100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

JINSI SADAKA YA ZAKA INAVYOWEZA KUBORESHA AU KUVURUGA HALI YAKO

 

JINSI SADAKA YA ZAKA INAVYOWEZA KUBORESHA AU KUVURUGA HALI YAKO

Bwana Yesu asifiwe !!!

Karibu katika somo letu jipya la jinsi zaka inavyoweza kuboresha au kuvuruga hali yako,

kuna tofauti kati ya zaka na sadaka;

ZAKA ni sehemu ya kumi ya baraka ambazo Mungu amekubariki,ambapo hii ni ya Mungu kisheria maana yake hahiitaji majadiliano tena kama utoe au husitoe,husipotoa ni wewe na kiburi chako,na huwezi kuepukana na madhara ya kutokuitoa.

SADAKA ni kile unachoweza kutoa juu ya zaka maana yake,ukiisha kutoa zaka ile 90% inayobaki ndiyo unaweza kuamua kutoa sehemu ya sadaka na sadaka hii haina masharti yoyote kwasababu ni sadaka ya hiari,kwahiyo kile unachoamua ndicho unachotoa na ziko sadaka za aina nyingi tu ambazo leo sio siku yake maalum kuzizungumzia.

Kuna watu hawatoi zaka katika madhabahu wazazohudumiwa si kwasababu hawajui wajibu wao na si kwasababu wamesahau na si kwa sababu hawana kitu Mungu alichowabariki BALI ni kwasababu wengi wao wanafikiri wakitoa zaka either wanaona ni nyingi kutegemeana na namna Mungu alivyowabariki, AU kama sivyo hawajui umuhimu wa zaka na maana halisi ya zaka AU wanafahamu lakini wanafikiri wakitoa hiyo zaka watamunufaisha   mchungaji/kuhani.

Lakini leo niko hapa kukwambia jambo hili ya kwamba haijalishi unajua umuhimu wa zaka na hautimizi wajibu wako kwa sababu zako binafsi au haujui na hautoi tu kwa sababu haujui lakini makundi yote hayo mawili lazima yatapita katika hali moja kwasababu Neno la Mungu liko wazi kila mahali na hivyo hata kama hujui husijaribu kujitetea kwamba hujawahi kuelezwa/kusikia maana ile kutokujua inamaanisha hukuwahi kutafuta kujua jambo hilo na mimi nina uhakika makuhani wa Bwana hawajawahi kuacha kunena jambo hili kwa kondoo ambao wako chini yao na ambao hawako chini yao japokuwa wanaelewa namna ambavyo wapokeaji wa Neno wanaweza wakapokea kinyume na wao walivyokusudia,lakini tafisiri za kibinadamu ambazo tunazijenga wenyewe katika fahamu zetu baada ya kusikia watumishi wa Mungu wakinena kwa habari ya jambo hili ndizo zinazoweza kutupotosha na kufungua mlango wa shetani/adui kupanda mbengu mbaya ndani yetu na kutupelekea kwenye wakati mgumu ambao hata hivyo si rahisi tukafahamu kwamba kuna aina ya mazingira tunayapitia ambayo ni matokeo ya kutokuwa waaminifu kwetu katika eneo hili muhimu la zaka.

Biblia inasema;

“Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.”  — Malaki 3:8

Anaposema unaniibia maana yake wewe ni mwizi na sote tunajua kuiba ni dhambi kwahiyo pamoja na kuwa mwaminifu katika mambo mengine mengi ya kiutumishi lakini ukishindwa kuwa mwaminifu katika eneo la zaka wewe utabaki kuwa ni mtumishi ambaye ni mwizi na kama ni mwizi maana yake huwezi kuepukana na adhabu ya mwizi,utamuona Mungu katika maeneo mengine mengi lakini katika eneo ambalo usitawi wake unategemea zaka itakuwa ngumu sana kumuona akidhihirika kama ulivyotarajia,haijalishi unajiona ni mtumishi mkubwa kiasi gani neno la Mungu linasema; “Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.”— 1 Petro 1:17

 Kwahiyo husitegemee kumuona Mungu katika maeneo ambayo wewe mwenyewe sio muaminifu,biblia inamuita yeye ahukumuye pasipo upendeleo,kwahiyo ikiwa anahukumu pasipo upendeleo uwe na uhakika hawezi kujipinga kwa kukupendelea wewe.

Maandiko yanasema;

Zekaria 5:3-4

Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama ilivyo upande wa pili.

Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.

KWAHIYO ukiiba iko laana inayoelekezwa katika nyumba yako na laana ikiingia mahali kazi yake ni kutafuna na biblia inasema na kuteketeza cha pili ulinzi unaondolewa katika kile kilitakiwa kulindwa.

