SOMO: NGUVU YA DHAMBI sehemu ya pili - Mwl:Afro Frayerne
Bwana Yesu Asifiwe !!!
Ezekieli 18:26-27
Mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu,
akafa katika uovu huo; katika uovu wake alioutenda atakufa.Tena, mtu mwovu
atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na
haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.
Karibu mwana wa Mungu tena madhabahuni pa
Bwana tukapate chakula cha kiroho kwa ajili ya usitawi wa maisha yetu ya kiroho
na kimwili maana imeandikwa hatutaishi kwa mkate sawasawa na kitabu cha mathayo
4:4 naye
akajibu akasema,imeandikwa,mtu hataishi kwa mkate tu,ila kwa kila Neno litokalo
katika kinywa cha Mungu.
inamaanisha kuna njaa nyingine ya kiroho ambayo
haitoweki kwa mkate wa mwilini isipokuwa kwa Neno la Mungu.
Kwa maana hiyo sasa nikukaribishe tukajifunze kwa ufupi kabisa kama lilivyo NENO LA SIKU, lakini kwa ufupi huo naamini kipo kitu kikubwa kinakwenda kuachiliwa kama sio kwako basi kwangu kwakuwa Neno la Mungu ni pumzi ya uhai nami naamini iko mbegu inaenda kupandwa katika roho zetu na nafsi zetu kupitia Neno hili la uzima.
Neno la siku la leo linatoka katika kitabu cha
Ezekieli kama tulivyosoma hapo juu mwanzoni,
Mwenye haki
atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, akafa katika uovu huo;
katika uovu wake alioutenda atakufa.Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha
uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake,
nayo itakuwa hai.
Katikati ya maneno hayo kuna taarifa ya mwaliko wa
toba na faida zake lakini pia kuna taarifa ya matokeo ya nafasi ambayo utaamua
kuketi kwayo,maana yake maamuzi yako ndiyo yaliyobeba mfumo mzima wa maisha
yako iwe ya kiroho au ya kimwili,ndiyo maana maandiko yananiambia kumbukumbu
la torati 30:19
Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo,kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti,Baraka na laana;basi chagua uzima, ili uwe hai,wewe na uzao wako.
Kwahiyo kuna vitu viwili mbele yako lakini maamuzi ya mwisho ni ya kwako kwamba ufate kipi katika hivyo viwili,lakini kitu cha msingi nilichotaka uone kwenye huo msitari ni kuwa UZIMA unatanguliwa na matendo ya HAKI, na UZIMA huohuo umebeba au umefungamanishwa na BARAKA
Na
MAUTI imetanguliwa na DHAMBI, na MAUTI
hiyohiyo imebeba LAANA au adhabu
kwasababu hakuna mauti kama hakuna dhambi na hakuna laana kama hakuna kosa
lililotangulia.
vivyo hivyo hakuna uzima wa kiroho kama hakuna matendo ya haki,na hakuna Baraka au mafanikio ya kiroho kama hakuna wema uliotangulia au matendo yaliyotangulia na kusimama kwa kuitafsiri haki ya Mungu.
VIPENGELE VYA MUHIMU KATIKA KUITAFSIRI NGUVU YA DHAMBI
KIPENGELE CHA KWANZA
1. Kitu cha kwanza cha muhimu
hapa ni kuelewa kuwa DHAMBI imebeba MAUTI,
Tunaposema dhambi imebeba mauti maana yake ni
kwamba popote penye mauti pana nguvu ya msukumo nyuma yake {kisababishi}
Maandiko yanasema,
“Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.” 1
Wakorintho 15:56
Kwahiyo kuna aina ya uchungu ambao mtu anaweza kuwa nao ndani unaotokana na makosa au dhambi yake mwenyewe, kwasababu uchungu au matokeo ya dhambi ni mauti na kinachoipa nguvu dhambi ni Torati {sheria}
Nguvu ya dhambi ni torati au sheria kwasababu kama
Mungu asingetaja kwamba uzinzi au wizi au uasherati nk ni dhambi maana yake
hata kama mtu angezini au kuiba bado shetani hasingepata nafasi juu ya huyo mtu
kwasababu alichokifanya hakijatajwa kama dhambi au ubaya.
