100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

NAMNA AMBAVYO MAANDALIZI YA UCHUMBA YANAVYOWEZA KUSABABISHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA MAPEMA

 

MIONGONI MWA SABABU ZINAZOSABABISHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA MAPEMA 

 KANAANI MPYA MINISTRY


FACEBOOK PAGE 

https://www.facebook.com/Kanaanimpya2020/


WHATSAPP GROUP 

https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf


TELEGRAM GROUP 

https://t.me/joinchat/zkBymjsosO8wZTE0


 Yesu asifiwe tena leo kuliko jana. 

Nimekuwa nikipata maswali Mengi kutoka sehemu mbalimbali na wakati mwingine nimeona mijadala mingi katika majukwaa mbalimbali mitandaoni watu wakijadili swala hili na kila mtu amekuwa na mtazamo wake katika jambo hili kutegemeana na mazingira yanayomzunguka na aina ya shuhuda za ndoa zilizovunjika ambazo amezishuhudia.


Hii pia imekuwa sababu kubwa kwa vijana wengi kuingiwa na hofu pindi wanapofika wakati wa kuchukua maamuzi kama haya kwasababu shuhuda hizi zimewavunja moyo na kuwafanya waone ni bora maisha ya usingle kuliko maisha ya ndoa na wengi wametumia kigezo hicho kugoma kuoa, 

lakini unisikilize kijana VASHTI kushindwa kudumu katika ndoa na mfalme AHASUERO haina maana kwamba ESTA agome kuolewa.

Tafuta kujua  Vashti alikwama wapi ili na wewe unapoingia kwenye nafasi yake husijikwae hapo alipojikwaa mwenzako.

 NDOA ni agano baina ya Mungu na  watu wawili ambao baada ya utimilifu wa agano hawaitwi wawili tena bali wanaitwa mwili mmoja;

 "na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

"Marko 10:8 

Kwahiyo kama ulifikiri mnaishi wawili katika ndoa yenu utakuwa hujajua vizuri na hapa kuna siri ya ajabu sana ambayo ni ya faida sana kwa wanaoijua na ni hasara pia kwa wasioijua kwasababu jambo lolote ambalo mmojawapo kati yenu atalitenda litakuwa linawahusu nyote wawili kwasababu ni mwili mmoja,

Inamaanisha mke akifanya jambo lolote liwe jema ama zuri ni sawa na mme amefanya jambo hilohilo au mme akifanya jambo liwe jema au baya ni sawa na mke amefanya jambo hilohilo.


Nimewasikia wanaume wengi wakilalamika inapofika saa hawawezi kuendelea na wake zao na hivyo kwa mujibu wa sheria ya nchi inamlazimisha mme au yule aliyetoa taraka kukubali kugawana mali walizochuma pamoja,hata kama mama alikuwa ni mama wa nyumbani hana shughuli yoyote ya kuingiza kipato anayoifanya na baba pekee pesa yake ndo imetumika kwenye mambo yote ya kimaendeleo lakini unapofika wakati wa kugawana wanagawana pasu au 50% na hii ndio imekuwa hasira ya wanaume wengi maana hujiona kama wao ndio walibeba mzigo wote wa maendeleo ya familia alafu ghafla tu mwanamke anataka kubeba vitu ambavyo hajavigharamikia.

Lakini ni kwasababu ninyi ni mwili mmoja unaweza ukashangaa kwama inakuwaje namna hii lakini mambo haya yapo kibiblia kabisa kama tulivyoona kwenye huo msitari hapo juu ingawa biblia haitenganishi watu bali inashauri wawe pamoja maana gharama ya kuishi maisha ya kutengana ni kubwa mno kuliko mmengefanya matengenezo kama nilivyoandika katika somo la UPONYAJI WA NDOA YAKO

Ndio maana maandiko yanasema

 “Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.” 

   1 Wakorintho 7:14 

Huu ni udhihirisho kwamba ninyi ni mwili mmoja kwahiyo hakuna namna mnaweza mkatengana lakini pia huu ni udhihirisho kwamba kila anachokifanya mmojawapo kati yenu kina sehemu katika mwingine ndio maana utakatifu wa mmoja wenu unaweza kuwa sababu ya mwingine kutakaswa. 

lakini pia baadhi ya mifumo ya kiroho unaweza kuikuta kwenye mifumo ya utawala wa huku duniani japokuwa inaweza kuwa na sura ambayo sio rahisi sana kuiona kwa jinsi ya mwili lakini utendaji wake unacopy rohoni na hii ni kwasababu kila kinachotokea katika ulimwengu wa mwili kinaratibiwa kwanza katika ulimwengu wa roho iwe ni upande wa Mungu au shetani. 

Ndio maana utaelewa pale ambapo maandiko yanasema;


 2 Wakorintho 10:3-5 

 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;

 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)

tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 


Ni hivi kabla jambo halijatendeka kwa jinsi ya mwili kibinadamu linaanzia kwenye mawazo na hapo biblia imetueleza "tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu;" maana yake tunapambana na mawazo ya adui kabla hajayabadilisha mawazo hayo kuyaingiza kwenye vitendo kwasababu akiisha kuyaingiza mawazo hayo kwenye vitendo yanabadilika na kuwa msingi wa kusudi lake, sasa gharama ya kubomoa msingi ni kubwa na kuna vitu vitakuwa vimeshaharibika tayari. 

Kwahiyo kabla vita haijawa vita inaanzia rohoni, kwa wale waombaji wanaelewa nikisema hivo kwamba ukitaka kumshinda mchawi haumfuati nyumbani kwake kumpiga ngumi au kumpeleka kituo cha polisi bali unakutana naye katika ulimwengu wa roho na mnamalizana hukohuko lakini madhara ya aliyepigwa yatadhihirika mwilini kwahiyo utamuona kesho yake hana hata ujasiri wa kupita mbele yako, vita inapigwa roho lakini inadhihirika mwilini. 

 kwahiyo kabla haijaja miaka saba ya njaa juu ya Misri ilianzia rohoni kwanza kwahiyo farao alikuwa anasemeshwa kitu ambacho kimeshatokea kwenye ulimwengu wa roho kwahiyo kazi yake ilikuwa ni kujiandaa kukabiliana na hali hiyo kwa kuwa na maghala ya chakula ya kutosha yatakayoweza kukidhi mahitaji kwa miaka yote hiyo. 

Mahali pengine ufalme wa sauli ananyanganywa rohoni kwanza kwasababu maandiko yanasema, 

 1 Samweli 13:13-14 

 Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya Bwana, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele.

 Lakini sasa ufalme wako hautadumu; Bwana amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye Bwana amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile Bwana alilokuamuru. 

 Kwahiyo sauli alinyanganywa ufalme wake rohoni kwanza kabla ya yeye  kuondoka ikulu na Daudi alipewa ufalme kabla ya kuingia ikulu 

maana yake mambo hayo kabla hayajatokea yalikwisha kumalizika katika ulimwengu wa roho.


 KWAHIYO 

Ndoa nyingi zinavunjika kuanzia rohoni kabla hazijafungwa mwilini.

