100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

HATA KAMA HUONI DALILI ZA USHINDI LAKINI BWANA ATATENDA MUUJIZA

 

HATA KAMA HUONI DALILI ZA USHINDI LAKINI BWANA ATATENDA MUUJIZA

2 Wafalme 3:17

“Kwa kuwa Bwana asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji; nanyi mtakunywa, ninyi, na ng'ombe zenu, na wanyama wenu.”

   

Bwana Yesu asifiwe  leo kuliko jana.

UTANGULIZI

Lengo la somo hili ni kubadili au kukuza ufahamu wako na namna ya kutambua msaada wa Mungu pindi unapokuwa katika hali ambayo huoni njia au dalili za ushindi.


      • Kuna mahali unaweza kupita na husipate hata mtu mmoja wa kusimama na wewe,
      • Kuna mahali unaweza kupita unakona ni giza tupu.
      • Kuna mahali unaweza kupita alafu ukigeuka nyuma kila mtu anakucheka
      • Zaidi kuliko kuna mahali unaweza kupita hata kama yuko mtu anayekutia moyo lakini unaona kushindwa tu.


Unapofika mahali pa namna hii unahitaji msaada wa Kimungu ndani yako maana katika majaribu ndipo ambapo shetani anapata nguvu ya kupanda mbengu ndani ya mtu kupitia mazingira yanayomzunguka. 

Mungu ananena na Israeli kwa habari ya ushindi dhidi ya Moabu Katika hali ya kukosa maji, maana jeshi na farasi wote wangekuwa dhaifu lakini Bwana wa majeshi anajifunua kwa Israel na kumwambia maneno amabayo ukitazama kwa namna ya mwilini ni tofauti kabisa na hali halisi. 

Anamuhaidi maji mahali ambako hamna hata dalili ya mvua kunyesha ni ukame tu kila mahali. 

Ndivyo ambavyo leo Bwana anakuhaidi ushindi mahali uliona kushindwa. 


Namaanisha hivi hata kama unaona kila kitu ni kibaya mbele yako omba msaada wa Mungu kama ambavyo Israel walitafuta kujua mapenzi ya Mungu. 

Maandiko yanasema katika hali ya kuchoka na kukata tamaa kwa hajiri  mbele ya mtoto wake Ishmail Bwana  anajifunua kwake kwa ishara ya msaada kutoka katika kukata kwake tamaa hata kuona matumaini tena. 

Biblia inasema Hajiri alikaa mbali na mtoto wake ili atakapokuwa anakufa hasimuone kama ambavyo yawezekana umekata tamaa na pengine kuna hali imekuumiza kwa muda mrefu au una kiu na jambo fulani lakini umekaa katika hali hiyo kwa muda mrefu kiasi cha kufanya tatizo lako kuanza kuliona kama sehemu ya maisha yako. Lakini leo niko hapa kukutangazia nuru na uzima katika jambo hilo haijalishi umedumu nalo kwa muda gani na limekutesa kwa kiasi gani lakini kwa jina la Yesu, 

natangaza uzima badala ya mauti, 

Natangaza kutiwa nguvu badala ya kuchoka, 

Natakangaza majibu ya matumaini badala ya kukata tamaa. 

Kama ambavyo Mungu aliitangazia Israel ushindi, nami nakuja kwako kwa jina la Yesu yakwamba hata kama hamna dalili wala kiashilia chochote cha ushindi lakini bonde lako litajaa maji na kiu yako itakoma. 

Maandiko yananiambia ya kwamba Hajiri katika kuchoka kwake alifika mahali pa kukata tamaa na akalia kwa sauti kuu, biblia inasema Mungu akasikia sauti ya kijana wake na akamuagiza aende akamshike mtoto wake maana yake alimrudishia mtoto wake kutoka mauti hata uzima, ndivyo  ambavyo anakuja kwako kwa namna ileile na kwa jinsi ileile alivyojifunua kwa Israel na kwa Hajiri na akajifunue kwako na kila kilichoonekana kufa au kuharibiwa na adui na sasa  kikapate kuhuishwa tena kwa jina la Yesu na katika Damu ya Yesu. 

Mwanzo 21;17-19

Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.

Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.

