100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

UFUNUO WA MAKANISA 7 - Mwl: Azory Michael

UFUNUO WA MAKANISA 7 
KWA AJILI YA MAKANISA 7 INJILI IMEKUJA KUTOKA PATIMO MPAKA ASIA

PATIMO ni eneo la kisiwa chenye urefu wa maili 10 na upana wa maili 6 ni kisima pekee kilichotumiwa na serikali ya rumi kama sero au gereza kwa watu wote walioonekana waaminifu na wafuasi kamili wa kristo YESU,hii ikawa sababu ya Yohana kutupwa huko.

INJILI PATIMO - Ni ujumbe wa kristo Yesu alioagizwa yohana kuuandika kwa ajili ya makanisa saba yaliyoko ASIA kama mfano wa nabii kutoka kwa Mungu unabeba ishara na huduma za kimbingu uliotumwa kwa makanisa kama mfano wa kanisa moja la MUNGU.

Ufunuo wa Yohana 11:19

“Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.

SABABU YA UJUMBE HUU - katika karne ya kwanza BK,miji mingi ya ASIA ilianzisha baada ya wafalme wao kwenye mahekalu yao kama ishara ya uaminifu wao kwa serikali ya RUMI.

Desturi ya kumuabudu mfalme ikafanyika sheria na ikiwa ni lazima,raia walitegemewa pia kushiriki katika matukio ya umma na sherehe za kipagani na kwasababu wakristo wengi walikataa kushiriki katika desturi hizi,walikabiliwana dhiki na hata nyakati Fulani kufia dini.

·        Ni ujumbe uliotumwa kwa ajili ya kuwasaidia katika changamoto zao.

·        Ni sababu moja muhimu iliyosababisha makanisa 7 tu kuchaguliwa kwanza hali zao za kiroho zinaendana na kanisa la Mungu katika nyakati tofauti za historia.

Jumbe 7 zimekusudiwa kwa mtazamo wa kimbingu kuonesha mandhari ya mfululizo mzima wa hali ya ukristo tangu karne ya kwanza hadi ya mwisho.

 

MPANGILIO WA MAKANISA YALIYOLENGWA HUKO ASIA

Ufunuo wa Yohana 1:11-20

 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;

na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.

Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;

na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.

Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

 

KANISA LA EFESO – maelezo yake utayapata katika;

Ufunuo wa Yohana 2:1-7

Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.

Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;

tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.

Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.

Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.

 

KANISA LA SMIRNA – maelezo yake utayapata katika;

Ufunuo wa Yohana 2:8-11

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.

Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.

Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

 

KANISA LA PERGAMO – maelezo yake utayapa katika;

Ufunuo wa Yohana 2:12-17

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.

Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.

Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

 

KANISA LA THYATIRA – maelezo yake utayapata katika;

Ufunuo wa Yohana 2:18-29

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.

Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.

Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.

Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;

nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.

Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.

Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.

Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.

Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

KANISA LA SARDI – maelezo yake utayapata katika;

Ufunuo wa Yohana 3:1-6

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.

Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.

Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.

 Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.

Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

KANISA LA FILADELFIA – maelezo yake utayapata katika;

Ufunuo wa Yohana 3:7-13

 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.

Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.

Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.

Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.

 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

 

KANISA LA LAODIKIA – maelezo yake utayapata katika;

Ufunuo wa Yohana 3:14-22

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Leo nimepata kibali cha kueleza kanisa 1 kati ya 7,kwasababu maalum kabisa lakini katika wakati ujao nitaelezea na mengine kadri roho mtakatifu atakavyoniongoza.

Leo nitaelezea kanisa la LAODIKIA – Kwa sasa kanisa lipo katika hali ya ULAODIKIA;

Ni mfano wa kanisa la leo,ni kanisa la mwisho kutajwa na YESU lilikuwa laodikia mji wa kitajiri uliokuwa katika barabara kuu ya kibiashara.mji huo ulikuwa mashuhuri kwa kiwanda cha kutengeneza sufu,na mabenki yaliyohifadhi kiasi kikubwa cha dhahabu na shule za kitabibu zilizo tengeneza dawa ya macho.

Ukwasi wake uliwajaza raia wake hali ya utoshelevu takribani mwaka 60 BK tetemeko lilipo haribu mji huu.