KWA MFANO
Kama sheria ya nchi ya Tanzania isingetaja kwamba
kubaka ni kosa au kuiba au kuua ni kosa maana yake kuua na kubaka ingekuwa ni
haki ya kila mtanzania na ingetokea mtoto wako akabakwa alafu ukaenda
kumlalamikia huyo mtu aliyembaka mtoto wako maana yake ni kwamba wewe mzazi
uliyelalamika kwa tukio la kubakwa kwa mtoto wako ndiwe ambaye ungebeba adhabu
kwa kupingana na sheria, kwasababu kitu ambacho kimeharalishwa kwa mujibu wa
sheria wewe ukikiita haramu ni kosa hata kama ni haramu kweli, na kitu ambacho
mamlaka husika imekitafsiti kama haramu na kukiwekea sheria, wewe ukitaka
kukiharalisha inatafisiliwa kwamba umevunja sheria hata kama una hoja za
kudhibitisha kwamba hicho kitu ni harali, ndiyo maana unasikia askari polisi
wamapomkamata muharifu hutumia Neno;
(sheria itafata mkondo wake)
Kwanini!!!!
kwasababu kinachoipa
nguvu haki na dhambi au kosa ni sheria au torati .
Kwahiyo mtu ni kiunganishi au kiungo kati ya torati na dhambi au kati ya torati na haki.
Unaweza kuhoji kwa namna gani???
Kwasababu katika bustani ya Edeni Adamu na Hawa
waliikuta sheria sawasawa na kitabu cha mwanzo 2:17 – walakini matunda ya mti wa ujuzi
wa mema na mabaya usile,kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa
hakika maana yake kabla Adamu na Hawa hawajaletwa busitanini
ulitengenezwa utaratibu kwanza wa kisheria utakaowapa wao uhalali wa kuishi
hapo ndio maana unaona baada ya kukiuka
utaratibu cheki kitu Mungu anazungumza,……………
Je UMEKULA wewe matunda ya mti niliyokuagiza USIYALE? Mwanzo 3:11b – maana yake anamwambia UMEVUNJA sheria
niliyokuagiza USIIVUNJE?
kwahiyo sheria au torati inasubiri mtu akakinzane
nayo ili imuhukumu au aende sambamba nayo ili impe haki yake.
Maana yake ni kwamba, anayeweza kusababisha haki
ionekane au ipate nafasi ni mtu kupitia kutenda sawasawa na torati ambayo nyuma
yake liko agano la Baraka.
na anayeweza kusababisha dhambi ionekane au ipate nafasi ni mtu huyohuyo kupitia torati ileile kwa kukinzana au kupingana nayo ambayo nyuma yake iko adhabu ya mauti na laana.
Kwahiyo mlango wa dhambi kwenye maisha ya mtu
haufunguliwi na shetani bali anaufungua mtu
mwenyewe kupitia namna anavyoitafsiri na kuitekeleza katika matendo torati au
sheria ya Mungu. Shetani anakuja kusimama kama mshitaki wa matendo
yako sawa na 1petro 5:8 na sio
msababishi wa matendo yako kwasababu hakuna muharifu anayejipeleka kituo cha
polisi na ukiona hivyo ujue huku nyuma kuna mazingira yanayomlazimisha kufanya
hivyo sio kwa hiari yake, ndiyo maana ukimuona kibaka anakimbilia kituo cha
polisi ujue anakimbia kuiponya roho yake dhidi ya wananchi wenye hasira kali.