Namaanisha hivi;

Ndoa nyingi zinanajisika rohoni kabla hazijawa ndoa takatifu na walioharibu hawafanyi matengenezo au hata kama wanafanya hawatengenezi kwa kiwango walichoharibu na hivyo wanapoingia katika ndoa wanakuta shetani amekwisha kuweka msingi wa kwake na wanaanza kutembea juu ya msingi wa adui maana yake agano la ndoa takatifu wanaliacha madhabahuni siku ile ya kufunga ndoa hivyo wanapokuja nyumbani hawatumikii kusudi la Mungu bali wanatumikia kusudi la shetani na tangu bustani ya Edeni shetani hajawahi kuwa na nia njema na ndoa maana unaweza kujiuliza shetani anawinda kitu gani, 

lakini maandiko yanasema

 "nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino." Mwanzo 3:15 


Biblia inaposema "na kati ya uzao wako na uzao wake" 

maana yake inazungumzia habari ya vizazi hata vizazi.

Me sijui kama umewahi kuwaza kwamba hivi nyoka anapomgonga mtu kwenye kisigino anapata faida gani maana angekuwa anameza mguu wote tungesema labda ni njaa alikuwa anatafuta chakula lakini kiuhalisia hata angekuwa na njaa bado haondoki na mnofu lakini ni laana ya vizazi vyote tangu Adam hata hivi leo, siku nyingine tutakuja kujifunza nini kinatokea nyoka akimponda mtu kisigino maana wengine wanaumwa na nyoka kwenye ndoto na matatizo yanatokea mpaka mwilini na hawajui nini cha kufanya.

Mpaka hapo unaweza kuelewa kwanini shetani anawinda ndoa kwa nguvu zote maana hapo ndipo lilio lango la uzao ambao aliambiwa utamponda kichwa kwahiyo anauwahi mapema ili ukawe upande wake, na apitishe watoto wa kwake hapo. 

Unaweza ukauliza kwa namna gani sasa uzao wa mwanadamu ukawe upande wake na shetani anawezaje kuzaa na mwanadamu!!! , 

kasome biblia yako vizuri maandiko yanasema

 "Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake" Mathayo 12:34 

Anaposema wazao wa Nyoka anamaanisha UZAO WA UASI maana yake shetani anaweza kuzaa na mtu kwa njia ya kupandikiza mbegu ya uasi ndani yake, automatically mtoto atakayezaliwa atakuwa ni wa kwako lakini ndani yake amebeba kitu kwa ajili ya shetani  kwahiyo hawezi kumdhuru badala yake atamtumia yeye kuwaponda visigino binadamu wenzake akiwa amevaa mwili wa binadamu lakini ndani amejaa mbegu ya uasi maana yake roho ya nyoka.

Kwa wale wanaofatilia masomo yangu wataelewa ninachokimaanisha haswa kwenye somo la UMUHIMU WA KUOMBEA MTOTO AKIWA TUMBONI 


Kwahiyo ndoa nyingi sana zimevurugika kwasababu shetani amewatangulia stand na akawahi seat kwahiyo nyie mkiingia kwenye gari mnakuta yeye ni mwenyeji wenu na anawakaribisha ndio maana utagudua ndoa nyingi zinazopata misukosuko ni zile zilizofungwa madhabahuni kuliko hata zile za watu wa mataifa, maana shetani anajua wale ni wa kwake alishawabana kwenye kona ambako anajua hawawezi kujitetea kwahiyo anang'ang'ana hata hizi ndoa ambazo haziko upande wake nazo aziingize kwenye himaya yake.

Na bahati mbaya sana wanandoa wenyewe ndio wanaofungua mlango wa adui/shetani kupata hiyo nafasi ya kupanda mbegu ya uasi ndani yake na kufanya mambo yote hayo.



Karibu katika sehemu ya pili ya mwendelezo wa somo hili tutakapokuwa tunaangalia ni sababu zipi zinasababisha ndoa nyingi kuvunjika lakini pia ni kwa namna gani wanandoa wanafungua mlango wa adui kwenye ndoa zao na uzao wao.

Leo niliona nikupe msingi  tu ili tutakapoanza kuziangalia hizo sababu uweze kuelewa kwa wepesi vinginevyo nyuma na hautakuwa umepata kile Mungu anataka upate,kwasababu ndoa ni Agano na taasisi kubwa kwahiyo Mungu yuko makini sana hapo kwasababu utumishi wa watu wengi unakwama hapo pindi wanapooa na hawajui ni kwanini kwasababu kusudi kuu la  Mungu kumleta Hawa kwa Adamu ilikuwa ni Hawa kusimama kama msaidizi juu ya kusudi ambalo Mungu amempa Adamu la kuilima na kuitunza Bustani ya Edeni sasa inapokuwa kinyume na hapo maana yake litakalotekelezwa ni kusudi la shetani kwasababu hakuna mtu ambaye hana Mungu anayemtumikia, Husipomtumikia Mungu wa kweli lazima utamtumikia shetani kwa lugha nyingine NDOA yako hisiposimama kwenye msingi wa Mungu wa kweli uwe na uhakika itasimama kwenye msingi wa shetani, kwasababu hakuna agano lisilo na mwenyewe.

========================================================================= DAY 2

 SABABU YA KWANZA

 1.KUOA AU KUOLEWA KWASABABU ZA KIMWILI NJE NA KUSUDI LA MUNGU

Nakusalimu katika jina takatifu la Yesu, na nikukaribishe tena katika mwendelezo wa somo letu la MIONGONI MWA SABABABU ZINAZOSABABISHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA MAPEMA.

Ziko sababu nyingi lakini miongoni mwa hizo ziko baadhi yake nimezipa umuhimu mkubwa, 

kwa kusema hivo sina maana  kwamba ambazo sitaziainisha basi hazina umuhimu la hasha!!!!

Bado roho mtakatifu anaweza kukufunulia zaidi kwasababu yeye ndiye mwalimu wetu sote, lakini hizi nitakazozielezea zinagusa maeneo mengi karibia ya kila mwanandoa kuanzia kipindi cha maombi ya uchumba, uchimba wenyewe  nakadhalika, kwasababu ziko nyingine zinatokana na mazingira yanayomzunguka mtu ambazo ni rahisi sana kuzipatia ufumbuzi, lakini leo nataka tuingie ndani kidogo.


Kabla sijaendelea, niwapongeze wale wote ambao wamekuwa wakifatilia masomo mbalimbali ambayo tumekuwa tukiweka katika madhabahu ya KANAANI MPYA MINISTRY ,nimepata shuhuda nyingi nami namtukuza Yesu kwa ajili yako wewe uliyetenga muda wako kwa ajili ya kutafuta maarifa ya Mungu na kipekee kabisa nimpongeze Ndugu mmoja aliyetutumia ushuhuda wake kutoka huko Mtwara akishuhudia namna ambavyo somo la UPONYAJI WA NDOA YAKO  lilivyoponya ndoa yake iliyokuwa inaelekea kuvunjika, 

ushuhuda wake ni kama somo na tutauweka huko mbeleni tunakoelekea naamini utafanyika baraka na msaada mkubwa kwa wengi wanaopitia kama alipokuwa akipitia ndugu huyu. 

 Tuendelee na somo...... 


KUOA AU KUOLEWA KWASABABU ZA KIMWILI NJE NA KUSUDI LA MUNGU. 

Sasababu hii nimeiweka kama sababu ya kwanza lakini sio kwa maana ya kwamba ni ya kwanza kiumuhimu bali ni kwa mpangilio tu, kila sababu ina umuhimu kwenye eneo lake. 

