100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

TOFAUTI KATI YA MATOKEO YA DHAMBI NA GHARAMA YA DHAMBI

 

SOMO:TOFAUTI KATI YA MATOKEO YA DHAMBI NA GHARAMA YA DHAMBI

MATOKEO YA DHAMBI Ni;

1.      Ukitenda dhambi maana yake unavunja ushirika wa uzao katika kristo Yesu kati yako na Mungu hii utaipata katika

1 Yohana 3:9

“Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.”

Biblia inaposema kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; inamaanisha inapokuwa kinyume na hapo kwa maana ya kutenda dhambi,tafsiri yake ni kwamba unakiuka sheria na kanuni za kuitwa mwana wa Mungu na Unapoteza haki ya kukaa ndani yake kwasababu maandiko yanasema aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, maana kuna tofauti kati ya mwana wa Mungu na mtu wa Mungu ndio maana kila mtu ni mtu wa Mungu lakini si kila mtu ni mwana wa Mungu.kinachotufanya tuwe na sifa ya kuitwa wana wa Mungu ni kukubali kuzaliwa upya katika kristo Yesu amabaye kwake pana ondoleo la dhambi ambayo inatufanya tupoteze hiyo sifa ya kuitwa wana wa Mungu,lakini ikiwa kinyume na hapo wewe  utabaki kuwa mtu wa Mungu na sio Mwana wa Mungu.

 

MIFANO YA MATOKEO YA DHAMBI

·        DHAMBI YA SODOMA NA GOMORA

Mwanzo 13:13,19:24-25 

“Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya Bwana.Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana.Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. ”



·      MAUTI YA KORA NA WENZAKE   

Hesabu 16:29-35 

Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi BWANA hakunituma mimi.Lakini BWANA akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau BWANA, Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka;nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni.Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi.Kisha moto ukatoka kwa BWANA, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.


 

·       MANUNGUNIKO YA WA WANA WA ISRAELI KWA MUNGU NA KWA MUSA 

Hesabu 11:1 Hesabu 21:5-6,

Kisha hao watu walikuwa kama wanung’unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago.

Hesabu 21:5-6

 Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.

BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.


 

·      ANANIA NA MKEWE SAFIRA WALIPOMDANYANGANYA ROHO MTAKATIFU

  Matendo ya Mitume 5:3,5,7,8,9,10.  

³ Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?

⁵ Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.

⁷ Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.

⁸ Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.

⁹ Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.

¹⁰ Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.

 Hiyo ni kwa sehemu tu ya mifano ya matokeo ya dhambi ambayo watu wa Mungu walitenda dhambi na wakajikuta wanaingia kwenye adhabu lakini unaweza kuyaepuka hayo yote kwa kutii sheria ya Mungu na kukubali kunyenyekea chini ya mkono wa Mungu.


 

GHARAMA YA DHAMBI Ni;

2.      Ni matokeo ya matokeo ya dhambi kabla na baada ya toba husipojua namna bora ya kutubu kutegemeana na  mbegu iliyopandwa kutokea kwenye uovu ulioutenda;

USHUHUDA

Mtu mmoja akaniambia kwamba ana miaka kadhaa katika ndoa yake na kwa muda wote wameishi kwa uaminifu, amani na upendo mkubwa pamoja na mke wake japokuwa hawakuwa na maisha mazuri sana lakini amani kati yao ilitawala.

ANAENDELEA AKISEMA,ilikuwa ni siku ya giza kwake wakati ambapo alianguka katika dhambi ya uzinzi kwa kutembea na mwanamke mwingine,ile hali akijua itabaki kuwa siri na hakuna mtu atafahamu na zaidi sana anasema alichunga kuficha kila dalili za usaliti kwa mke wake ili hasigundue maana alitambua ni kiasi gani alimpenda na kumuamini na hivyo aliona hali ya maumivu atakayoipitia baada ya kugundua mkewe anamsaliti.

ANASEMA, hali hiyo iliendelea kwa usiri mkubwa na siku moja mkewe akasafiri kwa sababu za kifamilia na wakakubaliana atarudi baada ya wiki mbili.

KIJANA ANASEMA,akaona kama ndio mwanya mzuri wa kufurahi (KWA MTAZAMO WAKE ALIONA NI FURAHA)na huyo mwanamke wa  Nje ya ndoa na akahamua kuhamia kwa huyo mwanamke mpaka mke wake atakapokaribia kurudi ndipo arejee nyumbani,

ANASEMA,alikaa kwa huyo mwanamke kwa siku tano pasipo jambo lolote baya kutokea na siku ya sita mwanamke huyo akamlazimisha wahamie nyumbani kwa mwanaume,

ANAENDELEA AKISEMA,nilishtuka kusikia hivo kwasababu pamoja na kwamba mke wangu hakuwepo lakini majirani lazima wangeweza kumfikishia taarifa pindi atakaporudi lakini mwanamke aliendelea kulazimisha na ikawa ugomvi ndani na mwisho mwanaume akamuelezea mazingira halisi nini kinamzuia lakini baadaye wakakubaliana kwamba watakuwa wakishinda kwa mwanamke na usiku wanaenda kwa mwanaume.

