100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

SOMO: MSAADA WA MUNGU KWA ULIMWENGU KATIKA MABADILIKO YA MSIMU HUU MPYA - C.Mwakasege

SOMO: MSAADA WA MUNGU KWA ULIMWENGU KATIKA MABADILIKO YA MSIMU HUU MPYA - C.Mwakasege

WhatsApp Group Link

Facebook Page

UTANGULIZI

MALENGO YA SOMO

  • Kukujulisha kuwa kuna mabadiliko makubwa yanakuja ulimwenguni na unahitaji msaada wa Mungu kukabiliana nayo.
  • Kukujulisha msaada wa Mungu uliopo ili ikiwa utataka akusaidie kufanikiwa katika mabadiliko yaliyoko sasa na yanayokuja ndani ya msimu huu mpya upate msaada wa Mungu.

Na hili si somo la kawaida bali ni mafundisho ya kimaandalizi. Kwa hiyo ni somo ambalo ndani yake kuna mafundisho lakini lengo lake ni kukuandaa na kukujulisha mambo ambayo yako.

 

JAMBO LA KWANZA

I. MABADILIKO HAYA (YA MSIMU HUU MPYA) YANAGUSA ULIMWENGU MZIMA KWA KUTUMIA LANGO MOJA

Yapo mabadiliko yanayokuja na mengine yamekwisha anza kutokea tayari yanagusa ulimwengu mzima kwa kutumia lango moja. Maana yake ni kwamba lango moja linaweza kuleta mabadiliko ulimwengu mzima.

Na pia tunajua kabisa kufuatana na kitabu cha Waebrania 11 Biblia inasema “kwa imani twafahamu ya kwamba ulimwengu uliumbwa kwa Neno la Mungu”. Kwa hiyo tunajua kabisa ya kwamba ulimwengu uliumbwa. Na kuna ulimwengu wa roho na wa mwili na ndani yake umebeba vitu vingi sana vilivyoumbwa na Mungu.

Na katika uumbaji wake ulimwengu hakukuwa na dhambi. Lakini maandiko yanatuambia ya kwamba dhambi iliingia ulimwenguni Warumi 5:12,14, na wala haituambii ilipotokea lakini tunajua ya kuwa dhambi iliingia ulimwengu kwa kupitia mtu mmoja. Kwahiyo mtu mmoja alikuwa lango. Na lango hili likafungua mlango kiasi ambacho kila kitu kilichokuja na dhambi kiliwafikia watu wote.

Kwa hiyo maana yake ni kwamba kuna malango ambayo yakifunguliwa ulimwengu mzima unaguswa katika msimu huo. Kwa hiyo kama ndani ya ulimwengu kuna mataifa na kuna watu binafsi ukiachia vitu vingine inamaanisha ya kwamba:-

1.Chochote kinachogusa ulimwengu kinagusa mataifa,

2.Chochote kinachogusa mataifa kinagusa taifa.

3.Chochote kinachogusa taifa kinagusa kila mmoja aliyeko ndani ya hilo taifa.

Na hii ni kwa sababu mataifa yako ndani ya ulimwengu na taifa liko ndani ya ulimwengu na wanadamu wako ndani ya ulimwengu. Kwa hiyo chochote kile kinachogusa ulimwengu hugusa mataifa. Kikigusa mataifa basi uwe na uhakika kuwa hakuna taifa litakalo pona.

Pia kikigusa kila taifa bas kila mtu ataguswa kwa  namna moja au nyingine. Kwa hiyo ukibadili ulimwengu utabadili pia na mataifa, na taifa na familia na mtu mmoja mmoja.

Na kwa sababu hiyo si suala la kujiandaa kukwepa bali ni suala la kujiandaa kiusahihi namna ya kusimama kwenye msaada wa Mungu ili uweze kupita salama na kwa ushindi. Maana hakuna mtu ajuaye upeo wa mabadiliko yanayokuja, kina cha mabadiliko yanayokuja, muda wa mabadiliko hayo yatakaa mpaka lini na hata kutokujua uzito wa mabadiliko hayo. Lakini hivi vyote Mungu anajua na ukitaka kupata msaada kaa naye kwa namna ambavyo haijalishi yanakuja na upeo mkubwa kiasi gani au yana uzito kiasi gani lakini wewe utakuwa salama ndani ya Yesu.

Tatizo kubwa sana watu wanamtaka Yesu lakini hawataki kumsikiliza anapotoa tahadhari na maonyo na maandalizi. Na wakati mwingine wanakuwa na imani sana kuliko Yesu mwenyewe. 

Watu wengi wanapopewa maonyo wanafikiri si kitu cha imani, lakini maandiko yanatuambia kwa imani Nuhu akiishi kuonywa na Mungu alikuwa anatekeleza maelekezo aliyopewa ambayo yalikuja kwa ajili ya mabadiliko yanayokuja katika ulimwengu mzima. Lakini si kila mtu alisikiliza yale maonyo maana wengine walipuuzia. Kwa hiyo Nuhu kila alichokuwa anafanya alichukua tahadhari, angepuuzia na yeye angeenda na maji! Haijalishi ana haki kiasi gani au anampenda Mungu kiasi gani. Kuwa ndani ya Yesu haitoshi kama utashindwa kufuata maelekezo anayokupa.


JAMBO LA PILI

UHARIBIFU UMETUMIKA KUFUNGUA LANGO LA MSIMU MPYA NA KUINGIZA MABADILIKO KATIKA ULIMWENGU MZIMA

Huu ni uharibifu ambao tumeuona toka 2019 ambao ulipewa jina la COVID19 na wengine wanaita Corona toka 2019. Huu mlango umekuja kama uharibifu lakini ndani yake umefungua lango la msimu huu mpya. 


MIFANO MICHACHE JUU YA MALANGO YA  UHARIBIFU  KIHISTORIA

MFANO WA KWANZA

Mwanzo 1:1-3

Mara ya kwanza niliposoma hiyo mistari nikafikiri ni kama vile umejaza ndoo hivi  halafu Roho Mtakatifu akakaa juu ya ndoo hivi juu ya maji Roho Mtakatifu akasema No! Kasome Biblia yako vizuri.

Ukisoma mistari inayofuata unaona Mungu anagawa maji kwa sababu maji yalikuwa yamejaa toka kwenye mbingu mpaka kwenye nchi na maandiko yanasema aligawa maji akatengeneza anga na lile anga akaliita mbingu na maji yaliyokuwa chini akayakusanya mahali pamoja halafu akayasambaza sehemu mbalimbali nchi kavu ikaonekana, kwa hiyo nikajua hiyo ilikuwa ni gharika ya kwanza. Kuna vitu vilikuwepo lakini Biblia haituambii kwa sababu huwezi kusema pamekuwa na ukiwa kama havikuwepo vitu, huwezi kusema pamekuwa na utupu kama havikuvuliwa vitu. 

Tunajua Mungu hakuumba giza lakini tunaliona kwenye Mwanzo 1:2 limetoka wapi? Angalia mahali Mungu aliingilia-katikati ya uharibifu! Lilikuwa lango la msimu mpya mkubwa sana ambao tunaendelea nao mpaka leo. Kwa sababu ndio msimu uliofunguliwa kwa ajili ya kutengenezea nyakati na siku kwa sababu siku inaumbwa baada ya nuru na giza kutenganishwa.


MFANO WA PILI

Mwanzo 8:1-22

Kwa hiyo gharika ya pili iliyotokea kipindi cha Nuhu, iliharibu mpaka siku, ule uharibifu ambao Nuhu alikuwa anafunguliwa kwenye ukurasa wake na lango jipya la maisha mapya alianza na uharibifu na kila kitu kilikufa  walipona yeye na watoto wake, na wake zao na mke wake. 


MFANO WA TATU

Mwanzo 41:57

Umewahi kufikiri njaa inaingia katika Dunia nzima halafu kuwe na chakula nchi moja tu inaitwa Misri. Lakini ni mbegu iliyokuwa inafunguliwa na iliyokuwa inapandwa kwa ajili ya msimu mpya ambao  tunauona kwenye kutoka 12:1-2


MFANO WA NNE

Kutoka 12:1-2

Unaona Mungu anazungumza anawaambia wana wa Israel Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. na kalenda ya Wayahudi inafuatilia hili mpaka leo.  Pia pale ndipo taifa la Israel lilifunguliwa kuwa saa ya ulimwengu kwa ajili ya majira na nyakati za kinabii zinazoujia ulimwengu mpaka sasa na mpaka mwisho. Walikabidhiwa Kuwa saa rasmi ndio maana kalenda yao haiendani na sisi wanaenda tofauti kwa kuhesabu wao. Mungu alikuwa anatengeneza si tu msimu mpya kwa ajili yao lakini alikuwa anatengeneza msimu mpya kwa ajili ya Dunia nzima lakini angalia mahali ilipotokea njaa Dunia nzima.


MFANO WA TANO.

Luka 22:20

Tunajua agano jipya lilianza rasmi Msalabani na linarasimishwa ndani ya watu baada ya Mungu kumfufua Kristo kutoka kwa wafu. Pasipo kumwaga Damu hakuna agano. Kwa hiyo agano jipya limeanzia msalabani baada ya  kufa kwa Yesu. 


MFANO WA SITA

VITA VIKUU VYA PILI VYA DUNIA (WWII) 

Maana vilianza mwaka 1939 vikaisha mwaka 1945 na vilianza na nchi mbili tu yaani Ujerumani wakiwa na Hitler walikuwa wanavamia Poland halafu mataifa mawili Uingereza na Marekani wakajiunga. Vile vita vikawa vinapiganwa na ndani yake kukawa kunapandwa mbegu ya mabadiliko ya msimu mpya kwa sababu vile vita vilitengeneza vitu vingi vipya ambavyo vinatawala ulimwengu mpaka leo. 

Vita hivi vilisambaa kila mahali duniani hadi hapa Tanzania vilipiganwa ila vilifungua Benki ya dunia (WB) - kusuluhisha suala la shida ya uchumi iliyokuwa kubwa sana na maskini walikuwa wengi, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) - kurudisha mzunguko wa fedha kwa sababu uliharibika kabisa, Umoja wa Mataifa (UN) - kutafuta amani na haki za binadamu dunia nzima kwa sababu Dunia ilihitaji sana amani.

Kwa upande wa Ulaya, Wayahudi walishiriki sana vita  na waliteswa sana. Mwaka 1947 baada ya vita hayo mashirika yaliyoundwa yalionekana hayasaidii kwa ukubwa sana sasa akawepo kiongozi mkubwa wa kijeshi akatengeneza kitu kinaitwa Marshall Plan.

Ulikuwa ni mpango kabambe wa Marekani kusaidia nchi za Ulaya kwa jinsi zilivyopata shida na ukaanza kutekelezwa mwaka 1948.

Baada ya miaka michache baadaye ilizaa Umoja wa Ulaya wa Kimaendeleo (OECD) na unaendelea mpaka leo. 

Kwa hiyo unaweza ukaelewa mfumo wa uchumi tulionao leo ulitokea kwenye uharibifu hata sasa usishangae utapitia kwenye COVID-19. Ndio maana nimeenda mbali kukueleza Kibiblia kwa sababu usipoeleza Kibiblia unaweza ukabanwa na kila mtu akisema chochote anachotaka kusema ila ukienda kwenye maandiko utapata maana halisi. 

Kilichotokea kwetu kwa sasa katika mazingira haya ni sawasawa na kile kilichotokea kwenye kile kipindi ambacho kipo kwenye kitabu cha  Kutoka 12:23 ukisoma sambamba na Kutoka 12:13 Hii ina maana ya kwamba lango hilo lilifunguliwa kwa kufa kwa wazaliwa wa kwanza. Kama hii taarifa asingepewa Musa na Biblia ikanyamaza hapo, ingekuwa mtihani kwetu kwamba nani kaleta pigo hilo wengi wangesema ni shetani kwa sababu hatumwoni Mungu akipita kwa style hiyo. 

Hapo mambo mawili yalitokea kwa yeye kuona damu (Mungu alipopita usiku huo)

1.Atazuia pigo la kwake (adhabu ya Mungu) 

2.Atamzuia mharibu (adhabu ya shetani) 


Popote ambapo Mungu anaweka cha kwake shetani naye atataka aingie. Mfano Mathayo 13:24-30 kuhusu habari ya mpanzi aliyepanda shamba lake na alipolala naye adui akaenda kupanda mbegu za magugu halafu zikaota zote na wale watu waliokuwa wakichunga pale shambani hawakujua tofauti zake mpaka ilipofika kipindi kuwa yale ni magugu. Yesu akawaambia waviache vyote viwili kwani washachelewa ingekuwa vizuri wangevitoa pale mwanzoni ila sasa waviache vikue na yaliyopandwa pale vikue mpaka wakati wa mavuno ndio watenganishe. 


JAMBO LA TATU 

KOSA LINAPOFUNGUA LANGO LINALOGUSA ULIMWENGU, ADHABU YAKE INAGUSA VINAVYOHUSIKA NA VISIVYOHUSIKA

Warumi 5:12,14 Haijalishi kosa limetokea kwenye nchi ipi au kwa mtu yupi, kama ni lango limefunguliwa unaweza ukaona hilo jambo liko mbali lakini uwe na uhakika litafika na kwako pia.