Inapofika saa ya kuoa au kuolewa ni vijana wachache sana wanaotafuta mke au mme kwa kutanguliza kusudi la Mungu ndani yao, wengi wao hutazama 

maumbo ya nje, 
sura za nje, 
maisha mazuri, 
viwango vya elimu,
ukabila nk.

Ambapo katika yote hayo  yapo yanayoweza kuwa ya msingi kutokana  na vipaumbele vya muhusika mwenyewe lakini pia yako ambayo hayana sehemu katika utukufu wa Mungu kwa ajili ya kusudi ambalo Mungu mwenyewe ameweka ndani yako. 

 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” Mwanzo 2:18 

Mungu anapomleta Hawa kwa Adamu haji tu bila sababu bali anakuja kuwa MSAIDIZI. 

msaidizi wa kitu gani???? 

Ukitaka kujua Hawa alikuja kufanya usaidizi wa kitu gani angalia msitari ule wa 15 biblia inasema;

 “Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza .” Mwanzo 2:15 

Kwahiyo kusudi lililowekwa Ndani ya Adamu ni KUILIMA NA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI. 

Maana yake ni kwamba HAWA aliletwa kwa ADAMU akiwa kama msaidizi wa kumsaidia kuilima na kuitunza Bustani ya Edeni. 


KWAHIYO;

                   Ilikuwa ni lazima HAWA awe ana na taaluma au ufahamu katika eneo la Namna ya kuitunza Bustani na lazima Mungu aliweka hicho kitu ndani yake. 

 Utauliza kwanini na umejuaje ????

Kwasababu maandiko yanasema;

 “nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.” Mwanzo 2:18c 


Tafsiri ya Neno KUFANANA kwenye msitari huu haina maana ya kufanana sura bali ina maana ya kile kilichoko ndani. {KUSUDI} 

ingekuwa hatari sana kama Adamu anawaza namna bora na mbinu za kufanya bustani isitawi na kupendeza alafu Hawa amewekewa ndani yake uwezo wa kupambana. 

Maana yake unapata picha gani inatokea pale ambapo Adamu anawaza bustani alafu Hawa anawaza vita itatokea sangapi ili aoneshe uwezo wake, kwahiyo ni rahisi kwa hawa kuanzisha ugomvi makusudi ili aweze kupambana maana ndicho kilicho ndani yake. 

Hivyo ndivyo ambavyo vijana wengi wameingia katika migogoro katika ndoa kwa kubeba mtu ambaye ndani yake hana alichokibeba kwa ajili yake,kwahiyo kinachotokea kila mmoja anatumikia kusudi lake ndani ya ndoa wakati agano linadai kila mtu awe na msaada juu ya alichokibeba mwenzake. 

Ikitokea namna hiyo na kwa sababu ni agano uwe na uhakika hakuna namna mtaendana kwasababu kila mtu huku ndani kuna kitu anasukumwa kufanya na anataraji umsaidie wewe kumfanikisha au kumuwezesha kufikia huko anakokuona huko ndani maana agano linadai hivo, 

sasa kama wewe ni mwinjilisti alafu umemuoa mtu ambaye ndani yake amebeba kitu kwa ajili ya mchungaji,unaweza kuona nini kitatokea, kwasababu mke atataka akuone nyumbani kila siku na wewe huduma yako ya uinjilisti inakulazimisha usafiri na wakati mwingine kama huduma yako imekua unakuwa na ratiba ambayo inakubana kiasi ambacho kwa wiki unaweza kuwa na siku moja au mbili za kukaa na familia yako na wakati huo mke anataka akuone nyumbani kila siku uwe na uhakika unaweza kuanza kumuona kama kikwazo katika huduma yako na kule kusafiri kwako hautakuona kama shida maana ndicho kilicho ndani yako na  unasikia kubarikiwa ukipata mialiko sehemu mbalimbali lakini kwa mwenzako ni kero kwasababu anaisi upweke na hata ungemshawishi msafiri pamoja bado hainogi saaana kwake maana anataka uhuru wa wewe mkiwa nyumbani kwasababu amebeba kitu kwa ajili ya mchungaji ambaye muda wote anawaza kondoo na namna ya kuwachunga na kuwalisha ndio maana wachungaji wengi hawapendi sana kusafiri maana akiondoka anaisi kabisa kuna kitu kimepungua huku nyuma kwahiyo hata kama akisafiri atapiga simu mara kwa mara kujua nini kinaendelea, huduma inaendaje na kama kondoo wako salama au la, ni kwasababu hicho ndicho kilicho ndani yake, kwahiyo akiwa mbali na kondoo lazima atahofia mbwamwitu kuvamia kundi la kondoo wake. 


Namaanisha;

wewe kijana sio kila binti aliye mzuri na mrembo anakufaa kuwa mke kwako na wewe binti sio kila kijana mtanashati anakufaa kuwa mme kwako, 

tafuta kujua  umebeba nini na huyo unayetaka kumchukua amebeba nini vinginevyo hautaepuka kuingia kwenye mgongano wa namna hii.

 Unaweza kujiuliza nitajuaje huyu ndiye au sio???? 

Biblia inasema;

 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.”  Mithali 19:14 


KWAHIYO

Sio, baba, mama, kaka, dada, rafiki, mzee wa kanisa, mchungaji, shekhe, padre wala yeyote mwenye idhini kibiblia ya kukupa mke nje na Mungu. 

Wanaweza kukupa mke namimi sijawazuia wasikupe lakini neno la Mungu linasema mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana 

Kwahiyo unaweza kumpata kwao lakini hasiwe mwema wala mwenye busara au akawa na hizo sifa lakini huko ndani hana alichokibeba kwa ajili yako, kwahiyo hata hizo busara hautaziona. 

Kosa jingine linalofanyika inapofika saa ya kijana kuomba kwa ajili ya kupata mke au mme, ni makosa yanayojitokeza namna ya kuomba na saa ingine hatupati maelekezo ya kina namna ya kuombea jambo hili na hii nimeiongeza makusudi kabisa kwasababu yaweza kuwa sababu ya kumchukua mtu hasiye wa kwako na ikapelekea ukaingia kwenye shida kama hii japokuwa ukiulizwa utasema lakini mimi niliomba.

Biblia inasema;

  "Mungu hulitazama neno lake apate kulitimiza" 

Kuna watu wakienda kuomba wanaomba mchumba hawaombi mke au mme. 

Sasa kaangalie biblia yako vizuri hakuna mahali popote ambako Mungu aliwahi kumpa mtu mchumba bali anatoa mke. 

Kwahiyo ukienda kuomba mchumba Mungu anacheki wapi alisema anatoa mchumba akikuta hamna ambako aliwahi kusema hivo anakaa kimya na wewe huku unang'ang'ana kuomba tu mpaka unakata tamaa saa nyingine anakusemesha sio kukujibu ombi lako bali anakusemesha ili kukurejesha kwenye Neno lake uweze kuomba sawasawa hata hivyo huelewi kwasababu unachoomba ni tofauti na kinachokuja ni tofauti. 

