100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

SOMO:JINSI AMBAVYO MAPAMBO YA MWILI YANAVYOWEZA KUMFANYA MTU AKAIKOSA MBINGU-Mwl Afro Frayerne

 

SOMO:JINSI AMBAVYO MAPAMBO YA MWILI YANAVYOWEZA KUMFANYA MTU AKAIKOSA MBINGU-Mwl Afro Frayerne

  𝕂𝔸ℕ𝔸𝔸ℕ𝕀 𝕄ℙ𝕐𝔸 𝕄𝕀ℕ𝕀𝕊𝕋ℝ𝕐    

 Bwana Yesu Asifiwe 

Karibu katika somo hili nililolipa kichwa cha JINSI AMBAVYO MAPAMBO YA MWILI YANAVYOWEZA KUMFANYA MTU AKAIKOSA MBINGU. Linaweza kuwa ni somo jipya masikioni mwako ama uliwahi kulisikia, lakini vyovyote vile bado natumia nafasi hii kukukaribisha tena wewe ambaye ulishalisikia na wewe ambaye bado yamkini kuna kitu kipya ambacho roho mtakatifu amekusudia ukipate kupitia madhabahu hii ya KANAANI MPYA MINISTRY. 

Tufuatilie;

Telegram Group

WhatsApp Group

Facebook Page

YouTube Channel


 Ezekieli 7:19-21 

 Watatupa fedha yao katika njia kuu za mji, na dhahabu yao itakuwa kama kitu cha unajisi; fedha yao na dhahabu yao hazitaweza kuwaokoa siku ya ghadhabu ya Bwana; hawatajishibisha roho zao, wala hawatajijaza matumbo yao; kwa sababu zilikuwa kwazo la uovu wao.Na uzuri wa pambo lake, yeye aliuweka katika enzi, lakini wao walifanya sanamu za machukizo yao, na vitu vyao vichukizavyo, ndani yake; ndiyo maana nimeifanya kuwa kama kitu cha unajisi kwao.Nami nitapatia katika mikono ya wageni pawe mateka yao, na katika mikono ya waovu wa duniani pawe mawindo yao, nao watapanajisi.

Nianze kwa kusema unapokipamba kitu chochote lengo kuu unakuwa unataka kipendeze kuliko namna kinavyoonekana kwa maana kwamba mwonekano wake wa kwanza haukuridhika nao na kama ni mtu mwingine aliyekitengeneza alafu wewe ukaja kukikuta kimekamilika maana yake ni kuwa unapochukua maamuzi ya kukipamba ni ishara kwamba unamkosoa  kwasababu ndani yako unaona pamoja na kwamba kajitahidi kukitengeneza lakini hajafikia ubora au uzuri unaotakiwa hicho kitu kiwe nao, kwahiyo unalazimika kuongeza urembo au mapambo au madoido yako binafsi ili kile kitu kiwe kizuri zaidi sawa na uonavyo wewe.


Sasa tukirudi kwa upande wa mwili wa binadamu kutokana na kitabu cha mwanzo inaonyesha kwamba, mtu namna anavyoonekana kuanzia juu mpaka chini ni kazi ya mikono ya Mungu sawa na

 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”Mwanzo 2:7

Inamaanisha sasa Mwili wa Binadamu umetengenezwa au kuumbwa na Mungu kwahiyo kitendo cha mtu huyohuyo kuupamba huo mwili ni sawa na anamwambia Mungu kwamba "hukumaliza kazi yako kwahiyo wacha nikusaidie" na wakati huo sote tunajua Mungu hajawahi kuumba kitu dhaifu wala kisichokamilika.

KWAHIYO mapambo katika mwili ni unajisi kwasababu unapoupamba mwili automatically unakosoa uumbaji wa Mungu na kuufanya kama vile haukukamilika kwahiyo unasimama hapo kwenye nafasi ya Mungu kuhakikisha unatimiliza kazi ambayo Mungu hakuikamilisha.

Ukiangalia ile ezekieli 7  pale anasema.............. Na uzuri wa pambo lake, yeye aliuweka katika enzi, lakini wao walifanya sanamu za machukizo yao, na vitu vyao vichukizavyo, ndani yake; NDIYO MAANA NIMEIFANYA KUWA KAMA KITU CHA UNAJISI KWAO...................

ukiendelea kusoma hapo msitari wa 21 utagundua msitari huo ndio unaompa uhalali shetani  wa wewe kuwa mali yake na atasimama na huo msitari kukushitaki mbele za Mungu kila mara na hivyo kukufanya ukose haki zako haijalishi unajiona ni mtakatifu kiasi gani lakini zaidi huwezi kuingia mbinguni huku mgongoni umebeba kitu kilicho najisi maana imeandikwa “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.”Ufunuo wa Yohana 21:27

Najua bado unapata shida kunielewa pale ninapokwambia kwamba mapambo ya mwili wako ni machukizo yanayotajwa katika ezekieli lakini twende pamoja na kwa msaada wa roho mtakatifu atakusaidia kujua ile kweli iliyoko ndani ya Neno lake. Nina uhakika wako watu wana maandiko ya kutetea machukizo hayo kwa kutaka kuyafanya yaonekane kama halali kama ambavyo wengine wanajitahidi kuhalalisha mavazi ya jinsia moja kuvaliwa na jinsia nyingine tena wengine wanayavaa hata wakiwa madhabahuni,

Ni kweli mimi ni binadamu naweza kukudanganya, lakini nina uhakika Neno la Mungu haliwezi kukudanganya na ni hakika kuwa na mimi ninayekueleza haya siku moja nitakufa, lakini Neno la Mungu litaishi hata saa ya unyakuo na litasimama kama sheria kuhukumu kwa kumtafuta aliyetembea nalo ili limpe haki yake na yule aliyekinzana au kupingana nalo ili limuhukumu naye kwa kumpa haki yake.

Sikulazimishi uyaishi haya ninayoyazungumza lakini ni wajibu wangu kukueleza ile kweli ili yamkini upate kuokoa nafsi yako na la ukishupaza shingo damu yako na itakuwa juu yako.

Nayasema haya kwasababu najua nitapata upinzani haswa kutoka kwa yule anayeamini hivyo vitu na kuvihalalisha lakini ni vizuri ukaangalia maandiko yanasema nini kisha linganisha kile unachokiamini au ulichoaminishiwa au hiki ninachokuambia na baada ya hapo naamini roho mtakatifu atakusaidia kukuonyesha njia maana katika neno ndipo penye majibu ya maswali yetu na hapo ndipo tunapokutana na Mungu na kuzungumza naye kwasababu biblia inasema, “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.” Zaburi 119:105

Kwahiyo kokote tunakoelekea tukitaka tuwe salama lazima Nuru ambayo ni Neno la Mungu liweze kutuongoza na kutuangazia ili tusije tukapotea njia.lakini pia huwezi kukaa mbali na dhambi au kufunuliwa kwamba jambo fulani ni dhambi au baya machoni pa Bwana ikiwa Neno la Mungu halina nafasi ndani yako kwasababu kinachotufungua akili na fahamu zetu ili tuweze kujua hapa pana uzima na hapa pana mauti bado ni Neno la Mungu lilelile kwasababu neno ndilo linalotupa maarifa ya kung'amua mambo yote hayo ndio maana utaelewa ule msitari unaosema, “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.”Zaburi 119:11

Kwahiyo Neno linatupa nguvu ya kuishinda dhambi maana yake pasipo neno ni ngumu sana kutembea katika utakatifu kwasababu mwanga wa kukuangazia uendako utakuwa haupo na taa ya kukuongoza uendako itakuwa imezimika kwahiyo utakuwa unatembea kama kipofu na hivyo kujikuta saa nyingine ukigongana na kisiki au kujikwaa au saa nyingine kudumbukia kabisa shimoni ndio maana ni muhimu sana kwa mwana wa Mungu yeyote kulijaza neno la Mungu ndani yake vinginevyo hautachelewa kutoka kwenye njia yako inayokutambulisha kama mwana wa Mungu.


