomba na wakahitaji msaada wa Mungu kuhakikisha uzuri huo wanaouona haupotei kwenye macho yao na Mungu akaamua kuingilia kati mazingira yale ya kumfanya musa anabaki hai ingawa hata kama wangeamua kumtoa akauawa sawa na amri ya kifalme hakuna mtu angewalaumu maana ni amri ya kifalme lakini hawakumkatia tamaa mtoto wao na walimtengenezea mazingira ambayo waliamini atakuwa salama hata kama atakuwa mbali nao.


Haijalishi unamuona mtoto ni mkaidi kiasi gani au hasikii wala hazingatii yale unayomsihi lakini husijaribu kumkatia tamaa kwasababu ukishamkatia tamaa maana yake hali ya kumsaidia ndani yako itayeyuka na baada ya muda ataanza kuharibikiwa zaidi ya alivyokuwa mwanzo na mtoto akiharibikiwa anayelaumiwa ni mzazi sio mtoto hata kama wewe mzazi unamtupia lawama mtoto kwa kumuona ni mkaidi lakini ni wajibu wako kumlea na kuhakikisha kila kuitwapo leo unapanda mbegu ndani yake ambayo itaacha na kuongeza nguvu zake za kiroho,

unaweza husione matokeo ya malezi yako kwa wakati huo lakini iko siku yamkini utakuwa haupo duniani au haupo karibu naye, anaweza akapita kwenye mazingira magum sana na mbegu ile uliyopanda ndani yake miaka mingi iliyopita ikamsaidia kumvusha ng'ambo ya pili,
Unaweza husielewe maneno haya lakini ukiona kukata tamaa ndani yako kwa ajili ya mtoto wako nenda mbele za Mungu kuomba upako mpya wa malezi kwa mtoto na ukishindwa kabisa omba Mungu akuinulie mtu atakayesimama mbele ya huyo mtoto kama mlezi badala yako, japokuwa kuna aina ya heshima hutaipata kutoka kwa mwanao pindi tu atakapoanza kupima na kulinganisha ubora wa aina ya malezi anayoyapata kutoka kwa mzazi na kwa mlezi.
lakini hutakiwi kukata tamaa kabisa hata kama huoni mwanao akibadili tabia yake ambayo wewe ukimtazama unaona kama anapotea kwasababu biblia inasema
*Rahabu yule kahaba kwa IMANI......................*
husiniulize nani alikuwa akimfundisha au kumlea Rahabu maana sitakujibu kwasababu biblia haisemi nani alikuwa karibu na rahabu kuhakikisha anamjenga kiimani lakini lazima yuko mtu aliyekuwa akimfundisha Rahabu habari za Imani wakati huo rahabu akiendelea na ukahaba wake kwasababu Biblia inasema *imani huja kwa kusikia*

kwahiyo kama huja kwa kusikia maana yake lazima Rahabu alisikia kwanza ndipo akaamini.
Lakini aliyekuwa akimlea hakumkatia tamaa maana mbegu njema aliyoipanda ndani yake miaka kadhaa iliyopita ilizaa matunda yaliyomfanya Rahabu kujengeka imani yake na kuhamishwa moja kwa moja kiroho baada ya muda mrefu kupita.


MUNGU WANGU MWEMA AKUBARIKI SANA

Post a Comment

0 Comments