Ile 1petro 5:8 inasema,mwe na kiasi na kukesha,kwakuwa MSHITAKI wenu ibilisi kama simba aungurumaye,huzunguka-zunguka akitafuta mtu ammeze {maana yake shetani akiwa kama mshitaki wetu anaendaga mbele za Mungu kuomba kibali cha kutushikilia kupitia makosa yetu tuliyoyatenda kwa kuivunja sheria ya Mungu na anapata uharali wa kile kibali automatically kwasababu neno la Mungu linasema atendaye dhambi ni wa ibilisi…………1Yohana 3:8a
kwahiyo ukitenda dhambi saa hiyohiyo unahama ufalme kutoka ufalme wa Mungu aliye hai na kuingia katika ufalme wa shetani kwasababu kanuni ya shetani ya kukushitaki ipo kisheria na inafanya kazi automatically kupitia Neno la Mungu,maana yake shetani haitaji kubisha hodi mlango wa mbinguni ili akushitaki bali mifumo ya kiutendaji wa kiroho ndiyo inayokushitaki automatically kwasababu unapovunja sheria wakati huohuo unaitwa mtuhumiwa, kwahiyo mifumo ya kiroho inapeleka tuhuma zako au kwa lugha nyepesi tunasema shetani anapeleka tuhuma zako mbele za Mungu kupitia mifumo ya kiroho alafu sheria ambayo ni Neno la Mungu inakuthibitisha kwamba wewe ni muharifu na umepatikana na hatia au la,
kwahiyo matokeo
yatakayotafisiliwa kisheria kupitia neno la Mungu ndiyo yatakayokuhukumu kama
wewe una haki ya kuwa mikononi mwa Mungu au una haki ya kuwa mikononi mwa
shetani kutegemeana na tuhuma zilizoletwa kwenye hiyo mahakama ya kiroho na
namna ambavyo sheria ambayo ni neno la Mungu ilivyozitafisiri hizo tuhuma zilizo
juu yako.
alafu ukiendelea kwenye hiyohiyo 1petro 5:9 inasema nanyi mpingeni huyo,mkiwa thabiti katika imani………………..
alafu ukiunganisha na ile warumi 10:17
inasema basi imani chanzo chake ni kusikia……….. kwahiyo tunapata
kuelewa kwamba katika bustani ya Edeni shetani alijenga imani kwanza kwa Hawa kupitia
maneno aliyomsikilizisha maana biblia imetwambia
imani chanzo chake ni kusikia baada ya hapo ndipo Hawa akaamini yale
aliyosikilizishwa kisha yakafanyika imani na
yakabomoa ule msingi wa imani ya kwanza aliyoelezwa na Mungu na
yakajenga msingi wa imani mpya uliopelekea kukosa sifa tena ya kuishi ndani ya
bustani baada ya kutenda dhambi na
mlango wa mauti kufunguka na mwisho kuruhusu laana kupata nafasi,
KUMBUKA huko mwanzoni tumejifunza kwamba MAUTI imetanguliwa na DHAMBI, na MAUTI hiyohiyo imebeba LAANA au adhabu.
Kwahiyo shetani anapokuja katika maisha ya mtu ujue
amepata mlango na akishapata mlango maana yake unaingia kwenye himaya yake na
atakufanya vyovyote anavyotaka kwasababu amekushikilia {nimetumia neno AMEKUSHILIA kwasababu hawezi
KUKUMILIKI kwasababu hana HATI MILIKI yako maana alishanyanganywa mamlaka sawa
na luka 19:10 kwakuwa mwana wa adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea}.
maana
yake husijaribu kumlalamikia shetani kwamba anakuonea,sio kweli bali yeye
amekushikilia kisheria {maana polisi
kituoni wanamshikilia muharifu,hawammiliki muharifu} na ili utoke kwenye
mikono yake lazima ujue sheria ya kukutoa hapo ulipokwama,kwasababu sheria
inapanguliwa kwa sheria ndio maana katika bustani ya edeni shetani alienda na
sheria ya uongo na alipoiachilia katika ufahamu wa Hawa na Hawa akaipokea na
ikapata nguvu kwenye ufahamu wake ndipo alipoivunja ile sheria ya kwanza
iliyomtaka asiyale yale matunda.
KIPENGELE CHA PILI
2. Kitu cha pili cha kufahamu
katika misitari hii ni kuwa MAUTI kupitia DHAMBI inakuondolea sifa ya kuitwa MWENYE HAKI.
Biblia inasema;
2 Mambo ya Nyakati 7:19-20
Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka
mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu;ndipo
nitawang'oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina
langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano
katikati ya watu wote.
Mungu mwenyewe anawambia wana wa israeli ya kwamba
wakiacha sheria yake, atawanyanganya nchi aliyowapa maana yake wakikinzana na
sheria iliyoko mbele yao watapoteza sifa au haki ya kumiliki hiyo nchi
waliyopewa.
