100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

DARAJA LA MAFANIKIO (THE BRIDGE OF SUCCESS) - Mwl:Jovin John

 

 DARAJA LA MAFANIKIO (THE BRIDGE OF SUCCESS) - Mwl:Jovin John

Tufuatilie;

Telegram Group 

Facebook Page

WhatsApp Group

YouTube Channel


         Bwana Yesu Asifiwe 

Matumaini ya mwanadamu hupotea pale aonapo vikwazo mbele yake, mwingine hukata tamaa kabisa na kukosa matumaini ya kupata kile anachokitafuta au hata kukata tamaa ya kuishi kabisa.

Kutoka 14:9-12

“Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. Hata Farao alipokaribia wana wa Israel wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia BWANA.Wakamwambia Musa, je kwasababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri?. Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, tuache tuwatumikie  Wamisri?  maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani”


Matumaini ya wana wa Israeli kupata ukombozi yakapotea ghafla baada ya kuona nyuma yao jeshi la Farao linakuja kwa kasi kuwaangamiza huku mbele yao wamezungukwa na Bahari (Bahari ya Shamu)

Li wapi tumaini la kupata ukombozi, wakakata tamaa huku wengi wao wakimnungunikia Musa ya kwamba angewaacha Waedelee kuwa watumwa Misri kuliko kufia jangwani bila kujua kuwa aliyemtuma Musa kuwatoa Misri anao mkono mrefu ambao unaweza kufanya chochote na kwa wakati wowote.

Ndivyo ilivyo kwa baadhi ya watu wengi yamkini hata sisi tulioamini, inafikia wakati tunapitia magumu tunakata tamaa na wakati mwingine kunungunika kuwa Mungu wetu hatusikii. Kumbuka daraja la mafanikio linajengwa taratibu na mjenzi ni Mungu mwenyewe ila yatubidi kuwa wavumilivu maana Mungu wetu hachelewi wala hawai bali kwa hujibu kwa wakati wake. 

Siku zote Mungu hamtupi mja wake na wamtumainio yeye ni kama mlima Sayuni, hawatatikisika milele hata wapitie magumu ya namna gani.

Mungu akalijenga daraja la mafanikio kwa wana wa Israeli kupitia mtumishi wake Musa:-

Kutoka14:13-14

“Musa akawaambia watu, msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo, kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya”

Matumaini ya wana wa Israeli kukombolewa yakaanza kurudi baada ya kuona taratibu daraja linajengeka.

Kutoka14: 15-16

“ BWANA akamwambia Musa mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele. Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari na kuigawanya, nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu”

Kutoka 14:21-22

“Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto”

Tumaini la wana wa Israeli kupata ukombozi likarudi, Mungu akalijenga daraja la mafanikio kwa safari ya Wana wa Israel kupitia mtumishi wake Musa. Wakashuhudia maajabu ya Mungu akiwapitisha katikati ya bahari huku maji yakitengeneza ukuta. Jeshi la Farao nao wakaona ajabu maana walikuwa hawasadiki kwamba yupo Mungu muumba wa mbingu na nchi awezaye kufanya chochote na kwa wakati wowote.

Hili ndilo DARAJA LA MAFANIKIO (THE BRIDGE OF SUCCESS)


Yamkini unapitia magumu na umekata tamaa kabisa ya kusudi la moyo wako, historia hii ya wana wa Israeli na ifanyike kuwa ushuhuda kwako sasa,

 jenga tumaini kwa MUNGU aliyeigawa Bahari ya Shamu, wana wa Israeli wakapita ndiye Mungu wetu hata sasa, atakupigania nawe utanyamaza kimya. Daraja la mafanikio linajengwa kwa ajili yako na mjenzi ni Mungu mwenyewe.

Hatua pekee ya kufanikiwa katika maisha ni kumpenda Mungu na kujenga tumaini katika yeye.

Mithali 8:17a

“Nawapenda wale wanipendao”

Ishi katika tumaini, mtegemee Mungu, Daraja la mafanikio linajengwa kwa ajili yako.


Mungu akubariki sana karibu tena katika kipindi kijacho.

Post a Comment

0 Comments