100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

NGUVU YA DHAMBI

NGUVU YA DHAMBI 

KANAANI MPYA MINISTRY


Telegram Group

https://t.me/joinchat/zkBymjsosO8wZTE0


Fafebook Page

https://www.facebook.com/Kanaanimpya2020


Whatsapp  Group

https://chat.whatsapp.com/IkMhhdEDNAdGnWi2H7sadf


 Bwana Yesu Asifiwe 

 Ezekieli 18:26-27 

 Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, akafa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa.Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.

Karibu  mwana wa Mungu tena madhabahuni pa Bwana tukapate chakula cha kiroho kwa ajili ya usitawi wa maisha yetu ya kiroho na kimwili maana imeandikwa hatutaishi kwa mkate inamaanisha kuna njaa nyingine ya kiroho ambayo haitoweki kwa mkate wa mwilini.

Kwa maana hiyo sasa nikukaribishe tukajifunze kwa ufupi kabisa kama lilivyo NENO LA SIKU, lakini kwa ufupi huo naamini kipo kitu kikubwa kinakwenda kuachiliwa kama sio kwako basi kwangu kwakuwa Neno la Mungu ni pumzi ya uhai naamini iko mbegu inaenda kupandwa katika roho zetu na nafsi zetu.


Neno la siku la leo linatoka katika kitabu cha Ezekieli kama tulivyosoma hapo juu mwanzoni,

Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, akafa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa.Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.

Katikati ya maneno kuna taarifa ya mwaliko wa toba lakini pia kuna taarifa ya matokeo ya nafasi ambayo utaamua kuketi kwayo.


 Kitu cha kwanza cha muhimu hapa ni kuelewa kuwa DHAMBI imebeba MAUTI,

Tunaposema dhambi imebeba mauti maana yake ni kwamba popote penye mauti pana nguvu ya msukumo nyuma yake {kisababishi} 

Maandiko yanasema, 

 “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.” 1 Wakorintho 15:56

 Kwahiyo kuna aina ya uchungu ambao mtu anaweza kuwa nao ndani  unaotokana na makosa au dhambi yake mwenyewe, kwasababu uchungu au matokeo ya dhambi ni mauti na kinachoipa nguvu dhambi ni Torati {sheria} 


Nguvu ya dhambi ni torati au sheria kwasababu kama Mungu asingetaja kwamba uzinzi au wizi au uasherati nk ni dhambi maana yake hata kama mtu angezini au kuiba bado shetani hasingepata nafasi juu ya huyo mtu kwasababu alichokifanya hakijatajwa kama dhambi au ubaya. 

 KWA MFANO 

Kama sheria ya nchi ya Tanzania isingetaja kwamba kubaka ni kosa au kuiba au kuua ni kosa maana yake kuua na kubaka ingekuwa ni haki ya kila mtanzania na ingetokea mtoto wako akabakwa alafu ukaenda kumlalamikia huyo mtu aliyembaka mtoto wako maana yake ni kwamba wewe mzazi uliyelalamika kwa tukio la kubakwa kwa mtoto wako ndiwe ambaye ungefungwa jera miaka thelathini kwa kupingana na sheria, kwasababu kitu ambacho kimeharalishwa kwa mujibu wa sheria wewe ukikiita haramu ni kosa hata kama ni haramu kweli, na kitu ambacho mamlaka husika imekitafsiti kama haramu na kukiwekea sheria, wewe ukitaka kukiharalisha inatafisiliwa kwamba umevunja sheria hata kama una hoja za kudhibitisha kwamba hicho kitu ni harali, mpaka hapo utaelewa kwanini askari polisi wakimkamata muharifu hutumia neno (sheria itafata mkondo wake)

Kwanini!!!! 

kwasababu kinachoipa nguvu  haki na dhambi au kosa ni sheria au torati . 

Kwahiyo mtu ni kiunganishi au kiungo kati ya torati na dhambi au kati ya torati na haki. 


 Unaweza kuhoji kwa namna gani??? 