Na kwa tafsiri ileile ya dhambi kufungua
mlango wa mauti juu ya mtu,inamaanisha MAREHEMU hanaga haki kwahiyo ukifa umepoteza sifa
ya kwanza ya kuwa binadamu na kwa maana hiyo hakuna namna unaweza kupata haki
za kibinadamu wakati wewe sio binadamu tena, hiyo ni kanuni ya kimwili
lakini ipo mpaka rohoni na ukitaka ujue ipo mpaka soma ezekieli
“Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai.” Ezekieli 18:27
Kwahiyo ukitenda uovu au dhambi kwa kanuni ya
kiroho unahesabika umekufa na hutaweza kupata haki zako zozote mpaka umekuwa
hai tena hata kama huku mwilini unafunga na kuomba siku 40 lakini kama toba
haina nafasi kwako uwe na uhakika unajisumbua tu kwasababu kanuni haziruhusu
hata wewe kusikilizwa, ndio maana hata mkimuweka marehemu mwezi mzima
bila kumzika hawezi kuhoji kwanini hamjamzika,
Hata kama marehemu alikuwa na mali nyingi alafu
ikatokea mkamzika bila sanda au jeneza bado hawezi kuhoji haijalishi huko
kwenye ulimwengu wa roho ananungunika kiasi gani lakini hawezi kufumbua kinywa
maana hana sifa katika nchi ya walio hai kwahiyo haruhusiwi kufungua kinywa
kuzungumza, akitaka apate majibu ya kueleweka lazima kwanza nafsi hai irudi
ndani yake alafu ndipo anaweza akaongea mkamuelewa na kwenye ulimwengu wa roho
ni hivohivo huwezi kumsogelea Mungu na kudai haki yako wakati wewe ni mwenye
dhambi, ukitaka haki yako jitakase kwanza ndipo unaweza kuhojiana na Mungu na kupata
haki yako.
Kwahiyo pointi yangu katika kipengele hiki ni kwamba ukichagua kuishi maisha ya dhambi maana yake umechagua kujitenga na haki yako mbele za Mungu.
Biblia inaniambia katika Ayubu 36:11-12 kama wakisikia na kumtumikia,watapisha siku
zao katika kufanikiwa,na miaka yao katika furaha.lakini wasiposikia wataangamia
kwa upanga nao WATAKUFA PASIPO MAARIFA. {sijui
kama uliwahi kufikiri maana ya hilo neno WATAKUFA PASIPO MAARIFA} anaposema
–watakufa pasipo maarifa- kumbe
unapotenda dhambi akili au ufahamu wako unakamatwa kwasababu unakuwa chini ya
ufalme mwingine na hivyo unaongozwa kwa kila kitu. Kama unafikiri nakutania
kaulize wafanyakazi wa umma au sekta binafsi watakueleza kwamba wao
wanatekeleza maagizo ya viongozi wao haijalishi maagizo hayo ni mazuri au
mabaya.
Inaweza kuwa ngumu kunielewa,wacha nijaribu hivi;
Rais wa nchi akitangaza na kutoa maagizo kwamba machinga wote waondolewe mjini,kinachofuata hapo ni utekelezaji kwa watendaji walioko chini yake hata kama miongoni mwa hao watendaji wapo wenye mawazo tofauti lakini hawaruhusiwi kupinga haijalishi huko mtaani hao machinga wanalalamika na kulia kiasi gani bado wataondolewa kwa nguvu na husiwalaumu hao wanaokuja kukuondoa wewe machinga kwasababu inawezekana kabisa na huyo anayekuja kukuvunjia anaumia moyoni lakini hana namna ya kukusaidia kwasababu yuko chini ya mamlka husika.