ANASEMA walifanya hivo ilipofika siku ya kumi na moja wakiwa ndani wamelala usiku wa manane ghafla mlango wa chumbani ukafunguliwa na mwanaume akahamaki kumuona mkewe amerejea nyumbani usiku,anasema hakupata shida kuwaza ameingiaje kwasababu walikuwa na utaratibu wa kila mtu kutembea na ufunguo wake lakini pia siku wanaagana alimwambi na yeye angeweza kusafiri kikazi kwasababu alikuwa ni mfanyabiashara wa nafaka na hivyo ni kawaida kwake kusafiri mara kwa mara kwa ajili ya kufatilia mazao katika mikoa mbalimbali pindi anapopata bei rafiki kutoka kwa mawakala wake walio mikoani. na zaidi pia alishtuka kwasababu mkewe karudi kabla ya siku walizokubaliana.

NIKAMUULIZA ANACHOHITAJI NI NINI,akasema,ametubu mbele za mke wake na mbele za Mungu na mkewe amemsamehe lakini ndani ya moyo wake hana amani na haoni tena kule kupendwa na kujari kutoka kwa mkewe kama  awali,japokuwa mkewe amemtangazia msamaha.

 

Ni ukweli kwanza amesamehewa kwa Mungu kwa dhambi hiyo aliyotenda maana neno la Mungu liko wazi yakwamba tutubu na tupate kurejea kwenye nafasi zetu lakini pana gharama ya dhambi ambayo kuitumikia ni lazima kama hujafahamu jinsi ya kwenda mbele za Mungu kwa mazingira kama hayo yanapojitokeza.

 SOMO LA; UPONYAJI WA NDOA YAKO


KWA MFANO 

mwizi akiiba alafu akakamtwa na kupelekwa mahakamani kasha akahukumiwa kifungo jera,alafu akiwa huko jera akamkumbuka Mungu wake akatubu,ni wazi kuwa atasamehewa lakini toba ile haiwezi kumtoa gerezani na wala hawezi kueleweka akienda mbele za mkuu wa gereza na kumwambia amuachie kwasababu amekwisha kuomba toba.

Sasa sina maana kwamba hauwezi kutokea muujiza wa kukutoa gerezani maana inaweza kufanyika rufaa na ukashinda kesi hata kama mwanzo ulipatikana na kosa au ukatoka kwa msamaha wa rais na au mamlaka husika zenye mamlaka kisheria lakini lazima kuna mahali utapita.

Huyu ndugu aliyekosana na mke wake haina maana kwamba alidumu hivo na mkewe bali tuliomba kwa miongozo maalumu na mkewe akiwepo,kwasababu ilikuwa ni lazima ushiriki wake uwepo kwasababu alioyekosewa sio mke pekeake bali na gano la ndoa limechafuliwa na agano la ndoa ili likamilike lazima wote wawili wahusike na kwasababu mungu anapowatazama wanandoa naona ni mwili mmoja ilikuwa ni lazima pamoja na kutubu kwa mwanaume lakini mke naye alitakiwa kutubu kw ajili ya dhambi ya mmewe na yeye mwenyewe akiwa kama sehemu ya huo mwili uliotenda dhambi.sasa sio kazi rahisi kumwambia aliyekosewa kwamba na yeye ameshiriki dhambi hiyo ya uzinzi na hivyo anatakiwa atubu.

Kwa lugha nyingine ni kwamba toba aliyoifanya mwanaume ilimfungua yeye lakini haikulifungua agano la ndoa  ndio maana yeye alisamehewa lakini kupitia mlango wa agano la ndoa shetani akazidi kupandikiza mbengu kwa mkewe na kumfanya aonyeshe picha ambayo yeye aliitafsiri kama alivyosema.

Wacha twende kwenye maandiko,biblia inasema

Mathayo 27:3-5 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.

Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.

Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.

Maandiko yanasema YUDA lirudisha vile vipande thelathini vya fedha na akajuta kwa kuisaliti damu hisiyo na hati,kule kujuta kulikuwa kunatosha kumpeleka kwenye nafasi ya toba lakini pamoja na kujuta na kurudisha hivyo vipande vya fedha lakini bado mauti ilishuka juu yake maana maandiko yanasema alijinyonga.

Swali la kujiuliza ikiwa maandiko yanasema ukitenda neno kwa mwana wa adamu utasamehewa kwanini kwake hakubaki kuwa hai,lakini nataka nikwambie kilichompelekea kujinyonga sio dhambi aliyoitenda bali ni gharama ya dhambi aliyoitenda kwahiyo usishangae ukifika mbinguni ukamkuta nayeye yupo maana maandiko yanasema alijuta na kama alijuta maana yake lazima aliomba kusamehewa.sasa husipomkuta huko mbinguni husiseme nilikudanganya lakini shabaha yangu nilitaka kukuonyesha tofauti ya hivi vitu viwili na namna ya kutoka unapokuwa umekwama kwenye kimojawapo.

Lakini zaidi sana roho mtakatifu atakufundisha zaidi kadri utakapoonyesha kiu ya kutaka kujua mapenzi ya  Mungu maana maandiko yanasema yeye hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa,maana yake kama anadumu katika kutuombea lazima yuko tayari kujifunua kwenye kwa namna ya msaada pale tunapohitaji msaada wake.

Linaendelea………………

MASOMO MENGINEYO

SOMO LA; UMUHIMU WA MALEZI KWA MTOTO SEHEMU YA PILI 


NENO LA SIKU;THAMANI YAKO INATEGEMEANA NA ULICHOKIBEBA


Post a Comment

0 Comments