100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

HUWEZI KUPOKEA ZAIDI YA KIWANGO CHAKO CHA IMANI - Mwl Afro Frayerne

HUWEZI KUPOKEA ZAIDI YA KIWANGO CHAKO CHA IMANI - Mwl Afro Frayerne

Mwl:Afro Frayerne

SHALOM SHALOM SHALOM

 MATHAYO 8:6-13 

 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu;nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile. 


Haleluya!!!

Nazungumza kwa habari ya IMANI na matunda yanayoweza kutokana na kiwango chako cha kuamini.

Sote tumesom habari za huyo akida juu ya hitaji lake kwa Yesu.

Alileta maombi yake kwa Yesu kama watu wengine tu walivyoleta mahitaji yao lakini kiwango chake cha IMANI kilisababisha apokee muujiza wake tofauti na wengine walivyopokea.

kwa kusema hivyo namaanisha kwamba kiwango chako cha IMANI kinaweza kumfanya YESU atamke Neno tu na popote ulipo ukapata kupokea, lakini wako watu viwango vyao vya imani ni mpaka wamuone YESU Majumbani kwao ndio wapate kuamini ile hali wanaomuhitaji Yesu kwa wakati huo ni wengi sana.

Biblia inasema, 

 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”    Waebrania 11:1 

Kwahiyo ikiwa tu yako mashaka ndani yako katika unachokiomba kwa kutazama mazingira yanayokuzunguka ni wazi kwamba kupokea kwako kunakuwa ni kugumu kwasababu imani inataka uamini kabla ya kuona, 


wako watu lazima wawekewe mikono ndipo waamini,

Wako watu wakiomba tu popote walipo huamini na wakapokea,

Wako watu katika kuwaza kwao tu katika roho mtakatifu huamini na wakapokea.

jifunze kukuza kiwango chako cha IMANI kiasi ambacho ukihitaji kumuona Yesu katika jambo lolote ni suala tu la kutamka na kuamini na muujiza ukatokea. Hii itakusaidia wakati ambapo upo katika mazingira ambayo ni magumu kiasi ambacho huoni msaada kutoka upande wowote, manake saa hiyo utahitaji kuutazama msalaba kwasababu ukiwa na kiwango kidogo cha IMANI na kadri unavyopita katika moto ndivyo ambavyo uwezo wako wa kumsikia Mungu hupungua, 

lakini IMANI yako ikiwa thabiti haijalishi unapita katika tanuru la moto bado tu utazidi kumuona YESU kama Bwana na mtetezi wako kwa kila hali na hata punje ya imani haitakupungukia.lakini pia ni muhimu sana kuomba kuongezewa IMANI kila mara unapopita mahali pagumu hata kama unajua unayo imani kwasababu kila mazingira yanahitaji kiwango kipya cha IMANI ili upate kupenya.


Maandiko yanasema, 

 “Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani.”   Wagalatia 3:11 

Mahali pengine maandiko yanasema

 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.”   Waebrania 10:38 

Kiwango cha imani yako kikiwa duni  kinakutenganisha na kupokea kwako lakini zaidi sana tunaona huwezi kumpendeza Mungu ikiwa Imani yako ni ndogo kiasi cha kusitasita katika maamuzi yako au maombi yako juu ya kumtegemea Mungu,zaidi sana biblia iko wazi kabisa yakwamba 

 1 Petro 5:8-9 

 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. 

Maana yake ili tuweze kumshinda mshitaki wetu ni lazima tuwe na imani thabiti vinginevyo ni ngumu sana kuvuka ng'ambo ya pito lako kwasababu kazi nyingine ya imani ni kukuonyesha unakoelekea kabla hujafika sawa na Waebrania 11:1

Safari ya mtu hasiye na imani ni sawa na mtu anayetembea umbali mrefu kwa miguu na hajui umbali uliosalia mbele yake kabla ya kufika unakoenda, ni rahisi kuishia njiani kwa kukata tamaa na pengine wakati anakata tamaa yamkini alibakiwa na mwendo kidogo kulinganisha na umbali wa ulikotoka. 