Kumbuka kipindi cha Nuhu katika Mwanzo 7:20-24 utaona kila kilicho na pumzi kilikufa. Mfano hata samaki wote walikufa isipokuwa wale wawili waliokuwa ndani kwenye safina tu. 

Kutoka 11:1-7 Mungu anasema bado pigo moja akizungumzia kuhusu wazaliwa wa kwanza kuanzia yule anayeketi kwenye kiti cha Farao hadi yule mtu wa kawaida. Fikiria kosa afanye Farao halafu adhabu impate mtu wa chini. Farao ndio mwenye shingo ngumu ya kuwa awaruhusu waende au wasiende lakini maandiko yanasema hakukuwa na nyumba isiyokuwa na msiba. 

Mfano mwingine ni wakati wana wa Israeli walipokuwa wanaingia katika mji wa Yeriko. Walimwacha Rahabu na ndugu zake tu waliokuwa katika ile nyumba. Na hii ni kwa sababu ya kile kiapo lakini wengine wote mpaka watoto wanaonyonyeshwa waliuawa sasa fikiria nao wamekosa nini? Hawana kosa lolote ila na wao waliuawa.

Tuangalie kwenye mfano tulionao, Mwaka 2019 Covid iliingia haijalishi iliingilia wapi lakini ninachotaka ujue ni kuwa inapita kila nchi. Suala sio mahali ilikotokea bali ni tunajiandaaje inavyokuja. Watakuja na watafiti kutafiti na kuja na majibu yao. Lakini COVID inagusa Mataifa yanayohusika na yasiyohusika. Umewahi fikiri kuona mtu anakufa kwa Corona lakini haijui kama inaitwa Corona?. Swali linalokuja hapa kibiblia na sio kisiasa, ninakuambia kitu ambacho Mungu kanipa kazi ni kwako ukifanyie kazi au ukiache, lakini kuna saa inakuja ni afadhali ujipange na Mungu kwa namna ambavyo itakusaidia.

Fuatilia utajua kila nchi Corona imegusa na kuna mabadiliko yanakuja, japo unaweza kukataa kubadilika lakini maadam mto unakuja utakubeba tu hata kama hautaki, sasa kama haujajiandaa hutojua utakupeleka wapi, utakusomba tu kama karatasi. 


JAMBO LA NNE 

TOBA ITAKUKUTANISHA NA MUNGU KATIKATI YA UHARIBIFU

Ndani yake kuna mambo kadhaa nataka niyachambue kidogo uweze kuelewa kidogo kidogo, Na kitu kimojawapo ni:- 


1.UPENDO WA MUNGU KATIKATI YA UHARIBIFU HUWA UNALETA TOBA

Kwenye Matendo ya Mitume 3;19 kuna aina ya toba hapo, maana zipo za aina nyingi.  Tofauti yake utajua kwenye matunda yake.

Inasema "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;"

Kwa hiyo ni toba ambayo inagusa mazingira ya nyakati. Maana yake kuna nguvu za Mungu zilizokuja katikati ya huo uharibifu na zimeweka madai ndani ya mioyo ya wanadamu kudai toba. Toba ina lugha nyingi na mojawapo ni kama unasema Mungu akusaidie kubadilika kwa sababu kuna mahali ulikosea na unahitaji msaada. Ndio maana unaweza tubu kwa dhambi ya Taifa.

Hii sio toba tu ya kwenda mbinguni, bali ni toba inayomruhusu Mungu aingilie nyakati zilizoko


2.TOBA KWA MUNGU INAFUNGUA MSAADA WA MUNGU KUPITIA DAMU YA YESU

Yohana 15:13 Aliutoa uhai tukiwa kifungoni tumehukumiwa katikati ya uharibifu na Shetani alitaka kuitumia hiyo nafasi kutumaliza alishangaa tu upendo wa Mungu umetubeba.


3. DAMU INASHUGHULIKIA KOSA LILILO ZAA ADHABU YA MUNGU NA UHARIBIFU WA SHETANI

Tumeangalia ile Kutoka 12:12 na 23 unaona kuna pigo la Mungu. Pia hapo hapo shetani kuna kitu alikuwa anawinda, na ndio maana Mungu alihakikisha sio tu kwamba alizuia adhabu lakini pia na mashambulizi yaliyokuja na hasira ya kutaka kulipa kisasi kwa watoto wa Mungu.

Kwenye Kutoka 8:5-11 pigo mojawapo ni  vyura vilivyojaa kila mahali, na Farao nae akaita wachawi nao wakaleta vyura yaani wakaongeza adhabu juu ya adhabu. 

Swali linakuja, mtu wa kawaida ambae hakuweko kule ambako Farao,wachawi na Musa walipokuwa wanapambana ghafla anaona vyura wanaingia je anaweza tofautisha kati ya vyura wa kutoka Mbinguni na kutoka kwa shetani?.

Sasa kwa mtu wa kawaida hawezi kutofautisha kati ya vyura ambavyo vinatoka kwa Mungu kama adhabu na vile ambavyo vimeletwa na shetani  kwa sababu anataka kujitutumua na yeye ili na yeye aonekane.

Sasa hapa nataka ujue kuwa haijalishi COVID imeingia katika mlango upi lakini yuko Mungu aliye hai ambaye anaweza akaiondoa. Haijalishi uharibifu unakuja kwa kutumia mlango upi lakini iko nguvu katika Damu ya Yesu ambayo inaweza ikatusaidia.


4. DAMU YA YESU INADAI MUNGU AWE UPANDE WETU KATIKATI YA UHARIBIFU HUU NA MABADILIKO YAKE

Ukiingia katika toba na ukaiitia Damu ya Yesu inaingia kazini wakati huo huo. Sasa kuna madai ambayo Damu ya Yesu inapeleka na moja wapo ni kuwa Mungu awe upande wetu katikati ya uharibifu huu.

Warumi 5:8 Pendo la Mungu linaonekana kwetu kwa Yesu kufa tungali wenye dhambi. Sasa unaweza kujua kwanini Mungu alimfuata Rahabu katikati ya ukahaba. Alimpa imani ya kuchomoka kule akiwa bado ni kahaba.

Mungu anakuja kukutoa kwenye dhambi ukiwa bado dhambini. Hakusubiri umetoka shimoni ndipo aseme nilikuwa nakusubiri hapa ndipo nikutoe. 

Ndio maana  katikati ya uharibu usijaribu kumtafuta shetani. Maana ni kawaida yake kutaka kujiinua kwa sababu ya kiburi chake akapigwa mbinguni akateremshwa huku chini na bado anataka kuendelea kujiinua katika kila kitu kinachoitwa Mungu na anataka kujiinua.

Kwa hiyo hata kama unaona mazingira yameharibika sana unaona kama Mungu kakukasirikia na hutegemei tena kama atakuja kukusaidia. Ila kumbuka kuwa ukiomba toba inadai Mungu aje kukusaidia.


5. MSAADA WA MUNGU UNAPOKUTOA KWENYE UHARIBU UNADAI ANAYESAIDIWA AWE UPANDE WA KWAKE KATIKA MABADILIKO YANAYOFUATA

Yohana 15:13-14 Huu ni upendo wa ajabu sana wa Yesu lakini baada ya kuutoa uhai wake kwa ajili yetu sisi rafiki zake na yeye anadai tufaute maelekezo ambayo anatupa.

Kitu kilichowakwamisha wana Israel kuingia katika nchi ya Kaanani katika kitabu cha Hesabu 14:11. Mungu alimwambia Musa kuwa hawa watu watanidharau mpaka lini. Alafu aliuliza swali la pili kuwa hawataniamini mpaka lini. Alafu anasema tena pamoja na ishara zote ambavyo nimefanya katikati yao nilipokuwa nawatoa Misri.

Lengo la Mungu kufanya ishara zote zile alipokuwa anawatoa Misri mahali ambapo hawakutegemea kama wangetoka ilikuwa ni kujenga imani zao  kwa Mungu ambaye anawatoa.

Sasa usishangae sana watu wanaomba Mungu awatoe katika janga hili la Corona lakini baada ya muda wanarudi tena katika vitu ambavyo havijakaa sawa halafu wanashangaa hawasogei tena. Kwa hiyo lazima kuwe na mabadiliko makubwa sana na sio kidogo.

Pia si tu Damu ya Yesu inadai tu Mungu akae upande wako katika uharibifu maana ndio maana ya toba lakini pia inaleta na madai kwako pia kuwa ukae upande wa Mungu. Utakapokuwa ndani yake  ushirikiane nae katika kufuata maelekezo yake.

Corona itaisha lakini hujui mbegu ambayo itaachia na kutoka. Mpaka sasa hatujasikia vita kuu ya tatu ya dunia (WW III) lakini tumesikia tu vita ya pili ya Dunia (WW II).  Lakini angalia kitu ambacho kipo Duniani. IMF, WORLD BANK, UN  pia baada ya vita ya pili ya Dunia kulitokea Cold war. Vita kati ya Mabepari na Wajamaa.

Hayo mabadiliko yote yalitokea baada ya vita ya pili ya Dunia. Hayo mabadiliko yalifuata kila nchi Duniani.  Maana sasa watu wengi wanajua tu hiyo Corona imetokea China lakini sasa imefika kila nchi Duniani. Pia nenda kagoogle yale mashirika ya umoja wa mataifa ambapo yalitokea. Utashangaa sana kuona ni  baada ya vita vya pili vya Dunia. 

Sasa nataka tukaombe toba kwasababu kuna sekta ambazo zitaguswa na Mungu kaniambia mabadiliko hayo ambayo yatakuja. 

*******************************


 UHUSIANO WA UHARIBIFU NA MABADILIKO KATIKA LANGO LA MSIMU MPYA

Na katika kujifunza na kuangalia jambo hili yako mambo kadhaa ambayo ningetaka tuyatazame na kujifunza:- 

JAMBO LA KWANZA

I. MUELEKEO WA MABADILIKO

Muelekeo wa mabadiliko ambayo ninayazungumzia sasa. Utaona inafanana-fanana sana na kitu kilichotokea na kugusa ulimwengu.

Yako mabadiliko kama manne hivi:-


BADILIKO LA KWANZA

MABADILIKO MENGINE YAMEKWISHA ANZA KUTOKEA NA MENGINE BADO YANAKUJA

 

BADILIKO LA PILI

MABADILIKO YA MSIMU HUU HAYATATOKEA YOTE KATIKA SIKU ZA KUFANANA KWA KILA ENEO

 

BADILIKO LA TATU

MABADILIKO YATAGUSA SEKTA MBALIMBALI KWA MUDA TOFAUTI NA KWA UPEO TOFAUTI NDANI YA MSIMU

 

BADILIKO LA NNE

MABADILIKO YATAGUSA MATAIFA MBALIMBALI KWA VIWANGO TOFAUTI NDANI YA MSIMU ILA HAKUNA TAIFA AMBALO HALITAGUSWA

 

Nitakapoanza kukupa MWELEKEO WA MABADILIKO YANAYOKUJA kwa kupitia hizo sentensi hizo nne zitakupa kupata picha. Mabadiliko mengine yameshaanza kutokea na nitakapokuwa nikizungumza nawe utaanza kupata picha.

 

JAMBO LA PILI

II. MGONGANO WA KUSUDI LA MUNGU NA LILE KUSUDI LA SHETANI KATIKA LANGO LA MSIMU MPYA

 

Waamuzi 5:8

“Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arobaini wa Israeli?”

Haya ni malango ya ulimwengu waroho ambayo yanazungumziwa. Soma*Kutoka 12:23,13,12*

Kwa hiyo ndani ya hiyo mistari miwili yaani 23 na 13 unaweza kuona pigo la Mungu na mharibu pia akiwa kazini. Na huyu mharibu tunampa jina la shetani akiwa na mipango yake akiiweka hapo kwenye lango hilo hilo. Kwa hiyo kwenye lango hilo hilo kuna pigo la Mungu na uharibu wa shetani. 

Mstari wa 12 nataka uone hili neno asemalo “nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri” kwa hiyo pia alikuwa anahukumu miungu ya Misri katika kipindi kile kile. Na walichokuwa wakigombania ni Lango lile la ule wakati. Lakini pia walikuwa wakigombania Israeli kama lango na wazaliwa wa kwanza kama lango.

Kwa hiyo si suala ni kitu gani kinaendelea sasa na tataizo la COVID ulimwenguni bali suala ninalotaka uangalie langoni kulipita nini?. Lango la COVID lilifunguliwa mwaka 2019 ndipo ilipotamkwa rasmi.

Tunaweza kuangalia sasa mambo yanayotokea nchi mbalimbali Dunani. Lakini nataka uangalie kwenye lango kulitokea nini! Kwa sababu unaweza usielewe kabisa vinavyotokea sasa kama hutajua kilitokea nini kwenye lango. Ugomvi upo langoni na hapo ndio mahali pa kuangalia sana.

Ukizungumzia suala la Covid-19 au Corona watu wanawaza kinachotokea sasa na mara nyingi sana wakikitazama hawakioni kwenye Biblia kwanini? Kwa sababu hawajui kilichotokea kwenye lango.

 

JAMBO LA TATU

III. KUSUDI LA MUNGU KUTOA ADHABU KWA MWANADAMU NI NINI?

Yeremia 23:20

“Hasira ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa.”

