100/recent/ticker-posts
KANAANI MPYA - Lisikilizeni Neno la Bwana............. MAOMBI NA MAOMBEZI --- Tupigie; +255767-155-623 Ujumbe mfupi/Whatsapp; +255620-179-783

UMUHIMU WA KUMUOMBEA MTOTO AKIWA TUMBONI

 

UMUHIMU WA KUMUOMBEA MTOTO AKIWA TUMBONI

WWW.DRAYWADRAY.COM

WhatsApp Group Link

YEREMIA 1:5

“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Somo letu leo linaangazia kwa habari ya umuhimu wa kumuombea mtoto aking'ali bado katika tumbo la mama yake kama kichwa cha somo letu kinvyosema.

Sio jambo geni kwa watu kumuweka wakifu mtoto pindi anapozaliwa lakini sio wote wanaofahamu umuhimu wa kumuombea kabla ya kuzaliwa kwake.

Sipingi mtoto kuwekwa wakifu anapozaliwa lakini kumuombea anapokuwa tumboni ni jambo la kwanza na kumuweka wakifu ni jambo la pili, shika hilo sana husije ukasahahu, kwahiyo husije ukafikiri nadharau tukio la mtoto kuwekwa wakifu anapozaliwa bali najaribu kupanua ufahamu wako ili upate kufaidi matokeo ya kile alichobebeshwa mtoto wako na Mungu.

Maana wakati ule mimba inatungwa ndipo saa ile pumzi ya uhai inaachiliwa ndani yake na ndipo saa ile kusudi la Mungu linaachiliwa ndani yake.

Kwahiyo kwa lugha nyepesi ni kwamba juhudi za kumlinda mtoto dhidi ya adui zinatakiwa zianze kabla ya mimba kutungwa.kwasababu hapa ndipo msingi wa mtoto wako unapoanzia kutengenezwa iwe ni upande wa Mungu au upande wa shetani. 


Biblia inasema "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,............" 

Maana yake kbla ya mimba kutungwa Mungu alimjua YEREMIA Vivyo hivyo shetani pia anaweza kumjua mtoto wako kabla hajaumbwa maana miongoni mwa vitu nyeti anavyofatilia shetani karibu zaidi na kwa nguvu zote ni uzao wa mwanadamu,na hii ni kanuni ya kiroho na ipo kibiblia katika MWANZO 3:15 “nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Kwahiyo uadui kati ya shetani na uzao wa mwanamke ulianzia hapa. 


Kwa wale wanandoa wa zamani wanaweza kuelewa hapa,

Siku hizi sielewi sawasawa kanuni zinazotumika lakini zamani kuna baadhi ya makabila ambayo  binti anapoolewa ile siku ya fungate (HONEYMOON) yenyewe wanatumwa Wawakilishi kutoka upande wa binti anaweza kuwa shangazi au bibi wa binti au yeyote aliyeaminiwa na familia, na huyo atakayetumwa siku hiyo atahakikisha yale mashuka yanayotumiwa siku ya kwanza kwa maana binti yule na kijana wanapokutana yanatakiwa kuchukuliwa na huyo mwakilishi wa binti yakiwa na damu iliyomwagika kwa maana ya BIKRA, maana heshima ya familia za zamani na hata sasa ni binti yao kukutwa hajaharibiwa ubinti wake. Na ili kuonyesha umuhimu wa jambo hilo ilikuwa binti akikutwa hana bikra ndoa hiyo ilikiwa inaishia hapo na kesho yake binti huyo anarudi nyumbani kwao na huyo mwakilishi wa familia.

Sasa basi kitendo kile cha kuchukuliwa kwa zile shuka zenye damu ya binti yao kilikuwa na maana kubwa sana katika ulimwengu wa roho maana damu zile zilikuwa zinawakilisha agano kati ya binti na kijana.

Kwasababu popote penye agano pana mwagiko la damu ndio maana

  • Ilikuwa ni lazima mwanakondoo achinjwe kama sadaka ili Isaka awekwe wakifu kwa Bwana. 
  •  Ilikuwa ni  lazima mwankondoo achinjwe usiku ule wa wana wa israel kutolewa katika mikono ya utumwa.
  • Ilikuwa ni lazima damu ya yesu imwagike msalabani kama ishara ya ukamilifu wa agano jipya.