Ngoja nijaribu tena hivi;
ukimpeleka mtoto wako kusoma katika shule
zilizoko chini ya usimamizi wa serikali,yakupasa ujue kwamba mtoto huyo anasoma
kutekeleza maono ya serikali na sio maono yake binafsi kwasababu anapokuwa
shuleni anafundishwa chini ya mwongozo wa mitaala iliyoandaliwa kimaalumu
kutegemeana na maono ya nchi inahitaji wasomi wa aina gani katika maeneo gani
kwahiyo inaandaa wanafunzi watakaokidhi mahitaji ya kitaaluma kutegemeana na
maono ya kitaifa ya miaka ishirini au hamsini mbele, ndiyo maana ukipata elimu
ya nchi Fulani alafu ukataka kuajiliwa nchi nyingine inaweza kuwa ngumu kupata
nafasi kwasababu maono yaliyobebwa katika mtaala wa nchi uliyosomea inawezekana
yakawa tofauti na maono yaliyobebwa katika mtaala wa chi unakoitaji kuajiliwa
maana yake kilichobebwa kwenye maarifa uliyopewa huko ulikokuwa hakina msaada
wowote katika ofisi hiyo unakoomba kazi kwasababu umebeba maarifa kwa ajili ya
maono ya nchi Fulani ambayo ni tofauti na maono ya nchi unakoomba kazi.
Ninachomaanisha ni kwamba, unapotenda
dhambi maana yake unakuwa chini ya shetani na ukiwa chini ya shetani maana yake
unaongozwa na mifumo ya ufalme wa shetani,kwahiyo KUFIKIRI kwako,KUWAZA
kwako,KUAMUA kwako,KUNENA AU KUZUNGUMZA kwako na KUTENDA au KUTEMBEA kwako
kunaamuliwa na mfumo wa utawala wa shetani,kwahiyo kwa lugha nyepesi sana ni
kwamba akili yako ya asili sawasawa na uumbaji wa Mungu inakuwa inatenda kazi
pale tu unapokuwa na sifa ya kuitwa mwenye haki wa MUNGU {maana yake unaposimama
katika njia ya Bwana},
lakini unapotenda dhambi tu, ile akili yako au
uwezo wako wa kifikra uliowekewa na Mungu unasimama kutenda kazi badala yake
unaingiziwa mfumo mpya kwenye mfumo wako wa kiakili ambao unafanya kazi badala
ya ule wa kwanza,kwasababu ule wa kwanza ulio wa asili unatenda kazi kutimiza
maono ya Mungu muumba wa mbingu na nchi na huu mpya unaoingia baada ya uasi
unatenda kazi kutimiza maono ya shetani ndio maana kuna aina ya matendo
unayoweza kuyatenda katika jamii alafu ukasikia baadhi ya watu wanasema, {huyu mtu hii sio akili yake bali kuna kitu
kinamuongoza}
kwahiyo mifumo yote hii miwili haifanyi
kazi kwa pamoja lazima mmoja ufanye kazi na mwingine usimame kwasababu
imeandikwa hapana ushirika kati ya nuru na giza sawa na 2wakorintho 6:14,
kwahiyo tunasema ule mfumo wa kwanza ni
wa asili kwasababu mtu ameumbwa na Mungu na mfumo ambao shetani anautumia ndani
ya mtu haimaanishi kwamba anaumba mfumo mpya ndani yako bali anatumia mfumo
uleule wa asili kwa kufanya kitu kinaitwa HACKING
AU UDUKUZI. Unasema sasa anawezaje kugusa kitu ambacho Mungu amekiumba???
jibu ni kwamba,
anaweza kwasababu dhambi ikipata nafasi mahali ulinzi unaondoka kwahiyo milango yote inakuwa wazi,………….ni sawa na umeweka password kwenye simu,hiyo inamaanisha mtu mwingine akihitaji kutumia simu yako lazima apate idhini kutoka kwako lakini ikiwa simu hiyohiyo utaamua kuiondolea security kwa maana ya password inamaanisha mtu yeyote anaweza kuitumia na kuona taarifa zako bila idhini yako. Vivyo hivyo ulinzi wa Mungu unapoondoka juu ya mwana wa Mungu uwe na uhakika shetani anaweza kufanya chochote na kwa wakati wowote mpaka ulinzi utakaporejea.
Kwahiyo ukitenda dhambi unakuwa mtumwa
wa shetani kwenye maeneo yote hayo kama ambavyo nitakuonyesha baadhi ya maeneo
hayo hapa chini;,
·
FIKIRA
Ø
2wakorintho
10:4-5
Maana silaha
za vita vyetu si za mwili,bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,tukiangusha MAWAZO na kila
kitu kilichoinuka,kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu,na tukiteka nyara kila
FIKIRA ipate kumtii kristo.