Kwasababu Tafsiri ya MCHUMBA ni mtu ambaye huna uhakika naye au ni mtu ambaye yuko chini ya matazamio kwa muda fulani kwahiyo unapomwambia Mungu akupe mchumba ni sawa na unamwambia kuwa hata yeye Mungu mwenyewe hana uhakika na mtu anayekufaa kwahiyo amlete yeyote alafu kwa pamoja mkamchunguze, sasa husifikiri Mungu anaweza kujibu hili ombi na kama uliwahi kuomba hivi nenda mbele za Mungu kwa toba kwa kutokujua namna ya kusema vizuri maana sio kila swali linafaa kumuuliza Mungu, 

biblia inasema, “Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,” Mithali 6:2 

Maana yake kupitia maneno yako unaweza kujikwaa na ukaumia, 

Na ni muhimu pia unapofika mahali pa namna hii unahitaji Mungu akukutanishe na mtu atakayekuwa sababu ya kusudi la Mungu ndani yako kusitawi ni vizuri ukaomba msaada wa roho mtakatifu yeye atakusaidia kuomba ipasavyo na kukufunulia zaidi maana wakati mwingine yule unayemfikilia wewe Mungu anaweza akamkataa sasa inaweza kuwa shida kwako kupokea hayo majibu kama hukumpa nafasi roho mtakatifu katika hilo,ni rahisi pia kukwama katika ngazi ya maamuzi Mungu atakapoanza kukufunulia kuhusu huyo  uliyempeleka maana anaweza kukuonyesha kitu kumuhusu huyo alafu ukaanza kukemea ukifikiri ni shetani ameingilia maombi yako kumbe ni Mungu anakuonesha uhalisia wa Mtu huyo unayetaka kumuoa, 

kwahiyo roho mtakatifu ana nafasi kubwa kwa kila aina ya maombi utakayoyaomba na hatahivo hatujui kuomba ipasavyo ndivyo maandiko yanavyosema kwahiyo ukitaka kufanikiwa katika kuomba kwako huwezi kukwepa kuwa chini ya mwongozo wa roho mtakatifu, 

 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” Warumi 8:26 

Katika sababu hii ya kwanza ambayo ni miongoni mwa sababu za  ndoa nyingi kuvunjika mapema ninapoenda kufika tamati, nikusihi mwana wa Mungu husikose mwendelezo wa somo hili katika sababu zinazofuata na mwisho kabisa wa somo roho mtakatifu atatupa namna bora ya kuomba ili hata aliyekwama ajue namna ya kutoka mahali alipokwama. 

Kwahiyo ukiomba mwambie Mungu akukutanishe na mke wa kwako, na kama unaye  kwenye mawazo yako, muulize Mungu kama huyo anafaa kuwa mke kwako au la, husipeleke Neno Mchumba mbele za Mungu vinginevyo utakwama. 

=========================================================================

DAY 3

SABABU YA PILI

 2.KUKOSEAKANA KWA MALEZI  YA KUWAANDAA WACHUMBA KUELEKEA KATIKA NDOA

Karibu katika mwendelezo wa somo hili nyeti linalohusu usitawi katika agano la ndoa.

Huu ni mwendelezo wa sababu zinazoweza kupelekea ndoa nyingi kuingia kwenye shida, migogoro wakati mwingine mpaka kuvunjika au kutengana kwa wanandoa.

Kipengele hiki cha  malezi nimetumia neno MALEZI ingawa wengi wamezoea kutumia maandalizi.

Kwasababu watumishi wengi wanakwama inapofika saa ya kuwaandaa watu wanaoelekea katika ndoa, nia yao ni njema ya kutaka kuwajengea msingi bora wa ndoa imara na yenye mafanikio makubwa ya baadae kijamii na kiroho pia lakini katika wengi wanaopewa mafunzo au maandalizi hayo ni wachache wanaoonyesha hayo matokeo kama walivyotazamia makuhani au wachungaji wao.

Yako mambo ya msingi sana ambayo hayo yasiposhughulikiwa kikamilifu ni ngumu sana kuona matokeo hayo yakitokea, kwasababu unawandaa watu ambao kila mtu amelelewa kivyake na amekua kivyake wakaja kukutana ukubwani, watu hawa ni ngumu sana kuwafanya wakawa kitu kimoja ikiwa hukubomoa kwanza msingi wa huko nyuma kwa kila mmoja kwasababu huwezi kujenga msingi juu ya msingi mwingine na jambo hili limewakwamisha wengi kwasababu kila mtu ameingia katika ndoa na tabia yake kutegemeana na aina ya malezi aliyopewa huko nyuma kwahiyo anakuja akiwa amebeba vitu ambavyo kwa yeye ndivyo anaona viko sawa wakati huo kwa mwenzake na yeye kwasababu amapewa malezi ya kwake katika jamii au familia tofauti na ya mwenzake vitu vilevile ambavyo mwenzake anaviamini yeye anakuja kuvipinga kwasababu hakujengwa katika msingi wa namna hiyo.

inapotokea namna hii na mmeshaanza kuishi pamoja uwe na uhakika mtakwazana tu.

Niko hapa kuwaambia vijana ambao hawajaoa bado na wanaelekea huko yakwamba ndo sio rahisi hata kidogo ikiwa utakwepa kuweka mambo haya sawa mapema lakini pia unaweza kujenga ndoa na familia yenye furaha, amani na upendo ikiwa tu utajenga msingi mapema kwa kuyaishi haya mapema kabla ya ndoa.

Aina ya malezi anayopewa binti yanaweza kuwa sababu ya yeye kuwa mwanamke wa aina fulani wa baadaye.

Aina ya maisha ambayo baba na mama wanayaishi katika ndoa yao yanaweza kuwa sababu ya kuwafanya watoto wao waishi maisha hayohayo hata baada ya kukua na kuanza kujitegemea kwasababu katika lile somo la

 UMUHIMU WA MALEZI KWA MTOTO - sehemu ya kwanza

UMUHIMU WA MALEZI KWA MTOTO - sehemu ya pili

tuliona namna ambavyo mazingira yanayomzunguka mtoto na kile anachokiona namna ambavyo vinaweza kumfanya awe mtu wa aina gani wa baadae.

Kwahiyo familia au ndoa njema ya kwako inatengenezwa kwanza na wazazi wako huko utotoni nini walikulisha na aina ya mazingira waliyokutengenezea lakini namna ambavyo wewe ulipokea yakakunufaisha au yakakuathiti, 

kwahiyo linapokuja swala la kuwandaa wachumba kuelekea katika ndoa haitolewi tu namna ya kuyaishi hayo maisha ya ndoa lakini ni lazima kwanza ucheki huko nyuma watu hawa walikulia wapi na wakalelewa katika mazingira gani na je mazingira hayo yalikuwa yanawajenga au kuwabomoa.

Kwahiyo kabla ya hayo mafundisho ya ndoa yenyewe ni muhimu kutambua hilo ya kwamba msingi wa malezi uliojengewa huko nyuma waweza kuwa sababu ya wewe kujenga ndoa imara na ya kudumu au waweza kuwa sababu ya ndoa yako kuharibika na husijue namna ya kujenga palipobomoka.