 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.

 Mimi sijui ni wakati gani unaupitia lakini nina uhakika Roho mtakatifu anajua nami ni shahuku yangu na nia yangu yakwamba taabu yako na shida yako na hitaji lako likapate kukutana na Yesu maana maandiko yanasema, 

“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Mathayo 11:28

Bwana na akapate kukutana na wewe saa hii unaposoma ujumbe huu kuanzia rohoni amani ya kristo na itawale hata mwilini ushindi ukadhihirike, 

Haijalishi umelia kiasi gani lakini Yesu yuko tayari kukufuta machozi, 

Haijalishi umengoja mme au mke kwa muda gani bado niko hapa kukwambia yakwamba maandiko yanasema

“Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;1 Petro 5:6

Kwahiyo utii wako na unyenyekevu wako unaweza kuamua hatima yako iwe njema au mbaya.

Kamuulize Ibrahimu na sarah huko mtaani kama utabahatika kukutana nao yakwamba maamuzi yao ya kumtaka Hajiri awazalie mtoto baada ya kungoja kwao kwa muda mrefu kama yalikuwa ya maana au la!!,. Sitaki kujua watakujibu nini lakini nataka nikwambie maamuzi yako wewe binafsi pasipo Mungu hayawezi kubadili mpango wa Mungu  juu yako na yanaweza yasikufae sana kama ambavyo ulitegemea kwasababu hapakuwepo na haja ya Ibrahimu kumpata Ishmail alafu baada ya muda anatenganishwa naye,kama baba na kama mzazi lazima alisikia huzuni moyoni mwake maana ile ilikuwa ni damu yake.Kwahiyo haijalishi unajiona umevumilia au kungoja kwa muda gani lakini yakupasa kuingoja saa iliyokubalika na Bwana.

Haijalishi Israeli wanateseka na kutumikishwa kiasi gani lakini ilikuwa ni lazima ipite miaka mia nne ndipo ukombozi utokee kama ambavyo Mungu alinena na Ibrahimu.

Kwahiyo dumu ukienda mbele za Bwana  na tafuta kujua mapenzi ya Mungu kwa mahali unapopapitia,  nina uhakika Bwana atajifunua kwako kuhakikisha anatimiza agano lake juu yako kwa maana Biblia inasema 

Isaya 49:16

Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

Hapa Bwana anawatangazia mema wana wa Sayuni kama ambavyo anakutangazia wewe leo ya kwamba anakufahamu vyema  maana amekuchora katika vitanga vya mikono yake na zaidi sana anayajua mawazo yetu kama maandiko yanenavyo “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.Yeremia 29:11

Inamaanisha Mungu hajawahi kutuwazia mabaya badala yake mahali popote tunakoweza kuwa tunapita na mioyo yetu ikaingia huzuni bado hatima yake ni njema sana kwetu kuliko kabla ya kupita hapo maana yake popote unapoweza kuwa unapita ni maandalizi ya hatua nyingine inayofuata. 

Hata kama unajisikia vibaya kiasi gani au unaona kama umeachwa na kila mtu lakini Yesu yuko upande wako na kila ulichokipoteza hakika Bwana ni mwaminifu na baraka zake hazina majuto kama ambavyo alimzidisha mara dufu Ayubu hata kwako atakuzidisha na kukufanya mkuu kuliko mwanzo, 

Ayubu 42:12

Basi hivyo BWANA akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake;............ 


Nimalize kwa kusema ya kwamba Bwana anakutangazia neema na uhuisho na urejesho mpya  wewe uliyejiona umeachwa na kusahaulika

“Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.” Isaya 54:7


Mungu wangu akubariki sana na akajifunue kwako kwa jinsi ya msaada lakini akupe nguvu na uwezo wa kuendelea kumtegemea yeye peke yake hata kama huoni wingu limetanda lakini Mvua itanyesha,hata kama huko jangwani lakini lakini chemichemi itatokea na kiu yako itakoma.

Roho mtakatifu azidi kukufundisha ili kwamba kila kuitwapo leo ukazidi kuimalika rohoni maana usalama na uimara wa mwilini unategemea sana  nguvu ya rohoni.

Amen

Post a Comment

0 Comments