Raia wake walikataa msaada kutoka Rumi wakidai wana kila kitu kilichohitajika ili kufanya kazi hiyo kwa kuwa mji ulikosa maji na yalipatikana kutoka au kupitia mfereji uliotoka kwenye chemichemi ya maji ya moto katika mji wa Hierapolis kwasababu ulikuwa mbali maji yalifika kwao yakiwa vuguvugu

Ufunuo wa Yohana 3:14-17

Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

 

Hosea 12:8

“Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.

Tathimini ya kristo juu ya laodikia,Yesu hakuwakemea wakristo wa laodikia kwa ajili ya dhambi ya kutisha au uasi.badala yake tatizo lao lilikuwa hali ya kuridhika iliyopelekea udhaifu wa kiroho kama yalivyokuwa maji yaliyofika kwenye mji wao huo hayakuwa na ubaridi wenye kuburudisha wala joto bali uvuguvugu,walidai kuwa matajiri na wasio hitaji chochote.lakini walikuwa masikini,uchi na vipofu katika hali yao ya kiroho.

Kanisa huko laodikia huwakilisha vyema hali ya kiroho ya kanisa mwishoni mwa historia ya dunia hii huonyeshwa kwa viunganishi thabiti vya vitenzi sawa na;

Ufunuo wa Yohana 16:15

“(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)”

Kuhusiana na maandalizi kwa ajili ya dhahama ya mwisho kanisa la mwisho litakuwa katika katika nyakati za hatari.

Misukosuko mikubwa ya kisiasa,kidini na kidunia na litakabiliwa na changamoto ambazo hazikuwahi kukumba kizazi chochote kilichopita.

Na hivyo kanisa hili lihali ya utosherevu wa mali na utajiri mpaka inafika mahali hawahitaji msaada wa MUNGU ile hali rohoni ni vuguvugu.

Onyo la kristo Yesu kwake lina maana gani???

Lina maana ya kina sana kwa ajili ya wote ambao ni sehemu ya kanisa la siku za mwishoni.

YESU anawahakikishia kwamba watu kwamba anawapenda na kwamba hatawaacha sawa na kanisa la leo ambavyo analipenda na hataliacha.

Ufunuo wa Yohana 3:20

“Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” anahitimisha kwa wito wake akisema nipo mlangoninabisha hodi,mtu akisikia sauti yangu  na kufungua mlango nitaingia kwake name nitakula pamoja naye kama mpenzi katika kitabu cha

Wimbo Ulio Bora 5:2-6

Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.

Nimeivua kanzu yangu; niivaeje? Nimeitawadha miguu; niichafueje?

Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni, Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.

Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondoza manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo.

Nalimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie.

akiwa amesimama mlangoni  na kubisha akisikia afunguliwe ili aingie ndani anahitaji karamu ya pekee ya kina pamoja naye.wito huu haupaswi kutupiliwa mbali.

Ufunuo wa Yohana 3:18-22

Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ni shauri ambalo Yesu aliwapatia watu wa laodikia.

je dhahabu na mavazi meupe  na dawa ya macho huwakirisha nini???

1 Petro 1:7

“ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”

Ile kwamba kujaribiwa kwa imani yenu ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto kuonekana kuwa kwenye sifa na utukufu  na heshima katika kufunuliwa kwake Yesu kristo.

Isaya 61:10

“Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.”

Waefeso 1:17-18

Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;

macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;

Haya yote huliambia nini kanisa la siku za mwisho lililo  mfano wa kanisa la LAODIKIA???

Ni wito wa kristo Yesu kwamba pamoja na utajiri,ukwasi na shule za matibabu za dawa za macho  na dhahabu bado kanisa linahitaji msaada wake maana tumaini la wito wake jinsi lilivyo na utajiri wa urithi wake maana kwamba kanisa lisiingie kwenye hali ya utoshelevu wa mali kiasi cha kutohitaji msaada wa MUNGU kwani hufanya hivyoni nje ya urithiwake katika watakatifu.

 

Namshukuru MUNGU kwa maarifa haya yenye uzima na kwa ajili yako uliyetoa muda wako kusoma Mungu wa Israel aishivyo akubariki nahitaji maombi yako ili nilete masomo mengi zaidi.

MUNGU AKUBARIKI SANA

Post a Comment

0 Comments