Mafundisho yanayotolewa mara nyingi ni ya kuwahamisha kutoka kwenye maisha ya uchumba na kuwapeleka kwenye maisha ya ndoa maana wako watu wanafikiri namna walivyoishi katika uchumba na kwenye ndoa wataishi hivohivo, wingu la uchumba ni la uchumba, unapoingia katika ndoa wingu la uchumba linahama linakuja wingu la ndoa na kila wingu linakuja na vitu vya vyake ambavyo havifanani kwahiyo ukitaka kuishi maisha ya ndoa kama maisha ya uchumba maana yake unakataa ndoa na unataka kurudi nyuma katika uchumba, na kwasababu kila agano linatafuta kutimiza makusudi yake litakulazimisha wewe uelekee kule linataka na kwasababu haupo tayari kubadili mind set yako itakusumbua na kukuwekea uzito tofauti na namna ulivyofikiri kipindi upo kwenye  uchumba.ndiyo maana utawasikia wengi wakilalamika kwa kusema yaani ningejua kama ndo huko hivi nisingekubali kuwa na wewe 

Lakini kiuhalisia mtu huyo ni yule yule tu kilichobadilika ni agano kwasababu wakati ule mtu huyu alikuwa ni mchumba na sasa ni mke au mme kwahiyo hakuna namna atakuwa yule yule kwasababu uchumba na ndoa ni nafasi mbili tofauti na kila nafasi mtu anaiishi kutokana na matakwa ya hiyo nafasi aliyoikanyaga. 


 KWAHIYO shuhuda nyingi za ndoa zilizovunjika unazozisikia huko mtaani utagundua sababu kubwa chanzo chake ni sehemu kuu mbili.

 1.AINA YA MALEZI ALIYOYAPATA KUTOKA KWA WAZAZI/WALEZI/JAMII 

 2. AINA YA MAANDALIZI AU MAFUNDISHO ALIYOPEWA WAKATI WA UCHUMBA KUELEKEA NDOA. 

Vitu hivi viwili ni muhimu sana kushughulikiwa mapema kikamilifu kwasababu msingi wa ndoa haujengwi na uchumba pekee bali malezi tokea utoto.

Kwa wale washauri wa mambo ya   ndoa na mahusiano wanaelewa ndio maana ukipeleka ndoa yako kwao kabla ya kushugulikia hicho kilichowafanya mkapelekana mpaka pale  miongoni mwa vitu ambavyo watakuhoji ni pamoja na background ya maisha yako kabla ya ndoa, familia uliyotokea, mazingira mliyokutana na huyo mwenzako kwa mara ya kwanza, marafiki zako ni watu wa aina gani na mengine mengi, kwasababu wanaelewa mazingira yanayomzuka mtu na malezi anayopewa  akiwa mtoto yana nafasi kubwa sana kumjenga  au kumbomoa hata awapo mtu mzima endapo hatoshugulikiwa saikolojia yake ikiwa yaliyomzuka sio mema.


Mafundisho unayopewa kipindi cha uchumba yatakusaidia sana endapo saikolojia yako imekaa sawa sawa nikiwa na maana kwamba malezi uliyopewa  yanajitosheleza na hakuna mahali popote yalikokuvuruga lakini mafundisho hayohayo yanaweza yasikusaidie ikiwa una tatizo kwenye eneo la malezi na huyo aliyekuandaa hakushugulikia hilo kwanza,itakuwa ni rahisi kuyasahau uliyofundishwa kwasababu hayo sio sehemu ya maisha yako

Kwasababu  kilichojaa moyoni ndicho kinachotoka nje.na ni ukweli kwamba kizazi cha leo kina changamoto  sana kwenye eneo la malezi na hakuna mtu anashugulikia hili kwa ujumla wake na hivyo kupelekea wengi kukwama katika maeneo mbalimbali hata nje ya ndoa. 


 NANI WA KUMBADILI MTU ENDAPO AMEATHILIWA NA MALEZI/MAZINGIRA??? 

1.Kwenye eneo hili la maandalizi ya ndoa ikitokea kupitia mafundisho uliyopewa ukabaini umeadhiliwa na malezi au mazingira mtu wa kwanza kushughulikia hali hiyo ni huyo anayekuandaa kukupeleka katika ndoa kwa kuhakikisha anabomoa msingi wa awali kuanzia kwenye fikra zako na kukujengea msingi mpya, ingekuwa ni simu tungesema unaiflash kabisa ama unaiformat inakuwa kama haijawahi kutumiwa na mtu yeyote kwahiyo baada ya kuformat unaanza kuiseti upya kutegemeana na wewe unataka setting yake ikaeje. 

Sasa hapa sitaelezea namna ya kubomoa msingi wa kwanza kwasababu kila mtu ana namna yake ya kuathilika, kuna walioathiliwa na wazazi wengine wameathiliwa na walezi {Maana unaweza kuwa na mzazi lakini ukalelewa kwingine} , wengine wameathiliwa na mazingira yaliyowazunguka, 

Kwahiyo namna ya kuwatibu watu hawa ni tofauti kwasababu lazima uwahoji ili uweze kujua wapi walikwama. 


2.mtu wa pili kubadili hali hii Ni muathirika mwenyewe kujitambua kwamba ameathirika na anatakiwa kubadili namna ya kuwaza, kufikiri na kuamua kwake ili apate mafanikio kwa huko anakoelekea. Nimemuweka huyu kama mtu wa pili kwasababu ili ajitambue lazima aelezwe kwasababu kusikia huja kwa neno la kristo, maana sio wote wanaojitambua kwamba wana shida katika malezi. 

Kwahiyo akiisha kuelezwa wapi amekwama na kwa namna gani amekwama ndipo anaweza kufata ushauri atakaopewa kwasababu ukimueleza mtu tatizo lake unambebesha mzigo, maana yake akishasikia mzigo ndani atatafuta namna ya kuutua huo mzigo na hiyo ndiyo itakuwa salama yake. Lakini pia katika eneo hili  inategemea ikiwa aliyeathirika ni mmoja huyu mwingine ana jukumu la kuendelea kumjenga kupitia mafundisho yale wanayofundishwa na yule mkufunzi ana wajibu wa kumfatilia kwa karibu kuhakikisha anatoka kwenye hali hiyo. 

=======================================================================

DAY 4

 SABABU YA TATU

3.KUTOKUSHUGHULIKIA HISTORIA YA KILA MTU KABLA YA KUOANA.

Karibu tena katika mwendelezo wa somo letu linalohusu NDOA na namna ambavyo wanandoa wenyewe wanaweza kuwa sababu  ya kudumu kwa ndoa yao ama kuvunjika mapema sana ikiwa baadhi ya maeneo hayatashugulikiwa kikamilifu kama ambavyo tumeainisha baadhi ya mambo hayo katika mwendelezo wa somo letu hili la MIONGONI MWA SABABU ZINAZOSABABISHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA MAPEMA.

leo ikiwa ni sehemu ya nne ya somo letu  ningependa kutumia nafasi hii pia kumshukuru Mungu kwa namna ambavyo amekuwa akituhudumia kupitia madhabahu hii ya KANAANI MPYA MINISTRY na tumeendelea kupata  shuhuda nyingi kutoka sehemu mbalimbali namna ambavyo watu wamekutana na Mungu kupitia masomo ambayo tumekuwa tukiyaachilia hapa kwa msaada wa roho mtakatifu namimi namtukuza Yesu kwa ajili ya kila mmoja ambaye Bwana amemtendea na hata yule ambaye bado hajaona muujiza juu ya maisha yake nina imani maarifa haya ni azina kwa ajili ya kesho yako au uzao wako, maana mwenzako alipokwama leo kwa kukosa maarifa ya kumsaidia wewe kesho hautakwama eneo hilo kwasababu iko mbegu imeachiliwa ndani yako tayari na wakati wa weww kupitia mahali hapo utakapowadia Neno la Mungu litaangaza ndani yako na kuachilia ambayo kwayo utaona njia ya kutokea kwako.