Inamaanisha ya kwamba katika zile siku zao waliweza kuelewa kidogo lakini si sana. Lakini Biblia inasema katika siku za mwisho itakuwa rahisi sana kulifahamu neno hili. Na hizi ni siku za mwisho maana zilianza kuhesabiwa kuanzia siku ile ya Pentekoste Roho Mtakatifu aliposhuka. Kwa sababu aliposhuka ndipo Petro aliposema ya kwamba “haya mnayoyaona yanatimiza maandiko, yanatimiza maneno aliyosema nabii Yoeli ya kwamba itakuwa katika siku za mwisho”

Kwa hiyo inamaanisha kuna kitu kilichofunguliwa kwenye ufahamu na  mbinguni ya kwamba sasa haya mambo niliyosema yatafahamika siku za mwisho. Kwa hiyo ni  ruksa kwa wanadamu kuyapata sawasawa na jinsi Mungu anavyotaka na Roho Mtakatifu akaingia kazini kuhakikisha ya kwamba anaachilia huo ufahamu kidogo kidogo.

Adhabu ina kusudi. Kwa sababu hasira imezaa adhabu, na ndani ya adhabu kuna kusudi. Maandiko yanasema “Hasira ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake”

 

Mithali 23:13-14

“Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.”

Kumbuka adhabu  inapotolewa na shetani naye anawahi hapo hapo. Hasa kama ni lango linahusika kwa hiyo ni vigumu sana kutofautisha chura wa Mungu(Adhabu ya Mungu) na chura wa wachawi (Kutoka kwa shetani).

Kama ni mzazi ambaye umenuia kitu kizuri kwa ajili ya mtoto wako maandiko yanasema adhabu inapotokea saa hiyo haionekani Kuwa nzuri, ni baadae utaona ikikusaidia kwa kiwango kipi ndipo unaanza kuheshimu kitu ambacho baba yako au mama amekufanyia. Baba au mama yeyote ambaye anampenda mtoto wake anapokuwa na hasira juu ya kile kitu ambacho hakubaliani nacho na anaona kabisa huyu mtoto anapanda mbegu mbaya katika maisha yake ya baadae  ujue hutanyamaza. Hiyo hasira haitarudi kwa sababu ndani yake kuna makusudi ya kutaka kuona huyu mtoto hapotei.

Kwa hiyo hasira ya Mungu ni matokeo ya upendo wa Mungu. Kwa sababu Mungu hawezi kutupenda na wakati huo huo akatuchukia. Kwa hiyo chanzo ya hasira ya Mungu sio chuki  bali ni upendo.

Kwa hiyo adhabu ya Mungu, kusudi lake 

  • Kuzuia kisichompendeza Mungu kuendelea, na ikifika adhabu namna hiyo ujue Mungu ametoa maonyo mengi sana.
  • Kuharibu mbegu na matunda mabaya,

Kwa sababu kunapokuwa na mabadiliko ya nyakati namna hiyo kuna mbegu pia katikati ya uharibifu zinapandwa. Kwa hiyo adhabu ya Mungu inapokuja haiji tu kwa ajili ya kuzuia ambacho hakimpendezi kisiendelee kuwepo lakini anafuatilia pia ndani mbegu zote zife na matunda yake yasiwepo.

Ndio maana ni vigumu sana kuelewa adhabu ya Mungu inapofika kwa watoto wachanga mpaka usome namna hii, inakuwa rahisi kwako mpaka uwe umesoma Biolojia kwa sababu wale wataalamu wa mifugo kuna mbegu wasingetaka ziingie kwenye Zizi au ziendelee kwenye kizazi cha wanyama wako.

Watu wengi hawaelewi kwanini wana wa Israel wake watoto wao sio walioleta shida kule jangwani, walioleta shida ni watu 10 tu. Lakini adhabu ya Mungu inapopita katika msimu mpya wanaingia na watu wasio husika. Kwa sababu Mungu anasema hawa watu watanidharau hata lini! Halafu wapo mlangoni mwa mto Yordani wavuke. Mtakaa  jangwani miaka 40 Mpaka kizazi kile kiishe. Kwanini asingewaua wote mara moja tu anao huo uwezo! 

Wale vijana walikaa kwenye adhabu ya miaka 40 wakizunguka na wao, kwa kosa ambalo sio la kwao. Mungu alikuwa ahakikisha Kuwa hakuna mbegu inavuka Yordani ambayo haijakaa sawa. Lakini ilimgharimu miaka 40. Halafu ilikuwa ni kitu cha ajabu sana kwa sababu Mungu alikuwa nao kule mchana na usiku, wakiomba maji na chakula walikuwa wanapewa. Ndio maana ukiona Mungu anakufanyia muujiza usije ukafikiri amekukubalia kuingia msimu mwingine, unapata muujiza lakini bado uko jangwani. Usifurahie kwa sababu yuko na wewe kwenye mzunguko! 

Wana wa Israel walikaa miaka 40 wanazunguka na Mungu tu wanafurahi kweli kweli na Mungu alikuwa anasubiri mpaka mtu wa mwisho afe ambaye hataki avuke. Ni vile tu tukifika mbinguni hatutakuwa na muda wa kuuliza vya huku duniani tena maana huko kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya lasivyo tungekuwa na maswali mengi sana ya kuzungumza na Yesu tunapokuwa na fellowship! Maana tutakuwa na fellowship nae milele. Lakini tunamshukuru kwa hivi vichache anavyotupa ili vitusaidie tuweze kumtazama Mungu katika upana.  

  • Kupanda mbegu nzuri, kwa sababu haui tu mbegu mbaya lakini anapandikiza mbegu nzuri. Ni kupanda mbegu za Mungu za mabadiliko ili zizae mabadiliko anayotaka. 

Kwa hiyo adhabu siku zote pia ina mbegu nzuri ndani. 


Soma Zaburi 65:8-9 na Zaburi 110:3. Katika zaburi ya 110:3 anazungumzia tumbo.

Katika Biblia ya kiingereza lile neno tumbo anazungumzia tumbo la uzazi, hazungumzii tumbo la chakula, kwa hiyo kama asubuhi ni tumbo na kama asubuhi ni lango inaamisha mambo kadhaa ambayo unahitaji kuyafahamu.

Maandiko yanatuambia nyakati ziliumbwa kufuatana na Matendo 17:26 na kwa kupitia mtu mmoja Mungu akafanya mataifa mbali mbali akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tokea zamani, kwa hiyo nyakati zimeumbwa kabla ya mtu. 

Katika kitabu cha Mwanzo 1, kitu cha kwanza ambacho Mungu alifanya kwenye ule mstari wa tatu ni kusema kuwe nuru na ikawa Nuru. Kwa hiyo kulikuwa ni msimu mwingine kwa sababu msimu wa kwanza Roho Mtakatifu alikuwepo lakini kulikuwa na ukiwa na utupu kitu ambacho hakikuwepo pale ni neno lake. 

Kwa hiyo unaweza ukawa na Roho Mtakatifu lakini ukawa bado gizani, hali ya ukiwa na utupu usikuachie. Roho Mtakatifu lazima afanye kazi na Neno. 

Mwanzo 1:3 unaona Mungu alipotaka kitu kipya kitokee alisema kuwe Nuru. Kumbuka kitu gani kilichotokea baada ya  nuru kuja. Mungu hakutaka kuondoa giza, kwa sababu maandiko yanatuambia kwenye Yohana 1 Nayo nuru yang'aa gizani wala giza halikuiweza.

Kwa hiyo nuru ikitokea giza linatakiwa kuondoka lakini Mungu akatenga nuru na giza ili ipate kujulikana ya kwamba msimu huu kuna nuru na kuna giza. Lakini akagawa akaliita nuru mchana na giza usiku akaita siku moja. Hakusema siku ya kwanza bali alisema siku moja. Maandiko yanatuambia asubuhi ni lango na jioni ni lango kwa hiyo unaona nyakati zilivyoanza.


1. LANGO LA NYAKATI NI TUMBO LA UZAZI NA LINAPOKEA MBEGU  ILI LIZAE KWA JINSI YA MBEGU

Kwa hiyo unaweza ukaelewa ugomvi uliopo kati ya Mungu na shetani kwenye lango la nyakati kwa sababu wote wanawahi hilo tumbo. Tumbo halina shida linasubiri mbegu tu, atakayewahi tumbo amepata kiwanda.


2. IKIWA ASUBUHI NA JIONI NI LANGO KWA HIYO SIKU INA MALANGO MAKUBWA MAWILI 


3. SIKU NI LANGO LENYE MALANGO MAWILI NDANI YAKE


4.IKIWA ASUBUHI NI TUMBO LA UZAZI KWA HIYO ASUBUHI NI LANGO LA TUMBO LA UZAZI


Kuna kitu kinaachiliwa kila asubuhi, unaweza kuelewa Maombolezo inaposema fadhili zako ni mpya kila siku asubuhi, kwa sababu ndipo zinateremshwa asubuhi.

Unaelewa ni kwanini kwenye sala ya Bwnaa tunasema "utupe Leo riziki yetu" hatusemi "utupe leo riziki itakayotosha miaka kadhaa ijayo " kwa sababu ni sala inayofungua lango la fadhili kwa siku. Mtu anaekufadhili maana yake anakuwezesha. Kwa hiyo fadhili za Mungu zinaachiliwa kila siku, Shetani akibana hapo langoni  itakuwa ngumu sana kwako kupita.

Na ndio maana moja ya baraka wana wa Israeli walipewa ni kumiliki lango la adui zao.


5.UKIONA TUMBO LA UZAZI LIMEZAA KITU UJUE MBEGU ILIPANDWA SIKU NYINGI KABLA

Kwa lugha ya kibinadamu ukiona mama anajifungua leo ujue mbegu ilipandwa miezi 9 kabla. Ninachotaka uone ni kuwa hupandi mbegu siku hiyo hiyo alafu ukavuna siku hiyo hiyo.


Isaya 13:11

"Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;"

Hiyo ni adhabu inayokwenda kwenye ulimwengu, na adhabu inapopelekwa kwenye ulimwengu lazima ujue haiendi kugonga watu kwanza inagonga mazingira yake ya kiroho na ya kimwili. Kwa sababu ulimwengu ni mazingira, Watu watapata shida kwa sababu mazingira yamepata adhabu.

Na adhabu ya Mungu inakusudi, ambayo inamaanisha kuna vitu vinavyoendelea katika ulimwengu wa kiroho na wa kimwili ambavyo Mungu havipendi na ameingilia kati kuvizuia, na pia kuna mbegu zilizopandwa kwenye ulimwengu wa roho ambazo hazimfurahishi na matunda yake yameanza kuonekana, na kaamua kuzinyamazisha. Lakini anatumia nafasi hiyo hiyo kupanda mbegu za kwake.

Waebrania 11:3 inasema Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

Kwa hiyo kama ulimwengu uliumbwa kwa neno, ukitoka kwenye utaratibu na kusudi la Mungu, Mungu atatoa maonyo kwa jinsi anavyotaka kuyatoa, tusiposikia maonyo adhabu inakuja inapiga ulimwengu.

Ndio maana lazima uelewe kwanini Mungu aliupenda ulimwengu kwanza, haisemi "Mungu aliwapenda watu", Wanadamu wamo ndani ya ulimwengu. 


JAMBO LA NNE 

4.KILICHOMKASIRISHA MUNGU NI NINI?

Vipo vitu viwili vikubwa,


CHA KWANZA 

I).WATU KATIKA ULIMWENGU KUSEMA WANAMWAMINI MUNGU HUKU HAWAMTEGEMEI.

Wapo wasiomuamini na hawamtegemei kabisa lakini kundi kubwa linamwamini Mungu lakini halimtegemei kabisa.


1 Timotheo 6:17

"Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, *bali wamtumaini Mungu* atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha."

Biblia haisemi "bali wamuamini" inasema "bali wamtumaini", kwenye kiingereza kuna "TRUST" na "FAITH" ni vitu viwili tofauti, msisitizo mkubwa sana wa Biblia hauko kwenye kumuamini bali kumtumaini.


Mwanzo 3:1-3

"Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa."

Angalia Shetani alivyokuwa mjanja hakukataa kuwa Mungu yupo lakini alikataa kuwa maneno aliyosema Mungu sio sahihi. Ulimwengu ndio ulioumbwa kwa neno na Mungu.

Shetani hana shida ukimuamini Mungu kwa sababu na yeye anaamini na kutetemeka, unakuwa tishio kwake ukianza kumtumaini na kumtegemea Mungu. 


CHA PILI 

II) KANISA KUTOKUSIMAMA KAMA MUNGU ATAKAVYO KATIKA ULIMWENGU.

Kuna nafasi ambayo Mungu ameiweka ndani ya kanisa na kanisa lipo ndani ya ulimwengu. Unajua ni kwanini Yesu alituombea kwa Mungu asitutoe katika ulimwengu, Yesu  anajua tunayo dhiki. 

Maandiko yanasema sisi ni chumvi, Chumvi peke yake sio Chakula inakuwa nzuri sana kama ikichanganywa na kitu kingine. Sisi tunataka tukae tu wenyewe, kaangalie chumvi iliyopo kabatini haina faida mpaka ichanganywe.

