100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

IJUE HEKIMA YA MUNGU


IJUE HEKIMA YA MUNGU

 Bwana Yesu Asifiwe

2Mambo ya Nyakati 1:7-12

“Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa , Ee Bwana Mungu wangu na limyakinie baba yangu Daudi neno lako, maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. Basi sasa, nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa, kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?. Naye Mungu akamwambia Sulemani, kwasababu neno hili lilikuwemo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za  wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi, bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu niliokutawaza juu yao, basi hekima na maarifa umepewa, nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo”.

Je ni kwanini Sulemani aliomba hekima?

Alijua kuwa katika hekima ndipo kuna vitu vyote, iwe uzima, utukufu, utajiri, Amani, ushindi, baraka nk.

  1. Katika hekima ndipo kuna uzima

Mithali 3: 35a

“Wenye hekima wataurithi utukufu…..”

  1. Katika hekima ndipo kuna utajiri

Mithali21:20a

“Kuna hazina ya thamani na mafuta, katika maskani ya mwenye hekima…..”

  1. Katika hekima ndipo kuna nguvu

Mithali 24:5

 “Mtu mwenye hekima ana nguvu, Naam mtu wa maarifa huongeza uwezo…..” 

 Katika hekima ndipo kuna kila kitu hata ambavyo havijatajwa apo juu, hekima ndio msingi wa mkristo na mtu yeyote mwenye kuishi sawa na mapenzi ya Mungu. Tunahitaji hekima katika maisha yetu zaidi ya vitu vyote maana hekima pia ndio uzima wetu.

Lakini je wajua ya kwamba Yesu Kristo ndiye hekima yenyewe?, Na kwamba Mfalme  Sulemani alimwomba Yesu Kristo mwenyewe ndio maana akapewa kila kitu.

Tusome maandiko aya :-



Luka2:40

“Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikua juu yake”.

Luka2:52

“Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu”.

1Wakorintho 1:30

“Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi”

Mithali 8:12-31

“Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu, natafuta maarifa na busara, Kumcha Bwana ni kuchukia uovu, kiburi na majivuno na njia mbovu, na kinywa cha ukaidi pia nakichukia, shauri ni langu na maarifa yaliyo sahihi, Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu, kwa msaada wangu Wafalme humiliki, na wakuu wanahukumu haki , kwa msaada wangu wakuu hutawala, na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia, nawapenda wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona, Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo na haki pia………….”

Huu ndio uthibitisho ya kwamba Yesu Kristo ndiye hekima mwenyewe, ambaye kwa hekima yake aliumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, akamuumba mwanadamu avitawale vitu vyote, kwa hekima alipoona watu wote tu wakosefu hakuna mkamilifu hata mmoja akazaliwa katika mwili na kuja kutukomboa, huku akikubali kuteswa, kudhihakiwa, kudharauliwa, kupigwa na kusulubiwa mwisho mauti ya msalaba kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu, yaani mimi na wewe.

Aidha migogoro ya wanadamu, malumbano , chuki, vita na kila aina ya uovu ni matokeo ya kukosa hekima. Mtu mwenye hekima huishi maisha safi ya kumpendeza Mungu na wanadamu na ndiye katika uyo baraka zote huambatana pamoja naye kama ilivyokuwa kwa Mfalme Sulemani . 

Hatuhitaji kuomba kitu chochote tujapopungukiwa hekima, tuombe hekima ambayo itaambatana na kila kitu kuanzia uzima, utajiri, heshima, baraka, amani nk.

Yakobo 1:5

“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa hekima, na aombe kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei, naye atapewa”




Mungu awabariki sana na karibu tena katika kipindi kijacho.

Mwl:Jovin John


Post a Comment

0 Comments