Baada ya kusema hayo nikukaribishe sasa katika mwendelezo wa somo hili katika sababu ya tatu ambayo nimeipa kichwa kinachosema;

KUTOKUSHUGHULIKIA HISTORIA YA KILA MTU KABLA YA KUOANA.

Biblia inasema,

 “Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,” 

 Kumbukumbu la Torati 5:9

Ni ukweli kwamba si kila mtu ametokea katika familia inayomcha na kumtegemea Mungu kwa ukamilifu kwa maana hiyo unaweza kujikuta unaishi maisha yasiyokuwa ya kwako kwasababu tu wako watu ambao ni uzao wa baba zako au babu zako waliotenda makosa na hakuna mtu aliwahi kuyatubia na kwa maana hiyo adhabu hiyo inatembea kizazi hata kizazi,

Huko nyuma mwanzoni kabisa mwa somo jili nilisema ziko familia unakuta wanaishi maisha ya kufanana, kwamfano, Ziko koo unakuta ukoo mzima hakuna mtu anamiliki hata baiskeli, ama unakuta hakuna mtu amesoma zaidi ya darasa la saba au unakuta hakuna binti ameolewa akadumu kwenye ndoa au vijana familia nzima wana tabia ya kufanana kama ni ulevi, uzinzi, wizi na mengine mengi.

Ukiona familia moja watu wote wana maisha ya kufanana kwa maana wanapitia hali moja chunguza background ya tatizo hilo lilianzia wapi.


 USHUHUDA 

dada mmoja alinipigia simu akilia miezi kadhaa imepita anasema mme wake ana hali mbaya na yuko hospitali hajitambui lakini wakipima vipimo hawaoni tatizo nikamuuliza baadhi ya maswali ya msingi na historia ya huyo mgonjwa kama amewahi kukutwa na tatizo hilo akanipa majibu mwisho nikamuuliza wana muda gani wameoana akasema mwaka mmoja na miezi kadhaa lakini akaenda mbali zaidi akasema familia ya mme wake wamemtangazia kumuua kwa maana wanamtuhumu kwamba yeye na familia yake wanahusika na tatizo hilo, nikamuuliza tena kwani ninyi mna historia ya uchawi kwenu??? akasema hapana nikamuuliza tena unaisi ni kwanini wanakutupia lawama, binti yule akazungumza kitu cha ajabu akasema yeye ni mtoto wa mwisho kwenye familia yao ya watoto wanne na wote ni wa kike lakini dada zake wote wako nyumbani wameachika kwa waume zao wengine wana watoto wengine waliachika miezi michache baada ya ndoa, binti yule wakati anasimulia wakati akilia ghafla roho mtakatifu akaniambia muulize baba yake yuko wapi.?? 

Basi nikamstopisha yule binti na nikamuuliza lile swali roho mtakatifu ameniambia nimuulize, binti akajibu baba yake hamfahamu na inasadikika alifariki yeye akiwa bado mdogo sana. 

Baada ya kujibu hivyo nikanyamaza maana sikujua nimuulize nini tena kwasababu swali hilo halikuwa la kwangu bali roho mtakatifu ndiye aliyemuuliza. 

Baada ya kukaa kimya kwa muda roho mtakatifu akaniambia mwambie mme wake ilikuwa afe leo hii usiku lakini hatakufa nami nikamwambia kwa ujasiri maana najua ni roho amenena ingawa sikujua atapona kwa njia gani, saa hiyo binti alikuwa analia ghafla nikasikia amenyamaza kama vile mtu ambaye hakutegemea jibu la namna hiyo alafu saa hiyohiyo roho mtakatifu akaniambia shida iko kwa mama yake mzazi na nikaonyeshwa kitu alichokifanya miaka mingi iliyopita kwa kushawishiwa na mtu ambaye alikuwa rafiki yake na kitu hicho kikapelekea yeye kuwa mjane maana yake mme wake akafariki na adhabu hiyo ikapita kwa watoto wake wote, nilivoona namna hiyo nikataka kumwambia yule binti chanzo cha tatizo la mme wake lakini roho mtakatifu akanizuia nikamuuliza kwa nini sasa nisimwambie akasema familia hiyo haijampokea yesu bado kwahiyo hata kama ukimwambia hawatajua namna ya kujikwamua hapo  badala yake watoto wote wataanza kumlaumu mama yao na iko vita itazaliwa tena, nikauliza tena kwahiyo nafanyaje hapa akasema  omba toba kwa ajili ya hicho ulichokiona na muombee mgonjwa kule hospitali kisha fanya maombi ya toba hayohayo pamoja ma mama yake. 

Nikafanya kama ambavyo nimeelekezwa na kisha nikamwambia aende hospitali akamchukue mme wake maana ni mzima sasa na sio mgonjwa tena na nikaongea na mama yale pia kwa njia ya simu nikamuelezea kila kitu na akakiri na tukaomba pamoja, amani ikarejea na furaha ikarejea na familia ile yote kuanzia kwa mama mpaka kwa watoto wakampokea Yesu kuwa bwana na mwokozi wa maisha yao na hata yule mme wake na binti naye akampokea Yesu nami nikamtukuza Mungu kwa ajili yao na sasa wanaishi kwa amani na kifungo kimeondolewa. 


Nimekueleza ushuhuda huu makusudi kabisa ili  upatae kuelewa ya kwamba kuna aina ya maisha unaweza kuyaishi na kutumikia adhabu ambayo pasipokuelewa kama ambavyo ambavyo waume za hawa binti walifariki kwa kosa ambalo chimbuko ni kwa wake zao na hata wahusika wenyewe wasijue. 

Kwahiyo ni muhimu kufahamu background ya familia unayotaka kuoa au kuolewa mapema na kama ukimuomba Mungu atakuonesha mapema na atakueleza cha kufanya,ingawa si vijana wengi wanatazama jambo hili mapema kabla ya kuoa au kuolewa lakini hili ni jambo muhimu sana kwa usitawi ndoa na familia. 


Biblia inasema, 

“Kaini akamwambia Habili nduguye,

[Twende uwandani]

”ikawa walipokuwa uwandani, kaini akamwinukia habili nduguye na kumwua. Mwanzo 4:8


 Mwanzo 4:23-24 

 Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;

Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba, Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba. 


Lameki ni uzao wa kaini sasa unaweza kuona makosa yaleyale aliyoyafanya kaini ya kumuua ndugu yake yanaendelea katika uzao wake japo ilipita miaka mingi sana tangu kosa lile lifanyike. 

Katika kipengele hiki nakutazamisha jinsi ambavyo eneo hili lisiposhugulikiwa kikamilifu linaweza kuvuruga hali yako ya ndoa itategemeana na huyo mwenzako au wewe mwenyewe unaandamwa na nini nyuma yako haijalishi umeokoka  au hujaokoka kwasababu Yesu alizibeba dhambi zetu na akafa msalabani kwa ajili ya ulimwengu lakini hiyo haimaanishi husitubu dhambi zako kwasababu tu yuko mtu alikufia vinginevyo ile siku  tunaokoka mlango wa dhambi ungekuwa unafungwa lakini swala la kumpokea yesu ni jingine na swala la kuishi maisha matakatifu ni jingine ndio maana maandiko yanasema,

 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Mathayo 7:21

Kikawaida tunapompokea Yesu tungekuwa tunasema sasa tunaenda mbinguni kwasababu tuko ndani ya Yesu lakini sivyo biblia inasema bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni

Kwahiyo unaweza kuokoka na bado jehanamu ukaenda ikiwa tu hutaishi kwenye hicho kipengele cha Kuyatenda mapenzi ya Mungu.