Nimekueleza mambo hayo makusudi kabisa ili upate kutafakari Neno la Mungu kwa kina na hii itakusaidia kujiepusha na mafundisho yapotoshayo na yadanganyayo maana ni rahisi kuchanganyikiwa pale ambapo mtu huyu anajiita mtumishi wa Mungu anakwambia hiki ni halali na mwingine anakuja tena naye anajiita mtumishi wa Mungu anakwambia hapana hiki ni haramu, unapofika kwenye kona ya namna hii kitu pekee kitakachokusaidia kujua wapi penye kweli ni kurudi kwenye NENO LA MUNGU wala husiamue kwa kutazama ukubwa au umaarufu wa huyo anayejiita mtumishi maana kweli ya Mungu haipo kwa mtu bali ipo kwenye Neno vinginevyo utayumbishwa na mawimbi ya bahari na kujikuta umetupwa ufukweni alafu ukieguka kulia na kushoto unakutana na mamba saa hiyo ukijaribu kuwaita wale watumishi hawapo na wala huwaoni.


Leo niko hapa kukwambia ya kwamba unaweza kuikosa mbingu kwa ajili ya hereni, cheni, mikufu, bangili, nywere za bandia, rangi za kucha, michubuo na mengine Mengi yanayogusa asili ya uumbaji wa Mungu. 

Inaweza kukupa shida bado kuelewa kwa undani lakini huko mbele nitakuonyesha ni wapi vitu hivyo vinageuka na kuwa machukizo kwa Mungu. 


Unaweza kuamini katika kuvaa mavazi ya heshima tu lakini ukaendelea kushikilia hayo mapambo mengine na husione kama kuna shida lakini biblia inasema,

Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.1 Timotheo 2:9-10

Kwahiyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu wanatambulishwa na mapambo yafuatayo, 

1.mavazi ya kujisitiri

2.adabu nzuri

3.moyo wa kiasi

4.matendo mema na mengine yanayofanana na hayo, 

Inamaanisha uthamani wa mapambo ya mwili wako mwilini hauna sehemu katika ufalme wa Mungu wala roho mtakatifu hawezi kushuka kwasababu umevaa mapambo ya gharama au thamani kubwa bali kitakachotambulisha kile ulichonacho huko ndani ya moyo wako ni mavazi ya kujisitiri yawe ya thamani au yasiwe ya thamani pointi ya msingi ni yawe ya kujisitiri lakini uamuzi wa kuamua uvae vazi la thamani gani ni wa kwako kutegemeana na uwezo wako isipokuwa vazi hilo liwe na sifa ya kusitiri mwili pamoja na mengine tuliyoyaona hapo juu kama adabu nzuri,moyo wa kiasi,matendo mema nk.

Mahali pengine maandiko yanatuambia,

 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 1 Petro 3:3-5

Misitari hii haina tofauti na ile ya

 1 Timotheo 2:9-10 lakini hii ya 1petro 3:3-5 inatupeleka ndani kidogo mpaka kutuelezea maana ya mapambo yenyewe haswa yanayokubalika kibiblia,

Ukiangalia ule msitari wa 3 anasema, "kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje" inamaanisha kujipamba kunakomfurahisha Mungu  ni kujipamba  kwa rohoni na sio kujipamba kwa Mwilini, anaongeza pale anasema kusiwe kujipamba kwa nje yaani kusuka nywere, kujitia dhahabu, kule Timotheo ameongeza na lulu, na mavazi.

Anasema mapambo yawe ni ya utu wa moyoni husioonekana na anaongeza kwamba  "maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani"

Kwahiyo utakatifu wako unatakiwa uwakilishwe na mambo hayo ambayo kwa Mungu ndio mapambo yampendezayo na hivyo ndivyo inavyowasitahili watakatifu kuishi.

Lakini pia kule mwisho kabisa anasema wanawake wa namna hiyo ndio waliomtumaini Mungu na kuwatii waume zao

Sasa kamuulize mwanaume yeyote duniani ambaye hajaoa kwamba anataka mwanamke mwenye sifa zipi, awe ana Mungu ndani au hana lakini nakuhakikishia miongoni mwa sifa atakazokutajia ni pamoja na sifa ya mwanamke mtiifu {yaani atakayemtii} 

Kwahiyo mabinti mnisikilize ni kwamba hata wanaume wanatafuta na kuvutiwa na wanawake wenye mapambo ya rohoni na sio mwilini.

Ni biblia imesema sio mimi kwahiyo husijaribu kunikasirikia maana nakwambia tulichokisoma hapo kwa pamoja.


Unaweza kujihoji na kunihoji ni wapi Mungu amezuia mapambo lakini katika kipengele hiki nianze kwa kusema mapambo yote kama hereni, mikufu, bangili nk yanayotumiwa yanatokana na madini kama dhahabu, fedha na mengine mengi kwa majina yake na hata yale ambayo hayahusiani na madini ni yale yanayogusa au kuficha asili ya Mungu kama nywere za bandia, kucha bandia, rangi za kucha, michubuo na mengineyo,


Kabla Mungu hajawalaani Adamu na Hawa na baadae kuilaani nchi,Mungu alipomuumba mtu kusudio lake ilikuwa ni ili aishi milele {maana yake kutokufa}. lakini  siku ile waliyotenda dhambi ndio siku waliyofungua mlango wa mauti na tangu wakati huo Adamu na Hawa wakapoteza sifa ya kuishi milele {maana yake wakapoteza ile nafasi ya umilele} hii utaipata katika kitabu cha mwanzo.


Mungu alipoilaani nchi ndipo tulipoanza kutawaliwa na mauti lakini kabla ya kuasi tulikuwa na nafasi ya kuishi mbinguni na duniani kwa wakati mmoja ndio maana ya kufukuzwa Edeni na Mungu alituumbia umilele na alikuwa tayari amekwisha kutuandalia vitu vya kujengea nyumba tutakazoishi milele ambazo haziharibiki kwasababu tusingeweza kujengea kitu ambacho baada ya muda kitaharibika kwahiyo kwa vyovyote vile aliandaa vitu kama dhahabu na madini Mengine ambavyo vinadumu milele pasipokuchakaa wala kupoteza uimara wake ili vitumike kujenga makazi yetu ya milele kwasababu dhahabu au madini mengine hayana expired date kwahiyo lazima vingetumika kujenga nyumba ambayo pia haitakiwi kuwa na expired date kwasababu watu wenyewe wa kuishi katika hizo nyumba hawana expired date maana yake hawafi.


Kwahiyo dhahabu na madini mengineyo yaliubwa kwa kusudi la UJENZI na sio kwa kusudi la MAPAMBO ya mwili. 

Najua unawaza kwa namna gani na nina uthibitisho gani wa maneno haya lakini mapema tu utapata majibu. 


Ufalme wa giza wanaelewa mambo haya kwasababu walikuwepo wakati vitu vyote hivyo vinaumbwa na kupangiwa matumizi.

Kwahiyo baada ya uasi wakati huohuo ufalme wa giza walijua utukufu wa Mungu haupo tena juu ya mwanadamu na uwezo wa Mungu au nguvu ya Mungu imeondolewa kwao. {unasema walijuaje}

Walijua  kwasababu Mungu alikwisha kumtahadhalisha Adamu kwamba, “walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo UTAKUFA HAKIKA .” Mwanzo 2:17 

kwahiyo walipokula tu kule kwenye ulimwengu wa giza mlango ukafunguka na ukizingatia ilikuwa ni misheni yao na mpango wao {unasema unajuaje}

Kwasababu walimtuma nyoka akaenda kumdanganya Hawa na hivyo alipofanikiwa lazima kule kwenye ufalme wa Giza alarm za ushindi zilitoa mlio na ghafla kitu cha kwanza walichofanya ni hiki, walificha hazina yote machoni pa adamu na hawa ambayo Mungu aliiweka kama azina kwa ajili ya ujenzi wa makao ya milele ya watu wake. {unasema una uhakika gani}

Nina uhakika kwasababu Adamu na Hawa kabla ya kuasi kwao walipewa uwezo wa mamlaka ya utawala juu uumbaji wote sawa na, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, NA NCHI YOTE PIA , na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Mwanzo 1:26 

anaposema na nchi yote pia maana yake Ardhi yote na kila kilicho juu ya ardhi, kwahiyo shetani alichukua funguo za hiyo mamlaka kutoka mikononi mwa Adamu ambaye alikuwa amepewa na Mungu na hivyo hata adamu Mwenyewe kuwa chini ya shetani kwasababu "huwezi kuwa na maamuzi mahali ambapo hauna mamlaka"

Na Mungu anapomfukuza Adamu kwenye Busitani ni udhihirisho kwamba Adamu hana haki tena ya kuendelea kuishi hapo maana yake hana mamlaka tayari na kama anayo basi ni kidogo na yenyewe ina mipaka.