Maandiko yanasema sisi ni nuru, kwanini tunataka tukae kwenye nuru wakati tunatakiwa tung'ae gizani. Ukilalamika unapowekwa mahali pagumu basi hujui wewe ni nani kwa Bwana, kwa sababu si kila wakati utapelekwa mahali pazuri tu Mungu anataka kionekane cha kwake ndani yetu wajue kuwa yupo Mungu alie hai ndani yako.

Maandiko yanatuambia sisi ni mbegu ya ufalme wa Mungu, Popote pale ulipo wewe ni mbegu ambayo Mungu ameipanda anategemea kuona matunda popote pale ulipo, kwenye biashara,  kazini kanisani. Ulipozaliwa mara ya pili iliwekwa mbegu ikakuzalia imani, Mungu anatamani kuona matunda na yapate kukaa.

Au wewe umekuwa kama watalaam wa siku hizi ambao wanatengeneza machungwa ambayo hayana mbegu? Maana kwa mtu wa kawaida ni ngumu sana kuweza kutofautisha kati ya chungwa ambalo lina mbegu ndani na chungwa ambalo halina mbegu?.

Sasa huwezi kuzaa kitu kwa sababu hauna mbegu ndani. Hii ni kwa sababu tumbo lako la uzazi halina mbegu ndani. Pia ndani ya tumbo lako kila siku asubuhi unaachilia tu mbegu ya dini. Ni sahihi tu  unalinda dini yako lako na unaweza ukasonga mbele.

Mungu hajafurahia kanisa kutokaa kwenye nafasi yake. Maana kama ni kulalamika na sisi tunalalamika pia. Biblia ni inatumbia kuwa unapobeba ufalme wa Mungu unafanyika chachu kwa ufalme wa Mungu.

Chachu inafanya  kazi sana ya kuumua. Maana ukiweka chachu kwenye unga utapata taabu sana kiutoa. Sasa wewe ni chachu ya ufalme wa Mungu Duniani. Je mahali ulipo ile chachu ilipo? Kama hakionekani basi uje kuwa tatizo halipo halipo kwa uongozi bali lipo kwako.


JAMBO LA TANO.

5.KUSUDI LA SHETANI KULETA UHARIBU KWENYE MALANGO


  • KUBADILI MAJIRA NA SHERIA

Daniel 7:25

Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.

Mabadiliko yote ili yawe ya kudumu itakiwa na sheria pia zibadilike. Kwa hiyo kuna sheria nyingi sana Duniani zitadilika. Pia kuna nchi mbalimbali zimeshaanza kutazama sheria zao kwa upya. Na lengo kubwa  ni kudhoofisha Watakatifu.

Biblia inatuambia kuwa kila jambo lina kusudi kwa  muda na majira maalumu. Kwa hiyo shetani akibadilisha majira  anakuwa anavuruga vitu vingi sana. Ukisoma Biblia utaona mifano mbalimbali.

Mungu aliwaambia Wana Israel kuwa watakaa utumwani Misri kwa miaka 400. Lakini walitoka baada ya miaka 430. Ile miaka 30 ya nyongeza ina maana shetani kuna kitu alikuwa anataka kupitisha pale ili kuwavuruga 

Siku zote Mungu yupo ontime lakini kama hamtaki kujiandaa hawezi kuwalazimisha. Ukisoma habari za Daniel unaona ya kuwa miaka michache ilipobaki kabla ya kuondoka Babebi alianza kufanya maombi ya toba.

Hii ni kwa sababu mbegu za majira huwa zinapandwa kabla majira hayajafunguliwa. Ili yakifunguliwa yale  majira yanatoka na matunda ndani yake ili yaendelee kuzaa.

Mtu akikunyang'anya mbegu anakuwa kakunyang'anya future. Ndio maana shetani naye anawahu hapo ili kupambana na watu wa Mungu ambao wameokoka. Sasa na wao badala ya kumtazama Mungu wanaanza kutazama mazingira ambayo yamewazunguka. Kwa sababu hiyo hata Roho Mtakatifu akisema nao hawasikii maana wanasubiri wanadamu ndio waseme .Wanadamu wakisema huwa maneno yao wanayaheshimu sana kuliko neno la Biblia ambalo Mungu kawaagiza. Sasa kwa mazingira hayo wanategema Roho Mtakatifu atuandae kutokea wapi?

Haijawa kazi rahisi sana kwangu kwenda katika Baraza la Mungu ili Mungu anipe mambo haya. Maana nimekuwa nikieleza mambo haya hatua kwa hatua tangu  mwaka 2017. Na mke wangu anajitahidi sana kuandika notes na tarehe  kwa hiyo katunza kumbukumbu.

Kuna watu hawajajindaa kumsikiliza Mungu na kila cha Mungu ambacho kinakuja wanaweka kiulizo. Wanasahau ya kuwa shetani na yeye yupo kazini katika lango hilo hilo ili aweze kuwabadilishia watu vitu.


  • KUWABADILISHIA MBEGU YA MUNGU

Adamu alikuwa ni mbegu ya Mungu Duniani na shetani akaiwahi pale pale katika Bustani. Sasa unafikiri kwanini shetani asiwepo katika hili lango la COVID 19. Kwa ajili kudhoofisha watu wa Mungu.

Maandiko yanatuambia katika 1Mambo ya Nyakati 12:32 wana wa Isakari ambao wanazijua  nyakati na mambo ambayo wana Israel wanatakiwa wayatende. Kwa hiyo katika ya nyakati kama hizo na umuhimu huo badi unawahu kwa mzee Isakari unawachukua watu wale na kupanda mbegu za kwako.

Hii ni kwa sababu hawa vijana wamendaliwa kujua nyakati na vitu ambavyo Israel wanatakiwa wavitende.Kama wasiposema ina maananisha wana Israel hawajatajua kitu cha kufanya.

Wakati wa sasa ni tofauti na ule wa zamani maana sasa tunae Roho Mtakatifu na tuna Biblia pia tunaweza soma. Wenzetu zamani  hawakuwa na hiyo nafasi ina maana Mungu alikuww anategemea watu waaminifu ndio waseme na watu.Majira ya sasa tumepewa nafasi nzuri sana tofauti na majira ambayo wenzetu walikuwa nayo 

 

  • KUWAFANYA WATU WANAOMUAMINI MUNGU WASIMTEGEMEE

Shetani pia hajabadilika kama alivyofanya kwa  adamu ndivyo anafanya na sasa. Akiona unamuamini Mungu anatafuta usimtegemee. Si kila kitu unamtegemea maana unaweza ukamwamini Mungu katika masomo na usimtegemee. Akina Daniel tunaona ya kuwa  walimuamini Mungu na akawasaidia katika masomo yao na maisha baada ya masomo aliwasaidia pia.

Ni rahisi sana ukamwamini Mungu katika utumishi wako na usimtegemee bali ukategemea ujanja wako na umaarufu wako tu. Pia hata kuomba huombi kwa sababu sasa umekuwa muimbaji  au mhubiri mzuri sana.

Badala ya kumtegemea Mungu sasa unategemea mialiko maana hata ukiitwa huombi tena kwa Mungu. Na si rahisi sana kukuona tena shetani naye anatoa vyura kama wale ambao Mungu alitoa vyura.

Ndio maana Paulo alipo waandikia 2 Wakorintho 11:3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.


JAMBO LA SITA

6. UMUHIMU WA KUOMBA TOBA YA MUDA MREFU

Katikati ya uharibifu Mungu huwa anaachilia toba na mtu ambaye anawahi hiyo toba kuifanya huwa anapata pendo la Mungu. Kuna toba za aina nyingi katika Biblia.

Mfano mmojawapo ni ile ya Matendo ya mitume 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana

Kwa hiyo ni toba ambayo inatengeza mazingira ya malango ya nyakati ili Bwana aweze kuyasimia. Unatubu mpaka hilo jambo limeondoka.

Lengo kuu la toba ya muda mrefu ni kumbadilisha Mungu asiendelee na adhabu bali awese kutusaidia katika maisha yetu.

Ezekiel 22:30 inasema nikatafuta mtu miongoni mwao atakaye litengeneza boma. Kwa hiyo Mungu anatafuta mtu kila mahali atakayesimama katikati ya Mungu na nchi ili Mingu asije akaipiga nchi kwa ghadhabu yake.

Mungu anasema na sikuona mtu maana yaje hakuna mtu aliyekuwa tayari kusimama katikati ya ghadhabu ya Mungu na  nchi. Kwa hiyo tutafanya toba hapa katika maeneo haya-:

3. Kanisa lisimame katika nafasi.

Maana watu wengi sana ni waoga wanaogopa kumtaja Mungu katikakati ya wenzao au mbele za watu.

Mungu anataka watu wamtafute Mungu hata kama ni kwa kupapasa papasa waweze kumuona. Mungu yeye haimsumbui hata kama unamtafuta kwa kupapasa papasa uweze kumuona. Mungu angalia moyo wako  hata kama umesema maneno machache yeye ataangalia moyo wako unasemaje na atakusaidia.

Tunasoma maandiko kuwa Mungu alimtafuta mfalme wa Yuda japo alikuwa ni mdogo sana lakini Mungu alimfanikisha. Nia yake ndani imlimsaidia Mungu kuweza kumfanikisha.


NAMNA YA KUOMBA MSAADA WA MUNGU KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWA MAOMBI YA AINA YA KUUTAFUTA USO WA MUNGU

2 Mambo ya Nyakati 7:13-14

“Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni;  ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”

Mstari wa 14 umetenganisha juu ya kuomba na kuutafuta uso wa Mungu maana Biblia inasema “kuomba, na kunitafuta uso” sasa ana maana gani hapa? Tusome na kitabu cha Yeremia

 

Yeremia 29:10-13

“Maana Bwana asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa. Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.”

Unaona  sauti ya Mungu ilikuwa ikitoka ndani yao na unaona kabisa wakitenganisha kuomba na kuutafuta uso wa Mungu. Kutafuta Uso ni aina fulani ya kuomba ambayo unahitaji kutazama kwa ndani kidogo kama tutakavyoangalia leo kufuatana na nyakati tulizonazo.

Kuna mambo angalau matatu ambayo ningetamani kuku-kumbusha na kuku-eleza kabla sijaendelea zaidi katika mtiririko wa leo:-


JAMBO LA KWANZA

A. MABADILIKO YALIYOPO TOKEA MWAKA 2019 NA YANAYOKUJA YANAGUSA ULIMWENGU WA KIROHO NA ULIMWENGU WA KIMWILI KATIKA MATAIFA YOTE NA KILA TAIFA NA FAMILIA NA TAASISI NA MTU BINAFSI.

 

B. MSAADA WA MUNGU WA KWANZA KABISA UNATUJIA NDANI YA MAZINGIRA TULIYONAYO (HAIJALISHI NI MAGUMU AU MABAYA AU MACHAFU KIASI GANI) KWA NJIA YA UPENDO WAKE

Biblia inasema kwenye Yohana 3:16 kwamba “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”  na Warumi 5:8 inatueleza jinsi ambavyo tunalitambua pendo la Mungu lilivyo ambalo lilikuwa ndani ya Kristo ambaye alitupenda tungali wenye dhambi. Maana angekuwa ametupenda tungali watakatifu basi tungekuwa tunapata shida sana kwenda mbele za Mungu tukiwa na dhambi.


C. MAOMBI YA TOBA YA MUDA MREFU YANAHITAJIKA SANA ILI KUMPA MUNGU UHALALI WA KUTUSAIDIA KATIKA LANGO LA NYAKATI.

Matendo ya Mitume 3:19

“Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;”

Maana yake ni Toba ambayo iko katika lango la nyakati. Iko katika kuingilia kati nyakati ili shetani asije akazivuruga, asije akavuruga kile Mungu alichokikusudia katika lango hilo.

 

Waamuzi 5:8

“Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni;”

 

JAMBO LA PILI

NI LILE LILILOTOKEA MWAKA 2019 NA LINALOENDELEA KUTOKEA ULIMWENGUNI KATIKA MSIMU HUU MPYA HASA KATIKA HIZI NYAKATI ZA MWANZO WA MSIMU

Mambo yaliyotokea mojawapo ni hili


KUYUMBA KWA KIPATO AU MAPATO NA AKIBA NA MATUMIZI YAKE

Kumbuka tulikotoka na ujue ya kuwa jambo hili linagusa ngazi za kimataifa, taifa,familia, taasisi, kampuni na mtu binafsi pia.

Na hii ni kwa sababu ugonjwa huu wa Corona ulipotokea mazingira ya kutafuta kuukabili ulibadilisha vyanzo vya mapato na kuvibana kwa hiyo kulitokea shida kwenye ajira na kulitokea shida kwenye biashara na baada ya hapo hata makanisa yaliyokuwa yanategemea sadaka na yenyewe yapo kwenye shida (Crisis).

Mpaka kuna nchi zilikuwa zinaangalia namna ya kupunguza misaada kwa nchi zingine. Lakini hili ni jambo ambalo lilishasemwa na Mungu kabla.

Wale ambao wanakumbuka nikiwa hapa  Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mbeya nilisema haya amambo ya msimu mpya ili watu wapate kujiandaa na kujipanga mapema kabla hayajaanza kutokea.

Nilizungumzia suala la mapato na kuweka akiba kwa mtu binafsi, na kwa taasisi, kanisa, biashara, ofisi naa nchi. [Pia  nikakupa na utaratibu na namna ya kufanya.

