100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

JIFUNZE KUISHI KATIKA NENO LA MUNGU




 
JIFUNZE KUISHI KATIKA NENO LA MUNGU

Mathayo 4:4

“Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”

WhatsApp Group


Msitari huo hapo juu yalikuwa ni mahojiano baina ya Yesu na Shetani.

Lakini pia msitari huu tumeutumia juzi katika somo la majaribu, kwahiyo kisikusumbue hata kidogo kuona msitari huo unajirudia kwa somo jingine, wakati mwingine ni muhimu sana na kuna faida kumsikiliza roho mtakatifu anataka nini na kwa wakati gani kwa maana yamkini yuko mtu mmoja tu Mungu anataka kumvusha mahali katikati ya kundi la watu wengi.


kwaNa kwasababu roho ni yule yule maana yake msitahi huohuo mmoja anaweza kuutumia mtume,

Akautumia nabii,

Akautumia mchungaji,

Akautumia mwalimu,

Akautumia mwinjilisti kwa mafunuo tofauti na ujumbe tofauti, na kwa vipindi tofauti Kwahiyo kisikupe tabu.


Leo roho mtakatifu anatufundisha kwa habari ya kujifunza kuishi kwa kulitegemea neno la Mungu kwenye kila mazingira,haijalishi unapita mahali pepesi au pagumu kiasi gani.

Nimewaona watu wengi wakichukua muda mrefu sana kudumu katika kuomba pasipo kudumu katika Neno.

Sina maana kwamba nakuzuia kuomba ama kuomba ni vibaya lakini nataka  kusema hivi, husijaribu kuishi kwa kutegemea maombi peke yake kwasababu kuna mahali shetani hutamshinda pasipokuwa na neno ndani yako la kumpinga nalo.


Sikia Yesu alikuwa katika maombi ya siku arobaini lakini siku anamaliza maombi yake biblia yangu inasema shetani akamjaribu na tazama namna alivyokuwa anamjaribu kiasi ambacho ingelikuwa sio mtu wa Imani na mwenye neno ndani yake ingekuwa rahisi sana kuanguka siku hiyo na ingekuwa hasara tupu ya maombi yake ya kujitaabisha kwa siku zote 40 alafu anakuja kuanguka siku ya mwisho.

Mathayo 4:1-11

Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Ni hivi maombi ya siku 40 hayakumsaidia Yesu kumuhepusha na shetani lakini pia maombi hayo hayo hayamkumsaidia kumshinda shetani.

Kwasababu shetani huyohuyo alikuwa anatumia biblia hii hii ya kwangu na wewe kumjaribu Yesu, maana alikuwa akianza kwa kusema Imeandikwa..................

Neno IMEANDIKWA maana ni kitu kilishanenwa na roho wa Mungu   kupitia watumishi wa Mungu na hivyo ilikuwa ni rahisi Yesu kujikwaa katika mtego huu kama asingekuwa na neno la kutosha ndani yake kwasababu kila alichokuwa anakisema shetani mbele yake kilikuwa kimeandikwa kibiblia. Lakini kilichomsaidia Yesu ilikuwa ni kuwa na neno la mungu ndani yake na pili kufahamu majira na nyakati halisi za kutumika kwa hiyo mistari aliyokuwa anamtajia shetani.

Haikuwa kwa wakati huo lakini ilikuwa na mazingira yake maalum ya kutumika tofauti na wakati huo aliokuwa nao Yesu.


Sasa sio rahisi sana ukatenganisha vitu hivi kama huna neno la kutosha ndani yako, na ndivyo walivyo wakristo wengi leo, wanaweza wakadumu katika maombi kwa muda mrefu alafu shetani akija kwa sura kama hii aliyokuja nayo mbele ya Yesu wanajikuta wanaangukia mikononi mwake kwa kufikiri ni Mungu anajibu maombi yao kumbe ni shetani yupo kazini,


Niseme hivi, shetani haogopi maombi yako bali Neno la Mungu ulilolijaza ndani yako ndilo linaweza kumtisha na kuleta ushindi juu yako kwenye kila aina ya mazingira.

Lazini zaidi sana biblia inasema....

“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”  Yohana 4:24

Kwa maana hiyo ni wazi kuwa Mungu hatembei katika isia bali anatembea katika Neno lake.

Sipingi kuomba kwako lakini najaribu kukutengenezea msingi na mazingira ambayo yatasababisha maombi yako hayohayo yawe na nguvu mara dufu ukiyaomba huku ukiwa umejaza neno la kutosha ndani yako maana yake adui hatopata nafasi ya kukulagai na kukuondoa kwenye dira au nafasi ya Mungu, maana yake akija kimwili utamshinda kwa maombi, kanuni na Neno na akija kwa neno utamshinda na wewe kwa Neno kama alivyoshinda Yesu, ikumbukwe Yesu hakumshinda shetani kwa kuomba bali alimshinda kwa kujibishana naye kupitia Neno la Mungu.

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema shetani anaijua biblia vizuri vinginevyo hasingekuwa anapata nguvu ya kupambana na sisi na kanuni mojawapo ya ushindi katika vita ni pamoja na kufahamu aina ya siraha anayoitumia adui yako, kwahiyo husijaribu kuweka biblia yako kitandani na kuifanya kama mto ukifikiri shetani atakuogopa la !!! Kwasababu Neno la Mungu halisemi hivyo........... 


Neno la Mungu ni nguzo Muhimu sana katika kutembea kwenye baraka za kimungu vinginevyo shetani atakuvuruga saa yoyote anayotaka na hutakuwa na ujasiri ndani yako wa kumzuia maana ukiwa huna Neno ndani yako ni rahisi pia kukata tamaa na unajua ukishakata tamaa ndani yako maana yake unaruhusu nguvu za Mungu ndani yako kuyeyuka,lakini ukiwa na Neno la Mungu ndani yako haijalishi unapita wapi bado litakuwa faraja kwako hata kama hakuna aliye upande wako lakini zaidi sana litafanyika taa ya miguu yako au nuru kwako mahali ulipoona giza ndivyo maandiko yanavyosema......................

“Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”  Zaburi 119:105


Mwana wa Mungu nimalize kwa kusema jifunze kutembea katika Neno la Mungu, maombi ni muhimu lakini yatakuwa na nguvu na msaada kwako ukiwa na Neno la kutosha ndani yako kwa maana sio tu shetani kukujaribu hata Mungu mwenyewe akitaka kuongea na wewe au kukujibu hitaji lako hatokuja kwako kwa njia ya maombi bali atajifunua katika Neno lake kwako sawasawa na.............. 

“Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.”   Zaburi 107:20


Mungu wangu akubariki sana na somo hili lifanyike baraka kwako na kwa kila asomaye roho mtakatifu apate kujifunua kwake kwa sura ya msaada na kiu mpya ya kutaka kulijua Neno la Mungu ikapate kuachiliwa kwa nguvu ndani yako ili kwamba Mungu aweze kukutumia kwa viwango vya juu katika huduma yako maana unalo Neno la kukuvusha lakini pia uwe na uwezo wa ndani wa rohoni katika Neno wa kumshinda shetani atakapojitokeza kwako kama njia ya kukurudisha nyuma,maana shetani hakati tamaa na anazo njia nyingi za kuwajaribu wana wa Mungu, hivyo ni Neno la Mungu pekee litakalokufanya umuone mapema kabla hajakufikia na kuacha ushindi ndani yako haijalishi amekuja kwa njia gani. 

“Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.”  1 Petro 5:8


"Mungu wangu akubariki sana"

Post a Comment

0 Comments