100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

MIONGONI MWA SIFA ZA MWANAFUNZI WA YESU

MIONGONI MWA SIFA ZA MWANAFUNZI WA YESU

 Mwl:Jovin John 

 KANAANI MPYA MINISTRY 

 Telegram Group

Facebook Page

WhatsApp Group


UTANGULIZI;

 Bwana Yesu Asifiwe 

Mwanafunzi ni mtu yule anayeishi kwa kufuata mambo au mwongozo jinsi anavyoelekezwa na mwalimu au kiongozi wake . 


 Yohana 8:31 

 “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;

” 

 Kwa mtu yule anayeishi na kufuata neno la Mungu ndiye mwanafunzi wa Yesu maana ameifuata ile kweli ituijiayo kwa njia ya neno la Mungu . 


 SIFA ZA MWANAFUNZI WA YESU 

Nimeziainisha baadhi lakini roho mtakatifu anaweza kukufunulia zaidi ya hizi kadri utakavyokuwa ukilisoma somo hili na kulitafakari kwa kina Neno la Mungu kupitia ujumbe huu niliokuletea leo. 


 1. UTAKATIFU

 1 Petro 1:15-16 

 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 

 Kama mwanafunzi wa Yesu utambulisho wa kwanza ni namna au jinsi ya kuenenda katika wokovu.

Utakatifu ndio nyenzo ya kwanza ya kumtambulisha mwanafunzi wa Yesu.Imetufaa kuwa watakatifu kama Baba yetu alivo mtakatifu.

Utakatifu ndio tiketi ya kumuona Bwana , kupokea Baraka kutoka kwa Bwana , kupata kibali kwa Bwana na watu wote n.k 



 2. UPENDO 

 Yohana 13:34-35 

 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. 

Mwanafunzi wa Yesu ni yule mtu anayewapenda watu wote haijalishi wamemfanyia mangapi , mazuri au mabaya . Maana kama Yesu angeangalia mabaya yetu hasingekubali kudharauliwa , kutukanwa , kupigwa , na kunyenyekea hata mauti ya msalaba , lakini kwa kutupenda akayakubali yote hayo ili atuokoe sote kwa pamoja , kwaiyo sasa hatuna budi kuiga upendo wa Bwana wetu Yesu Kristo aliyetupenda pasipokupima uzito wa matendo yetu maovu. 


 1 Yohana 4:19-21 

 Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.

Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.

Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. 



 3.UMOJA 

 Yohana 17:18-22 

 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 

Mwanafunzi wa Yesu anatakiwa kuwa na umoja na  ushirikiano na wenzake , kama jinsi ambavyo Mungu Baba , Mungu Mwana na Mungu roho mtakatifu walivo wamoja hata kuikamilisha kazi ya kuumba ulimwengu na kumkomboa mwanadamu pale alipotenda dhambi , na kumrudisha katika njia sahihi ya kuurithi Ufalme wa Mungu , yatufaa kuiga mfano huohuo tungali duniani sawa na, 

 1 Yohana 5:8 

 “Kwa maana wako watatu washuhudiao[mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.” 

 

Ebu tujifunze kupitia mfano wa watu hawa, 

 Isaya 41:6-7 

 Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu.Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike .


Tazama jinsi kwa umoja wao walivyotiana moyo kila mtu na mwenzake hata kazi yao ikasonga mbele , kwa umoja kila jambo linawezekana maana ndilo neno alilotuhusia Bwana Yesu, 

 Yohana 17 : 22 

 “Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.” 



 4. ANAYESAMEHE NA KUSAHAU 

 Marko 11:25 

 “Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.” 

 Mwanafunzi wa Yesu ni yule anayesamehe na kusahau haijarishi ni nani aliyemkosea na kosa gani alilomkosea . Hata kama ni kosa kubwa lililokuwa na madhara makubwa ni muhimu kama mwanafunzi wa Yesu kusamehe na kulisahau kwa maana hasiyesamehe hatasamehewa, 

 Mathayo 18:21-22 

 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. 


 Soma pia, 

  Luka 17 : 3-4 

 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. 


 5. MTII NA MNYENYEKEVU 

  1 Petro 5:6 

 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;” 

 Kwa jinsi ambavyo Bwana wetu Yesu Kristo alinyenyekea hata mauti ya msalaba , lakini mwisho wake akapanda juu sana akiketi katika kiti cha enzi , ndivyo inavyotupasa na sisi kuwa watii na wanyenyekevu ili kuweza kuzirithi Baraka za Mungu . 

Kumbuka ajiinuaye atashushwa lakini ajishushaye atakwezwa, 

Mathayo 23:12 

 “Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa.” 


 6.WAKILI AU MTUNZA SIRI ZA MBINGUNI. 

 1 Wakorintho 4:1-2 

 _Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu._ 

Mwanafunzi wa Yesu anatakiwa kuwa mtunza siri za Mbinguni na za duniani pia . Aidha mwanafunzi wa Yesu anatakiwa kutokuwa mwongeaji wa mambo yasiyo na msingi, 

 

 7. KUJITOA KWA MOYO 

 Kama mwanafunzi wa Yesu inatakiwa kuwa mtu wa kujitoa wakati wote kwa ajili ya watu pasipokutegemea mazingira yanatafsiri nini . 

Kumbuka atoaye ndiye apokeaye , huwezi kupokea bila kutoa ili uweze kubarikiwa Mungu huangalia kiasi cha kujitoa kwako kwake na kwa wenye uhitaji sio tu kwa Mali bali pia kwa moyo , nguvu, maana biblia inasema, 

 Mathayo 6:21 

 “kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.” 


Mungu akubariki sana karibu tena katika kipindi kijacho.

 UBARIKIWE SANA

Post a Comment

0 Comments