Najua bado unawaza kwa habari ya azina hizo kuumbwa kwa kusudi la  ya ujenzi na sio mapambo na ni shahuku yako kujua pia ni wapi panapoonesha kwamba shetani alizificha hizo hazina,

Wacha tuendelee nikuonyeshe uthibitisho kwamba azina alikuwa nazo shetani baada ya uasi biblia inasema,  Akampandisha juu, akamwonyesha MILKI zote za ulimwengu kwa dakika moja.

Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe ENZI hii yote, na FAHARI yake, kwa kuwa IMO MIKONONI MWANGU, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.Luka 4:5-8

katika mistari hii hakuna mahali ambapo Yesu anakanusha ukweli wa Maneno ya shetani Bali anajibu hoja yake, inamaanisha sasa mananeo haya ya shetani ni ya kweli kwamba MILKI, ENZI NA FAHARI YAKE VIKO MIKONONI MWAKE. {swali langu kwako ni kwamba alivichukua lini na alipata uhalali wa kuvimiliki kutokea wapi}


Lakini pia nikuthibitishie kwamba vitu hivyo viliwekwa kwa ajili ya UJENZI na sio MAPAMBO kwa kutazama andiko hili,

 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya YASPI, na mji ule ulikuwa wa DHAHABU safi, mfano wa kioo safi.

Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa YASPI; wa pili YAKUTI SAMAWI; wa tatu KALKEDONI; wa nne ZUMARIDI; wa tano SARDONIK; wa sita AKIKI; wa saba KRISTOLITHO ; wa nane ZABARAJADI; wa kenda YAKUTI ya manjano; wa kumi KRISOPRASO; wa kumi na moja HIAKINTHO; wa kumi na mbili AMETHISTO.Na ile milango kumi na miwili ni LULU kumi na mbili; kila mlango ni LULU moja.Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

Ufunuo wa Yohana 21:18-21

Huo ni ujenzi wa mji mtakatifu ambao unaweza kuona vitu vilivyotumika kuujenga ni madini tupu na vito vya thamani ambamo ndani yake wataingia watakatifu wa Mungu, ukiendelea mbele utaona ule msitari wa 27 unasema, “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Ufunuo wa Yohana 21:27

Makazi hayo ni ya milele sawa na ambayo tungeweza kuyajenga kama tusingeliasi na kuondolewa katika nafasi ya umilele.lakini asante Yesu ambaye ni wa neema na rehema anayetupa nafasi nyingine ya kuishi milele japokuwa nafasi ya kwanza tuliipoteza. 

Kwahiyo, Mungu aliumba dhahabu na madini mengine kwa lengo la kujengea lakini shetani ndiye aliyeingiza wazo la kuitumia dhahabu hiyo na azina  nyingine kwa kuvibalishia matumizi na kutengenezea  Vinyago yaani miungu badala ya MUNGU. 

Biblia inasema, Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Kutoka 32:3-4

Huu ni wakati ambao wana wa israeli walisimamisha sanamu, sanamu ambayo walilazimika kutoa vitu vyao vyao vya thamani vilivyotengenezwa kwa dhahabu ili vikatumike kutengeneza hiyo sanamu na kuanza kuiabudu, jambo ambalo lilisababisha hasira ya Mungu kuwaka juu yao kwasababu wamemsahau Mungu wao na kuiinua miungu mingine badala yake.


Najua bado una maswali mengi na unajiuliza ni kwa namna gani hereni, cheni, mikufu, bangili, na vitu vinavyogusa asili ya uumbaji wa Mungu kama vitu vya bandia katika mwili wako vinawezaje kuhusika na kuufanya mwili wako kuwa kama machukizo mbele za Mungu na kukufanya usipate haki yako.


Karibu katika mwendelezo wa somo hili na katika sehemu ya pili tutaanza na kipengele hicho.


Mungu wangu mwema akubariki sana na nikukaribishe katika mwendelezo wa somo hili.


================= DAY 2=================


Karibu katika mwendelezo wa somo la JINSI AMBAVYO MAPAMBO YA MWILI YANAVYOWEZA KUMFANYA MTU AKAIKOSA MBINGU.

Lengo la somo hili ni kuifunua kweli ya neno La Mungu ambayo yamkini imefichwa kwako kutokana na mazingira yanayokuzunguka au kiwango cha maarifa ulichonacho au aina ya mapokeo tuliyoyapata yanaweza kuifanya kweli ya Mungu iwe wazi kwetu au ifichwe  kutokana na msingi wa maarifa yenyewe tunaojengewa.


Tuendelee na somo letu,

Katika sehemu ya kwanza nilikueleza kwenye sehemu ijayo tutajifunza ni kwa namna gani mapambo ya mwili kama hereni, cheni, mikufu nk jinsi ambavyo vinaweza kuufanya mwili wako uwe machukizo mbele za Bwana pale unapoweka mapambo hayo katika mwili wako.

Biblia inasema miili yetu ni hekalu la roho mtakatifu kwahiyo wakati wote inabidi hekalu hilo liwe safi kwa ajili ya roho mtakatifu vinginevyo ataondoka maana yeye ni mtakatifu na hakai mahali pachafu.


Najua unawaza ni kwa namna gani mapambo hayo yanageuka na kuwa machukizo, kule sehemu ya kwanza tulijifunza vitu vingi kuhusiana na uumbaji wa Mungu na miongoni mwa vitu tulivyojifunza tuliona kusudi la Mungu la kuumba hayo madini na vito ambavyo leo ndivyo vinavyotumika kutengeneza mapambo ya mwili na wengine wanaenda mbali kwa kutengenezea sanamu na kuziabudu lakini pia tuliona kupitia maandiko namna ambavyo vitu hivyo vilianza kubadilishiwa matumizi na shetani tofauti kabisa na kusudi la Mungu na leo tutaona ni kwa namna gani vitu hivyo vinatafsiriwa kama machukizo mbele za Mungu.


 *Bwana akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;

nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;waifikilie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia.Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri.Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni vyombo vyenu vya uzuri ili nipate kujua nitakalowatenda.Basi wana wa Israeli wakavua vyombo vyao vyote vya uzuri, tangu mlima wa Horebu na mbele.     Kutoka 33:1-6

Kwa maneno hayo inamaanisha kuna maombi yako yanaweza yasijibiwe kwa sababu tu ya kuvalia mapambo kwasababu hapo juu wakati Mungu anampa maelezo Musa juu ya safari iliyokuwa mbele yao anawambia ili aweze kuzungumza nao sharti wavue vyombo vyao vya uzuri ambayo ndio mapambo, lakini ukirudi kule juu Mungu anamwambia musa kwamba, "mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu."

Inamaanisha alikuwa anawaonya mara nyingi na hawasikii au hawatii maonyo wanayopewa kwasababu mtu hawezi kukwambia una shingo ngumu kama hakuwahi kukuonya na ukashupaza shingo na biblia inasema "Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri."

Unaweza kuona kwamba walijua hasira ya Mungu itawaka juu yao mapema sana kwasababu tu ya hayo machukizo waliyoyavaa na usalama wao ukawa pale walipoyavua na Mungu aliwapa sharti hilo kwamba ili watembee pamoja naye ilikuwa ni lazima wajitenge na hayo mapambo au vyombo vya uzuri.