Kwahiyo kitendo cha damu ya binti kuchukuliwa kilikuwa na maana pana kwasababu lilikuwa ni agano linaloenda kukamilishwa kwa kuunganishwa uzao wa huyo binti na miungu ya familia au ukoo.

Ndio maana nikasema sijui leo mfumo halisi unaotumiwa maana mabinti wengi wanaingia katika ndoa wakiwa wamekwisha kuharibiwa tayari, hali inayosababisha desturi ya mila hizo kutoka kwa makabila hayo kuondoka taratibu lakini lazima kuna mbadala wa jambo hilo maana ni kanuni ya kiroho na ili ibadilishwe lazima iletwe mbadala wake,ndiyo maana mabinti wengi wa siku hizi wanapopata ujauzito wazazi haswa wa upande wa kijana wanajari sana kuwa karibu na huyo binti karibu kipindi cha ujauzito wake na kama yuko mbali nao wengine huwa wanalazimishwa kupelekwa nyumbani kwa wazazi wa kijana kwa kisingizio cha kulea ile mimba hata kama kijana anaishi mjini karibu na hospitali kubwa zinazoweza kumuhudumia huyo mjamzito.

Lakini maana yao kubwa ni kumnywesha madawa yule binti akiwa mjamzito wakimwambia kwamba ni dawa za kulea ujauzito na wengine huenda mbali mpaka kumchanja chale katika kitovu na sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kisingizio kilekile cha kulinda kiumbe aliye tumboni,

(na kitovu kinawakilisha muunganiko wa uzao wako, ndiyo maana mtoto anapozaliwa, wazazi wa kijana hususani bibi wa mtoto huwa wanang'ang'ania kubaki na vitovu vya watoto waliozaliwa)

lakini kama tulivyosoma huko juu yakwamba popote penye mwagiko la damu pana agano,

Kwahiyo kitendo cha kuchanjwa chale inamaanisha lazima damu  zitoke alafu ile dawa ipakwe pale na kwa manuizo maalumu yanayoambana na nguvu fulani nyuma yake, ilo tayari ni agano la kumukabidhisha mtoto aliyeko tumboni kwa miungu ya hiyo familia au huo ukoo.


Na hata baada ya kuzaliwa kwa huyo mtoto kuna aina ya matukio yananyika kwa huyo mtoto chini ya uangalizi wa wazazi kabla ya kumuachia binti kuondoka na mtoto wake, na miongoni mwa matukio hayo ni kama 

  • kumunyoa nywere mtoto alizozaliwa nazo, 
  • Kumkata kucha alizozaliwa nazo, 
  • Kukabidhi kitovu kwa wazazi wa kijana au bibi. 

Vitu vyote hivyo hukabidhiwa kwa mtu maalum katika familia na hata hivyo bado binti au mama wa mtoto aliyezaliwa hatakiwi na wala haelezwi vitu hivyo vinapelekwa wapi, lakini zaidi sana kama huyo mtoto aliyezaliwa ni mzaliwa wa kwanza kwa kijana wao, humlazimisha pia kama ni wa kike akampe jina la bibi yake yaani mama yake na kijana au bibi mzaa baba mtoto na kama ni wa kiume hulazimishwa kupewa jina la babu yake au jina la baba mzaa baba yake na mtoto aliyezaliwa,na ikiwa  kijana atagoma kufanya hivyo yatatokea matukio yatakayomlazimisha kukubaliana na maagizo hayo kama mtoto kuumwa mara kwa mara au afya ya mtoto kuwa dhaifu bila sababu au mtoto kulia wakati wote hata kama haumwi au inaweza kupelekea pia mtoto kufariki. 

Na hapa ndipo panapoamuliwa kiwango cha maisha anayotakiwa kuishi huyo mtoto hata baada ya kuwa mtu mzima, ndio maana utakuta kuna familia au ukoo mzima hakuna hata mmoja aliyesoma zaidi ya darasa la saba na aliyejitahidi kuendelea aliishia katikati, 

Lakini pia kuna familia wazaliwa wa kwanza wote hawavuki miaka kadhaa ya kuishi, ukifika tu huo muda wanafariki kwa matukio tofauti.