Hilo jambola msimu mpya sio kwamba litatikisa upatikanaji wa mapato na utunzwaji wa akiba, lakini na matumizi yake na kutakuwa na changamoto na vikao vingi sana kitu gani kifanyike ili kunusuru hiyo hali.

Kwa wengine lilikuja na maumivu makali kiasi kwamba yakaanza maswali ndani yao:-

Swali la kwanza. Kwa nini mimi? Hivi Watu wote wamepata shida kama ya kwangu, mbona mimi nimepoteza kazi lakini wengine bado wapo kazini, mbona biashara yangu imefungwa na wengine bado zinazofanya kazi?

Swali la pili Mimi sielewi ni kitu gani kinachoendelea?, wengine wamediriki na kusema simwelewi Mungu.

Swali la tatu Ndio nafanya nini?, nafanya kitu gani niongeze kipato, umewahi kufikiri hali uliyonayo ikienda kwa miezi sita ijayo au mwaka moja ujao utakuwa katika hali gani?.

Inaweza ikafika mahali Covid ikaisha lakini vipato vya watu vikabaki kuwa na shida.  Kumbuka kwenye lango la majira mapya mbegu hupandwa.

Swali la nne, Mungu yuko wapi! Mbona hili jambo nililikabidhi kwa Bwana mbona kuko hivi, mbona hili jambo ndio alianzisha Bwana kumetokea kitu gani.


JAMBO LA TATU.

3.MUNGU ANAPOTAKA TUMTAFUTE USO WAKE ANA MAANA GANI?

Katika kujibu hili swali nataka tuangalie vipengele vifuatavyo:-


KIPENGELE CHA KWANZA

1.UNAPOPITA MAHALI PAGUMU  MUNGU ANAPELEKA UJUMBE KWA WAHUSIKA ILI WAMTAFUTE

Zaburi 27:7-9

Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia, Unifadhili, unijibu.  Uliposema, Nitafuteni uso wangu, Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.  Usinifiche uso wako, Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira. Umekuwa msaada wangu, usinitupe, Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.

Nyakati pia nazo zina malango yake. Kwa hiyo ujue kuwa Mungu amepeleka ujumbe ili wamtafute Bwana maana kuna kizazi ambacho kitapokea huo ujumbe na kitaitwa kizazi ambacho kinamtafuta Bwana.

Kwa hiyo sasa tunahitaji kuamua kuwa sisi tutakuwa ni kizazi gani. Je ni kizazi ambacho kinamtafuta Bwana au  kizazi ambacho kinamdharau Bwana?.


KIPENGELE CHA PILI

2. KWANINI MUNGU ANATAKA TUTAFUTE USO WAKE KWANINI ASISEME TUITAFUTE MIKONO YAKE AU MIGUU YAKE?

Maana wengi huwa wanatafuta mikono ya Mungu.

Isaya 59:1-2

Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Hapa tunaona ya kuwa sio kwamba Mungu amejificha bali ni dhambi zetu ambazo zimefanya uso wake tusiuone.


Isaya 59:3-4

Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.

Sio yeye aliyesababisha uso wake ujifiche bali ni dhambi zetu zimeficha uso wake tusiuone. Dhambi inapoleta madhara kwa ulimwengu na adhabu yake inawapata na wale ambao hawahusiki. Kwa hiyo unapotubu usije ukajisahau ukatubu tu peke yako. Lakini kumbuka kuwa kuna mahali ilikotokea.


KIPENGELE CHA TATU.

3. KUUTAFUTA USO KUNA NINI NDANI YAKE TOFAUTI NA MAOMBI MENGINE

2 Mambo ya Nyakati 7:13-14

Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na *kunitafuta uso*, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

Katika hii mistari huwezi kuona haraka haraka lakini mpaka urudi katika:-

Yeremia 29:13

Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Katika  Yeremia 29:13 anasema Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

Hapa anazungumza juu ya maombi ya kawaida kabisa.

Lakini katika mstari wa 13 anazungumzia juu ya kumtafuta lakini mstari wa 14 anasema Nami nitaonekana kwenu.

Tofauti yake hapa ipo kwenye hali ya moyo wa mtu katika kuomba na kutafuta. Maombi ya kawaida ya kuutafuta uso na kuomba kawaida yanatofautishwa na hali ya moyo wa mwombaji.

Si kila mwombaji anaomba kwa sababu yupo kwenye shida. Ila huwezi kuutafuta uso wa Bwana kama hauko kwenye shida.


VITU VYA KUTAZAMA  HALI YA MOYO WAKO ILI UJUE UPO KATIKA HALI YA KUUTAFUTA USO WA BWANA AU KUFANYA MAOMBI YA KAWAIDA.


KITU CHA KWANZA

MOYO WAKO UNATAFUTA NINI? AHADI YA BWANA AU BWANA ALIYEKUPA AHADI?

Yeremia 29:13-14a

Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.  Nami nitaonekana kwenu..


Linganisha na Mathayo 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa

Lile neno tafuteni nanyi mtaona ni jumla. Kwa hiyo unapomtafuta Mungu je unatafuta nini?. Kuna watu wanatafuta ahadi za Mungu na hawamtaki Mungu. Ukiona wanatubu si kwamba wanatubu ili Mungu aweze kuwasikia wanatafuta uso wake, bali wanatafuta mikono ya Mungu.

Ukisoma habari za Musa katika Kutoka 33:15,16,14 utaona inasema Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.

Musa alisema itajulikanaje ya kuwa nimepata neema machoni pako? Watu wengi sana wanalinganisha kama wamepata neema machoni pa Bwana kwa sababu ya vitu walivyopata. Lakini Musa aligoma kuangalia vitu bali alikuwa anamtaka Mungu.

Alisema Mungu najua umeniahidi kwenda Kaanani na Malaika na ushindi kila mahali. Lakini kwa sababu Mungu uso wako hauendi pamoja na sisi usitutoe hapa.

Sasa Dunia nzima inakuta watu wengi wanaomba sana lakini lengo lao ni kutaka Corona iondoke lakini hawamtaki Mungu. Wanataka Corona ikiisha waendelee na maisha yao ya kawaida. Sasa hivi ndio watu wanagundua  kuwa kuna "*New normal*". Yaani kawaida mpya. Katika taarifa za habari za kiingereza ndio huwa wanasema sana hivyo.

Sasa kama watu wa kawaida kabisa wanajua kuwa ile kawaida ya zamani imeondoka. Kwa nini sisi watu wa Mungu tunadhani kuwa  ile kawaida ya zamani itarudi?

Unapokuwa kwenye shida au mahali papya au katika lango lolote lile, Mungu hasemi tafuta nikutoe kwenye hiyo shida bali anasema tafuta kwanza uso wangu. Maana yake tafuta Mungu ajulikane, afahamike na aonekane kuwa yuko upande wako.

Watu kesho wakiona umevuka basi wasitoe utukufu kwa mtu yeyote yule bali Mungu pekee ndiye apewe utukufu. Biblia inakuruhusu kuwa ukiisha kupata uso wake, sasa tafuta kitu unachotaka kutoka kwa Mungu maana sasa yupo hapo. 

1 Mambo ya Nyakati 16:10-11

Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.   Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.

Watu wengi wanatafuta nguvu za Bwana ila hawamtaki yeye mwenye nguvu. Wanataka miujiza na ahadi zake lakini hawamtaki Mungu. Wakiisha kupokea wanasema tutaonana tena wakati mwingine ujao. Kwa hiyo hawana habari naye.

Inapofika kumtafuta Bwana, Roho Mtakatifu hatakuwekea ndani yako kutafuta vitu kwanza bali atakuwekea ndani yako kutafuta uso wa Mungu. Atakuwekea kwanza utafute kutengeneza mahusiano yako na Mungu ili Bwana aonekane uso wake kwako na kila mtu ajue. Haijalishi ya kuwa  umechafuka kiasi gani lakini Bwana amekuonekania kabisa. Pia japo walifikiri hautafika ila wanashangaa unawapita kama basi lililojaa.

Bwana aliwasemesha akina Musa kitu cha ajabu sana alisema uso wangu utaenda pamoja nanyi na mimi nitawapa raha. Anapewa raha jangwani kabla hata hajafika Kaanani. Kwa hiyo katikati ya uchungu utasikia raha. Utakapokuwa unaendelea kuomba namna hiyo utaendelea kupata raha nafsini mwako zaidi ya machungu unayopitia.

Ndio maana maandiko yanasema Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Mathayo 11:28-30

Haupumziki kwa sababu Yesu kachukua mzigo wako bali ni kwa sababu umejitia nira yake na umejenga nae mahusiano. Watu wengi huwa wanafurahi kumtwika Yesu mizigo yao na hawataki kujitia nira kwa Yesu na ndio maana hawana furaha katika maisha yao.

Ukitafuta uso wa Bwana uwe na uhakika utapata raha hata ukiwa jangwani. Ukiendelea kuutafuta uso wa Bwana utaona raha ndani yako. Maana ukiwa pamoja na Bwana hata katikati ya jangwani maana hata Kaanani utakuwa na Bwana.


KITU CHA PILI.

2. KAMA UMEUMIA MOYONI NA JAMBO LILOTOKEA NA HUWEZI KUOMBA ISHI KAMA ZABURI YA 77

Zaburi 77:1-20.

1-2 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.   Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.

Si rahisi sana kwa watu wengi kumtafuta Bwana wakiwa katika raha. Wengi wataomba maombi ya kawaida kabisa. Ndio maana ukiomba maombi ya kawaida katika taabu unaweza usitoke haraka.Pia hapa tunaona ya kuwa Mwimba Zaburi alikuwa kaumia moyo wake na nafsi yake ilikataa kufarijika alipokuwa anaomba.

3Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.

Kwa hiyo ndani yake alikuwa anasikia kufadhaika na anajiuliza kwa nini Mungu ameacha yale mambo yamtokee. Pia anaendelea kusema 4-5 Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Naliona mashaka nisiweze kunena.   Nalifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita

Unapopita mahali pa taabu na nafsi yako inakataa kufarijika jifunze kumtafuta Bwana. Japo ndani yako kunaweza kutokea upinzani na roho ya uchungu kuingilia na kusema kama kuomba si umeomba siku nyingi sana hapa unapoteza muda tu. Kama ni Mungu anasaidia mbona wewe hakutaki. Unaweza kuzomewa na kila aina ya maneno.

Katika Zaburi hii unaona kabisa alipoona kuomba kunapigwa vita aliilazimisha nafsi yake. Kwa hiyo alipokuwa anamkumbuka Mungu alisikia kuzimia. Pia alipojaribu kutafakari matendo ya Mungu alisikia kufadhaika. Mungu alimtia nguvu zake ili aendelee kutafakari shuhuda za Mungu.

5-6Nalifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita.  Nakumbuka wimbo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu ikatafuta

Kwa maana hiyo roho yake ilienda ndani kwenye maktaba yake huko moyoni na kukumbuka siku ambazo aliimba wimbo mzuri   ambazo aliona furaha, ushindi, amani na namna alivyomuona Mungu.

Sasa siku shida ikiingia na mashaka yakija hivyo vitu vinafichwa na kukanyagwa kabisa huko ndani. Kwa hiyo unakuwa na huzuni na hata ukitaka kumtafuta Bwana unashindwa. Maana unajaribu hata kuplay nyimbo unashindwa kwa hiyo unakaa kimya.

Ukikaa kimya Roho Mtakatifu anaingia kazini na kuanza kufukua ndani yako  zile nyakati za furaha ulizotembea na Bwana na siku za ushindi ulizotembea na Bwana. Kwa hiyo utakumbuka matendo makuu ya Mungu na shuhuda za Bwana. Na unatiwa nguvu ndani yako na unasema Bwana moyo wangu utakutafuta.


 NAMNA YA KUOMBA MSAADA WA MUNGU KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWA MAOMBI YA AINA YA KUUTAFUTA USO WA MUNGU

Nataka kukuongezea mstari mmoja kutoka kitabu cha Zaburi

 

Zaburi 14:2

“Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.”

Kwenye Biblia ya kiingereza huo mstari wa Zaburi anaposema mtu mwenye akili inasema “mwenye uelewa”, “mwenye ufahamu”.

Haijalishi umesoma shule za darasani au hukusoma ila suala la kumtafuta Mungu ni la kila mtu kwa sababu Dunia hii imeumbwa katika majira ambayo yanabadilika na tangu dhambi iingie kumekuwa na ushindani mkubwa sana kwenye lango.

Leo nataka kuzungumza na wewe vitu vichache kabla sijarudi kwenye kile kitu cha kumtafuta Mungu. nataka kukuongezea wigo kidogo juu ya 

BAADHI YA MABADILIKO AMBAYO YANAAMBATANA NA KUYUMBA KWA MAPATO NA AKIBA NA MATUMIZI KWA SABABU YANAGUSA VYANZO VIKUU VYA MAPATO (YAANI AJIRA NA BIASHARA) AMBAVYO NI SEHEMU KUBWA YA UCHUMI

Kumbuka hapa sizungumzii juu ya maendeleo bali nazungumza juu ya uchumi.