Katika sababu hii ya tatu ya mwendelezo wa somo letu Nimalize kwa kusema ni muhimu sana kushugulikia historia ya kwako na ya mwenzako kabla ya kuingia katika eneo la ndoa lakini zaidi sana mpe roho mtakatifu nafasi kwa sababu kuna vitu kibinadamu ukivichunguza ni ngumu kupata majibu yake kwasababu ikiwa adhabu inaweza kupita kwa vizazi vinne maana yake BABA, MTOTO, MJUKUU NA ANAYEFATA HAPO uwe na uhakika ni ngumu sana kujua chanzo cha tatizo pasipo roho mtakatifu ikiwa kosa lilifanyika nyakati za baba ya babu yako kwa maana hiyo hutakuwa hata na mtu wa kumuuliza hata kama ukiamua kufatilia lakini kupitia roho mtakatifu kila kitu kitakuwa wazi na itakupa wepesi na uhakika wa kwamba Mungu yuko na wewe kwenye jambo hilo ndio maana ameamua kukusaidia.

====================================================================

DAY 5

 SABABU YA NNE

4.KUSHIRIKI TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA

Karibu kwa mara nyingine tena katika mwendelezo wa somo letu la   "Miongoni mwa sababu zinazosababisha ndoa nyingi kuvunjika mapema"

Leo tutajifunza kipengele cha mwisho katika vile vipengele nilivyoandaa kukuletea katika somo hili, lakini kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza ya somo hili kwamba vipengele hivi sio ukomo  bali roho mtakatifu aliye mwalimu wetu sote  anaweza kukufunulia zaidi kutegemeana na mazingira uliyopo na msingi wa uchumba wako.

 “Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.”  Mambo ya Walawi 20:10

Pointi yangu kwenye huu msitari iko hapo kwenye huo msitari wa 10c unaosema, "mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.”

KWAHIYO mtu yeyote anayezini awe ni mwanamke au mwanaume haijalishi yupo kwenye uchumba au hayupo kwenye uchumba, kwa kitendo hicho tu cha uzinifu "roho ya mauti inapita katika maisha ya mtu" ndio maana ya ya kusema "hakika watauawa"


Madhara au umauti yanayotokea baada ya kuzini yanategemeana na msingi wa huo uzinzi wenyewe uliotendeka, nikimaanisha mauti hiyo itakayotokea itaandama zaidi kilichobebwa nyuma ya huo uzinzi wenyewe.

Kwakuwa aina ya uzinzi tunaouzungumzia ni uzinzi wa kipindi cha uchumba, maana yake mbegu inayoachiliwa inaenda kuvuruga step au hatua inayofata kwasababu kilichoko nyuma ya uchumba ni ndoa na ndio matazamio  ya hao waliozini.

Na watumishi wa Mungu wamekuwa wakiweka utaratibu maalum wa kuhakikisha wachumba wanawaweka mbali kipindi cha uchumba ingawa hakuna utaratibu rasmi wa kushugulikia jambo hili lakini kila dhehebu limejitahidi kulinda maadili ya vijana katika eneo hili ingawa pia wakati mwingine kwasababu ya utandawazi kazi au juhudi hizi zimekuwa hazizai matunda yaliyotegemewa kwasababu wahusika nao wamekuwa na PLAN B ya kukamilisha kile wanataka huku wakijihesabia kwamba wao wameshakuwa pamoja na hivi karibuni wataenda kufunga ndoa na hivyo kutokuona shida wala    kizuizi cha kuwazuia wao kukutana kimwili. 

Sina uhakika sana kama kweli wote hawajui madhara ya jambo hilo kwenye usitawi wa ndoa yao hiyo wanayoiendea ama wanajua na wanaamua tu kupuuza lakini niko hapa kusema hivi, 

ikiwa yuko yeyote aliishi maisha hayo kipindi cha uchumba na sasa yuko katika ndoa, usalama wako ni kuomba toba na husijaribu kabisa kujihesabia haki kwa kujiona kama vile ilikuwa ni haki yenu na mlikuwa sawa kufanya mlichokifanya.


unisikilize kwa umakini, UCHUMBA sio agano, bali NDOA  ndio agano, kipindi cha uchumba ni hatua ya kuelekea katika ukamilifu wa agano la ndoa au ni kipindi cha matengenezo ya msingi wa nyumba ya  ndoa imara kabla ya ndoa yenyewe, na hiki ndicho kipindi ambacho mambo yote haya ambayo tangu tumeanza somo hili mpaka tunahitimisha, ndio wakati ambao unatakiwa kuyafanyia kazi kwa ajili ya usitawi wa kusudi la Mungu na agano imara la ndoa yenu, 

ukiingia katika ndoa na mambo haya hujayafanyia kazi maana yake ujitayarishe kukutana na matokeo ya madhara ya kutokushugulikia mambo haya mapema na hapo ndipo utakapoenda kukumbana na migogoro ya ndoa tuliyoiona katika somo la UPONYAJI WA NDOA YAKO


Maana yake utakuwa na kazi mbili,

 kwanza utatakiwa kuangalia ni wapi ulifanya makosa katika kipindi cha uchumba na pili utatakiwa kuangalia migogoro uliyokutana nayo katika ndoa je ni matokeo ya kutokupata mafundisho sahihi na maamzi sahihi wakati wa  kuandaliwa na kuhama kutoka katika uchumba na kuingia katika ndoa???

Kwasababu mambo yote haya yana sehemu yake, unaweza ukafaulu kwenye kutengeneza uchumba safi na imara kama maandalizi ya ndoa lakini ukafeli kwenye kuhama kutoka kwenye uchumba kuingia katika ndoa kwa maana ya aina ya mafundisho ya namna ya kutembea katika maisha ya ndoa uliyoyapata pamoja na msingi ulioandaliwa, sasa itakuwa hatari sana kama utakuwa umefeli sehemu zote mbili maana itakuwa tabu kutambua chanzo cha tatizo linalotokea kama ni kwenye maandalizi ya  uchumba au kwenye mafundisho ya kuelekea katika ndoa ingawa bado unaweza kutoka hapo ulipokwama kwa msaada wa roho mtakatifu lakini unaweza kuepusha gharama zote hizo kwa kuhakikisha unatembea katika yote haya.


Jambo hili limewagharimu wengi sana pasipo wao kuelewa na kwasababu walifanya jambo hilo kwa siri, unakuta hata hawatubu na saa ingine hata mchungaji hajui kilichotokea huko nyuma kwahiyo wanakuwa ni watu wenye ndoa ya changamoto na migogoro mingi ambayo inapitia mahali ambapo hata kama ukiwaombea huoni matokeo chanya yakitokea kwasababu kuna mahali wamekorofisha na either wanaogopa kusema kwa kiongozi wao wa kiimani au hawajui kama chanzo cha hiyo shida ni kosa walilolitenda kipindi cha uchumba, wanang'ang'ana tu kuombewa na wanasahau kwamba njia pekee ya kuondoa uovu ni toba.

