100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

JINSI YA KUJIUNGANISHA NA UKOO WA YUDA NA UFALME WA KRISTO-Mwl Azory Michael

JINSI YA KUJIUNGANISHA NA UKOO WA YUDA NA UFALME WA KRISTO-Mwl Azory Michael

UTANGULIZI

1.      Asili ya yuda na ufalme wa kristo.

2.      Jinsi ambavyo mtu anaweza kuishi kwenye falme mbili kwa wakati mmoja (UFALME WA KRISTO NA UFALME WA GIZA/SHETANI

3.      Kusudi la uzao wa yuda na ufalme wa kristo.

4.      Jinsi ya kufahamu ikiwa upo kwenye falme mbili na namna ya kusimama kwenye ufalme mmoja.

5.      Namna ya kujiunganisha na ukoo wa yuda na ufalme wa kristo.

6.      Jinsi ya kuomba ili kujiunganisha na kujiunganisha na ukoo wa yuda na ufalme wa kristo.

 

JNSI YA KUJIUNGANISHA NA UKOO WA YUDA

Mwanzo 49:8-10

Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. 
Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? 
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. 

Mwanzo 1:26

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Wanadamu wote duniani ni matokeo ya kusudi la mungu kufanya mtu kwa mfano wake akatawale vitu vyote vya nchi,hata hivyo wanadamu hawa walishindwa kutunza maagizo ya MUNGU hivyo ikapelekea mfumo wa maisha yao na nchi kulaaniwa ikiwa ni pamoja na hukumu,adhabu na sheria zingine zenye mfumo mpya wa maisha.

Mwanzo 3:1-19

Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.  Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?  Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.  Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala. Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

Hayo ndiyo matokeo ya uasi wa wanadamu kwa MUNGU wao wakaambulia laana,adhabu na mfumo mpya wa kisheria ulioelekeza katika uzao moja kwa moja tena ukifunua au kudhihilisha kile kinachoitwa vita ya kiagano.katika (mwanzo 3:14) MUNGU namlaani nyoka kwa kile kafanya kuliko wanyama wote na hayawani wa mwituni na anamwamulu kula mavumbi siku zote za maisha yake wakati huo ukumbuke mwanadamu ameubwa kutokea katika mavumbi.

Mwanzo 3:15 MUNGU anamwambia nyoka ameweka uadui kati ya uzao wa huyo na mwanamke na uzao wa nyoka,kwamba uzao wa nyoka utauponda uzao wa mwanamke kisigino na uzao wa mwanamke utauponda uzao wa nyoka kichwa.

Nilitaka uone upana na ukubwa wa vita ya kiagano iliyopo hapo kati ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka na namna ambavyo ilitosha kuharibu mataifa yote na dunia kiujumla kwa njia ya vinasaba vya damu ya ADAMU.

 

KUSUDI LA UZAO WA YUDA NA UFALME WA KRISTO

Ni kutimiza mpango au kusudi la MUNGU lililovurugwa katika busitani ya edeni.

Hiki ndicho kile ambacho ni kusudi la MUNGU halisi linalobeba kile kilichokuwa kimekusudiwa tangu mwanzo pamoja na kuwa na upinzani mkubwa katika bustani ya edeni na adamu na hawa wakapoteza nafasi ya kutimiza, LAKINI bado MUNGU aliwapa neema katika uzao wa wawe na uwezo wa kuponda kichwa cha nyoka na kutimiza kusudi la MUNGU .

Agano la kale linaweka wazi mpango wa MUNGU kuhusu uzao wa mwanamke mwanzo 12:1-4   1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. 4 Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.

MUNGU  anaanza mpango wa kutafuta uzao atakaoufanya kuwa taifa teule kwa ajili ya kutimiza kusudi lake,anamtumia Ibrahim kama baba wa mataifa mengi na mwenye uzao mwingikama nyota za mbinguni na kama mchanga wa bahari mwanzo 17:1-7    1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. 3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, 4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, 5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.

BAADAYE = mwanzo 21:12

12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. 
kwahiyo image ya uzao halisi kwenye kusudi na mpango wa  MUNGU wa kufanya uzao utakaoponda kichwa cha nyoka iko ndani ya isaka.