KWAHIYO
mtu akitaka husimtii mtu mwingine ila yeye au husiamini au husisikilize kitu
kingine isipokuwa hicho anachokueleza atahakikisha anateka fikira zako
kwanza,wasababu akiisha kuteka fikira zako utayari wa kumsikiliza na kumtii
unatokea ndani yako.
Kwahiyo
shetani akifanikiwa kubana fikira zako tafsiri yake ni kwamba,amekamata uwezo
wako wa kusikia,kuelewa au kuchanganua pamoja na uwezo wako wa kuamua kwasababu
maamuzi ni matokeo ya kile kilichoamuliwa kwenye fikira zako.
·
KUWAZA
Ø
Ayubu
21:27
Tazama
nayajua mawazo yenu na mashauri mnayoazimia kwa uovu juu yangu
Inamaanisha
dhambi yoyote inayokuja kwa mfumo wa kimaamuzi inaanzia kwenye mawazo badae
inaingia kwenye fikira kisha inamalizikia katika matendo.
Kwahiyo
kabla mtu hajatenda dhambi hali hiyo inaanzia kwenye mfumo wake wa kuwaza.
Maana yake shetani akikamata fikra zako moja kwa moja amekamata mfumo wako wa kuwaza kwasababu vitu hivi vinategemeana katika utendaji wake wa kazi.
{TOFAUTI KATI YA FIKIRA NA MAWAZO}
Kufikiri na kuwaza ni vitu viwili tofauti ingawa kwa haraka vinaweza kuonekana kama ni kitu kimoja,na vinaonekana hivyo kwasababu utendaji wake wa kazi ni wa karibu sana na unategemeana kwasababu hakuna kufikiri kama hakuna kuwaza na hakuna matokeo ya kuwaza kama hakuna kufikiri.
MAWAZO ni package iliyoko ndani ya FIKRA ambayo kazi yake ni kuleta hoja alafu hoja hiyo ikishaletwa FIKIRA inaingia kazini kuchakata au kuchanganua hoja iliyoletwa.
Kwahiyo FIKIRA kazi yake ni kutengeneza mipango mikakati ya kutekeleza hoja iliyoletwa kwa kuhakikisha inakusanya na kutafuta details zote zitakazowezesha hoja husika kutekelezwa.
MFANO
Mtu anasema nataka kujenga nyumba,hili ni WAZO
Baada ya hapo ataanza kumtafuta fundi ampe gharama za msingi,tofari kiasi gani mchanga,cement na kila kinachotakiwa,mtu akiwa katika hatua hii za kwenda huku na huko kufatilia mafundi tofauti na gharama za vifaa vya ujenzio huwezi kusema hili ni wazo bali process hizi ni kazi ya FIKIRA,kwasababu hawezi kuanza kutafuta mafundi na vifaa vya ujenzi kama hajawa na wazo la kujenga.
{MAWAZO/WAZO 2mambo ya nyakati 6:8}
{FIKIRA mithali 24:32}
·
KUNENA AU KUZUNGUMZA
Ø
Wakolosai
4:6
Maneno
yenu yawe na neema siku zote,yakikolea munyu,mpate kujua jinsi iwapasavyo kila
mtu.
Mahali
pengine maandiko yanasema;
Waefeso
4:29
Neno
lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu,bali lililo jema la kumfaa mwenye
kuhitaji,ili liwape neema wanaosikia.
Maandiko yanatueleza wazi kabisa kwamba kwenye vinywa vyetu yanaweza kutoka maneno yaliyo maovu au yakatoka maneno mema yanayoweza kufanyika msaada kwa wanaosikia.tena maandiko yanaendelea kusema kwamba maneno ya kinywa chako yanaweza kuzalisha neema kwa wanaosikia.
Maana yake shetani akifanikiwa kukamata kinywa chako,moja kwa moja amefanikiwa katika mambo makuu mawili.
1.akibana kinywa chako,amefanikiwa kuzalisha uovu kupitia wewe kwa maana ya kukamata nafsi yako.