Wako watu wanaingia kwenye uchumba na wanakutana kimwili na kwasababu linakuwa jambo endelevu wakati mwingine wanajikuta binti anapata ujauzito na wanashindwa kutoa kwasababu ni wapendwa kwahiyo wanaharakisha taratibu za mahari na vitu vingine ili ndoa ifungwe mapema waingie huko kabla ujauzito haujaonekana, maana yake wanatengeneza picha ili ionekane kama vile mimba ile imeingia kipindi cha ndoa sio kipindi cha uchumba. 

Lakini kuna hatari kubwa sana hapa inayokiandama kizazi chako ambayo wengi wa wanaofanya hivyo hawajajua, 

Biblia inasema,

 “Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.”Mwanzo 21:10 

Kwa wale wasomaji wa biblia wanaelewa habari hii kwamba ibrahimu alichelewa kupata uzao akiwa na mkewe sara, mwisho wa siku mke akamshauri mme alale na mjakazi aliyeitwa hajiri ili angalau wapate uzao na mrithi kwasababu walifika mahali pakujikatia tamaa na wakaona kama hawawezi kupata mtoto tena. 

Na ikawa kama walivyokubaliana na mjakazi akapata mtoto mwisho wa siku maandiko yanasema mke halali wa ibrahimu siku moja akamuona mtoto wa mjakazi anafanya dhihaka na  

Sara akataka afukuzwe yeye na mama yake kwasababu uthamani wa mtoto yule kwa sara ulikuwa ni kipindi kile yeye hajapata mtoto lakini ukirejea hapo nyuma inaonyesha Mungu aliwapa uzao katika kipindi cha uzee, kwahiyo yule mtoto wa mjakazi hakuwa na thamani tena machoni pa  sara ingawa yeye ndiye aliyekuwa msababishi. Na uthamani wa mtoto huyo ulipotea kwasababu sara alishapata uzao ambao ni mtoto wake isaka kwahiyo hakuona sababu ya mtoto huyo wa kambo kuendelea kuwepo hapo.


Jambo hili likawa baya sana kwa ibrahimu kwasababu pamoja na kwamba ni mtoto wa kambo kwa sara lakini ni mtoto wa ibrahimu  huyu na ni damu yake hii.

Sasa kumbuka wakati wanafanya maamuzi haya ya mwanzo ya ibrahimu kulala na mjakazi hawakumshirikisha Mungu kwahiyo ibrahimu alipofika mahali pa namna hii "njia panda" 

Anawaza amfukuze mtoto na mama yake kama mke alivyotaka au la!!!


Sikia kitu Mungu anamjibu ibrahimu,

“Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.”Mwanzo 21:12

Sijui kama unaelewa huu msitari pale Mungu anapomwambia ibrahimu kuwa kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.

Kwa kusema hivi maana yake Mungu anamnyima mzaliwa wa kwanza wa ibrahimu nafasi ya kilango kwasababu kikawaida baraka hizi anazotamkiwa isaka ilitakiwa atamkiwe ishmair ambaye ndiye mzaliwa wa kwanza.

 Unaweza kuhoji ni kwanini?? 

Jibu ni kwasababu ingawa ishmair ni mtoto wa ibrahimu lakini ni mtoto aliyepatikana nje na agano,

Kwahiyo mtoto anayezaliwa katika ndoa ambaye mimba yake ilitungwa kipindi cha uchumba huyo sio mtoto wa ndani ya ndoa bali ni mtoto wa nje ya ndoa kwasababu mimba yake wakati inatungwa hakuna agano lililokuwepo wakati huo la kumthibisha yeye kwamba yuko ndani ya agano, kwahiyo kuna baraka ambazo mtoto huyo kwakweli zilikuwa haki yake lakini hatazipata kwasababu ya makosa ya wazazi wake na upande mwingine wazazi wanatengeneza vita ya malango kwasababu kuna heshima na aina ya upendeleo na  vitu ambavyo ishmair atavitaka akiamini yeye ni mzaliwa wa kwanza na ana haki navyo lakini atavishuhudia akipewa isaka, hapawezi  kuwepo na amani kati ya wawili hawa.

Esau hawezi kumuelewa Yakobo kiwepesi kwa kuchukua haki yake ya uzaliwa wa kwanza, sasa ukiwa kama mzazi kuna aina ya vita unaweza kuishuhudia katika uzao wako na husijue namna ya kuiondoa ikiwa hujui wapi ulikovuruga.

Ukiachilia mbali na hilo jambo jingine au madhara mengine ya kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa ni kupitisha roho ya mauti katika ndoa yako, maana yake unafungua mlango wa adui kupanda mbegu ya kwake kwenye ndoa yako pasipokujua, kwahiyo shetani anaweza akaamua aivuruge ndoa yako na awatenganishe au awaache lakini mbegu ile ya mauti aipandikize kwa uzao wenu na huduma zenu kwasababu anao uhalali wa kuyafanya yote hayo kwasababu kinachompa shetani uhalali katika maisha ya mtu ni dhambi na kinachomnyima uhalali ni damu ya Yesu, ndio maana ukiachilia damu ya Yesu mahali shetani hawezi kukatiza hapo.

Ziko ndoa nyingi sana hazina amani kwa kosa hilo, wako watoto wengi wameharibikiwa kwasababu ya kosa walilolitenda wazazi wao, ziko ndoa zimevunjika kwasababu ya kosa hilo, ziko ndoa zinaishi kwa matumaini kwasababu ya kosa hilo, kwahiyo husije ukafikiri ni jambo jepesi sana kama ambavyo wahusika wanalichukulia linaweza kutesa maisha yako na ya uzao wako lakini asante Yesu kwasababu yupo kwa ajili yako lakini unaweza kuepuka kutumikia adhabu na gharama ya kosa hilo kwa kuyaepuka yote hayo mapema.

Kipengele hiki kimeelezwa kwa kina kwenye somo la uponyaji wa ndoa yako namna ambavyo madhara ya yake yanaweza kuharibu na kuvuruga ndoa yako na uzao wako kwa wale walioko ndanibya ndoa kwa maana ya kutoka nje ya ndoa kufanya uasherati. 

Pamoja na hayo biblia inasema, 

 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.”Mithali 6:32

Kwahiyo siku mnafanya kitendo hicho ndio siku ambayo nafsi na akili  zenu zilinaswa mikononi mwa shetani. Maana yake mlango wa uangamivu ulifunguka kwenu na nafsi ikikamtwa uwe na uhakika shetani akifanikiwa kubana nafsi yako na uwezo wako wa kufikiri maana yake huwei kuwaza nje na yeye mwenyewe huwezi kushi maisha ambayo huko hutu kiasi ambacho ukapingana naye. kwahiyo mnaingia katika ndoa mkiwa wafungwa wa fikra na nafsi, kufikiri kwenu na kuamua kwenu na uhuru wenu kuna kitu kinawaamulia na sio ninyi. 


Nimalize kwa kusema hapa ndio mwisho wa somo letu la MIONGONI MWA SABABU ZINAZOSABABISHA NDOA NYINGI KUVUNJIKA MAPEMA


 Mungu wangu akubariki sana na tukutane tena katika somo lijalo.

 **MWISHO**

Post a Comment

0 Comments