Mwanzo 25:21-23  21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba. 22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana. 23 Bwana akamwambia,Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.

kwa mujibu wa kitabu hiki cha mwanzo 25:21-23 inatutazamisha  YAKOBO kama mbeba kusudi na lengo lililo kwenye uzao wa yuda  na ufalme wa kristo.

Mwanzo 27:27-30  27 Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana. 28 Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo. 29 Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe. 30 Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake. 

Mwanzo 29:31-35 NA mwanzo 30:1-24 maandiko haya yanataja uzao wa yakobo kwa wake zakeLEA NA RAHELI pamoja na wajakazi wake ZILPA NA BILHA kwamba ni wazazi muhimu sana katika somo hili la kujiunganisha na uzao wa Yuda na ufalme wa Kristo kwa mtazamo wa kiroho kwa uzao wao na wa watoto 12 kama malango.

YUDA Ni mtoto wa YAKOBO na ni lango la kuingia katika ufalme wa kristo.

Watoto 12 wote wa yakobo ni malango au njia ya kuingia katika mji mtakatifu au Jerusalem mpya.ni tofauti kubwa iliyopo kati ya yuda na ndugu zake 11,yeye ni lango la ufalme wa kristo hapa duniani kutokana na mwanzo 49:8-10 na pia ana sifa ya pamoja na wenzake kuwa lango la kuingia mji mtakatifu kutokana na ufunuo 21:10-12  8  Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.9  Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.10  Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;

 

Kusudi la ukoo wa yuda na ufalme wa kristo ni;kupata watu wenye sifa na wana fimbo ya enzi pamoja na sheria kwa ajili ya kutawala pamoja naye kwenye ufalme wake sawa na zaburi 50:6 Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.

Mathayo 25:34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

Nilitaka uone ufalme wa kristo unavyotumia mlango wa ukoo wa yuda kisheria kurithisha ufalme.

NB huwezi kurithi ufalme bila sheria ya ufalme huo , kwahiyo yuda na ukoo wake wote wamepewa sheria ya kifalme na ndugu zake watamsifu na kumwinamia kwasababu ya enzi na jinsi mkono wake ulivyo shingoni mwa adui zake.na kama wana sheria ya ufalme basi ukitaka ufalme wa kirsto kuumiliki basi tafuta sheria ya ufalme huo kwa yuda ili ujiunganishe na ukoo wa yuda.

 

WATU WANAISHI KWENYE UFALME WA GIZA NA UFALME WA MUNGU KWA WAKATI MMOJA

Mwanzo 3:3-7  4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. 

Nilitaka kukuonyesha hapo juu namna gani watu wanaweza kuishi katika falme mbili kwa wakati mmojahali ambayo inasababisha kukosa uaminifu kwa upande wa MUNGU.

Waamuzi 16:1-2  1 Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake.

2 Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.

 

1wafalme 11:1-14

1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.

3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.

4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.

5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.

9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,

10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.

11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.

12 Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako.

13 Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua.

14 Ndipo Bwana akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; yeye alikuwa wa wazao wake mfalme wa Edomu.

 

SOMA mathayo 7:15-16

Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

 

Endelea kujifunza madhara ya kuishi katika falme mbili kwa wakati mmoja;

 

2mambo ya nyakati 16:7    Wakati ule Hanani mwonaji akamwendea Asa mfalme wa Yuda, akamwambia, Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea Bwana, Mungu wako, kwa hiyo limeokoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako.

 

Soma tena yohana 18:10-11  Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko.Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?

Hapa tunaona ni jinsi gani ilivyo rahisi mtu kupinga kusudi la MUNGU akidhania anatenda haki hii ni kwasababu tu ya kutumika katika falme mbili kwa wakati mmoja kulimfanya yesu amwambie petro rudi nyuma shetani

Tangu adamu hata hivi leo watu wengi wa dunia hii wamejikuta wanaishi na kutumikia falme mbili kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ufanisi wa kiutendaji.

 

Ufunuo wa yohana 12:9-10 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

Hapa tunaona dunia na watu wake awali ilikaa na kuongozwa na ufalme wa MUNGU pekee lakini baadae kidogo ufalme mwingine wa giza uliiangukia dunia na watu wake na kutawala.

 

Ufunuo wa yohana 12:12-13 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.