Na kuna baadhi ya familia mabinti wao hawadumu katika ndoa na kama ni vijana hawadumu katika ndoa na wake zao. 

Ama vijana au watoto wote wa familia wanakuwa na tabia ya kufanana either walevi au wazinzi au wezi na tabia nyinginezo.

Nakadhalika kutegemeana na maagano yaliyowekwa na wazazi waliowatangulia. 

kwa kusema hivyo sina maana kwamba kila wazazi wanaoonyesha kujari pindi mtoto wao wanapokuwa katika kipindi cha ujauzito basi hilo lengo lao,wengine wanafanya kwa nia njema kabisa kama sehemu ya wajibu kwao lakini ukishaona vinaanza kutokea vitu kama hivyo nilivyovitaja au vinavyofanana na hivyo kuwa makini sana maana si kila familia imempokea Yesu, na kama Mungu wa kweli hayuko hapo uwe na uhakika yuko mungu mwingine anatawala hapo.

KWAHIYO ni muhimu sana kuombea tukio hilo la kupata mtoto kabla ya mimba kutungwa maana hapo ndipo adui anatengeneza msingi kwa mtoto, na ndipo Msingi wa Mungu pia unaweza kutengenezwa kuhakikisha kusudi la Mungu ndani ya huyo mtoto linalindwa tangu akiwa tumboni na hata baada ya kuzaliwa.

Waamuzi 13:2-5

Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti. maana yake ni kwamba unatakiwa kufanya maandalizi mapema kabla ya mimba kutungwa kwasababu hapo wakati malaika anamtokea mke wa manoa ilikuwa ni kabla ya mimba kutungwa na anakuja kumpasha habari njema za kufunguliwa kwake lakini haishii hapo bali anampa na maelekezo ya kufanya na namna ya kuishi maana yake anatakiwa kubadili mpaka mfumo wake wa kuishi  kwa ajili tu ya mtoto atakayepitia katika tumbo lake,biblia inasema Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi kwa kumwambia hivo alikuwa anamaanisha akienda kinyume na hapo maana yake ataharibu au kuvuruga kusudi la Mungu ndani ya yule mtoto.

Ikiwa Mungu anaweza kutengeneza maandalizi kwa ajili ya mtoto anayekuja maana yake hata shetani anaweza kutumia nafasi hiyo kupanda mbegu mbaya ili mtoto anapoingia tumboni anakutana na kitu kinatakachompokea na itakuwa ni gharama kubwa pia kumkomboa mtoto kutoka katika maagano ya aliyounganishwa nayo ingawa inawezekana lakini unaweza kuepusha gharama zote hizo kwa kumlinda mapema na kumkabidhi mikononi mwa Mungu akiwa bado tumboni maana kwa akili zako tu za kibinadamu ni ngumu kumlinda.lakini pia unapomkabidhi mikononi mwa Mungu akiwa tumboni inakupa wepesi wa kumuandaa mapema kwa msaada wa roho mtakatifu kutegemeana na kile Mungu amembebesha huyo mtoto maana Mungu aliwaambia wazazi wa samsoni wasimnyoe mtoto nywere pindi atakapozaliwa maana asili ya nguvu zake ilikuwa hapo na siku ziliponyolewa tu ndio ilikuwa siku ya anguko lake na mauti ikapata nafasi,sasa huwezi kuelewa yote hayo mpaka Mungu amekusemesha cha kufanya na kwa wakati gani kwasababu Mungu anajari sana mpaka chakula anachokula mama mjamzito kwa ajili tu ya afya ya mtoto aliyeko tumboni ndivyo maandiko yanavyosema;

“lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.” Waamuzi 13:7

NDIYO MAANA ni hatari sana kwa kijana au binti kuoa au kuolewa na mtu wa imani tofauti kwasababu hakuna namna unaweza kukwepa kushiriki maagano ya mwenzako na haitaishia kwako tu mpaka  uzao wako utaonja hiyo adhabu, ndio maana viongozi wa dini wanapigana na kupambana sana waumini wao wasioe au kuolewa na watu wa imni tofauti na wao, kwa maana wanaelewa gharama ya mtu kuoa mtu wa imani tofauti na ya kwake.