Kumbuka jambo hili, uchumi mzuri unatakiwa uzae maendeleo mazuri lakini si kila maendeleo mazuri ni matokeo ya uchumi mzuri. Na hii ni kwa sababu Uchumi ni mazingira ya kumsaidia mtu kufanikiwa kimaisha bali maendeleo ni vitu kuwepo na kuongezeka

Maendeleo yanahusu vitu na kwa sababu hiyo huwa tunajitahidi sana yahusu watu. Na wale ambao wanafuatilia masuala ya uchumi Duniani na maendeleo yaliyopo Duniani watajua kabisa mjadala na mazungumzo yaliyopo ni juu ya maendeleo kuhusu watu na yasihusu watu. 

Uchumi ni mazingira. Ukiharibu mazingira basi umeharibu uchumi. Na ni mazingira ya kiroho na kimwili. Je hujawahi kuona ulikuwa na mwenzako halafu gafla akawa na duka? Ukimfuata kuzungumza nae na kumwambia ndugu Mungu amekusaidia kwa kweli naona umeshafungua na duka. Lakini unashangaa anakuambua ndugu uchumi ni mbaya. Unajiuliza hili likoje,lakini kaangalie wanaouza maduka huku wakilalamika kuwa uchumi ni mbaya  angali na maduka wanayo. Na ulitegemea uone wanasema wana uchumi mzuri.


USHUHUDA

Mungu aliponiita kwenye utumishi alinieleza mambo mazito sana ambayo kwa namna ya kibinadamu ingekuwa ngumu sana kuelewa.

Wakati fulani zilikuja pinde tatu za mvua kwa njia ya ndoto. Niliona zimekita juu katika nyumba  ambayo tulikuwa tunakaa wakati ule(ilikuwa ni nyumba ya kupanga). Alafu zilieleka juu na kupotelea mbinguni.

Nikaenda kusoma Biblia ili kujua pinde za mvua maana yake nini. Niliona ya kuwa kuna agano ndani yake pale. Kwa hiyo namba tatu (yaani zile pinde tatu ambazo niliziona) ni namba ya Yesu. Kwa hiyo nilianza kuomba ili Mungu anipe kujua maana nilijua kile sio kitu cha kawaida kabisa.

Wakati naendelea kuomba ili Mungu anisaidie, siku nyingine nilizungukwa na upinde wa mvua kwa hiyo nikitembea nao ulikuwa unatembea kunifuata. Nilishangaa sana.Si mara kwa mara huwa naona hivi vitu ila kuna wakati fulani pia sikumbuki vizuri kama tulikuwa tunatokea Arusha kwenda Dodoma au Dodoma kuja Arusha. Tulipofika Makuyuni niliona upinde wa mvua ukija juu ya Boneti ya gari tulilokuwa nalo.

Kila mtu aliyekuwa kwenye gari aliona ile hali tukitembea nao unatembea nasi. Kwa hiyo nilichukua simu yangu nikapiga picha na ile picha ninayo mpaka leo. Ule upinde ulikuwa unaenda na sisi na ulitembea na sisi mpaka ukapotea.

Kwa hiyo nilipomuomba Mungu juu ya jambo hili alisema muuliza mama yako. Tulipatana  nini mimi na yeye juu yenu.

Wakati huo mama alipokuja  kututembelea nyumbani kwetu Arusha. Sasa baada ya kufanya sala ya usiku na kila mtu alikuwa kaenda kulala nilimuuliza  mama juu ya lile suala ambalo Mungu aliniambia nimuulize.

Wakati ule namuuliza mama alikuwa amesahau. Alisema Wakati akiwa darasa la nane katika shule ya Masista kule Tosamaganga Iringa  walimuomba nae akasomee Usista kwa sababu waliona maisha yake katika utumishi.

Mama alikataa kwa sababu alikuwa anataka apate watoto maana yeye ni mtoto wa kike wa pekee nyumbani kwao. Mama aliniambia kuwa alienda porini akaomba kwa Mungu akasema “Mungu ninajua unaniita katika utumishi lakini naomba nikaolewe ila watoto ambao nitakao zaa nimekupa wakutumikie”.

Fikiria jambo hilo sasa wakati Mungu ananigusa na miaka ambayo nilizaliwa. Wakati ule Mungu ananionesha hayo na siku nasema na mama ilikuwa  ni miaka ya 80  mwanzoni.


UHUSIANO WA  AJIRA NA VYANZO VYA MAPATO. NA MBEGU ZA MABADILIKO AMBAZO ZIMEPANDWA KUANZIA MWAKA 2019 NA AMBAZO ZITAENDELEA KUPANDWA.


KITU CHA KWANZA.

1).KUPOTEZA KAZI KUTAKUWA KUKUBWA SANA KULIKO AJIRA MPYA NA KUNA AJIRA AMBAZO HAZITARUDI SASA NDIO ZIMEFIKA MWISHO WAKE.

Hili jambo unahitaji kulifuatulia sana. Maana unaweza usione sasa katika mahali ulipo ila kama hujaliona basi ujue kuwa litakuja. Tangu mwaka 2019 COVID-19 ilipoingia eneo hilo ni mojawapo ya maeneo ambayo yameathirika sana. Kwa hiyo  hiyo ni mbegu ambayo imepandwa.

Kuna ajira ambazo zimepunguzwa ghafla. Hata yule mtu ambaye kakuajiri anakuambia kabisa kuwa si unaona wewe mwenyewe hali ilivyo sasa.

I) PIA TAASISI ZA KIFEDHA HASA BENKI AMBAZO ZINA AKAUNTI NYINGI SANA ZA WATU AMBAO WAMEAJIRIWA ZITAATHIRIKA SANA.

Itafika mahali watu kwa kukosa pesa wanashindwa kuweka hela katika account zao za benki. Pia akiba  ambazo  watu walikuwa nazo  katika benki hizo wataanza kuzichukua kwa wao kukosa fedha za kujikimu. 

Taasisi za fedha zitaanza kukimbizana kukusanya madeni maana watu wengi ambao walikopa hela katika benki sasa hawana ajira za kuweza kuwasaidia ili waweze  kufanya marejesho. 


II) ITATISHIA UENDESHAJI  NA AJIRA ZA  BENKI

Hii ni kwasababu gharama za uendeshaji zitapanda juu wakati mapato ambayo wanapata yatakwenda chini. Hii itasababishwa na mikopo mingi Kutolipika wakati huo.


III) KUNA BENKI AMBAZO ZITAKUWA NA  MKAKATI WA KUUNGANA (MERGERS)  ILI ZISIFILISIKE

Kuna baadhi ta benki ambazo zitakubaliana na zile ambazo hazitakubaliana.Lakini kutakuwa na vikao sana vya management(utawala)  ili kujadili masuala kadhaa.


KITU CHA PILI.

2). KUBADILIKA KWA MFUMO WA KUFANYA KAZI

Hii hali imeanza kubadilika na sehemu kubwa itabadilika kwa jinsi ya kudumu. Hii ni kwa sababu COVID-19 ilipoingia, kati ya ushauri ambao umekuwepo na unaendelea ni watu kupunguza msongamano na kufanya wale walioko ofisini wasiende ofisini kuepusha msongamano. Lakini wakagundua lazima kazi ziendelee sasa wale wenye uwezo na wana watu ndani ya ofisi zao wanaweza wakafanya kazi kwa kutumia kompyuta na mtandaowakiwa nyumbani kwao (Working from home) 

Katika kipindi cha mwaka 2020 tuliona watu wakianza kufanyia kazi nyumbani na Ofisini walibaki  watu wawili au mtu mmoja kwa ajili ya kujibu maswali fulani na kukaribisha Wageni.

Vikao vingine vya kitaifa na kimataifa vilikuwa vinafanyika katika maeneo fulani na watu husafiri kutoka walipo lakini sasa hivi vikao hivyo vinafanyika kwa njia ya mtandao. Kwa hiyo hakuna haja ya kuweka ofisi itakayokaliwa na watu wengi bali watu wawili au mtu mmoja. 

Kwa hali hiyo majengo mengi ya ofisi yameanza kukosa watu (hayana wateja). Sasa wewe ambaye unataka kuwekeza kwenye majengo ya ofisi unahitaji kurudi kwa Bwana ili Mungu akupe namna ya kufanya ili usije ukalia baadaye. 

Kwa sasa hivi wengine wanaweza wasielewe ni sawa na wakati ule wa Nuhu kwa sababu alikuwa akitangaza lakini watu walikuwa wanamtazama kama vile hawamwoni lakini mvua ikawashukia. 

Mbegu nyingine iliyopandwa ni juu ya matumizi ya teknolojia. Mfano yale mahoteli yaliyokuwa yakitegemea mikutano kadhaa ili wapate pesa kwa namna hiyo sasa hivi watu wanafanya vikao online kwa njia ya mtandao (internet)

Mfano:

Mwaka 2020 Corona ilipoanza huku Tanzania mikutano ya semina haikuwezekana mpaka serikali ilipoingilia kati na watu walipoomba na waliomba kweli kweli. Ule muda mdogo ulipitisha vitu vingi. 

Kwa hiyo utaona teknolojia inavyoweza kuondoa watu kazini. 


USHUHUDA

Wakati fulani nilikwenda Ujerumani nikatembelea kiwanda kinachojihusisha na kilimo ambacho kilikuwa na watu 300 hadi 500, yule mwenye kiwanda akaniambia amepunguza watu 300 baada ya kubadilisha teknolojia ya uendeshaji. Unaelewa maana yake nini watu 300 kupunguzwa kazi tena kijijini?Akanionyesha na jinsi zile roboti za mashine zinavyofanya kazi. 

Lakini litakuweko jambo lingine ambalo ni changamoto ya kutafuta vyanzo vipya vya mapato si mtu binafsi, serikali, mataifa.

Pale kwenye lango wakati Mungu anatafuta sisi tuutafute uso wake,  Yeremia 29:11 inasema __maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi asema Bwana" Anaesoma kiswahili anaelewa sio kiswahili kizuri kuanza na neno "maana" Lakini kwenye Biblia unaweza kuanza nalo ili kuweka msisitizo zaidi.

Ule msitari wa 7 anasema wakautakie amani ule mji aliowapeleka kama mateka ndani yake, maana amani yake itakuwa juu yao pia, maana yake wakauombee mafanikio kwa sababu katika mafanikio ya mji na wao watapata mafanikio humo. 

Danieli sura ya 9, Danieli anaandika anasema "mimi Danieli kwa kuvisoma vitabu nikapata ufahamu za Hesabu zilizokuweko na yamebaki majuma mawili" alipata ufahamu ndani yake, Na Waebrania 11:3 inatuambia "Kwa imani twafahamu" kwa hiyo inamaanisha aliposoma imani ikajengeka ndani. Akajua Muda wa wao kutoka ulifika lakini hawawezi kutoka bila maombi lazima kuutafuta uso wa Bwana.

Yale maombi ya Danieli yaliachilia mambo mengi sana mpaka tukajua kipindi atakachosulubiwa Yesu Kristo. Kulikuwa na Wayahudi wengi sana, lakini ile kwamba Danieli alisoma inamaanisha kilikuwa kinapatikana ,na kama alisoma yeye sasa wangapi waliweza kusoma? Kwanini alinyanyuka peke yake kwa siku 21 alizoomba?.

Kuna kitu ambacho Mungu anakipitisha ndani ya watu ili kutafuta watu watakaoomba. Ile zaburi 14 msitari wa 2 inasema anachungulia Duniani ili aone kama kuna watu wenye akili ili wamtafute Bwana

Mahali ulipo kwenye eneo ulilopo, Biashara, kanisani,kazini, kwenye elimu ,kwenye Ardhi popote pale ulipo, Ni Mungu amekuweka kama muwakilishi wake maana wewe ni chumvi, wewe ni balozi wake akitaka kusema kitu anakutafuta kwanza wewe.

Haijalishi hofu uliyonayo imetokea wapi maana unaweza ukailamu China kuwa kwanini imeleta COVID hii haitakusaidia. Maana hamna mtu anapenda uwe katika hiyo hali uliyonayo. Maana kama ni hivyo basi ujue yeye ana hali ngumu sana. 

Petro alipopata hofu alimuita Yesu, sio wewe unapata hofu unaanza kutukana na kuzira.  Kwa hiyo geuza hofu uliyonayo maana ni rahisi sana ukawaambukiza na watu wengine hiyo hofu na wasijue kitu cha kufanya. 

Je kila mtu akiacha kufanya biashara kwa sababu mtu mmoja tu amekwama au kila mtu akiacha kutafuta kazi kwa sababu kwenye kazi fulani alifukuzwa Je itakuaje? Ina maana baada ya muda ulimwengu utakuwa katika hali mbaya.

Bwana atakupa neno lake maana hata kama hauna mtaji neno lake ni mtaji maana ndilo lilitumika kuumba ulimwengu wote huu. Kwa hiyo tega sikio lako kusikiliza kitu ambacho anakuambia.

Kama Mungu anakupa maelekezo na wewe unatazama mazingira unasema hili haliwezekani, ujue hujamjua Mungu maana kwake yote yanawezekana. Kama Mungu kasema basi kanyaga maji vuka bahari ya shamu, vuka mto Jordani maana yuko Mungu aliyesema.

Yusufu alipata akili kutoka kwa Mungu za kulisha Dunia yote. Yusufu alikuwa kwenye agano la kale. Sisi tupo kwenye agano jipya kwa hiyo inatakiwa tumsikie Mungu vizuri sana kuliko wakati ule. 