Kwahiyo kuna mahali Mungu hajifunui kwetu kwa kiwango sitahiki sawa na nguvu na uwezo wake kwasababu kuna vitu tumevishikilia ambavyo ni machukizo mbele zake, 

 swali la kujiuliza ikiwa Mungu ni yuleyule jana, leo na hata milele na analitazama neno lake apate kulitimiza lakini pia Yesu mwenyewe alisema ikiwa mtu atakuwa na imani ataweza kutenda hata zaidi ya aliyoyatenda, jiulize sasa kwa nafsi yako ni mara ngapi mengine ambayo hata hayafikii miujiza na matendo ya yesu umetamani kuyatenda lakini hukufanikiwa na ukicheki ni hakuna mahali ambako umekosea kwenye utakatifu wako lakini kuna nguvu za Mungu huzioni kwa kiwango kilekile kama ambavyo Mungu huyo unamuhubiri katika mataifa, ni kwasababu kuna mazingira ya kimwili na kiroho ambayo yanazuia kiwango cha nguvu za Mungu kisionekane na badala yake hata hivyo vidogo tunavyovifanya na kuvitenda vinatokea tu kwasababu ya Neema ya Yesu kristo lakini ingekuwa nje na hapo maana yake hata hayo yasingetokea.


Unaweza kujitetea kwa nguvu zote kadri uwezavyo lakini nakuhakikishia hakuna neno la Mungu hata moja kuanzia mwanzo mpaka ufunuo ambalo Mungu atalipa kisogo, kila neno litatimia na kila neno limebeba ujumbe wa Mungu. 

Maana yake popote ambapo Mungu amesema USIFANYE alafu wewe kwa kujifanya ni wa kiroho sana UKAFANYA ujue unakinzana na neno la Mungu au hujasoma mahali panaposema “Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.” Mathayo 5:18

Mahali pengine maandiko yanasema,

 “Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati.” 

Luka 16:17

Kwahiyo ujue tu hakuna neno ambalo litapotea bali siku ya mwisho kila neno ulilokinzana nalo litasimama kinyume na wewe.


Katika kitabu cha mwanzo biblia inasema,

  Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako.

Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu.

 Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea.

 Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu.

 Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.

Mwanzo 35:1-5

Mungu alimwambia yakobo ya kwamba aelekee betheli kama tulivyosoma hapo juu, kisha baadq ya maelekezo hayo tunamuona yakobo akiwaambia watu wa nyumbani mwake waondoe miungu iliyopo kati yao maana yakobo alijua kabisa Mungu hasingeweza kutembea nao kuelekea betheli wakati wana miungu mingine kwahiyo ilikuwa ni lazima miungu yote waiache nyuma ndipo waweze kuambatana na Mungu wa Israeli.

Sasa cheki kitu walichokifanya wale watu baada ya kupewa maagizo na yakobo kuhusu kuondoa miungu waliyonayo, biblia inasema "Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na PETE zilizokuwa MASIKIONI mwao"

Kitu cha kujiuliza hapa ni kuwa Yakobo hakuwambia wavue mapambo yao au urembo wao wa masikioni yeye aliwambia watoe miungu lakini wao wakaenda mbali zaidi pamoja na kutoa miungu waliyoambiwa lakini walijua kiko kizuizi kingine kati yao ambacho kinaweza kuwafarakanisha na Mungu wao huko njiani waendako na biblia inasema baada ya Yakobo kupokea hivyo vitu kutoka kwao alienda kuvificha maana yake wakati wanaenda betheli waliviacha nyuma sasa kama hizo pete za masikioni ambazo kikawaida zinaonekana kama mapambo zilikuwa na shida gani na kama zilikuwa ni haki yao na halali mbele za Mungu kwanini walizivua, hiyo inamaanisha mapambo hayo hayakubaliki mbele za Mungu lakini pili ukiwa nayo yanakufarakanisha na Mungu kwa kusababisha hasira ya Mungu kuwaka na tatu ni kizuizi cha maombi yako kupata kibali kwa Bwana kwa mujibu wa maelezo tuliyoyaona katika kitabu cha kutoka kwa wana waisraeli maana maandiko yametueleza baada ya kutoa hayo mapambo yao ndipo Mungu alikuwa tayari kutembea nao.


Ukisoma kutoka sura ya 12:35-36

 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.Bwana akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara. 

 utaona wana wa israeli wanachukua vyombo vya dhahabu na fedha na mavazi sawa na Neno la Mungu kwa Musa, Mungu alijua watakapofika nchi ya ahadi lazima watatakiwa kuwa na mahali pa kumuabudu kwahiyo aliwambia wachukue hivyo vitu sio kwa maana ya mapambo na kutengenezea sanamu kama wao walivyofanya huko njiani. Kwa maana hiyo dhahabu hizo na fedha zilitakiwa kutumika kujenga hekalu la Mungu na vyombo ya hekaluni kwa hiyo kwa kubadili vitu hivyo kwa matumizi yao binafsi walivinajisi ndio maana utaona Mungu hayuko tayari hata kutembea nao na kuwasikiliza maombi yao wakiwa wamevivaa japokuwa yeye mwenyewe ndiye aliyewambia wavichukue hivyo vitu kutoka kwa wamisri lakini kwa kuvinajisi Mungu akavikataa kwasababu kwa kitendo hicho tu walichokifanya cha kuvifanya kama vyombo vya uzuri au mapambo katika miili yao na kuvitengenezea sanamu walibadili utukufu wa Mungu kwa sanamu.


Biblia inasema,

 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.   1 Wakorintho 3:16-17

Hapa biblia inatwambia kitu cha muhimu sana ambacho ningetamani ukione,

1.anasema sisi ni hekalu la Mungu, yaani mimi na wewe.

2.anasema roho wa Mungu anakaa ndani yetu, yaani mimi na wewe.

3.anasema endapo mtu ataliharibu hekaluna la Mungu {yaani MWILI}, naye  Mungu atamuharibu huyo Mtu. 

Na jambo hili lilitokea wakati wa wana wa israeli walipotengeneza sanamu, {unasema unajuaje}

Kwasababu wakati ambapo Musa amejitenga akiwa katika kuomba na huku chini wana wa israeli wakaamua kutengeneza sanamu Mungu alimwambia Musa maneno haya, 

 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri WAMEJIHARIBU NAFSI ZAO ,wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

Kutoka 32:7-8

Neno wamejihabri nafsi zao maana yake wameharibu utu wao, kwasababu ili uitwe mtu kamili lazima uwe na nafsi hai na ili iitwe nafsi hai lazima iwe na pumzi ya Mungu ndani yake,kwahiyo kwa kitendo kile walifungua mlango wa uangamivu katika nafsi zao au roho zao. Kwahiyo kuna vitu tumevishikilia na pasipokuelewa ama tunaelewa lakini tunataka kwendana na dunia tunajikuta nafsi zetu zimekamatwa mahali ambapo hatuwezi kujitetea kwasababu uangamivu unatengeneza mauti.

Jambo la

4.anasema hekalu la Mungu ni takatifu ni  ambalo ndilo ninyi.

Kwahiyo inamaanisha kitu chochote kilicho kinyume kikigusa mwili wako ndani au nje uwe na uhakika kimelichafua hekalu la Mungu na kwasababu hekalu limechafuka au kunajisika hakuna namna ambavyo nafsi yako huko ndani inaweza kuwa salama maana roho mtakatifu hayupo tena na mlango wa uangamivu umefunguka.


Katika msitari huu nimewasikia watu wengi wakijijaza maneno na kuwajaza wengine kuwa Mungu haangalii mwili bali roho ya mtu, lakini ni uongo mkubwa sana kwasababu Mungu anajishugulisha na hivyo vitu vyote maana maandiko yanasema, “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Warumi 12:1

Kwahiyo ukamilifu wa ibada yako unaanzia mwilini kwanza, sasa ikiwa Mungu hana haja na mwili kama wengine wasemavyo inakuwaje mwili huo unaingizwa na kuwa sehemu ya ibada, lakini pia nikumbushe jambo moja tu kwamba hakuna kitu chochote ambacho Mungu amekiumba bila makusudi kwahiyo wewe ukiona jambo fulani halina maana ujue hujajua mapenzi ya Mungu juu ya hicho kitu.