Zaka ni sehemu ya kumi Baraka ambazo Mungu anambariki mtu,ambayo sehemu hiyo kibiblia siyo ya mtu bali ni ya Mungu ndiyo maana ukiila biblia inakuita mwizi tena mwizi anayemuibia Mungu.

Jambo la muhimu kujua ni kuwa unapotoa zaka hautoi kwa mwanadamu bali unampa Mungu,maana wako watu watu wanafikiri zaka zao wanampa mtu,anaweza akawa mtu ikiwa unamkabidhi hiyo zaka akiwa nje na wito wake lakini akiwa ndani ya wito mbingu zinmtambua kama mwakilishi wa Yesu mwenyewe maana hakuna ukamilifu wa madhabahu kama hakuna kuhani,neno la Mungu na madhabahu yenyewe.kikipungua kimojawapo ni wazi kwamba madhabahu haijakamilika kuitwa madhabahu,ndiyo maana kuna vitu Mungu hawezi kusema na mtu mwingine vinavyoihusu madhabahu aliyomkabidhi mtu mwingine ikiwa bado aliyekabidhiwa yuko hai,mara nyingi utafunuliwa udhaifu wa kuhani ili umuombee lakini husijaribu kuchukua nafasi yake kwasababu umeona udhaifu wake.

Biblia inasema;

“kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” — Warumi 3:23

Anaposema wote wamefanya dhambi maana yake ni kila mwenye mwili,kwahiyo makuhani nao ni watu kama watu wengine  hivyo husifikiri kwamba yeye hana madhaifu,lakini pia husipime uwezo wake wa kihuduma kwa kulinganisha madhaifu yake,Mungu akikuheshimu kwa kiwango cha kukushirikisha madhaifu ya kuhani husijaribu kuyaweka wazi maana pamoja na madhaifu hayo unayoyaona wewe bado ana nafasi kubwa sana mbele za Mungu ya kusimama kama kuhani aliyeko zamu na akapewa mafunuo ya kukusaidia kukuvusha wewe uliye chini yake.

 

Wako watu wanatoa zaka kwa uaminifu na mimi nina uhakika wanamuona Mungu kama wanavyotaraji kwasababu maandiko yanasema yeye hulitazama neno lake apate kulitimiza kama alivyonena katika malaki yakwamba;

Malaki 3:10-11

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.

Kuna tofauti kati ya zaka na zaka kamili;watu pekee wanaoweza kukutana na Baraka hizi ni wale wanapeleka zaka kamili,ikiwa unapunguza zaka na kupeleka pungufu ni afadhali husitoe kabisa kwasababu haitakusaidia zaidi sana itaacha laana juu yako; Matendo ya Mitume 5:1-5

Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,

akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.

Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?

Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.

Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.

Kwahiyo nje tu na zaka,sadaka yoyote unayoweza kuitoa pungufu na dhamiri yako ya ndani inajua ni pungufu uwe na uhakika haiwezi kukuacha salama kwasababu anania na safira wote walikufa kwasababu ya kumdanganya Mungu,na hapa ndipo unapoweza kuelewa kwamba sadaka ile waliihaidi mbele za petro na walipoazimu kuficha sehemu ya thamani kwa siri Mungu alijifunua kwa mtumishi wake petro,sasa kwa wewe unayefikiri kwamba sadaka yako unampa mchungaji unaweza kuelewa kupitia mfano huu kwasababu hapakuwepo na shinikizo lolote kwa ndugu hawa kuhaidi sadaka yao lakini ile kutamka tu mali ile ambayo ilikuwa ya kwao ilihama kutoka mikononi mwao katika ulimwengu wa roho na kuhesabika ni mali ya Mungu na hivyo walivyoizuia kwa siri walikuwa wanazuia mali ya Mungu na sio mali yao tena na Mungu aliwahukumu kwa kifungu cha malaki 3:8 kinachosema; “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.” 

Wako watu wengi sana wanapita katika mnyororo huu na wanashangaa inapofika saa ya shuhuda inakuwa tofauti kwao na watu wengine lakini ni kwasababu kimwili mnaonekana nyote mmetoa na mchungaji anawatamkia Baraka lakini Baraka hizo haziwezi kukufuata kama sadaka yako haijakamilika au ina dosari mbele za Mungu,sana tu badala ya Baraka itaacha laana,laana ambayo itakuja imebeba adhabu juu ya kosa ambalo umelifanya madhabahuni pa Bwana maana ukitoa sadaka pungufu humdanganyi mchungaji bali unamdanaganya Mungu ndivyo maandiko yanavyosema katika matendo ya mitume 5:1-5

Linaendelea………………………………………

Post a Comment

0 Comments