Shida ya Mungu si kukueleza mabadiliko ambayo yatakuja bali ni kutafuta watu ambao watatafuta uso wa Mungu na kulia maana maelekezo ya Mungu hayatoki hivi hivi tu. Japo maelezo hayo yanaweza yasitoke kwako lakini Mungu akapeleka kwa mtu mwingine na ikawa msaada sana kwa ulimwengu.

Yule aliyegundua  bulb alikuwa anajiwazia yeye mwenyewe lakini tunatumia mpaka sasa na ulimwengu mzima.

Yeye alifikiri ni wazo la kwake kumbe ni msaada kwa ulimwengu.

Wale vijana ambao walifikiria kutengeneza ndege kwa mara ya kwanza sijajua walikuwa wanawaza nini. Sijajua kama walikuwa wamechoka kutembea au la lakini ndani yao lilishushwa wazo lile kwa ajili ya ulimwengu.  Walihangaika nayo muda mrefu sana. Ndege ya kwanza iliruka mita 75 tu. Hata uwanja wa mpira haukufika. Lakini sasa wanarusha ndege na vyombo vya anga za mbali mpaka kwenye sayari zingine na  mwezini.

Watu wengi sana wanafurahia huduma za Benki ya Dunia (WB) lakini iliibuka baada ya vita vya pili vya Dunia. Kwa hiyo uwe na uhakika kuwa walikuwepo wapendwa ambao walikuwa wanamlilia Mungu usiku na mchana. Na Mungu akaanza kuotesha mbegu ndani ya watu.

Kila kitu unachokiona ujue kuwa kuna mbegu ilidondoshwa ndani  watu  baada ya watu wa Mungu kuomba. Na kama Mungu akitaka kudondosha mbegu anaidondosha katika udongo ambao ni tifu tifu.


KUTAFUTA USO WA MUNGU ILI AKUPE UFAHAMU  NA UELEWA JUU YA KITU CHA KUFANYA AMBACHO KITAKUSAIDIA

Soma Yeremia 29:11-14. Kuna watu ambao wamekuwa wakiomba juu ya utumishi wao, biashara zao, familia zao na maisha yao. Mungu kawasemesha kupitia mstari huu wa Yeremia 29:11.


KATIKA MISTARI HII YA YEREMIA NATAKA TUONE MAMBO MATANO:-


1.HOFU YA KILICHOTOKEA JANA ISIHARIBU MAANDALIZI YAKO KWA AJILI YA LEO NA KESHO.


2. MSHITUKO KUTOKANA NA KITU KILICHOGUSA MAISHA YAKO JANA NA LEO. HUO MSHITUKO USIKUZUIE KUWA NA MAANDALIZI YA SIKU ZIJAZO


3.MUNGU ANAJUA KITU AMBACHO UNATAKIWA KUKIFANYA ILA KITAPATIKANA KWAKO IKIWA MOYO WAKO UTAUELEKEZA KUMTAFUTA YEYE

Hii utaona baada ya mstari wa 11 anaposema ninayo mawazo ya kukufanikisha sasa na siku zako za usoni. Katika mstari wa 12 anazungumza namna ya kupata kwa kumuita, kumuomba na kuku-sikiliza. Mstari 13 anasema mkinitafuta nami nitaonekena kwenu. 


4.KIU YA MOYO WAKO KUUONA USO WA MUNGU IWE KUBWA KATIKA HALI AMBAYO UNAPITIA KULIKO HOFU YA KUTOKUJUA KUOMBA IPASAVYO

Kuutafuta uso wa Mungu maana yake kuna vitu ambavyo Mungu anavifuatilia ndani ya yule mtu anayeomba. Moyo wa huyo mtu unakuwa na uhusiano na maneno ambayo anayasema.Soma Matendo ya mitume 17:26-28. Ikifika nyakati za  kumtafuta Bwana, Mungu haangalii mdomo wako tu bali anaangalia moyo wako una kiu kubwa kiasi gani. 


USHUHUDA

Wakati fulani nilipotoka kuokoka na nguvu za Mungu zilinishukia kwa ajili ya utumishi. Kuna siku nilikuwa nimelala nikiwa na maswali mengi sana moyoni mwangu.Nilipoamka asubuhi  Mungu alinieletea ujumbe ndani ya moyo wangu akisema. "Nimeona mahangaiko ndani ya moyo wako, nitakuongoza katika njia ikupasayo."

Wakati ule sikuwa na ufahamu wa vitu vingi sana ambavyo siku hizi vinanisaidia kuomba kwa wepesi kidogo.Lakini wakati ule kiu yangu iliyokuwa ndani yangu ilikuwa ni kubwa sana. Maana sasa huwezi kuieleza kwa maneno. 


5.MAOMBI YA AINA YA KUUTAFUTA USO WA MUNGU YANAFUNGUA MOYO WA MTU KUPATA UFAHAMU NA UELEWA WA MAELEKEZO YAKE NA KUYATEKELEZA.

Mithali 28:5

Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote.

Kwa hiyo ukimtafuta Bwana sio kwamba utakutana tu na uso wa Mungu bali hata ndani yako utapata uelewa.Huwezi kumtafuta Bwana ukaendelea kulalamika.Lakini sasa tuna waombaji wengi sana ambao wanaomba huku wanalalamika. Maana yake ndani yao hawajapata uelewa.

Ukisoma Daniel 9:1 - 4 utaona ya kuwa Daniel kwa kuvisoma vitabu hasa kitabu cha Nabii Yeremia alipata ufahamu wa kujua kuwa anatakiwa kuomba maombi ya kumtafuta Bwana.Kumbuka wakati huo yalikuwa yamebaki majuma mawili kutimia kwa ule unabii.

Angalia tena   Daniel 9:20 -2 4 . Hapa unaona Malaika alimjia ili ampe ufahamu wa kuomba. Ile kwamba umepata msukumo wa kuomba haina maana ya kuwa unajua kuomba bali unahitaji ufahamu wa namna ya kuomba. Si rahisi sana ukajua undani na upeo na upana wa mabadiliko yanayokuja.


VITU UNAVYOTAKIWA KUFANYA UNAPOPITA MAZINGIRA MAGUMU.

JAMBO LA KWANZA.

FAHAMU UPEO WA KUMTAFUTA BWANA

Unaweza kuutafuta uso wa Mungu kwa ajili yako,eneo, watu na  nyakati husika. Daniel alienda kumtafuta Bwana kwa ajili ya mambo makuu mawili; Mji Mtakatifu na Watu wake Israel. Malaika alipokuja alimwambia aombee na nyakati! Kwa hiyo usitafute na kumwomba Mungu bila kujua ni nyakati gani unazozisema.


JAMBO LA PILI

OMBA MWENYEWE IKIBIDI 

Mtafute Bwana  wewe mwenyewe peke yako ikibidi. Daniel alimtafuta Bwana peke yake kwa ajili ya Yerusalem na Israel wote waliokuwa uhamishoni Babeli. Kwa hiyo unaweza kumtafuta Bwana kwa ajili ya Dar es salaam, Mbeya,Arusha, Tanzania, Marekani na nchi yako. 

Unaweza ukasema kwa sababu tabia zangu sio nzuri kwa hiyo Mungu hanipendi, jitie moyo na Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.


JAMBO LA TATU.

UNDENI VIKUNDI VYA KUUTAFUTA USO WA BWANA

Unda kikundi na mwenzako cha kuutafuta uso wa Bwana. Popote walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu nipo pamoja nao. Kwa hiyo kikundi ni mwombaji zaidi ya moja jumlisha Yesu. Msisubiri kiongozi ndio aseme au kanisani watangaze wewe omba! 


JAMBO LA NNE

4.ANDIKA UFAHAMU AU UELEWA UNAOUPATA UNAPOOMBA NA KUTAFAKARI AU BAADA YA KUOMBA

Tafuta utulivu wa kutafakari kwa sababu katika kutafakari uelewa unaongezeka na kumbuka ukiandika ufahamu unaongezeka na kumbukumbu inatunzika zaidi. Sasa jifunze kuandika hapo hapo usisubiri kesho maana unaweza poteza hiyo pointi.

Kwa hiyo Mungu akikusemesha andika. Wakati ule COVID 19 ilipoingia mwaka 2019 nilienda mbele za Mungu kuuliza. Kuwa je ni kitu gani kimeingia katika ulimwengu wa roho na ni kitu gani tunatakiwa kufanya. Kwa hiyo nilikuwa naomba ili nipate kujua na Mungu aliponisemesha niliandika.


JAMBO LA TANO.

5.FUATILIA KATIKA MAOMBI ZAIDI JUU YA WAZO AMBALO LINAKUJA NA KUJITENGENEZA (BIASHARA, UTUMISHI, MAISHA).

Kwa hiyo haijalishi hilo wazo ni jipya linakuja au la. Jitahidi sana kulifuatilia kwa njia ya maombi.

Soma Isaya 55:6-8,11. Kwa hiyo kama Mungu anajua mawazo ambayo anakuwazia ni mawazo ya amani Mawazo ya amani maana yake ni mawazo ya kukufanikisha. Kwa hiyo neno hilo Mungu kama analeta ndani yako linakuja kama wazo.

Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi. Isaya 55:12.

Kama ni wazo la kutekelezwa utasikia furaha kusonga nalo mbele. Kwa hiyo hapo amani itakuongoza hata kama kuna ubishi maadamu amani ipo utasonga mbele.


KINACHOTOKEA NA KITAKACHOTOKEA NA KULETA CHANGAMOTO ZA KIMAWAZO KATIKA MAENEO MATATU.

I)KUTAFUTA VYANZO VIPYA VYA MAPATO

II)KUONGEZA MAPATO KWENYE VYANZO VYA ZAMANI

III)KUTUNZA VYANZO VYA MAPATO VILIVYOPO ILI VISIZIMIKE.

Kwa hiyo inawezekana vyanzo vipya vya mapato havipo ila basi vilivyopo visizimike. Hili jambo linaenda katika ngazi mbalimbali za kimataifa, kitaifa na mtu binafsi.


LANGO LA COVID-19 LILIPOFUNGUKA MWAKA 2019 LILIFANYA MAMBO MATATU:-

I). MAPATO KUPUNGUA NA YASIWE NA UHAKIKA KWA WENGI.

Japo katikati ya mazingira  hayo kuna watu wanapata na wanaendelea  na pesa nyingi sana.


II). MZUNGUKO WA FEDHA KUPUNGUA NA KWENDA POLE POLE KATIKA BIASHARA NYINGI.

Kwa hiyo pesa nyingi za watu zipo sehemu kuu mbili.  Katika bidhaa ambazo hazijanunuliwa na zingine ziko benki. Kwa hiyo zinasubiri hali iwe nzuri. Sasa benki nazo zimejikuta zina pesa nyingi sana ambazo hazijui zifanyie nini. Hii ni hasa kwa zile benki ambazo wateja wake ni wafanya biashara. Kwa maana hiyo kuna wafanyakazi watapunguzwa kazi maana uhitaji wa mikopo umepungua sana.


KATIKA ENEO HILI KUNA MAMBO MAWILI YA KUFANYA.

UWE MWANGALIFU SANA KATIKA MATUMIZI YAKO.

Kwa kuchambua matumizi yaliyo ya lazima na yasiyo ya lazima. sawa sawa na Tito 3 :14 Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.

Hili si eneo ambalo utaona mabadiliko kwa haraka. Ila linakuja kwa hiyo chunga sana matumizi yako.


WEKA AKIBA  KIDOGO KIDOGO NA  MARA KWA MARA KATIKA HUO HUO  UCHACHE WA KIPATO CHAKO.

Kupungua kwa kipato sio kisingizio cha kuacha kuweka akiba. Ukiweza lile la kwanza  maana yake utaweza kupata fedha za kuweka akiba. Katika matumizi ambayo ni ya lazima kesho ina maana yatawekewa bajeti leo kwa hiyo hutakosa hela ya kuweka akiba.


III).VIFO VINGI KUTOKEA TANGU MWAKA 2019 LAKINI HIVI VIFO VIMELENGA WATU AMBAO NI VYANZO VYA MAPATO AU VYANZO VYA MAWAZO YA KULETA MAPATO

Maana yake hawa watu lazima huenda ni wabunifu au ni wazuri katika kupanga vyanzo vya mapato na kuweka akiba. Kwa lugha nyingine maana yake wao ni walinzi wazuri sana wa mapato  yaani ya ofisi au serikali au familia.

Ukisoma Kutoka 1:15 utaona wakati ule ambao msimu wa kutoka kwa Wana Israel Misri ukiwa umekaribia sana.Mungu aliamua kuleta mtoto ambaye atazaliwa kwa ajili ya kuwatoa Misri yaani Musa.Wakati kila mtoto aliyekuwa anazaliwa wa kiume alikuwa anauawa.

Kutoka 11-12  hapa utaona wakati Wana Israel wanajiandaa kutoka Misri. Vifo vilikuja na kufuata wazaliwa wa kwanza. Kutoka 1 tunaona ya kuwa kila mtoto wa kiume aliyekuwa anazaliwa alikuwa anauawa. Hawakuwa na shida ya kila mtoto wa kiume bali shida yao ilikuwa ni Musa.