Biblia hapa haijsema moyo bali imesema mwili, Mungu anayo makusudi katika roho ya mtu na Mungu anayo makusudi katika mwili wa Mtu kila kimojawapo katika hivo lazima kimrudishie Mungu utukufu kwa nafasi yake kwasababu  haiwezekani Mungu akwambie mwili wako ni hekalu la roho mtakatifu alafu wakati huo useme kwamba Mungu hana haja na mwili wako, kwanini hilo hekalu halikukaa sehemu nyingine mpaka akaamua likae katika mwili.


Kama nilivyosema kuwa, Mungu akitaka kuuzungumzia mwili ananena na akitaka kusema juu ya moyo au nafsi ananena pia,

Kwenye Ezekieli maandiko yanasema,

 “Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.” Ezekieli 36:26

Hapa Mungu anazungumzia moyo anasema nitawapa moyo mpya hazungumzii mwili hata kidogo lakini pia katika kitabu cha warumi 12:1 anazungumzia mwili pekee na sio moyo, anasema "itoeni miili yenu".


Kwahiyo husiruhusu mtu yeyote akudanganye kwamba Mungu anaangalia moyo peke yake bali mwili, roho na nafsi yako vyote hivi ni mali ya Bwana na vinatakiwa kutumika kwa ajili ya Mungu aliye hai.

Lazima ukajionyeshe umekubaliwa na Mungu katika utakatifu wote, katika mwili, nafsi na roho yako na kimojawapo katika hayo ukikivalisha machukizo kwa kujidanganya kwamba Mungu anaangalia kimoja na kukiacha kingine ujue unapotea na zaidi sana kama ni mwili unaupuuza na kuutoa mikononi mwa Mungu maana yake unaliharibu hekalu la Mungu ambalo linatakiwa liwe takatifu na Mungu amesema atakuharibu na wewe.


Biblia inasema Mungu aliwazuia wasitumie mapambo ya namna hiyo katika miili yao pindi watakapotaka kukutana naye sawa na

Kutoka 33:1-4

 _ Bwana akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;

 nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;

 waifikilie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia.

Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri.

Ili ujue kwamba mapambo ni machukizo kwa Mungu jiulize kupitia misitari hii kwasababu hapa tunakutana na kile ambacho tumekiona katika kitabu cha mwanzo wakati ambapo Yakobo anawambia watu wa nyumbani mwake watoe miungu yao alafu wao wanatoa miungi pamoja na pete za masikioni mwao, alafu hapa tena ujumbe ambao Mungu anampa Musa kwa ajili ya wana wa israeli unapopelekwa kwao wao wenyewe hata kabla Mungu hajasema maandiko yanasema ule msitari wa 4 kwamba, "Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hapana mtu aliyevaa vyombo vyake vya uzuri."

Inamaanisha walijua kwamba jambo hili ni baya machoni pa Bwana na ukiendelea mpaka msitari wa 6 unaona tena Mungu anakuja anawambia jambo lilelile la kuvua hivyo vitu ndipo atakajua la kuwatenda.

Na lazima walijua vitu hivi ni machukizo kwa Mungu kwasababu kama wangelikuwa hawajui kweli basi wasingelishtuka na kuvivua mpaka ambapo Mungu angelikuja kusema. 


Najua watumishi wa Mungu, watu wengine na wanathiolojia ambao wanaweza kutafsiri kwa tafsiri zao ili kutetea imani au matakwa yao binafsi na hivyo kupindisha ukweli lakini nakuhakikishia hilo andiko linazungumzia mapambo na vitu vya urembo kuwa ni haramu kukaa katika mwili ambao ni hekalu la roho mtakatifu. 

Nami nakusihi uwe msomaji wa neno la Mungu na muombe roho mtakatifu akusaidie kupata kilichobebwa ndani ya Neno ili mtu yeyote akisimama na kupindisha maana halisi ya neno husika iwe rahisi kwako kuelewa. 


Mimi nakwambia jambo hilo ni baya machoni pa Bwana kwasababu Mungu aliwaambia kwanza waondoe hayo machukizo yaliyo kati yao, 

Kwenye sehemu hii kuna watu wanaweza kusema  lakini hilo lilikuwa ni agano la kale, lakini na mimi narudi kwako kwa namna ya agano jipya kwamba ikiwa unaamini kwamba wewe ni mmoja kati ya warithi wa wa baraka za Ibrahimu aliyepita toka agano la kale mpaka agano jipya maana hao hao wana wa israel ambao Mungu aliwaambia waondoe hivyo vyombo vya uzuri ni uzao wa huyo Ibrahimu ambaye wewe ni mrithi wa baraka zake, “Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.” Mwanzo 15:13, basi ujue kila andiko lililoandikwa kuanzia agano la kale mpaka agano jipya linakuhusu na litasimama kinyume na wewe siku ya mwisho ikiwa utalipuuza na kulipinga au hujasoma mahali panaposema,

 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. Mathayo 5:17-18

Yesu alijua lazima kuna watu watafikiri kuwa kwa kuwako agano jipya basi lile la kale limefika ukomo au halina kazi lakini anasema hakuja kutangua bali kutimiliza kazi ya torati na manabii.


Kwahiyo kama bado unategemea baraka za ibrahimu ambazo zimetamkwa kuanzia agano lilelile la kale basi ujue torati inakuhusu pia. Na kama kweli unatii mbingu hakuna namna utakwepa kutii neno lote la Mungu.


Hapa ndio mwisho wa sehemu ya pili ya somo hili,


Nikukaribishe tena katika mwendelezo wa somo hili, najua bado una maswali katika kipengele hiki kwasababu tumeona Mungu alikuwa akiwaka hasira na kuwatangazia maangamizi watu wanaoyafanya mambo hayo ya machukizo, sasa inaweza kuwa unatamani kuniuliza kwamba  ikiwa niyasemayo ni kweli kwanini leo hatuangamizwi wakati tunayatenda na tunaingia kanisani na wengine wanahudumu mpaka madhabahuni wakati wamevaa hivyo vitu.

Nikwambie tu katika sehemu inayofuata ya somo hili nitakueleza na kukujibu swali hilo kwa kina na nitakuonyesha ni kwa namna gani hakijabadilika kitu na bado watu wanatembea chini ya hasira ya Mungu na kwanini maangamizi hayo hayatokei moja kwa moja.


Mungu akubariki


========== DAY 3 ==========

 Bwana Yesu asifiwe

Karibu tena katika mwendelezo wa somo la JINSI AMBAVYO MAPAMBO YA MWILI YANAVYOWEZA KUMFANYA MTU AKAIKOSA MBINGU.

Leo ikiwa ni sehemu ya tatu ya mwendelezo wa somo hili, nianze kwa kuwapongeza wale wote ambao wamekuwa wakitutumia shuhuda zao  kwa habari ya matendo makuu ya Bwana aliyowatendea na wengine wakishuhudia namna walivyokutana na Mungu katika mazingira tofauti tofauti baada ya kufatilia masomo mbalimbali ambayo watumishi wa Mungu wamekuwa wakiyaachilia katika madhabahu hii ya KANAANI MPYA MINISTRY kwa msaada wa roho mtakatifu. 

Na mimi kwa niaba ya Watumishi wote wa madhabahu hii ninawashukuruni kwa mrejesho wenu na ninamrudishia utukufu Yesu kwa matendo yote makuu hayo ambayo ameyatenda kwetu na kwenu pia. 

Mungu aliye hai awabariki sana, awatunze, awalinde na kuwahifadhi zaidi sana mkazidi kukua, kusitawi na kuongezeka kiroho na kimwili kwa ajili ya utukufu wa jina la Bwana na mkafanyike shuhuda kokote mlipo na kupitia kwako watu wa mataifa wakamfate Yesu wako unayemtumikia. 