2.akibana kinywa
chako,amefanikiwa kupitia wewe kuvuruga watu wengine na wewe kufanyika sababu
ya wao pengine kumtenda dhambi Mungu,
kwasababu atatumia kinywa chako kunena mabaya na katika mabaya unaweza kutukana mtu na ukishamtukana maana yake umetengeneza hoja ya majibizano,kwaiyo katika kukujibu mtu anaweza kujikuta na yeye anajibu yaliyo mabaya ambayo yatafanyika kitanzi kwake na kujikuta anatenda dhambi pasipo kutarajia.
Maandiko yanaposema basi
UMETEGWA kwa maneno ya kinywa chako,UMEKAMATWA kwa maneno ya kinywa
chako.mithali 6:2
Kuna maneno mawili
hapo,{kutegwa na kukamatwa} na yote yanatokana na maneno ya kinywa.
Inamaanisha shetani anaweza
akatumia maneno ya kinywa kukuwekea mtego kwa kukutega na anaweza akatumia
maneno ya kinywa chako kukunasa au kukumata kupitia kile unaongea au kile
unajibu.
·
KUTENDA/MATENDO
Yeremia
21:12
Ee
nyumba ya daudi,bwana asema hivi,hukumuni hukumu ya haki asubuhi,mkawaponye
waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu,gadhabu yangu isije ikatoka kama
moto,ikaunguza,asiweze mtu yeyote kuuzima,kwa sababu ya uovu wa MATENDO YENU.
KWAHIYO matendo ya mtu kinaweza kuwa
chanzo cha kuzalisha uovu katika maisha
ya mtu au watu au jamii. Ndiyo maana biblia inasema,wanakiri kwamba wanamjua
Mungu,bali kwa MATENDO yao wanamkana,ni wenye machukizo,waasi,wala kwa kila
tendo jema hawafai.Tito 1:16
Hapa anazungumza na watu waliookoka
kabisa walioko makanisani kwasababu huwezi kumjua Mungu ikiwa hukuwai
kumsikia,kwahiyo anaongea ambao wamekwisha kusikia na kuamini lakini mienendo
na matendo yao haimtafsiri Mungu huyo wanayemtaja.
Kwahiyo wanabaki kuwa ni watu wa Mungu
kanisani na sio wana wa Mungu.
Lakini sehemu nyingine Neno la Mungu
linasema,
1timotheo 4:12
Mtu awaye yote asiudharau ujana
wako,bali uwe kielelezo kwao waaminio ,katika usemi na mwendo,na katika upendo
na imani na usafi
{ukijitangaza kwamba unamjua
Mungu,chunga sana usemi wako,mwenendo wako,imani na usafi katika mambo yote
kwasababu jambo moja tu linaweza kubadili maana halisi ya utambulisho wako
mbele za watu na mbele za Mungu.}
Tito 2:6-7
…………………7.katika mambo yote ukijionyesha
wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema,na katika mafundisho yako
ukionyesha usahihi na usitahivu.
Matendo yako inabidi yawakilishe kilichoko ndani,kwa maana nyingine ni kwamba mtu anakutafisiri kwa namna unavyoonekana nje hata kama sivyo ulivyo rohoni kwasababu ili watu uwashawishi katika jambo Fulani ni lazima wewe mwenyewe uwe muumini wa hicho unachowashawishi wakifanye na namna pekee ya kuwafanya watu hao waamini kwamba wewe mwenyewe ni muumini ni kusoma matendo au mwenendo wako.
Shida kubwa iliyo kwa waamini ni hii kwamba,
watu wengi wanamuhitaji Mungu,lakini hawapo tayari kutembea naye,kwasababu namna pekee ya kumpenda na kutembea na Mungu ni kuliishi Neno lake.
Ukijichunguza ukagundua tabia na
mwenendo wako havimtafisiri Mungu,basi ujue wewe haujaanza kuliishi Neno la
Mungu maana yake wewe sio wa Mungu bado.
KIPENGELE CHA TATU
kitu cha tatu cha kufahamu ni kwamba HAKI ya mtu imefungamanishwa katika TOBA (uhalali au utakatifu).
