100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

ILE KWAMBA UMEACHWA NA KUSAHAULIKA HAINA MAANA KWAMBA WEWE SIO WA THAMANI-Mwl:Afro Frayerne

 ILE KWAMBA UMEACHWA NA KUSAHAULIKA HAINA MAANA KWAMBA WEWE SIO WA THAMANI-Mwl:Afro Frayerne

KANAANI MPYA MINISTRY

Tufuatilie;

Facebook Page

WhatsApp Group

Telegram Group

YouTube Channel


Esta 4:11

“Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.


Bwana Yesu asifiwe sana!!! 

Utukufu kwa Yesu!!! 

Nakusalimu katika jina kuu na takatifu la Yesu na nikukaribishe tena mezani pa Bwana ili kwa pamoja tuweze kujifunza na kupata chakula cha kiroho ambacho Mungu ametuandalia leo. 

Ujumbe ambao roho mtakatifu ameuandaa leo kwa ajili yetu unatokea katika kitabu cha esta na maandiko mengine tutakayokutana nayo huko mbele kadri tutakavyoendelea kujifunza kupitia roho mtakatifu. 

Kama kilivyo kichwa cha somo letu kwamba, ILE KWAMBA UMEACHWA NA KUSAHAULIKA HAINA MAANA KWAMBA WEWE SIO WA THAMANI. 

Ni rahisi sana kujishusha thamani na kujiona wa kawaida sana na wakati huo ukiumia na pengine kujuta pia pale unapopitia katika wakati kama huu wa kuachwa na kusahauliwa, lakini Neno la Bwana linakuja kwako leo kukutia moyo na kukwambia ya kwamba haijalishi watu au wanadamu wanakuonaje kwa namna ya nje ama  wanakuchukuliaje lakini  leo Yesu amenituma nikueleze ya kwamba uthamani wako hauko mwilini wanakotazama wao bali uthamani wako huko rohoni wasikoona wao. 

Amenituma nikwambie nguvu ya ushindi wako husiuwekeze kwao bali uwekeze kwa Mungu. 


Hallelujah!!! hallelujah!!! 

Sio jambo la kawaida mwanamke kutokukumbukwa na mmewe kwa muda wa siku thelathini lakini hali hii anaipitia malkia esta na hata pale ambapo ndugu zake wanahitaji msaada wake ambao ni lazima aupate kwa nfalme, mfalme yule ambaye amemtenga kwa muda wa mwezi mzima lakani taarifa ya kumtaka asimame kwa ajili ya ndugu zao inapoletwa kwake angalia kitu anazungumza, ............wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini. 

Maana yake anaona jambo hili la kusahaulika kama vile ni kikwazo kwake kwenda mbele za mfalme. 

Maana yake hana ujasiri ndani yake wa kumkaribia mmewe akiisi hana thamani na hawezi kumshawishi mfalme awaokoe ndugu zake. Esta alijua kabisa kwamba ni ngumu sana kwa mtu hasiyekuthamini akavutwa na ushawishi wako. 


Hivyo ndivyo ambavyo either mimi au wewe tumesahaulika katika maeneo mbalimbali , 

Inawezekana Umesahaulika katika huduma na kutengwa kabisa, 

Inawezekana Umesahaulika katika familia hata vikao vya kimaamuzi hushirikishwi isipokuwa unapewa tu taarifa ya yaliyoazimiwa kifamilia, 

Inawezekana Umesahaulika katika jamii kiasi ambacho hata hakuna mtu anaona uthamani wako, 

Inawezekana Umesahaulika katika ndoa na umuhimu au uthamani kwako kwa mkeo au kwa mmeo haupo kama kwa esta mbele za mmewe mfalme. 

Inawezekana Umesahaulika ofisini kwako, unafanya kazi kwa kujituma na kwa ubunifu mkubwa mpaka muda wako wa ziada unautumia kwa ajili ya kazi lakini inapofika promotion time wanakuwa promoted watu wengine na wewe unaachwa huku unasitahiri. 

Inawezekana umesahaulika hata kwa ndugu zako hata wakati unapita katika wakati mgumu hakuna hata mtu anataka kujua hali yako au kutaka kujua unaendeleaje au unakabiri vipi hali iliyoko mbele yako.

Inawezekana kabisa wako watu uliwahi kuwasaidia lakini hakuna hata mmoja anakukumbuka, wote wamekusahau. 

Lakini leo ni saa ya kukumbukwa kwako  kwasababu haijalishi hao uliowategemea wakusaidie au wakusikilize wamekusahau kiasi gani lakini leo Yesu atakufanya ukumbukwe na uthamani wako utakuwa mara dufu kuliko mwanzo kwasababu anayewainua watu ni Yeye mwenyewe na sio watu na baraka pekee zisizo na majuto wala malipo zinatoka kwake. 