Somo letu leo tutaendelea pale tulipoishia jana na katika yote niliyokuhaidi nitajitahidi kuyagusia kwa msaada wa roho mtakatifu lakini pia kwa wewe ambaye hukubahatika kupata sehemu ya kwanza na ya pili ya somo hili ni muhimu sana ukalifatilia kuanzia mwanzo ili uweze kuelewa kwa kina kwa huko tunakokuelekea kwasababu tulichokisema jana hatukirudii leo kwahiyo kama jana hukuweza kusikia uwe na uhakika leo utasikia kipya na sio cha jana kwa maana hiyo ili uweze kuelewa sawasawa ni vizuri ukafatilia kuanzia mwanzo.

Katika sehemu iliyopita mwishoni nilisema, katika hoja Na ufafanuzi wote nilioutoa tangu mwanzo wa somo mpaka hapa bado yamkini kuna mtu anapata shida kuelewa kwamba ikiwa hivyo ndivyo  je ni kwanini hatuangamizwi kama hao walivyokuwa wakitangaziwa ya kwamba ghadhabu ya Mungu itawaka juu yao na wengine pengine wanahoji kwamba mbona tukiombeana tunapokea au tunapata tuyaombayo.

Lakini nataka nikwambie kwamba mambo yote hayo huyaoni yakitokea mwilini kwasababu tunatembea katika kipindi cha neema, biblia inasema, 

 “Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.” Warumi 6:14

Kwahiyo husiogope wala husiwe na wasiwasi kwasababu hautapigwa na radi, moto hautashuka na kukuteketeza wala hautapigwa mawe hadi kufa lakini ukumbuke kwamba Neema hii haifanyi kazi kwa waliokufa bali kwa walio hai, maana yake unapokufa hukumu inarejea palepale kufanya kazi yake baada ya mauti kupita juu yako hautapata nafasi ya kutubu wala kufanya chochote kile kinachoweza kukusaidia kufanya tena matengenezo kati yako na Mungu maana Neema inakuwa haipo tena au hujasoma mahali panasema, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;” Waebrania 9:27

Lakini mahala pengine panasema hivi,

 “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.”2 Wakorintho 5:10

Maana yake hapo hakuna Neema bali ni hukumu.

Tunaweza tukadunda leo tukaalikwa twende hata kwenye semina kujifunza maarifa mapya tukagoma, ibadani tukaenda kwa kujisikia, kutubu mpaka pastor/mchungaji alazimishe maombi ya toba kwa kanisa zima lakini nakuhakikidhia saa inakuja ambako hutamsikia yeyote akikuhamasisha kuomba au kujifunza neno la Mungu bali utatafuta hiyo nafasi hata hivyo hautaipata wala hutamsikia yeyote anakwambia tubu makosa yako kwasababu huo mlango wa hiyo nafasi utakuwa umefungwa tayari.


Ujumbe huu ni kwa ajili ya wanaoitaka mbingu kweli na sio kwa wanaoipenda dunia, kwasababu kila mtu anatamani kujipamba na kupendeza mbele za watu,

Lakini itakusaidia nini  kuwafurahisha watu na ukamchukiza Mungu? 

maandiko yanasema, “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.” 1 Petro 2:11 

 Zaidi pia itakusaidia nini kupendeza kwa namna ya mwilini kwa kujipamba na kujiremba kwa vitu vya thamani alafu baada ya hapo ukaenda jehanamu???


Mwili wako ni hekalu la roho mtakatifu na linajitosheleza katika ukamilifu wake kwa asili ya uumbaji hivyo kuliongezea vitu vingine kinyume na Mungu ni sawa na kukosoa uumbaji wa Mungu na tunamfanya kama vile aliumba au kutengeneza kitu dhaifu au kilemavu ambacho hakijakamilika.

Kwahiyo mwili wako ni mali ya Mungu huwezi kuutumia vyovyote kinyume na mwenye nao, nafsi yako iweke kwa Bwana na mwili wako hakikisha umeutoa kama dhabihu kwa Bwana vinginevyo unaweza kuuacha mwili nyuma na kujitia moyo kwa kufikiri upo salama lakini kumbe haupo salama hata kidogo kila kilicho upande wako iwe ni mwili, nafsi au roho vyote hivyo vinatakiwa kutumika kwa ajili ya Mungu aliye hai.


  • Zama hizi ni za uovu, na tunatembea  katika nyakati ambazo watu wamemsahau, wamemzoea na kumuacha Mungu.
  • Tunatembea nyakati ambazo hakuna tofauti kati ya kanisa na dunia, kwasababu kinachofanywa huko kwa watu wa dunia ndicho hicho kinachofanywa kanisani.
  • Tumefika wakati ambapo hakuna tofauti kati ya Debora na delila na huko ndiko kumepelekea Mungu ameacha kujifunua kwa nguvu kubwa sawa na ukuu na utukufu wake kwasababu machukizo yameingia mpaka makanisani kwa wana wa Mungu mahali ambako madhabahu ya Bwana imewekwa kwa ajili ya watu kukutana na Mungu.
  • Kikawaida lazima umtambue delila kwa kumuona na lazima ukamtambue Debora kwa kumuona, lakini kanisa la leo huwezi kutofautisha kati ya kahaba na mtoto wa Mungu maana, 

wote wana mvao mmoja,

Wote wana mwonekano sawa.

Sasa kwa namna hii hatuwezi kuiona mbingu. Maana huu ni wakati ambao mtu anaweza kusimama akaipinga kweli ya Mungu na watu wakamshangilia na hakuna mtu anamkemea wala kujitokeza kuisema iliyo kweli,na wanafanya hivyo wakati mwingine kutetea matendo yao maovu ili yaonekane kama ni mema na yenye haki lakini nakwambia kweli ya Mungu itabaki kuwa kama kweli ya Mungu. 

Na hii inatokea kwasababu tunaitaka mbingu lakini hatupo tayari kutembea na Yesu, maana yake kuna vitu hatupo tayati kuviachilia alafu tunajiita kwamba tumezaliwa mara ya pili, ukizaliwa mara ya pili maandiko yanasema yakupasa ukauzike utu wa kale na uanze kutembea sawa na kristo, 



Pana gharama kumtumikia Yesu maana vitu vingine haijalishi vinang'aa na kumeremeta kiasi gani lakini inakubidi uviache kwa usalama wako na ili uzidi kutunza ushirika wako na Yesu maana kuna vitu utavipoteza baada ya wito na kuna vitu utavimiliki baada ya wito kwasababu kisicho cha Mungu kitakufa na kilicho cha Mungu kitazaliwa.

Biblia inasema

 Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;

mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. Wakolosai 3:8-10 


 Mahali pengine maandiko yanasema, 

 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.” 1 Timotheo 4:12

Sasa huwezi kujiita umeokoka wakati huo matendo yako hayana tofauti na mtu wa mataifa, biblia inasema tunatakiwa kuwa kielelezo katika usemi, na mwenendo na katika upendo na imani na usafi lakini pia tukiuvaa utu mpya yatupasa tuwe na ufahamu kwa mfano wake yeye aliyeuumba,

Sasa unawezaje kuwaza maovu alafu ukasema wewe umeuvaa utu mpya au umezaliwa mara ya pili,? 

Unawezaje kuvipa kipamumbele vitu vya dunia na ukaacha maagizo ya Mungu alafu ukasema wewe ni wa Mungu,? 

Unawezaje kupingana na kweli ya Mungu na ukaufanya uovu wako uonekane kama ndio ukweli alafu ukajiita wewe ni mwanafunzi wa Yesu?


Unisikilize, niko hapa kukwambia hayo niliyokwambia wenda ukasikia na kuyaishi au ukayapuuza lakini maombi yangu kwa Bwana ni kwamba usikie na kupona maana walio wa roho lazima tuishi kiroho lakini inafika wakati unashindwa kutofautisha afya ya kiroho ya mtu wa dunia na afya ya kiroho ya mwana wa Mungu kanisani, wote wako sawa kwasababu wanawaza mamoja na wanatenda mamoja.