Lakini ni tofauti sana kwa mtu anayetembea njia hiyohiyo huku akijua anakoelekea, haijalishi patakuwa na umbali mkubwa kiasi gani bado atahakikisha kabla ya kuanza hiyo safari anafanya maandalizi ya kutosha kama  kubeba maji au chakula cha kutosha njiani kitachomuwezesha kufika mwisho wa safari yake, na hiyo ndiyo kazi mojawapo ya imani kwa mwenye haki wa Mungu maana yake ukiisha kuomba kwa Imani na Mungu akakufunulia hatima ya hicho unachokiomba inakupa uhakika wa safari yako haijalishi njiani utakutana na akina goriathi wangapi lakini hautavunjika moyo kwasababu huku ndani una picha ya   hatima ya safari yako, 

kwahiyo ni rahisi kujua umebakiza mwendo kiasi gani wakati ukiwa katikati ya safari.

Ukisoma ile habari ya wanafunzi wakati wapo kwenye boti na Yesu alafu ghafla hali ya hewa ikabadilika  wakiwa baharini na mawimbi yakaifunikiza boti yao alafu wote wakakosa cha kufanya na hofu ikawaingia lakini wakakumbuka wanaye Yesu ndani ya boti na walipomwendea sikia kitu Yesu aliwajibu, 

 “Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu”    Mathayo 8:26 

"MBONA MMEKUWA WAOGA ENYI WENYE IMANI

Biblia ya kiingereza inatumia neno  " little faith"

Kwahiyo imani yako ikiwa ndogo mlango wa hofu unafunguka juu yako kwa sababu Yesu aliwaambia wanafunzi Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba na woga ukipata nafasi ndani yako maana yake shetani amepata mlango wa kupanda vitu ndani yako ambavyo mwisho wa siku ni rahisi tu kuikosa mbingu, hii utaipata katika ufunuo wa yohana, 

 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”   Ufunuo wa Yohana 21:8 

Biblia inasema WAOGA NA WASIOAMINI, kwahiyo haijaishi unajihesabia haki kiasi gani kama upo kwenye kundi la wasioamini na hapa maana yake hata wale ambao hawajamkiri Yesu iwe wamo kanisani au nje ya kanisa maana mtu anaweza kuwemo kanisani lakini Imani yake haimtafsiri Yesu katika maisha yake. 

Sasa wote tunaelewa kwamba njia ya mtu kuiona mbingu ni kuwa na Yesu ndani, 

 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”    Yohana 14:6 

Sasa huwezi kuwa na Yesu kama humuamini haijalishi umeokoka, upo kanisani na sadaka na zaka unatoa lakini ikifika saa ya kuangalia qualifications za mtu kupenya kwenye mlango wa Mbingu nakuhakikishia huyu mtu atabaki na ndio maana ya maneno haya, 

 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.”   Mathayo 7:21 

Maana yake katika wokovu kuna zaidi ya kuokoka, ukimpokea Yesu haimaanishi kwamba unawekewa uzio wa kumzia hasiondoke pale unapokengeuka, unaweza ukampokea na bado akaondoka na anayeweza kumfanya abaki na wewe ni wewe mwenyewe na anayeweza kumfanya aondoke ni wewe mwenyewe kupitia namna unavyoipokea na kuitafsiri sheria ya Mungu katika matendo, 

Kwasababu ukitembea ndani ya sheria ya Mungu pasipokukengeuka maana yake umeitii sheria ya  Mungu na kwa kuitii sheria ya Mungu maana yake umetenda mapenzi ya Mungu sawa na Mathayo 7:21b.

Kwahiyo kuokoka au kuwa kanisani tu hakutoshi bali unahitajika kuwa na imani toshelevu ambayo mtu akikutazama kwa nje imani ile uliyonayo inatafisiri picha ya uliyembeba huko ndani kupitia kuwaza kwako, Kunena kwako na Kutenda kwako kwasababu kilichojaa ndani ndicho kinachotoka nje,  “Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.” Yakobo 2:26

Mahali pengine maandiko yanasema, 

Tito 2:7-8 

 katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu,

na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.

Kwahiyo tukitaka kujua ndani yako kukoje tunapima huku nje kwasababu imani inaumba, kama inaumba maana yake ikikita mizizi huko ndani hakuna namna itashindwa kutoa matokeo huku nje. 

Mungu akubariki sana na nimalize kwa kusema, KUPOKEA KWAKO KUNAAMULIWA NA KIWANGO CHAKO CHA IMANI.maana yake {huwezi kupokea zaidi ya kiwango chako cha imani} 

Karibu tena katika kipindi kijacho

Post a Comment

0 Comments