Na hili lilikuwa ni  agizo la Mungu kwa wana wa Israeli ya kwamba wasioe watu wa mataifa, (mtu wa mataifa ni mtu mwenye imani tofauti  na ya kwako)

Yakobo alipata wakati mgumu baada ya kumuoa Raheli binti yake Labani,

Ilipofika saa ya kuondoka kwa yakobo katika nyumba ya Labani mkewe Raheli aliondoka na miungu au vinyago vya baba yake Labani , jambo hilo likaleta shida kati ya yakobo na labani babaye na mkewe.


Kwahiyo ukimuoa binti wa imani tofauti uwe na uhakika utabeba na mzigo wa miungu ya nyumbani kwao, kwasababu binti huyo ama kijana huyo wa imani nyingine unayetaka kumuoa au kuolewa naye amekua na kulelewa katika misingi ambayo ni tofauti na wewe ulivyolelewa lakini pia kubwa kuliko inawezekana yale unayoyaona wewe ni HASI yakawa  ni CHANYA kwa mwenzako na unayoyaona ni CHANYA yakawa HASI kwa mwenzako na wakati huo mnaishi nyumba moja na mnalala kitanda kimoja,

Iko saa mtapata watoto na kila mmoja wenu atataka watoto wakaabudu katika dini/dhehebu lake kwasababu hiyo ndiyo anayoiamini,

Kwa wale waliofunga ndoa za serikali inaweza kuwa rahisi sana kunielewa kwenye eneo hili.

Na ili muweze kuendana lazima mmoja akubali kuweka imani yake chini na kufata ya mwenzake, sasa inategemeana ni Mungu yupi amepata nguvu ya kushinda na kumuangusha mwingine., maana unaweza kujikuta unaingia katika shida ambayo hukuitegemea ya kumucha Mungu wako kwa kisingizio cha kutafuta amani ya ndoa yako na bado amani hiyo husiipate na uzao wako ukaingia kwenye shida maana hili haliishii kwa wazazi tu bali linawatafuna mpaka watoto na ikiwa imani iliyovunjwa ni ya kimila ni wazi kuwa umetangaza vita kati yako na miungu ya kwenu maana hakuna Mungu anayekubali kuwa chini ya Mungu mwingine hata kama anaona nguvu zake ni ndogo atahakikisha anapambana kuwa juu ya mwingine sasa katika mapambano hayo wanaopata shida ni wale walio katika maagano hayo ya pande zote mbili.


Sio siku maalum leo kuzungumzia habari za ndoa lakini nimesikia ndani kukueleza hilo mapema maana linagusa kwa karibu sana uzao wako na maisha yako binafsi maana kuna watu wanaharibikiwa tu maisha yao baada ya kuingia katika ndoa na wanabaki kulalamika kwamba mke au mme aliye naye ana gundu kwa msemo wa vijana wa mjini, pasipokuelewa msingi wa matokeo hayo umesababishwa na wao wenyewe au misingi ya malezi kutoka kwa wazazi wao wa pande zote mbili na hakuna kati yao aliyesimama kuvunja maagano na msingi wa adui na kuinua msingi wa  Mungu wa kweli katika maisha yao au utumishi wao au ndoa yao. 


Nimalize kwa kusema Mungu wangu akubariki sana na zaidi sana afanyike msaada kwako pindi unpojiandaa kupata uzao na kulea ili kwamba kilichobebeshwa ndani ya mtoto wake kiwe halisi na kwa muda sahihi sawasawa na mapenzi ya Mungu baba. 

Mfanye mwanao;

  • ajulikne na Mungu wa kweli kabla ya mimba yake kutungwa
  • mfanye mwanao atakaswe akiwa bado tumboni na kutengwa kimalum kabisa kutegemeana na alichobebeshwa na Mungu. 
  • Zaidi sana hakikisha wewe mwenyewe na mwenzako mko upande wa Mungu huyo mnayehitaji msaada wake juu ya uzao wenu na muwe watu wenye kunia mamoja kwa maana ya imani moja katika kristo Yesu. 

MUNGU WANGU AKUBARIKI SANA, NA AKAFANYIKE MSAADA WA PEKEE KWAKO NA KWA NDOA YAKO NA KWA UZAO WAKO.

MASOMO MENGINE YANAYOHUSU NDOA NA MALEZI











Post a Comment

0 Comments