Lakini biblia inaniambia,

 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” 2 Wakorintho 5:17

Hii ndio kwa sababu unatakiwa kuwa mwangalifu husije ukadanganyika na kuangukia mikononi mwa shetani na dunia hii na mikononi mwa wapotoshao wanaokutazamisha uovu kama wema na mwisho wako ukawa mbaya na mbingu husiione ndio maana mara zote katika masomo mbalimbali ninasisitiza watu kulijaza kwa wingi neno la Mungu ndani yao maana bila hivo itakuwa ngumu sana kumjua yupi mkweli na yupi anayepotosha kwasababu wote wanatumia biblia hiyohiyo kama maandiko yasemavyo,“Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi.” Marko 13:6


Ukiamua kumtumikia Mungu basi jitoe kimamilifu na maisha yako yawe ya kiroho haswa sawasawa na neno la Mungu

 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”       Yohana 4:24

Kwahiyo tukisha kuwa wana wa Mungu basi tuishi kama wana wa Mungu na sio watu wa Mungu, kwasababu kuna tofauti kati ya mtu wa Mungu na mwana wa Mungu. {unasema kwa namna gani}

Kila mtu ni mtu wa Mungu kwasababu kila mtu ameumbwa na Mungu, lakini mwana wa Mungu ni yule anayeyaishi na kuyatenda mapenzi ya Mungu.

Maandiko yananiambia,

 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.  2 Wakorintho 6:14-16

Hii ina maana husiwe na kitu chochote chenye ushirika nao, kam utakaa kama wao, au ukaonekana kama wao, au ukaongea kama wao, au ukatembea kama wao kwa maana ya mwenendo wako, hiyo inamaanisha una ushirika nao, kwahiyo kwa mujibu wa hayo maandiko lazima kila kitu kiwe tofauti na wao, lazima mtazamo wako uwe tofauti na mtazamo wa dunia,

Ukijichunguza alafu ukaona hamna kitu kilicho tofauti na wao maana yake bado upo katika dunia na sio katika kristo.


Kwa habari ya mapambo ya mwili ambayo ndio mada kuu haswa ya somo hili tuliona huko nyuma sehemu ya kwanza ni mapambo ya aina gani ambayo Mungu anapendezwa nayo lakini tukabaini ni mapambo ya namna gani yanayotafsiri utu wa ndani na uchaji wa Mungu lakini pia tukaona ni namna gani mapambo ya  mwili ya dunia yanavyokuwa machukizo mbele za Mungu, vitu kama HERENI, MIKUFU, BANGILI, NYWERE ZA BANDIA, MICHUBUO na vitu vyote vinavyogusa asili ya uumbaji wa  Mungu katika mwili wako ni machukizo mbele za Mungu.

Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.

 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Ufunuo wa Yohana 17:4-5

Iwe unakubali au unakataa lakini Neno la Mungu litasimama wakati wote,

Husipotii neno la Mungu amri ya mwisho utakayoitii ni Mauti. Kwasababu mauti haiji kukuonya wala kukuhubiri bali inakuja kukupeleka kwenye hukumu yako iwe unataka au hautaki,

KUMBUKA;

            Mungu alimwambia Musa kuwa wasipoondoa machukizo yaliyokuwepo kati ya wana wa israeli Mungu hasingeenda pamoja nao, KWAHIYO kuna vitu vikiwa kanisani uwepo wa Mungu hautakuwepo.


Hapa ndio mwisho wa sehemu hii ya tatu, 

Karibu tena katika mwendelezo wa somo hili. 

Yale mambo amabayo hatukuyagusia katika sehemu hii kama niliyokuhaidi katika sehemu iliyopita tutaanza nayo katika sehemu ya nne ya somo hili. 


========== DAY 4 ==========

     Bwana Yesu Asifiwe tena!!! 

Nakusalimu katika jina lililo kuu kupita majina yote jina la Yesu. 

Nikukaribishe tena katika sehemu ya nne na ya mwisho ya somo letu la JINSI AMBAVYO MAPAMBO YA MWILI YANAVYOWEZA KUMFANYA MTU AKAIKOSA MBINGU. 

Nikushukuru na nikupongeze wewe ambaye umefatilia somo hili tangu limeanza hata hivi leo tunapofika tamati,namtukuza Yesu kwa ajili yako wewe ambaye ulisikia au kusoma somo hili na mwisho ukahamua kuliingiza katika vitendo, ni imani yangu kwamba kuna kiwango kipya cha kiroho ambacho kimeongezeka kwasababu sio kila anayesikia neno la Mungu analiishi, wengine wanayapuuza na kuyabeza, wengine wanayasikia lakini kutokana na kutokuyapa kipaumbele baada ya muda yanatoweka kwao na wengine hawana muda kabisa wa kuyasikiliza lakini kwa wewe ambaye umeamua kuliingiza neno hili katika vitendo nakuhakikishia hautabaki kama ulivyo na umechagua fungu lililo jema kwa maana biblia inasema,

 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.”1 Wakorintho 1:18

Kwa maana hiyo kwako wewe uliyechagua kuliishi somo hili kuna kiwango kipya cha nguvu za Mungu kinaachiliwa ndani yako na ni maombi yangu kwa Bwana kwamba neema hii ya kusikia neno na kuliishi hisiondoke kwako bali kila kuitwapo leo ikafanyike baraka kwako na kwa wanaokuzunguka ili ukafanyike ushuhuda mwema kwa wakuzungukao na kupitia mfumo wa maisha yako binafsi na wengine wapate kuvutwa na kuja kwa Yesu, “Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.” 1 Petro 2:12


Tuendelee na somo letu,

Katika sehemu ya kwanza mpaka sehemu ya mwisho ya somo hili tumejifunza vitu vingi sana lakini mada lengo kuu likiwa ni kuhusiana na mapambo ya mwili ni kwa namna gani yanakuwa machukizo mbele za Bwana, na huko ndani tuliona mwanzo wa vitu vyote hivyo na makusudi ya Mungu kuumba hivyo vitu ambavyo wanavitumia na kuvibadilisha kuwa mapambo lakini zaidi sana tukaona aina ya mapambo yanayompa Mungu utukufu namna yalivyo tofauti na mapambo haya ya mwilini lakini pia tukaona na kipengere cha mavazi pamoja na utofauti wa matendo au mwenendo wa maisha halisi ya watakatifu wa Mungu na watu wa mataifa, pia tuliangazia ni kwa namna gani mwonekano wako unaweza kutafsiri kilichoko ndani pia tukajifunza kwamba mwili wetu ni hekalu la roho mtakatifu na namna ambavyo Mungu anamuhukumu mtu anayeliharibu hekalu lake na kwingineko tukaona ni kwa namna gani asili ya Mungu ikibadilisgwa inakuwa ni dhambi maana ni sawa na kumkosoa Mungu kwasababu mtu ameumbwa na Mungu tena yeye mwenyewe mungu akasema,

 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu..................” Mwanzo 1:26

Kwahiyo mtu ni asili ya Mungu, ndio maana hakikisha kila kiungo chako kinafanya kazi kwa ajili ya Mungu, kikiwako kimoja ambacho hakifanyi kazi upande wa Mungu ujue panatakiwa matengenezo sehemu kwasababu maandiko yanasema,

 “Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.

” Waefeso 5:30

Sasa ikiwa tu viungo vya mwili wake alafu mwili wako wewe umeuwekea vitu ambavyo ni machukizo maana yake unakinajisi kiungo cha mwili wa Yesu na kwa maana hiyo sasa mwili wako ni mali ya Mungu wewe umeazimwa kwasababu mwili kamili ni Yesu na ndio maana halisi ya mwili huo kuwa hekalu la roho mtakatifu maana yake unatakiwa husijishugulishe na mambo yoyote yanayokinzana na Roho mtakatifu maana yeye ndo yuko hapo katika hilo hekalu.


Kuna watu wanafikiri mwili wao hauna sehemu katika utimilifu wa utumishi wao kwa Mungu lakini huko nyuma katika sehemu zilizopita tuligusia namna ambavyo Mungu anauhitaji huo mwili na anatutaka tukautoke kwake, “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Warumi 12:1

Sasa inawezekanaje kitu kisicho na thamani kikatakiwa kuwa dhabihu ya kumpendeza Mungu.

