100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

TARUMBETA SABA {7} KAMA ISHARA YA HUKUMU – Mwl: Azory Michael


 

TARUMBETA {7} SABA  KAMA ISHARA YA HUKUMU – Mwl: Azory Michael

Ufunuo 8:13

“Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.”

Ufunuo 8:3-6

Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige.

Tarumbeta huonyesha hatua za Mungu za kuingilia kati kwa niaba ya watu wake, Ufunuo hutumia vielelezo vya tarumbeta kama ishara.

Katika agano la kale tarumbeta vilikuwa vyombo muhimu vya maisha ya kila siku ya Israeli ya zamani.

Hesabu 10:8-10

Wana wa Haruni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta; nazo zitakuwa kwenu ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote.Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

                                                            2Mambo ya nyakati 13:14-15

Na Yuda walipotazama nyuma, angalia, vita vikawa mbele na nyuma; wakamlilia Bwana, na makuhani wakapiga mapanda.Ndipo wakapiga kelele watu wa Yuda; ikawa, watu na Yuda walipopiga kelele, Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.

·         Sauti zake ziliwakumbusha watu juu ya ibada hekaluni ,tarumbeta pia katika vita wakati wa mavuno na wakati wa sikukuu.

·         Upulizaji wa tarumbeta uliambatana na maombi wakati wa ibada hekaluni au wakati wa sikukuu.

·         Tarumbeta zilimkumbusha  MUNGU juu ya agano lake na watu wake,pia ziliwakumbusha watu wawe tayari kwa ajili ya siku ya BWANA.

 “Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia;” Yoel 2:1

·         Wakati wa vita sauti ya tarumbeta  iliyoambatana na maombi ilimwita MUNGU awaokoe watu wake,dhana hii ni msingi wa wokovu kwa watakatifu.

 

Ufunuo 8:3-4

Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.

Pamoja na maelezo ya huduma za kila siku hekaluni huko Yerusalem yaliyobainishwa hapa;

Kitabu cha kiyahudi cha ufafanuzi {biblia} hueleza kwamba katika kafara ya jioni mwanakondoo aliwekwa kwenye madhabahu na kuhani aliyeteuliwa alichukua chetezo cha dhahabu hekaluni ka kufukisha uvumba kwenye chetezo cha dhahabu katika mahali patakatifu na kuhani alipotoka alitupa chini chetezo kiasi cha kutoa kelele au sauti kuu,katika hatua hiyo makuhani saba walipuliza tarumbeta zao wakiashiria mwisho wa huduma za hekalu kwa siku hiyo.

·         Mtu anaweza kuona lugha ya huduma ya jioni ilivyotumiwa katika Ufunuo 8:3-5 ni muhimu kwamba malaika wanapokea uvumba kwenye madhabahu ya BWANA ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.

“Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.” Ufunuo 5:8

uvumba  huwakilisha maombi ya watu wa MUNGU  .

·         Tarumbeta hufatia kifo cha YESU kama mwanakondoo na huendeleza mfululizo katika historia nzima hadi marejeo.

 Ufunuo 11:15-18

Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Munguwakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki.Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.

 

“Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.” Ufunuo 8:5

 

“Naye akamwambia mtu yule aliyevaa bafta, akasema, Ingia kati ya magurudumu yazungukayo, yaani, chini ya kerubi, ukaijaze mikono yako yote miwili makaa ya moto, toka katikati ya makerubi, ukayamwage juu ya mji. Akaingia ndani mbele ya macho yangu.”Ezekieli 10:2

·         Malaika anajaza moto kutoka kwenye  chetezo kutoka kwenye madhabahu  husika ambapo maombi ya watakatifu yaliyowasilishwa.

·         Hii ishara huwakirisha kwamba hukumu za tarumbeta 7 huwaangukia wakazi wa dunia katika kujibu maombi ya watakatifu.

·         Watu wa MUNGU hawajasahaurika na MUNGU ataingilia kati kwa niaba yao katika wakati wake.

·         Tukio la kiishara kwa tarumbeta katika ufunuo hudokeza  juu ya hatua ya MUNGU ya kuingilia kati katika historia kama jibu la maombi ya watu wake wakati ambapo kimsingi muhuri unawahusu wale wanaodai kuwa watu wa MUNGU.

“Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.” Ufunuo 8:13

Tarumbeta 7 hukamilisha historia nzima tangu wakati wa yohana hadi hitimisho la historia ya dunia hii Ufunuo 8:3-6

Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige.na injiri ikihubiliwa duniani.

 

Tarumbeta zinapulizwa na huku maombezi yakiendelea mbinguni na injiri ikihubiliwa duniani.

Hukumu za tarumbeta hizi ni kwa sehemu tu na huathiri theluthi tu ya uumbaji.

Tarumbeza 7 hutangaza kwamba muda umewadia kwa ajiri ya MUNGU kutwaa utawala wake sitahiki {tarumbeta 7 zinahusika takribani katika vipindi husika vinavyohusika na makanisa 7}

1.       Tarumbeta mbili za kwanza hutangaza kwamba muda umewadia kwa ajili ya MUNGU kutwaa utawala wake sitahiki {tarumbeta 7 zinahusika takribani katika vipindi husika vinavyohusika na makanisa 7

Ufunuo 8:7-8

Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu.

2.       Tarumbeta ya tatu na ya nne huonesha mwitikio wa mbingu kwa uasi wa zama za kati na baada ya matengenezo.

Ufunuo 9:1-21

Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu. Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani.Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye.Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.

3.       Tarumbeta ya tano na sita hueleza hali katika ulimwengu wa roho kipagani na baada ya zama za maarifa zinazobainishwa kwa utendaji  mkubwa wa nguvu za kishetani zinazokusanya ulimwengu wote kwa vita ya HAR-MAGEDONI

Ufunuo 16:12-16

Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.

4.       Tarumbeta ya 7 hueleza juu ya ufalme wa dunia kupita na ufalme wa kristo kutwaa mamlaka yake kuu na kumiliki pia huufunua muda hekalu la MUNGU kufunguliwa na sanduku la agano kuonekana ndani ya hekalu kama mkataba wa watakatifu kuishi na MUNGU wao.

 Ufunuo 11:15-19

Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Munguwakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki.Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi. Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.

 

Na hapo ndio mwisho wa somo hili kwa wakati huu.

Mungu akubariki sana

 

Post a Comment

0 Comments