 

·        Walikula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya kwahiyo laana,adhabu  na hukumu pamoja na uadui wa kudumu wa uzao wa nyoka na uzao wa mwanamke ukaanza kwa namna ambayo watu wanatafutwa na falme mbili kwa njia ya uzao.

Uzao wa nyoka unaunda kizazi cha nyoka na baba yao ni ibilisi ambao ni ufalme wa giza

 

yohana 8:44   Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

 

·        Uzao wa mwanamke unaudwa na ukoo wa yuda na ufalme wa kristo

mwanzo 49:8-10 Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. 
Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? 
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.

 

UASKOFU,UCHUNGAJI,UTUME,UOMBAJI,UINJIRISTI,UIMBAJI,USHEMASI,UKUHANI NA UNABII havitoshi na sio kigezo cha kukukomboa na mfumo huu wa uvuli wa nguvu za falme mbili,kumbukamatunda ya mti yalikuwa ni ujuzi wa mema na mabaya mwanzo 3:4-7

 

1.      Wewe ni mwana wa MUNGU  kutoka katika ukoo gani??

2.      Husijaribu kumtumikia MUNGU kama hujajua kama umeunganishwa na ukoo wake.

3.      Mungu huanza kwanza kwa kuwatenga watu kwa ajili ya kusudi lake , neno kutenga maana yake WAKIFU , na kuchaguliwa humaanisha haswa kuingizwa kwenye ukoo wake kwa njia ya vinasaba au damu yake.

 

Mathayo 2:1-6

Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,2  Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.3  Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.4  Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?5  Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,6  Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

 

Sikia;yuda ni ukoo au uzao ambao ndani yake una uwezo wa kutoa mtawala au mfalme ambaye ni kristo.

Damu ya yesu ilimwagika ili itumike kubadili vinasaba vya damu ya ukoo wa yuda kisheria,haki na enzi ili kupata sifa ya kurithi ufalme wa kristo.

 

MFANO;

Mkimbizi au muhamiaji akiwa katika ufalme wa nchi nyingine hukosa haki ya kurithishwa chochote cha ufalme huo na ufalme huo hauwi ufalme wake mpaka atakapotafuta uraia wan chi hiyo au ufalme huo.

 

Nasema jiunganishe na ukoo wa yuda ndipo utapata ufalme wa kristo.

Yohana 3:3-7 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.4  Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.6  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.7  Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.

 

2wakorintho 5:17

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

 

·        Utu wa zamani ulizaliwa na damu na nia ya mwili haiwezi kuurithi ufalme wa MUNGU.

·        Ukoo wa yuda ni moja ya uzao wa mzee wa yakobo aliyekuwa na watoto 12 kwa mfumo wa malango ya taifa teule takatifu  alilokusudia kulitenga kati ya mataifa,kabila na lugha kwa upekee alitaka ainue taifa la Israeli liwe taifa teule takatifu lenye tabia na mifumo ya kimungutofauti na mengine.Makabila haya 12 ya Israeli hatahivyo hayakwenda kwa ukamilifu ukilinganisha na kusudi la MUNGU hivyo Mungu akafanya mpango mwingine kwa kinywa cha Yakobo (Israeli) alipowabariki wanae ,yakobo anatamka mpango wa MUNGU kwa yuda mwanaye kufanywa mwenye kusifiwa mkuu kati ya nduguze na mwenye kuinamiwa,sheria haitoki miguuni pake na fimbo ya ufalme isitoke kwake na enzi pia mikono yake kuwa shingoni mwa adui zake kama samba jike katika kuwinda.(mwanzo 49:8-10)

 

JINSI YA KUFAHAMU KAMA UNAISHI KATIKA FALME MBILI KWA WAKATI MMOJA

Yohana 3:3-7

Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.4  Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.6  Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.7  Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.

Unapoona hujazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa roho inatosha kukupa picha kwamba uvuli wa dhambi wa dhambi ya adamu unatenda kazi chini ya ufalme wa giza ikishindana na ufalme wa kristo katika maisha yakokutokana na

yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

 

Yohana 15:1-6

Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.2  Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.3  Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.4  Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.5  Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.6  Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.

 

Wagalatia 5:16-17

Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.

 

Ufunuo 2:12-16

12  Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.

13  Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

14  Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

15  Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.

16  Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.

