100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

SIKU YA TAABU - Mwl Jovin John

 SIKU YA TAABU

NITAMUITA NANI WAKATI WA TAABU?

 

 

Bwana Yesu Asifiwe

 

Yona 2:1-7

“Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki akasema, Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu, naye akaniitikia, Katika tumbo la kuzimu naliomba, nawe ukasikia sauti yangu. Maana ulinitupa vilindini, Ndani ya moyo wa bahari; Gharika ya maji ikanizunguka pande zote; Mawimbi yako yote na Gharika zote zimepita juu yangu. Nami nikasema nimetupwa mbali na macho yako; lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; vilindi vilinizunguka; mwani ulikizinga kichwa changu; Nalishuka hata pande za chini za milima; hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; lakini umenipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee, BWANA, Mungu wangu, Roho yangu ilipozimia ndani yangu, nalimkumbuka BWANA, Maombi yangu yakakuwasilia, katika hekalu lako takatifu”.

 

Baada ya Kujiepusha na uso wa Bwana akakimbilia Tarshishi badala ya kwenda Ninawi kupeleka habari njema kama alivyoagizwa  na Mungu hatimaye mtumishi wa Mungu Yona anatupwa baharini kutokana na gharika iliyowapata katika chombo alichopanda. Naye Yona anamezwa na samaki mkubwa, anakaa ndani ya samaki kwa siku tatu haoni uso wa dunia, hali wala kunywa, uku akipumua kwa shida. Hakika ni mateso makubwa, hatimaye anakumbuka ya kwamba yupo Bwana wa Mabwana, Muumba wa Mbingu na nchi naye aweza kumrehemu na kumtoa katika mateso ayo.

Yona akamwiita Mungu amuokoe katika taabu yake, naye Mungu akasikia na kujibu.

     Yona 2:10

“BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona Pwani”.

 

Stefano akamwita Mungu pia. Akalia na kumwita Mungu na mwisho anasema Bwana Yesu pokea roho yangu.

     Matendo 7: 54-60

“Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa moyo, wakamsagia meno. Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, tazama? naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashaidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake”.

 

Hana naye akamwiita Bwana kwa taabu yake ya kutopata mtoto na kudhihakiwa kila siku:

       1Samweli 1:4-7

“Hata siku ilipofika Elkana alipotoa dhabihu, humpa mkewe Penina sehemu, akawapa na watoto wake wote, waume kwa wake sehemu zao; lakini Hana humpa sehemu mara mbili, maana alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amemfunga tumbo. Ila mwenzake humchokoza Sana, hata kumsikitisha, kwa sababu BWANA alikuwa amemfunga tumbo. Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda kwa BWANA, ndivyo yule alivyomchokoza; Basi, kwaiyo, yeye akalia, asile chakula”.

Hana akamwiita Mungu kwa taabu yake naye Mungu akasikia na kujibu.

         1Samweli 1:20

“Ikawa wakati ulipowadia Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA”.

 

  Yawezekana katika taabu yako ndugu wakakutenga, majirani wakakukimbia, kadharika watoto wako, wazazi wako, marafiki zako, yamkini hata waumini wenzako lakini Bwana Yesu hawezi kukukimbia kamwe.

Mwiite Bwana naye atakuitikia atakuonesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua maana ametupa nafasi ya kumwiita. Katika mambo ambayo kwa akili na fahamu zetu twaona ya kwamba haiwezekani, hayo ndiyo Mungu wetu hushughulika nayo. Akili na mawazo ya mwanadamu yanapoishia ndipo Mungu anapoanzia.

         Yeremia 33:3

“Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”.

Yeye yupo karibu zaidi ya chochote, anasikia na anajibu kwa wakati.

        Isaya 55:6,b

“Mwiteni, maadamu yu karibu”

Kumbuka kuwa tupo katika ulimwengu uliojaa taabu, masumbuko, shida, adha na mateso ya kila namna, usichoke kumwita Mungu wakati wa taabu yako maana yeye yupo kukusikiliza na kuwa msaada wakati wa taabu yako.

 

Mungu awabariki sana na karibu tena katika kipindi kijacho.

Mwl: Jovin John

 

Post a Comment

0 Comments