Maandiko yanasema,
“Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati
za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;” Matendo ya Mitume 3:19
Anaposema,tubuni
basi mrejee inamaanisha ulikuwa umepotea au ulikuwa haupo eneo husika au
ulikuwa haupo kwenye ramani,maana anaposema urejee inamaanisha uhame kutoka
eneo Fulani na uende eneo jingine.kwahiyo tunapata kuelewa kwamba kumbe mtu
akitenda dhambi anahamishwa na kutolewa kwenye nafasi yake,ndiyo maana tukirudi
katika bustani ya edeni kuna msitari wa ajabu sana,maandiko yanasema;
Mwanzo 3:9
Bwana Mungu akamwita Adamu,akamwambia huko wapi??
Kwa kusema hivyo husije ukafikiri kwamba Mungu
alikuwa hamuoni Adamu mahali alipo,alikuwa akimuona kwasababu hakuna lolote
lililofichika katika macho ya Mungu,
kwanza maandiko yanasema,AKAMWAMBIA, Inamaanisha alikuwa anamuona,kwasababu huwezi kumwambia mtu ambaye humuoni.kama ingelitokea msitari huu wa 9 ukakomea hapa kwa kusema; Bwana Mungu akamwita Adamu, alafu ndio adamu akaja akajibu ule wa 10,tungesema kweli Mungu alikuwa hamuoni Adam.Lakini ile kumuita na kumuuliza swali inamaanisha alikuwa namuona.isipokuwa alichokuwa anahoji hapo Mungu ilikuwa ni nafasi ya Adamu kwasababu alikomuweka hayupo badala yake ameshaondolewa au amekwisha kuhama sawasawa na matendo ya mitume 3:9 inayosema tubuni basi mrejee…….
Kwahiyo Mungu alikuwa anahoji nafasi ya adamu
kiagano,kwasababu kiti chake kiko wazi alafu mwenye kiti hayupo.ndivyo hivyo
ambavyo leo hii mtu akitenda dhambi moja kwa moja unatoka kwenye nafasi yako na
hivyo Mungu anapotaka kukuhudumia lazima akukute kwenye nafasi yako,na damu ya
Yesu ndio pekee yenye uwezo wa kukurejesha wewe kwenye nafasi yako.
Kwahiyo nyakati za burudisho sawa na Matendo ya Mitume 3:19 ……zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;” zinatokea baada ya toba na kwa maana hiyo ni kwamba hakuna tumaini lolote lililo jema ndani ya dhambi kwasababu kwa kusema kwamba tubuni zije nyakati za kuburudishwa inamaanisha kabla ya hapo hizo nyakati hazikuwepo.lakini pia huohuo msitari unasema, kwa kuwako kwake Bwana maana yake toba inamfanya Mungu arejee kwako,kinyume chake ni kwamba ulipotenda dhambi aliondoka.
Isaya 1:18-20
Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa
nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera,
zitakuwa kama sufu.
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa
cha Bwana kimenena haya.
Toba ndio njia pekee ya kuturejesha kwa bwana nje
na hapo huwezi kusikika hata ukiomba,huwezi kusaidiwa hata ukipiga kelele
kwasababu dhambi inakuja kukuondolea sifa ya wewe kupata haki zako zote,sasa
ili sifa hiyo ilejee kwako lazima kiwepo kitu ambacho kinaweza kurejesha
uhalali wa wewe kudai haki yako na ukapokea.
Kama tulivyojifunza huko juu,unapotenda dhambi
unakuwa mikononi mwa shetani ukiwa kama mateka,na sote tunajua hakunaga mateka
ambaye ana uhuru wa kuomba msaada huko nje wa kukombolewa mpaka walioko nje
wapange namna ya kuja kwenye hiyo ngome na kumkomboa.kwetu sisi tulio katika
kristo tunayo neema hiyo na ni ya bure,kupitia damu ya Yesu unaweza kukombolewa
wakati wowote unapohitaji huduma hiyo ya ukombozi,sawasawa na kitabu cha injili
ya mathayo;
mathayo 26:28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya
agano,imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
Vifungo vinaweza kuwa vya aina nyingi lakini kila kifungo kinasababishwa na mlango wa dhambi kufunguka katika maisha ya mtu,kwahiyo ili upate uhalali wa kutoka kwenye hicho kifungo kwanza lazima upate nafasi ya kutubu na kukombolewa kupitia damu ya Yesu.
Mungu wangu mwema akubariki sana na hapa ndio mwisho wa somo letu
Tukutane tena wakati mwingine
Amen

0 Comments