 

·        Ujumbe wa kristo kwa pergamo = pergamo kilikuwa ni kituo cha imani  mbalimbali za kipagani ikiwa ni pamoja na itikadi ya aselepius,mungu wa kiyunani wa uponyaji aliyekuwa akiitwa “mokozi”na alikuwa akiwakilishwa na joka na watu waliotoka kila mahali ili kuja kwenye tambiko la Asclepius ili waweze kuponywa.

·        Pergamo ilikuwa na kazi kubwa ya kueneza itikadi ya kumwabudu mfalme,desturi iliyokuwa ni amri ya lazima kama huko smirna.ndiyo maana haishangazi kwamba maandiko yalisema wakristo huko pergamo waliishi kwenye miji akaapo shetani na penye kiti chake cha enzi.

 

 

 

BAADA YA KUFAHAMU UPO CHINI YA MAONGOZI YA FAMLE MBILI,SASA TUTAZAME NAMNA YA KUINGIA NDANI YA UKOO WA YUDA NA UFALME WA KRISTO.

 

Kutokana na kitabu cha 1waflme 4:25

Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.

 

Yohana 15:3-5

 

Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.2  Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.3  Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.4  Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.5  Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

 

Pia kitabu cha MIKA 4:4

Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha Bwana wa majeshi kimesema hivi.

·        Tumia damu ya yesu kupaka milango ya nyumba yako miimo miwili na kizingiti cha juu ili iwe ishara itakayozuia kuharibiwa kwako katika nyumba utakayokuwemo usiku huo.nyumba ni neno pana sana kibiblia halina maana moja,kwahiyo hakuna ufalme husio na nyumba  kwa ajili ya watu wake.

Yohana 14:1-3

Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

Kutokana na maandiko haya tunapata picha kwamba kila ufalme una nyumba au makazi ya watu wake,iwe ni Mungu au shetani,kwahiyo unapoomba katika roho ukatamka kupaka damu ya Yesu kwenye miimo ya milango na kizingiti cha ju,ghafla katika roho inaachiliwa  hali ya pigo na uharibifu juu ya eneo husika kwasababu hali hiyo ndani yake imebeba ujumbe wa Mungu wa kutoka kwenye ufalme wa giza na utumwa na kuingia ndani ya ukoo wa Yuda na ufalme wa kristo.

·        Hakikisha unatafuta namna ambayo utahakikisha matumaini yako umeyaweka kwa Mungu

Zekaria 3:10

Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, ninyi mtamwalika kila mtu jirani yake chini ya mzabibu, na chini ya mtini.

Ingawa Israeli ilikuwa imeadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake,ulikuwa ni wakati wa kuishi tena katika uhusiano na Mungu kulingana na ahadi zake.

Mtu wa Mungu zekaria ambaye jina lake linamaanisha {Bwana anakumbukwa} alianza huduma yake ya kinabii miezi michache baada ya baada ya hagai kuanza huduma yake.

Hagai 1:1-4 & zekaria 1:1-4

Alitambua mipango ya Mungu kwa wakati uliopo na ujao kwa njia ya mfululizo wa njozi za kinabii juu ya ufalme wa milele wa Mungu uliokuwa unakuja haraka.lakini nambii alitoa wito kwa wale walioishi katika wakati wakekumtumikia Bwana kwa wakati huu.

 

 

 

ASILI YA UKOO WA YUDA NA UFALME WA KRISTO

1WAKORINTHO 2:14-16

Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.

Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

 

 

YOHANA 1:12

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Asili ya mwanadamu nje na ukoo wa yuda haipokei mambo ya roho wa Mungu maana nia ya kristo hukaa kwa watu wa rohoni ambao ni ukoo wa Yuda na ni lazima yuda kama lango la kisheria ,enzi na heshima sawa na mwanzo 49:8-10 atumike kwa dunia nzima ipate mtawala au mmiliki atakayewaunganisha watu wote kwa asili moja tena yenye nia ya kristo ili waweze kupokea mambo ya roho wa Mungu.{kwa njia ya vinasaba au damu na maji}

 

Luka 1:36-56

Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa;

kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.

Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,

akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti.

Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;

akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?

Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.

Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.

Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;

Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;

Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu.

Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.

Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza.

Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.

Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake;

Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele.

Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.