Unaweza ukasema lakini mwili ni mavumbi na mavumbini utarudi, {ni sawa kabisa}

Lakini je unapoubeba huo msitari umewahi kujiuliza hayo mavumbi yanayotajwa ni ya namna gani na kama ni mavumbi je ni mali ya nani si Mungu ndo aliyaumba na kama aliyaumba kwa mujibu wa kitabu cha mwanzo aliyaumba kwa kusudi la kumuumba mwanadamu alafu baada ya kazi yote ya uumbaji na mwanadamu huyo akiwemo, kisha Mungu akasema, “Na siku ya saba Mungu ALIMALIZA KAZI YAKE YOTE aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.” Mwanzo 2:2

Huwezi kusema "alimaliza kazi yake yote" ikiwa kuna vitu havijakamilika huko nyuma,

Sasa nikuulize wewe unayebadili asili ya uumbaji wa Mungu kwenye mwili wako kwa kutoboa masikio na kuvaa hereni, unayejichubua, unayesuka kwa nywere bandia, unayebadili nywere zako kwa kemikali na zionekane kama za watu wengine ambao sio asili yako, wewe unayeweka kucha bandia, rangi, kope bandia na kuvaa vitu vilivyo machukizo mbele za Mungu, je kwa kufanya yote hayo katika mwili ambao Mungu alishamaliza kuumba na akaupangia kazi maalum na akamtuma roho aje kukaa hapo na ukatukuzwa na kuwa hekalu je mpaka hapo bado huoni kama ni dhambi?????

Biblia inasema,

 “Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;”Warumi 1:26

Pengine hujaelewa sana hapo wacha nikupeleke sehemu nyingine, mahali pengine maandiko yananiambia, “Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama wanyama wasio na akili.” Yuda 1:10

Anasema "na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo".

Unajua shetani anatumia mbinu na njia nyingi kuhakikisha wana wa Mungu wanaenda jehanamu na kwa maana hiyo anatumia vitu vidogo sana na mazingira yanayotuzunguka ili kutukosesha kwa Mungu na maandiko yanasema wakati wote husimama kutushitaki, “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.”Ufunuo wa Yohana 12:10 

ni mpango wa shetani husiingie mbinguni na biblia inasema anatushitaki usiku na mchana, sasa ujue tu kwamba mtu hawezi kukushitaki kama hakutuhumu kwa jambo lolote maana yake shetani anapoenda mbele za Mungu usiku na mchana anaenda akiwa na hoja za kukushitaki na hoja hizo anazitengeneza yeye kwa kupitia mazingira yanayokuzunguka na atakuaminisha uongo wakati mwingine ambao sio kweli, ukishakengeuka tu hoja yake ya mashitaka kwako mbele za Mungu inapata nguvu na atakushinda tu kama hujafunguka ufahamu wako na ukatubu,

Kwahiyo husije ukafikiri shetani anaenda kukushitaki uongo mbele za Mungu la anaenda kukushitaki kitu ambacho umekitenda kweli. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha anateka ufahamu wako akijua tu ufahamu wako ukikamatwa ni rahisi kuhama kutoka kwenye njia ya Mungu, saa nyingine unaweza ukawa unajua na wakati mwingine husijue, katika yale madogo unayoyabeza na kuyapuuza hayohayo ndiyo anayoenda kukushitaki kwayo na Mungu hawezi kubishana naye kwasababu Mungu ni mkweli na mara zote hulitazama neno lake kwahiyo ukitembea nje na neno lake ujue hayo mashtaka yatapata nguvu tu kwasababu yeye hajipingi maana imeandikwa,

“Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” Mathayo 24:35


Nikusihi mwana wa Mungu kubali kuongozwa na roho wa Mungu katika mambo yote ili kwamba uweze kuzishinda hila za shetani na roho mtakatifu atakufunulia mbinu na mikakati ambayo adui anatumia kwa ajili ya kuwapeleka jehanamu watakatifu wa Mungu kupitia vitu vidogovidogo na kukamata ufahamu wao ili wasije wakang'amua na kupona.


Mpendwa wangu katika Kristo, 

Fikiri tu umejitunza kwa uaminifu na umefanya kazi ya Mungu kwa moyo wako wote na changamoto nyingi za utumishi ulizozipitia ukipigania kupata taji yako alafu ghafla tu unaikosa mbingu kwa ajili ya HERENI, CHENI, MIKUFU, BANGILI,MICHUBUO, KOPE ZA BANDIA, RANGI, NYWERE ZA BANDIA na mambo yote yanayogusa na kubadili ASILI YA MUNGU kwenye mwili wako.


Biblia inasema,

“Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.”Warumi 10:17

Yamkini baada ya kusikia maneno haya yote tangu sehemu ya kwanza mpaka hapa, ndani yako imani imejengeka na ufahamu wako umefunguka na ukijaribu kujichunguza unabaini ulikuwa mfuasi wa mapambo yote hayo au mojawapo na pengine uligusa asili ya Mungu kwa kutoboa sehemu mbalimbali za mwili wako au ulichora michoro katika mwili wako au ukabadili nywere au kucha zako au kiungo chochote katika mwili wako kiasi ambacho alama hizo au matobo hayo hayawezi kuondoka lakini ndani yako umekata shauri la kuachana na mambo yote hayo na sasa unasema nipo tayari kutoa mwili wangu kama dhabihu kwa Bwana lakini ukicheki kwenye masikio au kwenye ulimi au kwenye kitovu unaona matobo ulikokuwa ukiweka vito ama ukijiangalia kwenye kioo unaona ngozi uliyo nayo sio ya asili na ile ya asili ilishaondoka na huwezi tena kuirejesha au nywere zako zimebadilika kabisa kwa kemikali na mengine yote, alafu ghafla unasikia sauti ndani yako inakusemesha kwamba "wewe umeshaharibika, pamoja na kuamua kubadilika lakini huwezi kupokelewa maana una tatoo na haziondoki, una matobo masikioni na hayazibiki, umebadilisha nywere kwa dawa na hazirudi"

Hiyo ni sauti ya shetani na hasingetaka ubadilike, lakini pamoja na yote hayo aliyokutazamisha na mimi nakuja kwako kwa neno la Bwana kwa kukueleza kuwa,

Mungu wetu ni wa huruma na rehema,

Yeye anasamehe na kusahau

Nenda mbele za Bwana kwa toba huku ukifuta kwa damu ya Yesu kila kinachompa uhalali shetani wa kushikilia mwili wako na futa  damu ya Yesu chapa za shetani mwilini mwako na kuachilia nafasi kwa ajili ya chapa za Yesu sawa na

 “Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.” Wagalatia 6:17

Ili kila akutazamaye badala ya kuona mavazi ya kikahaba mwilini mwako akaone mavazi ya utukufu,

Badala ya kuona mwenendo wa zamani ambao haukuwa na tofauti na mwenendo wa watu wamataifa, sasa akikutazama akaone sura ya Yesu kupitia mwenendo wako na mwonekano wako na matendo yako yatafsiri kilichopo ndani ambacho Mungu amekubebesha,kubali kutubu ili kwamba zije nyakati mpya katika maisha yako zilizobeba furaha yako iliyofungamanishwa katika kristo Yesu

 “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;" Matendo ya Mitume 3:19

Mpendwa wangu kubali tu kuuzika utu wa kale na upate utu  mpya ambao huo utakupa nafasi ya kukutana na Mungu pasipo kizuizi,  mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

Waefeso 4:22-24

Omba maombi ya namna hiyo kadri roho mtakatifu atakavyokuongoza kutegemeana na eneo lililovurugika na aina ya mbegu iliyopandwa na Mungu wetu ni mwaminifu sana pindi tu utakapotubu yeye hataona tena hayo machukizo mwilini mwako kwasababu yeye ni wa rehema mno na anatupenda sana na ni furaha kubwa Mbinguni pale mwenye dhambi anapotubu na kurejea,

Biblia inasema

 “Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.” Waebrania 8:12 


 Waebrania 10:16-17

Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo,

Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.


Mungu wangu akubariki sana na ujumbe huu ukafanyike baraka katika maisha yako na katika utumishi wako.

Hapa ndio mwisho wa somo hili tukutane tena katika kipindi kijacho.


 Mungu wangu mwema akubariki sana

Post a Comment

0 Comments