Unajua kuna kuachwa na kuna kusahaulika na ujumbe wa Mungu leo umekuja kuzungumza na WALIOACHWA na WALIOSAHAULIKA. 

Nina uhakika hautabaki hivo ulivokuwa na hautaonekana tena kama wengine walivyokuona.

Wacha kilichomfanya Esta akapata nafasi tena mbele za mfalme na ndugu zake wakawa salama, 

Biblia inasema, 

 Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,

Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.

Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza .

 Esta 4:15-17

Hekima pekee ambayo malkia Esta aligundua inaweza kumsaidia ilikuwa ni kwenda kwa maombi mbele za Bwana haijalishi kanuni ya kifalme inazungumza nini kwa yule anayekiuka utaratibu wa kuingia kwa mfalme lakini ndani yake aliamini Mungu anaweza kumtetea inagawa nina uhakika hakujua atamtetea kwa namna gani ndiyo maana akasema nami nikiangamia na niangamie

Maana yake alijua Mungu anao uwezo wa kubadili mauti iliyotangazwa kwao na kuwa uzima ila hakujua ni kwa namna gani hilo lilatatekelezwa au kutimia


Mwana wa Mungu unapoona unapita mahali pa namna hii njia pekee ni kwenda mbele za Mungu maana huyo ndiye anayejua uthamani wako, haijalishi wengine wote wamekukataa lakini yeye atakupokea wakati wowote na atakusikiliza na kukupa haki yako sawa na neno lake. 

Ukiendelea kusoma habari za esta na ndugu zake pale walipoamua kumlilia Bwana utagundua kwamba Sheria ya Mungu ilisimama juu ya sheria ya kifalme katika ufalme wa mfalme ahasuero, 

 Esta 8:1,2,7 

 Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani...........Mfalme Ahasuero akawaambia malkia Esta na Mordekai, Myahudi, kusema, Tazama, nimekwisha kumpa Esta nyumba yake Hamani, naye mwenyewe wamekwisha kumtundika juu ya mti, kwa sababu aliwatia mikono Wayahudi.


Hallelujah!!! hallelujah!!!


Kupitia msaada wa Mungu Esta anapata kibali tena kwa mfalme,

Modekai anainuliwa na kuketishwa juu katika nafasi ya adui yake, 

Zaidi sana yule aliyesiamama na kutangaza mauti juu ya wayahudi anatundikwa nankufa kifo cha aibu.

Hivyo ndivyo ambavyo Mungu anawapigania wenye haki wake na wale wanaomkimbilia.

Husijitaabishe kutafuta kibali kwa watu bali tafuta kibali kwa Mungu na kwa habari ya utambulisho wako kwa watu Atakayekutambulisha ni Mungu na sio wewe.

Ninayo furaha sana kukwambia ya kwamba Yesu anakupenda sana na yuko tayari kukutetea, kukuinua na kukufanikisha katika yote, jambo pekee unalotakiwa ni kumuelekea kwa moyo wako wote na kwa  unyenyekevu.

Inawezekana unaumia sana moyo kwa kuona watu wanakupuuza na kukukebei na hawakujari lakini watu haohao uliwahi kuwasaidia katika nyakati fulani. Sikia husiumie na husiwaze kuwahusu wao bali dumu kwa uaminifu mbele za Mungu kwasababu kadri unavyowatazama watu wakusaidie ndivyo taratibu unavyoondoa tumaini lako kwa Mungu na kuliweka kwa binadamu. 

Wacha tuone habari za mtu mwingine aliyewahi kupitia mazingira yakausahauliwa;

Biblia inaniambia,

 Mwanzo 40:6-15 

 Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo?Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie.Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu.Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva.Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu.Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.Ila UNIKUMBUKE mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.Kwa sababu hakika naliibiwa kutoka nchi ya Waebrania, wala hapa sikutenda neno lo lote hata wanitie gerezani.

Kwenye ule msitari wa 14 Yusufu namsihi yule mnyweshaji ambaye walikuwa wamefungwa katika gereza moja kwamba pamoja na kumtafisilia ndoto yake lakini analo ombi la ziada kwamba atakaporejea  katika nafasi yake akamkumbuke.

Na maandiko yanasema vile Yusufu alivyowatafisiria wale wafungwa wenzake ambao walikuwa watumishi katika jumba la kifalme hivyo ndivyo ilivyokuwa mmoja alikufa na kuondolewa katika nafasi yake na mwingine alirejeshwa katika nafasi yake, lakini baada ya kurejeshwa katika nafasi yake hakumkumbuka Yusufu kama alivyokubaliana naye kule gerezani.

 Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake. Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake.............Lakini huyo mkuu wa wanyweshaji hakumkumbuka Yusufu, alimsahau.Mwanzo 40:20,21,23 

Lakini pamoja na hayo hatuoni kama Yusufu aliacha kumuomba Mungu maana maandiko yanasema aliyekuwa anamsaidia kutafsiri zile ndoto alikuwa ni Mungu kwahiyo inamaanisha pamoja ma kuwa gerezani lakini Yusufu hakuacha kumtumikia Mungu na wala hakukatisha ushirika wake na Mungu.

Je ni mara ngapi umeshindwa kuomba baada ya kupitia magumu? 

Je ni mara ngapi umezila hata kwenda kanisani kushiriki ibada baada ya kusikia watu wanakusema vibaya au baada ya mchungaji kukutenga katika huduma?

Ni mara ngapi umefanya kazi kwa hasira ofisini baada ya kugundua kazi unafanya wewe lakini wanapongezwa wengine?

Haijalishi nini kiko mbele yako, haijalishi umeomba kwa muda gani na hujajibiwa lakini husimuache Mungu wako, saa ya Bwana Itakapowadia utashinda na utavuka na kila mtu ataona yakwamba umevuka.

Maandiko yanasema baada ya miaka miwili kupita tangu tukio lile lililotokea gerezani la Yusufu kuwatafisiria ndoto watumishi wa farao waliokuwa wamefungwa pamoja, jambo lilelile la ndoto likampata mfalme farao mwenyewe na akakosa mtu wa kumtafisiria miongoni wa waganga qalio katika misri na watu wote walioaminiwa kuwa wana hekima, ndipo Yule mnyweshaji akamkubuka Yusufu gerezani kisha akaenda mbele za farao na kumueleza namna mtu yule alivyowatafisiria ndoto na zikawa vilevile, maandiko yanasema farao akatoa amri mtu huyo ambaye ni yusufu aletwe mbele zake na aje akamtafisirie hiyo ndoto ambayo imewashinda wengine wote, baada ya yusufu kuletwa mbele za Mfalme maandiko yanasema, 

 Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri.Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani

Basi farao akamsimulia yusufu mambo yote aliyoyaona kwenye ndoto, kisha yusufu akampa maana ya njozi aliyoiota, Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.

Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.Na wale ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa. Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu.

 Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri.Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi.Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana.

Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi.Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba.Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji.Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa.Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote.Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri.Mwanzo 41:25-43

Kilichomfanya Yusufu kukumbukwa sio yule mnyweshaji bali ni yeye kutokumuacha Mungu wake kwasababu kama angepoteza ushirika wake ma Mungu hata kama wangemkubuka bado pia asingewasaidia kwasababu aliyekuwa anampa maana ya njozi hizo ni Munhu kwa mujibu wa maelezo yake, hivyo hasingepata cha kujibu kwasababu Munhu hasinhesema naye chochote wakati hawana ukaribu tena, kwahiyo yule mnyweshaji ni daraja tu lakini Ukaribu wake na Mungu ndio uliomfanya akapata kibali mbele za farao kiasi ambacho anapewa nafasi kubwa kuliko hata yule mnyweshaji mwenyewe maana yake baada ya mfalme anayefata kimamlaka ni yusufu mwenyewe.


Mwana wa Mungu nimalize kwa kusema katika kuachwa na kusahaulika kwako husijitenge na Munhu wako maana huyo pekee ndiye anayeweza kukuinua tena,

  • Ndiye anayeweza kukufanikisha tena,
  • Ndiye anayeweza kukupa nafasi tena,
  • Ndiye anayeweza kukupa heshima tena na ukaonekana wa thamani kati ya waliokudharau,
  • Ndiye anayeweza kumfanya mkeo au mmeo akakukumbuka haijalishi amekusahau kwa muda gani,
  • Ndiye anayeweza kukupa kibali na kukuinua tena katika huduma yako, 
  • Ndiye anayeweza kukuketisha pamoja na wakuu baada ya kusahaulika kwa miaka mingi kazini kwako. 


Weka tumaini lako kwa Bwana, hata kama wanakuudhi wewe wapeleke msalabani, hata kama wanakuwinda na wanataka kukuangamiza wewe muite Yesu. 

Jambo moja kumbuka husisahau kwamba, 

Wanaokudharau wanakutazama kwa nje lakini kilichoko ndani yako hawakioni na anayeweza kukifanya kitokeze nje ni Mungu pekee. 

Muite Mungu wako amiliki na kutawala pamoja na wewe mahali ambapo unaisi umeachwa na kusahaulika. 


Mungu akubariki sana, tukutane katika kipindi kijacho.


                   Amen

Post a Comment

0 Comments