Nilitaka uone kwamba pamoja na mariam kupata neema kwa Mungu hali akikaa galilaya na nazarethi  na taifa teule bado alitakiwa kwenda mji wa Yuda au kwa lugha nyepesi ukoo wa yuda sawa na somo letu.alienda huko ili katika ukoo huu akutane na mtu ambaye amebeba ushuhuda wa kile ambacho haswa kimemfanya mariam aje huku.ukisoma ile yohana 1:26 maandiko yanasema; Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake.

v  YOHANA ni mtoto wa Elizabethi kutoka katika mji wa Yuda {ukoo wa Yuda}

v  Ukoo wa yuda umebeba utambulisho wa ufalme wa kristo

v  Ukoo wa yuda unatengenez njia ya nia ya ufalme wa kristo

 

 

MAELEZO KIDOGO KUHUSU ASILI

Mfano  wa samsoni

Waamuzi 13:4-5

Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;

kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.

Maandiko haya yanatupa kujua asili ya nguvu zake zilikuwa zinatambulishwa kwa  kwa njia ya nywere zake.roho wa Mungu alikuwa akishuka kwake kutimiza utambulisho wa nguvu zilibebwa ndani ya nywere zake.

Unadhiri wake ni juu ya kuiokoa israelina mikono ya wafilistina ili iwe hivyo ilikuwa ni lazima mama azingatie masharti au maelekezo Fulani nay eye mwenyewe kuzingatia maelezo au masharti Fulani ili hizo nguvu ziendelee kudumu juu yake.

 

Mwanzo 49:8-9

Asili ya ufalme wa kristo umewekwa ndani ya ukoo wa Yuda.ufalme wa kristo ulishuka kwenye ukoo wa yuda ili kutimiza ili kutimiza utambulisho wake ulio ndani ya ya yuda yaani ufalme wa kristo wenye neema,kweli na haki.

Watu huimba tumepata simba katika ukoo wa yuda na huku hawajui wao pia ni ukoo wa yuda kwahiyo walipaswa kuimba ,tumepata samba katika ukoo wetu wa yuda ,kama samsoni alivyopata nguvu katika nywere zake mwenyewe.

 

 

 

NAMNA YA KUOMBA ILI KUJIUNGANISHA KATIKA UKOO WA YUDA NA UFALME WA KRISTO

1.      Omba toba kwa ajili ya sili ya ukoo wako zaburi. 51:5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.

 

2.      Tumia neno la Mungu kujitenga na ukoo wako,maana neno pekee hutumika kutenga vitu vya asili kwa ajili ya asili nyingine,mwanzo 1:6 na kujiungamanisha na ufalme wa kristo

Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.

 

3.      Tumia damu ya Yesu kupata au kuomba haki ya ukoo wa Yuda na ufalme wa kristo,                    yohana 1:12-14   Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

 

 

4.      Omba neema ya kuwa ndani ya ukoo wa Yuda na ufalme wa kristo. Matendo ya mitume 17:28  Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

 

5.      Omba kupata asili ya ukoo wa Yuda na ufalme wa kristo. mwanzo 49:8-10 Yuda, ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watakuinamia. Yuda ni mwana-simba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakaye mwamsha? 
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. 

 

 

Warumi 10:17-18

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.

 

 

Zaburi 60:7

Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,

 

Hesabu 24:17-19

Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.  Na Edomu itakuwa milki Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake; Israeli watakapotenda kwa ushujaa. Mwenye kutawala atakuja toka Yakobo, Atawaangamiza watakaobaki mjini.

 

 

Isaya 9:6-8

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.  Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo. Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli.

 

Nimetumia vitabu vingi kwenye hatua hii ya 5 ili upate kuelewa kwa undani  kidogo kuhusu asili ya ukoo wa yuda na ufalme wa kristo katika mihimili mikubwa miutatu yaani;MAMLAKA,UTAWALA NA UMILIKI.

 

 

6.      Kmshukuru Mungu zaburi 107:1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

 

 

Hapa ndio mwisho wa somo hili nikukaribishe tena katika kipindi kijacho.

 

MUNGU AKUBARIKI SANA.

Post a Comment

1 Comments

  1. NIMEBARIKIWA NA BLOG HII MUNGU AZIDI KUWABARIKI NA KUWAJALIA MAARIFA SAHIHI YA KIMUNGU ILI MUNGU AZIDI KUWATUMIA KWA AJILI YA KULITANGAZA NENO LAKE KWA MATAIFA YOTE. AMEN

    ReplyDelete