Kwasababu torati ipo mezani ilishatungwa kwahiyo inasubiri mtu akakinzane nayo ili imuhukumu au aende sambamba nayo ili impe haki yake.

Maana yake ni kwamba, anayeweza kusababisha haki ionekane au ipate nafasi ni mtu kupitia kutenda sawasawa na torati ambayo nyuma yake liko agano, 

na anayeweza kusababisha dhambi ionekane au ipate nafasi ni mtu huyohuyo kupitia torati ileile kwa kukinzana au kupingana nayo. 

Kwahiyo mlango wa dhambi kwenye maisha ya mtu anaufungua yeye mwenyewe kupitia namna anavyoitafsiri na kuitekeleza katika matendo torati au sheria ya  Mungu. 


Kitu cha pili cha kufahamu katika misitari hii ni kuwa MAUTI kupitia DHAMBI inakuondolea sifa ya kuitwa MWENYE HAKI

Biblia inasema;

 2 Mambo ya Nyakati 7:19-20 

 Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu;ndipo nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote. 

Mungu mwenyewe anawambia wana wa israeli ya kwamba wakiacha sheria yake, atawanyanganya nchi aliyowapa maana yake wakikinzana na sheria iliyoko mbele yao watapoteza sifa au haki ya kumiliki hiyo nchi waliyopewa. 

Na kwa tafsiri ileile ya dhambi  kubeba mauti juu ya mtu inamaanisha MAREHEMU hanaga haki kwahiyo ukifa umepoteza sifa ya kwanza ya kuwa binadamu na kwa maana hiyo hakuna namnanunaweza kupata haki za kibinadamu wakati wewe sio binadamu tena,  hiyo ni kanuni ya kimwili lakini ipo  mpaka rohoni na ukitaka ujue ipo mpaka soma ezekieli

 “Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.” Ezekieli 18:27 

Kwahiyo ukitenda uovu au dhambi kwa kanuni ya kiroho unahesabika umekufa na hutaweza kupata haki zako zozote mpaka umekuwa hai tena hata kama huku mwilini unafunga nankuomba siku 40 lakini kama toba haina nafasi kwako uwe na uhakika unajisumbua tu kwasababu kanuni haziruhusu hata wewe kusikilizwa, ndio maana hata mkimuweka marehemu mwezi mzima  bila kumzika hawezi kuhoji kwanini hamjamzika, 

Hata kama marehemu alikuwa na mali nyingi alafu ikatokea mkamzika bila sanda au jeneza bado hawezi kuhoji haijalishi huko kwenye ulimwengu wa roho ananungunika kiasi gani lakini hawezi kufumbua kinywa maana hana sifa katika nchi ya walio hai, akitaka apate majibu ya kueleweka lazima kwanza nafsi hai irudi ndani yake alafu ndipo anaweza akaongea mkamuelewa na kwenye ulimwengu wa roho ni hivohivo huwezi kumsogelea Mungu na kudai haki yako wakati wewe ni mwenye dhambi, ukitaka haki yako jitakase kwanza ndipo unaweza kupata haki yako. Kwahiyo pointi yangu katika kipengele hiki  ni kwamba ukichagua kuishi maisha ya dhambi maana yake umechagua kujitenga na haki yako mbele za Mungu. 


 kitu cha tatu cha kufahamu ni kwamba HAKI ya mtu imefungamanishwa katika TOBA (uhalali au utakatifu).

Maandiko yanasema,

 “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;”  Matendo ya Mitume 3:19

Kwahiyo nyakati za burudisho zinatokea baada ya toba na kwa maana hiyo ni kwamba hakuna tumaini lolote lililo jema ndani ya dhambi kwasababu kwa kusema kwamba tubuni zije nyakati nyakati za kuburudishwa inamaanisha kabla ya hapo hizo nyakati hazikuwepo.


 Isaya 1:18-20 

 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.


Mungu wangu mwema akubariki sana na hapa ndio mwisho wa Neno letu la siku.


 Tukutane tena wakati mwingine

                   Amen

Post a Comment

0 Comments