Thamani ya Musa ilifanana na idadi ya watoto wote wa kiume ambao walipangwa kufa. Adhabu inapoenda kwenye nyakati na uharibifu unapotokea kwenye nyakati unawafikia na watu ambao hawahusiki.

Kutoka 11 hapa unaona waliuawa wazaliwa wa kwanza na kitu ambacho kilikuwa kinawindwa  utakipata katika Zaburi ya 78:51 Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu.

Kwa hiyo hakuwa na shida ya wazaliwa wa kwanza bali shida yake ilikuwa ni katika malimbuko ya nguvu za Hamu. Walikufa watoto na wanyama ambao hawakustahili. Ugomvi ukitokea kinachotafutwa ni nguvu.

Wakati Yesu anazaliwa katika wakati ule wa Herode alipokuwa anasuburi Mamajusi  wa mashariki waweze kumuambia  habari za mahali alipozaliwa mtoto. Na hawakurudi kumuambia na ndipo tunaona ilitolewa amri ya kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri  chini ya miaka miwili wauawe.

Kasome kwenye historia ya vita kuu ya pili Dunia (WW II) iliyoanza mwaka 1939 mpaka 1945 (Kasome kwenye Wikipedia)  inakadiriwa watu waliokufa kuwa milioni 70 mpaka 85  sawa na 3% na wakati huo dunia ilikuwa na watu bilioni 2.3. 

Alafu Mungu akaniambia nitazame upya,nikamuuliza Mungu nijue anataka kunionyesha kitu gani, akaniambia niangalie kama taifa la Israeli lipo, nikagundua taifa la Israeli lilizaliwa 1948, Mungu akaniambia vita vilisukumwa na kuua wayahudi milioni 6 ila hawahesabiwi.

Shetani hakuwa na shida na mataifa mengine yaliyoenda vitani kupigana, alikuwa na shida na Taifa la Israeli, kwa sababu muda wa kuwa Taifa kubwa ulikuwa umesogea, na ile roho mbaya ikasukumwa ndani ya Hitler akavamia Poland. Vita kubwa ilisukumwa hapo ya kutafuta wayahudi kila mahali.  Walikufa watu karibu milioni 85 kwa ajili ya kutafuta wayahudi ili tu wasiwe Taifa.

Ukisoma kwenye Kitabu cha Esta walitakiwa wafe wote, kipindi cha Musa walitakiwa waangamie wote  kwa sababu Israeli ni taifa alilolitengeneza Mungu ili ajulikane yeye ni nani, na kwa  sababu hiyo likiangamia basi unaua mbegu kubwa sana ya uaminifu wa Mungu

Nakueleza hivyo kwa sababu natamani upate picha ya kitu kinachoendelea juu ya COVID toka 2019 Dunia nzima, angalia watu wanaokufa tunaambiwa ni watu wazima. Sasa wewe unafikiri ni watu wazima no!. Nenda sekta kwa sekta, kwa mfano waliotupa taarifa kuwa COVID ipo ni wa sekta ya afya.

Umewahi fikiri wamekufa Madaktati wangapi kutokana na COVID ulimwenguni?. Najua takwimu za kila nchi ila siwezi kuzitaja, ninachotaka ni kukufikirisha ili upate kile Mungu anataka. Kumpata Daktari mmoja unahitaji kumsomesha miaka 7. Fikiria kwenye Taifa moja wafe 200, sasa kuziba pengo la hao madaktari kama hauna akiba ya madaktari unahitaji miaka 7 kupata 200 wengine. Unaelewa maana yake nini kusubiri miaka 7 ili uwapate 200 wengine? Wakati katikati ya Tatizo unawahitaji.

Sasa zipo mbegu kadhaa zinazopandwa katikati ya Uchungu na mambo yote.


1. WATU KUANGALIA THAMANI YA MAISHA KULIKO KIPATO.

Hii ndio mbegu ya kwanza kabisa iliyopandwa, Kwa sababu utaratibu wa kwanza uliotolewa wa kukabiliana na COVID ni lock down. Watu wakaamua kujali maisha kuliko kipato, lakini baada ya muda wakagundua hawawezi wakaishi bila kipato. 

Zile nchi zilizoanza mapema kuweka lock down watu wake zikawa fundisho kwa nchi nyingine zilizofuata baadae.  Hizo zingine Hazikuweka watu lock down. Kwa maana ushindani ukawa mkubwa sana ndani ya watu kati ya thamani ya maisha na kipato, kiasi kwamba watu walio kwenye nchi zilizoweka lock down wakaandamana kuzitaka serikali zao ziondoe lock down, kwa sababu kipato kinataka kichukue nafasi yake. 


2. WATAALAMU WENGI KUBADILI KAZI ZAO ILI KUPATA ZILE ZINAZOWAPA URAHISI WA KULINDA AFYA ZAO NA KUPATA MATIBABU

Kwa sababu wakiendelea kwa staili wanayofanya watakufa.  Pamoja na kwamba ni wataalamu na wenyewe ni binadamu wana miili. Kwa hiyo usishangae sana unapoona wanabadili kazi zao ni kwa sababu kuna mbegu imepandwa ya kuanza kufikiria juu ya thamani ya maisha kwanza.


3. KUTATOKEA MSUKUMO MKUBWA WA KUJAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI BILA UTARATIBU WA KIMUNGU NA BILA KUFUATA MIFUMO ILIYOWEKWA

Hii itatokea katika Mataifa mbalimbali na watakuwa na sababu ya kusema  hizi sio nyakati za kawaida hizo nafasi zinatakiwa kujazwa haraka sana.

Ukisoma Biblia utaona ya kuwa wanafunzi wa Yesu baada ya Yesu kupaa na Yuda kufa kwa kujinyonga. Waliamua kumtafuta mtu wa kumbadili katika nafasi iliyoachwa wazi.

Katika Biblia hatuoni wanafuzi wa Yesu wakiomba kama Yesu alivyofanya na alipokesha usiku kucha mlimani kuomba ili aweze kupata wanafunzi sawa sawa na Luka 6:12. Ila  wao waliamua kupiga kura wakitarajia kuwa watampata mwanafunzi.

Ukisoma Biblia unaona kweli walimpata  lakini humuoni popote katika utumishi zaidi ya pale ambapo ndipo jina lake lilitajwa kuwa kapata kura na sasa amekuwa Mwanafunzi. Hii ni kwa sababu yule mwanafunzi hakuwa chaguo la Mungu bali ni Wanafunzi wenyewe walikuwa na haraka sana ya kupata mwanafunzi wa kumbadili Yuda.

Ni kweli kuna uhitaji wa haraka ila inatakiwa kutafuta uso  wa Mungu kwanza. Kaeni katika maombi ili muweze kupata kiongozi ambaye ni mzuri. Hilo jambo hata kama lina haraka kwa hiyo  mpelekeeni Mungu hati ya haraka kwa njia ya maombi kuwa mnahitaji mtu kwa haraka.


4.MIFUMO YA ELIMU ITALAZIMIKA KUPITIWA UPYA ILI KUPUNGUZA MUDA WA KUANDAA WATALAAM BILA KUHARIBU UBORA WA UTALAAMU HUSIKA

Kuna baadhi ya  Nchi zimeanza kutazama hili suala ila linakuja kwa nchi mbalimbali. Maana itakuwa si rahisi sana kuendelea kupata madaktari baada ya miaka saba. Kwa hiyo   unapunguzaje muda wa miaka saba  bila kuathiri ubora wa utalaamu wao. Hapo ndipo panahitaji sana maombi kwasababu kuomba kwa Mungu ili atupe njia nzuri ambayo itaweza kusaidia jambo hili. 

Kwa hiyo mahali ambapo pana mchakato mrefu wa namna ya kupata Wachungaji nao lazima itafutwe njia nyingine tena. Kwa hiyo kila Sekta itapitiwa kwa upya.Je unawezaje kumpata Profesa au Daktari (Yaani wale wa kusomea kwa kupata PHD)kwa muda mfupi bila kuathiri ubora wa ile taaluma?. Maana hawa watu tunawahitaji mapema sana. Kwa hiyo hili suala nalo linahitaji maombi lasivyo litatuharibia ubora wa kupata watu hao  na kuleta shida tu.


5. KUTAFUTA NJIA ZA KULINDA AFYA ZA WATU WALIO SEHEMU KATIKA MAPATO NA MAWAZO YA KUPATA MAWAZO

Hili ni lile kundi kama la Wana wa Isakari ambao walikuwa wanazijua nyakati na mambo ya kufanya katika nyakati hizo. Kwa hiyo yanakuja mabadiliko ya kisera, kisheria na kimfumo.

Kwa hiyo sera ikibadilika na Sheria nayo inabadilika ili kuweza kulinda mabadiliko ambayo sasa yamekuja. Sheria ikiwekwa unatengenezwa mfumo  wa kuyafanya mabadiliko hayo yaweze kusambaa.


MFANO.

Watu wa Sekta ya afya ndani yao wameanza kufikiri na wengine wataendelea kufikiri namna ya kuimarisha mfumo wa afya zaidi kuliko kuachia kuimarisha eneo la matibabu.

Ivi unajua ni kwanini inaitwa Wizara ya Afya au Shirika la Afya na sio Wazara ya Matibabu au Shirika la Matabibu?. Kazi yao ni kulinda afya kwanza. Lakini mazingira ambayo yapo yamelazimisha zaidi Dunia nzima kuwekeza zaidi katika matibabu badala ya Afya.

Lakini  COVID inatufundisha kuwa tutunze afya kwanza na tusisubiri kuugua. Hiyo ndio mbegu ambayo imepandwa sasa. Mfano kunawa mikono, kupaka sanitizer, na kuvaa barakoa.Haya mabadiliko yanakuja maana sasa saa imefika ambapo suala la afya litatiliwa sana mkazo. 

Ninaona ofisi zikiweka watalaam wa afya kama vile ambavyo yanaweka watalaamu wengine. Kazi yao itakuwa ni kushauri wafanyakazi kupima afya zao na kuwasaidia watu ili waweze kufanya mazoezi. Pia kwa sababu watu wengi hawapendi mazoezi  kuna baadhi ya ofisi zitaweka kabisa na eneo la gym ili watu wengi waweze kufanya mazoezi.


6. UCHUNGU NA HUZUNI KUGEUKA MSUKUMO WA MAOMBI YA KUUTAFUTA USO WA MUNGU

Watu wengi sana wanapita kwenye hali ambayo huwezi kujua uchungu wake na huzuni waliyonayo. Lakini ikiendelea hali ya namna hiyo itakumaliza hutafika mbali. Hii ni kwa sababu huzuni ikiwa nyingi itakuzuia usiendelee na shughuli zako za kila siku.

Hivyo ndivyo Yesu alisema roho yangu ina huzuni nyingi sana kiasi cha kufa. Kwa hiyo aliacha kuhubiri, kutoa ushauri na kuponya wagonjwa. Hii ina maana shughuli zake za kila siku zilisimama.Hali ilimsukuma Yesu kwenda kuomba. Sasa fikiria Yesu angekuwa na huzuni nyingi kiasi cha kufa na asingekuwa na msukumo wa kuomba ina maana angebaki analala nyumbani, na angekuwa na full depression.Pia hapo hapo na magonjwa mengine nyemelezi yangemuingia. 

Nilisoma habari za watu waliokufa kutokana  na athari za vita yaani kama magonjwa yaliyojitokeza baada ya vita ya  Vya pili vya Dunia walikuwa ni mamilioni ya watu.Hawa watu hawakufa vitani bali walikufa baada ya magonjwa yaliyotokea baada ta vita vya pili vya Dunia (WW II). Hii ina maana sekta mbalimbali zilikuwa zimevurugika na watu hawana msaada tena.

Hata kwenye wakati wa COVID nao ni vivyo hivyo. Maana hapo unaweza ukafikiria tu watu kuugua lakini bado hujaangalia hali ya mioyo yao au mahali ambapo wanapita. Hawa watu wanaweza wasiseme ila nyuso zao zinaonesha kilichoko  mioyoni mwao.

Ukiwa na uchungu ndani yako unapunguza speed ya kufanya kitu na pia speed ya kufikiri inapungua. Kwa hiyo tukiwa katika hali ya uchungu namna hiyo  Mungu huwa anashusha roho ya toba ili tuweze kuutafuta uso wa Bwana. Ili katikati ya uchungu namna hiyo Mungu aweze kukushushia nguvu kama zile alizoshushiwa Yesu alipokuwa na huzuni nyingi kiasi cha kufa.

Hizo nguvu za Mungu ambazo atakupa ili utafute uso wake utakuwa msaada sana kwa wengi. Maana utaponya mioyo yao, utaleta matokeo makubwa sana kiasi ambacho Mungu anaweza akaleta mawazo mapya ndani ya ofisi yako au katika nchi au Ulimwengu wote.

Kwa hiyo katikati ya hali ya namna hiyo Mungu ataanza kutoa maelekezo ili wajue mahali pa kukanyaga.

Maombi: Maombi ya uchungu ili kuweza kuzaa kitu ili tumaini la Mungu liendelee kuonekana katika nyakati hizi.

Basi na kufikia hapa ndio mwisho wa somo hii. 

Mungu akubariki sana kwa kufuatilia somo hili. Endelea kuomba na kuutafuta uso wa Mungu.

Post a Comment

0 Comments